Zomea zomea yamwangukia Mwakyembe

Wakuu siku ya jana, mh Mwakyembe, amezuiliwa na wakazi wa Kyela kuingia stendi ya Kyela na kuzomewa na wakazi wa hapa wakidai aliwaahidi lami na hajatekeleza, toka juzi hakuna gari linaloingia stendi, natamani sana kuwatumia picha lakini nipo via mobile

unatakiwa kudhibitisha hili badala ya kuwa kama tetesi na majungu
 
Wangemchapa na bakora kabisa maana kapoteza pesa zetu nyingi kuzunguka Marekani akidai anaichunguza Richmond matokeo yake kaishia kumfichia Bwana Mkubwa madudu yake na akakubali kurubuniwa Pipi ya Unaibu Waziri na kutulia tuli kama keshafika Kileleni.

MWAKYEMBE nae KWISHNEAA...

Watu mkizoea majungu na kukurupuka basi mnakufa navyo. Wewe huo upuuzi wa kwamba mamfichia bwana mkubwa madudu umeuokota huko mtaani kwenu nini? Jadili mada hapa ambayo ni kuzomewa na ahadi ya lami, usitake kuchanganya watu hapa. Kwanza habari yenyewe imebaki kuwa uvumi tu usio na uthibitisho.
 
mwakyembe ni Fisadi kuliko wengine, na ni muongo sana lakini si Mwanasheria? ndio mabingwa wa kusema uongo na kukufanya uamini kuwa ni kweli, halafu jeuri mno, hatuwataki wanasheria na maprofesa, ndio waangamizaji kimya kimya

Tafuta nchi yako ya kubagua watu kama unavyotaka. Wewe unataka mchoma mkaa ndiyo aongoze. Mbona hata huko kwenu Chadema hao ndo wamejaa, akina Safari, Baregu, Kahigi na akina Lissu, Mdee, Akoonay. Sasa mbona hukuwakataa hao au kwa sababu ni kokoto wenzio? Upeo finyu wa kutoa blanket condemnation pasipo sababu wala ushahidi!
 
Mwakyembe kaonjeshwa uwaziri akasahau ahadi zake kwa wapiga kura wake wa kyela....kazi anayo
 
Watu mkizoea majungu na kukurupuka basi mnakufa navyo. Wewe huo upuuzi wa kwamba mamfichia bwana mkubwa madudu umeuokota huko mtaani kwenu nini? Jadili mada hapa ambayo ni kuzomewa na ahadi ya lami, usitake kuchanganya watu hapa. Kwanza habari yenyewe imebaki kuwa uvumi tu usio na uthibitisho.

Unanuka harufu ya magamba, pole sana!
 
Kudadadeki Mwakyembe..... Ongeza SPEED na uzidi kuwapa mchongo wa maisha hao Wanyakyusa na ushamba wao.

Wana Kyela niliwaambia sana hapa JF kabla ya uchaguzi kuwa kumchagua Mwakyembe ni kupoteza muda...

Hawahawa akina Kasyabone, Malafyale, Mwafrika, Kanda2 na wengine kibao wakawa wanakesha wakimshambulia Mtanzania(Mwakalinga) usiku na mchana na kumsifia Mwakyembe jinsi alivyo mpiganaji.

Sasa leo hii na hiyo TUSK FORCE yenu kiko wapi?

Ukiolewa na Bwana mlevi huku ulikuwa ukijua kuwa ni mlevi, basi wewe vumilia tu harufu ya Pombe, vitunguu, na kipigo ikibidi kama siyo makelele na ugomvi.

Mwakyembe kwa sasa ndiye kiongozi anayefaa KYELA ili kuwafunza adabu WATANI wangu huko. Mlikataa PEMA sasa mtakiona. Mtafungiana sana barabara hadi mwishoni mfunge na barabara ya kuingia Kyela na kwenda Mpakani.

Makelele mengi na kujisifu kuwa eti Siasa za Kyela ngumu, mumpe Mwakyembe na yeye term 2, blaa blaa nyingi na mkawa mnakesha mkizunguka vijijini na hadi kwenye makanisa mkishangilia TUSK FORCE. Alivyokuja Slaa mkapiga makelele kabisa kuwa "Nyie na Mwakyembe tu....." Vumilieni hiyo ndowa yenu maana hata Mwaka haujaisha. Alikuja na Kikwete na ataondoka na Kikwete.......

NAMPA HONGERA NYINGI SANA MWAKYEMBE KWA KUWASHUGHULIKIA VIZURI TU WANYAKYUSA WA KYELA.
 
Pole Mwakyembe kwa kuwa mnafiki chama chako cha kifisadi wewe utachukiaje ufisadi??? Wahenga walisema "Birds with the same feathers flock together" how come wewe ujifanye msafi katika chama kichafu... Ole wako 2015 inakuja kwa kasi... Angalia utakosa mwana na maji ya moto..Usahuri..Jiunge CDM ili uendeleze mapambano
 
Kuna tatizo hapa; mtoa taarifa anaongelea hali iliopo huko mbeya ambapo wamefunge stendi na kuwa kuna zomea zomea dhidi ya Mkyembe kudai utekeleza wa ahadi zake wakati wa kampeni! Lakini wachangiaji wamegeuza hii thread uwanja wa matusi!

Kila mtu ni lazima ajenge heshima yake binafsi na ya JF kwa michango yake sio kuongea ili mradi kupoteza muda, hatakupoteza muda ni matumizi mabaya ya rasilimali adimu!

Ni vyema kuoanisha maneno na ushahidi pamoja na kufunganisha michango na mada husika.
 
Dr Mwakyembe si CCM. ni opportunist huyo. itikadi yake tangu tutorial assistant UDSM hadi anapata uwakili na sasa mbunge na waziri ni mpinzani wa siasa za Tz. sielewi anajisikiaje kusema CCM oyee. He is not one of them. subirini mtaona.
 
Mwakyembe Kyela hajafanya lolote la maana,kakuza jina kupitia Richmond na bado akashindwa yeye na wenzake kushinikiza wale waliotajwa kwenye taarifa yake wawajibishwe.Kyela ni mji unaoendelea kupitia nguvu ya wafabiashara wadogowadogo na si kupitia viongozi wa siasa ambao ni makada wa CCM.NA KWA JINSI NINAVYOJUA KUWA WANANCHI WA KYELA HUWA HAWAPENDI KUFANYA MAKOSA MARA MBILI NI WAZI KWAMBA MWAKYEMBE ATAKUWA NA WAKATI MGU SANA KATIKA MIAKA HII MITANO NA HIVYO KURAHISHA JIMBO KUCHUKULIWA NA CHADEMA,VIVA CHADEMA, WE ARE ON THE RIGHT TRUCK.
 
Dr. H. Mwakyembe (MP) ninavyojua mimi ni miongoni mwa viongozi wachache sana wachapakazi tuliokuwa nao, linalomkwaza mh. dr. Mwakiembe ni sera mbovu na siasa za chama cha magamba. Nyota yake iliwaka cku nyingi ila wakati wa sakata la richmond alithihirisha umakini wake kwa masilahi ya taifa. Tatizo lilojitokeza ni kwamba mh. Dr mwakyembe hakusoma akili za JK kuwa alikuwa anafanya usanii wa kumchafua swaiba wake EL ktk hilo scandal, JK hakuwa na dhamira ya kweli ya kudeal na richmond bali kudeal na EL ambaye alimzidi kwa kila kitu haswa kwnye kufanya maamuzi magumu. USHAHIDI UKO WAZI JARIBU KUANGALIA NAMNA ALIVYOCHUKUA HATUA KTK SAKATA LA RICHMOND, FULL USANII. PILI NI UTEUZI WA JK KUMTEUA MWAKIPESILE KUWA RC-MBEYA inafahamika wazi kuwa MWAKIPISELE ana chuki binafc na Mh. Dr.Mwakiembe tokea akose ubunge. Na ameendelea kumwacha mwakipisile Mbeya ili amwangamize Mh. Dr. kisiasa. Ukifuatilia kwa makini utagundua kuwa kutoonekana kwa viongozi wa mbeya ktka huo mkutano ni njama zilizofanywa na mwakipisile, HUU NI URATIBU MBOVU NDANI CHAMA CHA MAGAMBA.

hatima ya haya yote cdm wakijipanga vyema wanachota majimbo ya mbeya kiulain sana kwa sabbabu za uratibu mbovu chin ya JK. Hata kule kwa mwandosya sio shwari, Tunajua Chama CHA MAGAMBA kimechelesha kumalizia mradi mkubwa na mzuri wa uwanja a ndege simply kwa Sababu chuki za kisiasa, WAZEE WA MAGAMBA WAWE MAKINI KINYUME NA HAPO 2015 WATAPOTEZA KWA UZEMBE KAMA ILVYOKUWA MAJIMBO YA SHINYANGA. PIA WASITEGEE TENA UCHAKACHUAJI UTAWARUDISHA MADARAKANI
 




*Ni kwa serikali kugomea mapendekezo yake ya Richmond
*Washangaa Rais Kikwete kuwapa madaraka aliowatuhumu
*Wasema akijiuzulu atalinda uadilifu na heshima yake


Na Tumaini Makene

MZIMU wa sakata la kampuni tata ya Richomond, umezidi kuwaandama wanasiasa nchini, sasa ikiwa ni zamu ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ametakwa kujiuzulu kutoka serikalini ili kutunza uadilifu wake baada ya serikali kupuuzia maagizo ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la kashfa hiyo.

Ameambiwa kuwa iwapo ataendelea kung'ang'ania kubaki katika serikali ya namna hiyo, atakuwa anafanya hivyo kwa sababu ama ya 'uroho na ulafi' wa madaraka au kutokuwa na uwezo wa kusimamia misimamo ya uongozi adilifu, tofauti na Watanzania wengi wanavyomwelewa.

Hayo yalisemwa jana na mmoja wa makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Fred Mpendazoe, ambaye katika bunge lililopita kabla hajajiuzulu ubunge wake wa Kishapu alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Akizungumza katika mikutano ya Operesheni Sangara ya chama hicho katika Nyanda za Juu Kusin, mkoani Mbeya, amesema kuwa Dkt. Mwakyembe ndiye alikuwa mwenyekiti wa kamati hiyo teule ya bunge, ambayo katika moja ya mapendekezo kwenye ripoti yake, ilitaja watendaji wa serikali waliohusika katika kashfa hiyo, mmoja wao akiwa ni Bw. Bashir Mrindoko, ambaye wakati wa sakata la Richmond, alikuwa ni Kamishna wa Nishati, katika Wizara ya Nishati na Madini.

Bw. Mrindoko ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji, alikuwa kwenye orodha ya kamati ya Dkt. Mwakyembe ikipendekezwa achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu mpya wa Wizara kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC.

Bw. Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua kampuni hiyo kusitisha mkataba wake na serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa zabuni ya umeme wa dharura haujaanza.

"Mwakyembe anapaswa kujiuzulu ili kulinda hadhi yake ya uadilifu kama wananchi wengi wanavyomjua, hakuna haja ya yeye kuendelea kuwa katika serikali ambayo haiheshimu mapendekezo ya kamati yake ambayo bunge liliyaazimia...lakini kama ataendelea kung'ang'ania kubaki ndani ya serikali ataonekana ni mroho wa madaraka au hana msimamo thabiti katika kusimamia misimamo ya uongozi adilifu," alisema Bw. Mpendazoe.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Bw. Kabwe Zitto, aliwaambia wananchi katika mikutano yake kuwa chama hicho kimepanda chati kwa asilimia 400, kati ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na 2010, kwani kabla ya uchaguzi wa mwaka jana kilikuwa na madiwani 101 sasa wameongezeka kufikia 466, huku wabunge wakiongezeka kutoka 11 mpaka 48.

Huku akiwataka wananchi kuendelea kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, kuhakikisha chama hicho kinashinda na kuchukua dola, Bw. Zitto alisema kuwa mgombea urais wa CHADEMA uchaguzi mkuu mwaka jana, Dkt. Willibrod Slaa alishinda lakini matokeo yake 'yakachakachuliwa'.

Aliwashukuru wananchi kwa kuendelea kukiunga na kukipandisha chati chama hicho ndani ya muda mfupi hata kumpatia kura nying 'za ushindi' Dkt. Slaa, akiwataka waendeleze moyo huo wakijipanga zaidi kwa uchaguzi mkuu ujao.

Wakati huo huo imeelezwa kuwa ufisadi mkubwa ikiwemo rushwa na ukosefu wa uwajibikaji wa serikali kwa watu wake umesababisha kuyumba kwa uchumi wa nchi na kumilikiwa na watu wachache, huku Watanzania wengi wakiachwa kando wakigubikwa na umaskini unaochangiwa na makali ya maisha yanayoonekana kuongezeka kila siku.

Hali hiyo imesababisha 'mahubiri' ya amani miongoni mwa Watanzania kutokuwa na uhalisia wowote, ikidaiwa kuwa mtu asiyekuwa na uhakika wa kupata haki ya mlo, elimu na matibabu bora hawezi kuwa na amani ya kweli, katikati ya utajiri wa raslimali zilizoko nchini.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Bi. Chiku Abwao katika mikutano ya maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mbalizi, mmkoani Mbeya katika mikutano yake mbalimbali ya Operesheni Sangara kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Alisema kuwa chama hicho hakitakubali Watanzania waendelee kufanyiwa dhuluma na viongozi wao wenyewe, ambao wamesahau kuwa uongozi ni dhamana ya kuwajibika kwa watu wala si kujinufaisha au kujineemesha binafsi.

"Umaskini tulionao si wa kurogwa wala hatukuumbiwa na Mwenyezi Mungu, ni matokeo ya kukosekana akwa uongozi unaowajibika kwa maslahi ya wananchi wake wanaolipa kodi kila siku lakini kodi hiyo haionekani ikirudi kwa kwao kwa maana ya huduma za kijamii.

"CHADEMA hatuwezi kuvumilia hali hii, ndiyo maana safari hii tumejipanga kupambana vilivyo bungeni kuhakikisha serikali inawajibika kwa wananchi wake hasa katika suala la kukuza uchumi na kupunguza umaskini wa Watanzania.

"Hali ya wananchi inazidi kuwa mbaya, umaskini na ukali wa maisha unazidi kuongezeka kila kukicha, lakini hakuna mikakati imara na mahsusi kuhakikisha mwananchi anapata nafuu ya maisha. Tunataka serikali ishushe bei ya umeme na pia sehemu ambazo umeme haujafika ufikishwe, ili wananchi wapate nafuu ya maisha...suala la nishati ni muhimu sana katika maendeleo ya uchumi wa nchi na mwananchi mmoja mmoja.

"Hivi majuzi tumeandamana huko Mwanza mkamsikia Rais Kikwete akiagiza sukari ishuke bei mpaka sh. 1,700 lakini mpaka leo hakuna uhalisia katika agizo lake hilo, sukari pamoja na bidhaa nyingine muhimu kwa wananchi zinazidi kupanda...anatoa agizo akisahau kuwa mahali sahihi pa agizo lake hilo ni bungeni ambako serikali inaweza kushusha kodi za baadhi ya bidhaa na huduma ili kumpatia ahueni ya maisha Mtanzania maskini," alisema Bi. Abwao.

Kwa upande Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi wa CHADEMA, Bw. Wilfred Lwakatare alisema kuwa vitendo vya ufisadi vinavyoachiwa kutamalaki kuanzia ngazi ya chini katika serikali za mitaa mpaka serikali kuu ni moja ya chimbuko la kuyumba kwa uchumi wa nchi unaomilikiwa na watu wachache, hivyo kusababisha wananchi wengi kutengwa, wakiendelea kugubikwa na umaskini unaodhihirika katika ukosefu wa kipato na huduma za msingi za jamii.

Alisema kuwa kwa jinsi hali ya uchumi inavyozidi kuwa ngumu imefikia mahali hata vijana hawataki kuwa na familia kwa maana ya kuoa na kuolewa kwa hofu ya kushindwa kumudu maisha ya kuhudumia familia.

http://www.blogger.com/post-edit.g?blogID=1185314680614945258&postID=7623559469018901655
 
Mawazo ya mdau wa facebook kuhusu kilichotokea jana Kyela:

Jana palikuwa hapatoshi uwanja wa siasa mjini Kyela baada ya CHADEMA kuivamia wilaya hii yenye neema kibao lakini watendaji wake ni sifuri na kuanza kumwaga sera zake bila uwoga wowote!Mh Sugu alianza kwa kumponda JK,Ridhiwani,Makamba,Nape,Lowasa,na Mwakyembe mwenyewe kwamba ni mafisadi walioshindikana kama wanabisha wampeleke mahakamani kwani CDM hawaogopi watasema ukweli daima nakama wanabisha wakamfungulie kesi kwani CDM inawanasheria hadi haijui itawaweka wapi,Sugu alikuwa akiongea kwa kjiamini zaidi na akiwa ana apa kwa msisistizo anayoyasema ndipo akasema amejitolea kuwa mbunge wa Kyela hadi hapo CDM itakapo chukua jimbo hili rasmi 2015,Alisema Mwakyembe amepewa unaibu uwaziri ili ashindwe kuikosoa serikali,alisema mbunge amekuwa msanii na anatoa ahadi hewa na kushindwa kuwasaidia wananchi wake,;Barabara ya matema imekuwa kitendawili aliahidi yeye na JK 2005 hadi leo imekuwa kitendawili,Stand kuu inatia aibu imekuwa bwawa la kambale wakati wanapoke a ushuru kila siku,aliahidi kuweka lami barabara za mjini hajatekeleza,Ni aibu kijiji anachotoka mbunge hakuna maji ya bomba,umeme.Ameshindwa kuwatafutia wakulima wa Cooa soko la uhakika hatimaye wanauza kwa bei ya chini kwenyemakampuni nayeye mwenyewe akiwa na hisa huko,,Mchele wa Kyela unatamba kwenye masoko ya Dar na Zanzibar lakini mkulima wa Kyela hafaidiki wanalanguliwa na wapemba na wajanja wachache,,wakati yeye kamaa mbunge ilibidi awaawasaide kuunda bodi ili isimamie soko la wakulima na wenyewe wapatewapate faida!!!!!!y
 
makini mwakye naye huyu vipi jamani hela zote za kwenda majuu kuijua richmondi naye ameficha madudud amekunywa bia kaingia ubia na wazee wa migogoro
 




Dr-Harrison-Mwakyembe-300x244.jpg

MZIMU wa sakata la kampuni tata ya Richomond, umezidi kuwaandama wanasiasa nchini, sasa
http://uniqueentertz.blogspot.com/2011/05/drmwakyembe-atakiwa-kujiuzulu-chadema.html ikiwa ni zamu ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ametakwa kujiuzulu kutoka serikalini ili kutunza uadilifu wake baada ya serikali kupuuzia maagizo ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la kashfa hiyo.
Ameambiwa kuwa iwapo ataendelea kung'ang'ania kubaki katika serikali ya namna hiyo, atakuwa anafanya hivyo kwa sababu ama ya 'uroho na ulafi' wa madaraka au kutokuwa na uwezo wa kusimamia misimamo ya uongozi adilifu, tofauti na Watanzania wengi wanavyomwelewa.
Hayo yalisemwa jana na mmoja wa makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Fred Mpendazoe, ambaye katika bunge lililopita kabla hajajiuzulu ubunge wake wa Kishapu alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
Akizungumza katika mikutano ya Operesheni Sangara ya chama hicho katika Nyanda za Juu Kusin, mkoani Mbeya, amesema kuwa Dkt. Mwakyembe ndiye alikuwa mwenyekiti wa kamati hiyo teule ya bunge, ambayo katika moja ya mapendekezo kwenye ripoti yake, ilitaja watendaji wa serikali waliohusika katika kashfa hiyo, mmoja wao akiwa ni Bw. Bashir Mrindoko, ambaye wakati wa sakata la Richmond, alikuwa ni Kamishna wa Nishati, katika Wizara ya Nishati na Madini
Bw. Mrindoko ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji, alikuwa kwenye orodha ya kamati ya Dkt. Mwakyembe ikipendekezwa achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu mpya wa Wizara kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC.
Bw. Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua kampuni hiyo kusitisha mkataba wake na serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa zabuni ya umeme wa dharura haujaanza.
 




[font=&quot] [/font]
dr-harrison-mwakyembe-300x244.jpg

[font=&quot] mzimu wa sakata la kampuni tata ya richomond, umezidi kuwaandama wanasiasa nchini, sasa[/font]
http://uniqueentertz.blogspot.com/2011/05/drmwakyembe-atakiwa-kujiuzulu-chadema.html[font=&quot] ikiwa ni zamu ya naibu waziri wa ujenzi, dkt. Harrison mwakyembe ambaye ametakwa kujiuzulu kutoka serikalini ili kutunza uadilifu wake baada ya serikali kupuuzia maagizo ya kamati teule ya bunge iliyochunguza sakata la kashfa hiyo.[/font]
[font=&quot] ameambiwa kuwa iwapo ataendelea kung'ang'ania kubaki katika serikali ya namna hiyo, atakuwa anafanya hivyo kwa sababu ama ya 'uroho na ulafi' wa madaraka au kutokuwa na uwezo wa kusimamia misimamo ya uongozi adilifu, tofauti na watanzania wengi wanavyomwelewa.[/font]
[font=&quot]hayo yalisemwa jana na mmoja wa makada wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), bw. Fred mpendazoe, ambaye katika bunge lililopita kabla hajajiuzulu ubunge wake wa kishapu alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini.[/font]
[font=&quot] akizungumza katika mikutano ya operesheni sangara ya chama hicho katika nyanda za juu kusin, mkoani mbeya, amesema kuwa dkt. Mwakyembe ndiye alikuwa mwenyekiti wa kamati hiyo teule ya bunge, ambayo katika moja ya mapendekezo kwenye ripoti yake, ilitaja watendaji wa serikali waliohusika katika kashfa hiyo, mmoja wao akiwa ni bw. Bashir mrindoko, ambaye wakati wa sakata la richmond, alikuwa ni kamishna wa nishati, katika wizara ya nishati na madini[/font]
[font=&quot]bw. mrindoko ambaye hivi karibuni aliteuliwa na rais kikwete kuwa naibu katibu mkuu katika wizara ya maji, alikuwa kwenye orodha ya kamati ya dkt. Mwakyembe ikipendekezwa achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri katibu mkuu mpya wa wizara kuhusu udhaifu wa richmond development company llc.[/font]
[font=&quot]bw. Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua kampuni hiyo kusitisha mkataba wake na serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa zabuni ya umeme wa dharura haujaanza.[/font]

hivi viongozi wetu wako makini kweli????????????????? Yaani mtu anafanya madudu anapewa tena post akafanye madudu!
 
Mwakyembe alikuwa mwenyekiti tu, na alishafanya kazi yake vizuri sana
Wajibu wa kusimamia mambo yale ulikuwa wa BUNGE zima si yeye peke yake
Wananchi nasi tulikuwa na wajibu wetu tumeshindwa, yeye alipaswa kufanya nini tena na spika alitupilia mbali shauri lile!!
Wala hapaswi kujiuzulu, labda bunge zima la kipindi kile maana ilikuwa ndo kamati yao, na ripoti ile ilipita na kuungwa mkono na wote.
 
Back
Top Bottom