Joeli
JF-Expert Member
- Apr 25, 2011
- 4,941
- 3,417
Kwa muda sasa Mozilla wamekuwa wakifanya jitihada kutoka na operating system yao, mpaka sasa tayari modeli mbili za simu zimeshatoka, ambapo ya kwanza ilikuwa ZTE open ambayo ilianza kupatikana hispania na sasa inapatikana uingereza na marekani.
Tofauti na simu zingine, simu ya firefox inauzwa kupitia eBay pekee, inaenda kwa paundi 60 za uingereza sawa na dola 80 za marekani ambapo ukinunua unapata free shipping.
Simu yenyewe haina specification za kutisha ila its all about new operating system.
Habari zingine....
Mozilla simulator pia inapatikana kudownload kwa ajili ya kutest firefox os kwenye desktop yako bureeeeeeeeeee. kama unapenda kuijaribu, pitia tovuti ya firefox os uweze kuishusha.