Zuchu kuimba MABUNO kuna hatari kubwa kupoteza kizazi kijacho

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,594
3,081
Salaam! Msanii pekee wa kike kutoka wcb amekuwa akitoa mfululizo wa nyimbo ambazo kiutamaduni zinaathiri kizazi chetu cha baadae "honey wangu akinuna namkatia mabuno" imagine watoto wangapi wanaimba hii nyimbo?

Ombi langu kwa Basata msifungie nyimbo zinazokashif mamlaka tu! Camera yenu imulike upande wa hii lebo na kizazi chake wanaibomoa na kuirarua jamii.
 
Hata naelewa basi😃😃... nasikia tu watu wanaimba
Mnapenda sana kuwashutumu wasanii kwa kuharibu maadili ikiwa nyie hao maadili hamyazingatii kwa watoto wenu.

Sasa hivi, nikikuambia unitajie series bora na unazozipenda utataja

1. Game of throne iliyojaa ngono tupu.

2. Breaking bad ambayo imejaa uuzwaji wa madawa ya kulevya.

3. Strike, imejaa ngono na ufiraji wa kutisha.

4. Money heist (wizi na ujambazi).

Sijui hayo maadili unayachukuliaje?

Siku hizi ndoa zinavunjika sana na wanawake wanajiuza ovyo mtaani.
 
Hapa home tuna dogo toto la mchungaji 4years aga linaimba...
”Mwenzenu mimi sijui kutongoza, Wakijipitisha namwaga helaa"

Afu wengine nilikua nawasikia wanaimba ”Bebi mwagia ndani"

Nikijaribu kuwakanya nahisi kama ndo ntawafundisha matusi naamua niwaache kama nilivowakuta.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom