Zoezi la sensa limeshatiwa doa tayari!

yani hilo zoezi kiufupi limeshafeli..wananchi hawajatayarishwa vizuri.kwa mfano mikoa yenye waislam wengi kama pwani,wananchi wengi hawataki ata kuliskia..na shekhe ponda ndo huyo wanamsikiliza..sasa serikali ingeanza na kumuelimisha kwanza sheikh ponda alafu ili atumie nguvu aliyonayo kuwashawishi waislam, kwasababu yeye mwenyewe elimu kidogo tatizo ndo maana haelewi maana ya sensa..ni maoni tu.

shekh ponda ni kichwa ndio mana wengi tuko nae bega kwa bega. Wacha serikali ifanye majaribibio.
 
Nilitegemea walimu kutowekwa katika sensa ila nikahisi nafasi yao itachukuliwa na wananchuo waliohitimu juzi tu lakini kata yetu ya ubungo(pengine nahisi ndo kata yenye wanafunzi wengi hapa tanzania)...wanachuo waliochaguliwa hawafiki hata 20 ni jumla ya watu 356, asilimia kubwa ya waliochaguliwa wameandikwa kuwa ni form 4's, ikiwa pia sio kweli kwani nahisi hao ni std sema tu wameamua kutuzuga..
Nakuambia ni wale waliotoa rushwa mkuu! Linaloshangaza ni kuwa unaoona wameandikwa f4s hakuna anayewajua mtaa ule. Ebu subiri siku ya Sensa utaona wale mama lishe, mke wa mtendaji na mashoga zake ndo wako ndani ya nyumba. Nasikia hii kitu inajulikana mpaka juu na ata ikiwa unamjua mtu aliyechomekwa itamaliziwa wilayani! Inatia hasira sana kuchezea vitu vya msingi wkt hela yenyewe ya ufadhili au mikopo!
 
dah huku pugu mpk naingia mitambon sijaona wala kusikia majina ya walioteuliwa , mida flani ivi nilikwenda ofsi za kata zilikuwa zmefungwa, so bdo ni kizungumkuti haeleweki ila naendelea subiri!
 
Nimetoka kazini na nilipofika nyumbani niliuliza kuhusu habari ya kazi ya sensa, niliambiwa kuwa dau la kupata nafasi ni sh. 150,000/=, fedha ambayo unatakiwa utoe pale wilayani ili wakupe nafasi ya kuwa miongoni mwa wasimamizi wa sensa. Pia, inasemekana kuna baadhi ya watendaji wanajaribu kuunganisha ndugu zao kwenye hizo nafasi au kuuza kwa watu wengine kwa bei niliyotangulia kusema.

Nafikiri kuwa nchi yetu inaelekea kubaya zaidi hasa linapokuja suala la rushwa za kazi, upendeleo, na matumizi mabaya ya madaraka.

Tuombe Mungu atunusuru na kadhia hii mbaya na hatari kwa maendeleo ya nchi yetu.
 
Mwalimu Nyerere ktk kitabu chake, Nyufa, cha mwaka 1995 alisema "sasa Tanzania inanuka rushwa..... tunataka kiongozi anayejua hivyo, ambaye atasema rushwa kwangu ni mwiko, mwaminifu kabisa kabisa hawezi kugusa rushwa na ... watoa rushwa watamjua hivyo" yale aliyokuwa anazungumzia Mwalimu leo yanaonekana wazi wazi mchana kweupe viongozi wa ccm wanakula rushwa kuliko rushwa yenyewe. Mungu ibariki Tz utuepushe na adhabu hii kwetu sisi wanyonge wa Tz kwani nchi inamilikiwa na wachache na watanzania umewapa uwoga mwingi mno. Heri shujaa aliyekufa Kuliko mwoga anayeendelea kuishi. Mtanzania usikate tamaa
Ha ha ha ha ha......................! Da, mpa CCM itoke madarakani. Nyerere ange tutengenezea jinsi ya kupindua genge la majizi angetuweka pazuri hii leo!
 
leo asubuhi nilimpigia simu rafik yangu ambaye aliomba usimamizi wa sensa huko lindi katika halmashauri ya kilwa ameniambia amekosa japo kuwa ana diploma na degree ya procurement cha kushangazi wamechukuliwa waalimu ambao wengi wao n form 4 wenye certificate
Nadhani wanahitaji vilaza. Ni vigumu kugawa kazi hii kwa illitirate kama watendaji kata wakafanya vizuri. waliowengi ni f4 dvn 0 alafu et wamchukue msomi kama huyo! Huyo jamaa angesaidia sana.
 
kilwa, nachingwea na ruangwa lindi, zoez limegubikwa na utata mtupu. 1. hakuna usaili wa makarani na wasimamizi wa sensa 2. wamechagua wafanyakazi wa halmashauri eg mabwana shamba, maendeleo ya jamii, maafisa elimu wasaidizi, wahasibu n.k 3. baadhi hawana vigezo eg wako zaidi ya miaka 45, si wenyeji wa maeneo husika, na baadhi wana matatizo ya macho (hawawezi kusoma bila miwani)
 
Baadhi ya walimu waliogoma katika manispaa ya morogoro wataenguliwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi inayotegemewa kuanza kuanzia jumatatu wiki ijayo. Zoezi hilo limefanyiwa kazi kwa kutumia ripoti za walimu walioripoti kwenye vituo vyao vya kazi tarehe 31/07 na 01 / 08 ambapo waratibu elimu walikuwa wanapita mashuleni.
 
Huu ugoigoi na kujuana sijui kutaisha lini. watu wameomba ukarani wa sensa, hawajajulishwa watu wamepiga interview kimyakimya ili watu competent wasipate. Kata ya Saranga, Kimara.
 
Huu ugoigoi na kujuana sijui kutaisha lini. watu wameomba ukarani wa sensa, hawajajulishwa watu wamepiga interview kimyakimya ili watu competent wasipate. Kata ya Saranga, Kimara.
Unajaza seva ya jf bure wakati hata kuichangia hutaki. Thread gani hii??
 
Huu ugoigoi na kujuana sijui kutaisha lini. watu wameomba ukarani wa sensa, hawajajulishwa watu wamepiga interview kimyakimya ili watu competent wasipate. Kata ya Saranga, Kimara.
Kijana usikurupuke, soma hapa....

Forum: Jukwaa la Siasa [FONT=Verdana said:
Tanzania's Political Forum. Tafadhali hakikisha hoja unayoiweka hapa ni ya kisiasa kweli![/FONT][/COLOR]
 
Back
Top Bottom