mdau kaandika haya kwenye facebook kuhusu sakata la Kyela na kufungwa stand:
kiukweli ni kwamba CCM kwa hapa mjini wafanye kazi ya ziada saana kuwashawishi vijana waikubali jana ilikuwa ni aibu tupu diwani anatukanwa matusi ya nguoni ,mkurugenzi na wengineo kasoro DC ndio aliyekuwa anasikilizwa na Mbunge ndio hawataki hata kumsikia wlishamfukuza mara mbili na akipita anazomewa na alienda Ikolo(kijijijni kwao)walimzomea na kugoma kumsikiliza kutokana na ahadi ya maji aliyowa ahid ikabidi atoe 250,000 lakini wakadai wanachotaka ni maji,boda na ngana napo hakupata mapokezi mazuriKwakifupi Chama tawala wajipange upya vinginevyo CHADEMA wanachukua jimbo,Viongozi waliofika jana jioni ni Mbunge wa Mbeya mjini J.Mbilinyi(Mr 2,Sugu) Mbunge wa Hai Freeman Mboye na Dr Slaa na viongozi wengine wanawasili leo,Ila walipokelewa na wananchi wengi saana na wananchi waliwalazimisha watembee kwa miguu waone ubovu wa barabara na stand!Mengi mtayapata jion baada ya mkutano!!