Zoezi la sensa limeshatiwa doa tayari!

Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,399
255
Zoezi la kumpata Karani mwandamizi na Karani wa Sensa limevamiwa na wahuni. Watendaji wa Kata wanachagua kwa RUSHWA ya shulling 20,000/= .

Wanachagua wale wa darasa la saba au yeyote ilimradi ametoa rushwa. alimu wametupwa pembeni kwa maagizo maalum kutoka juu kuwa wamegoma.

Ni hatari kama hali hii itaachwa iendelee hivi kwakuwa kuna uwezekano wa kuharibu suala zima la kupata takwimu sahihi na kuharibu pesa za watanzania.

Nawasilisha.
 
Katika hali ya kushangaza watendaji wanapiga simu kwa watu na kuwauzia nafasi. Kinachotia shaka ni jinsi UZEMBE huu unavyoachwa kwenye zoezi hili muhimu. Mambo ya sensa katika eneo muhimu sana ni hili la ukusanyaji taarifa (Data Collection). Iwapo eneo hili litaaribika basi maeneo yote yanayofuata yatakuwa yamehariba pia! Yaani maeneo ya Data Organization, Data Analysis, Data Interpretation and Report Writing. Tusubiri kupata data zisizo sahihi kwa uzembe huu.
 
yani hilo zoezi kiufupi limeshafeli..wananchi hawajatayarishwa vizuri.kwa mfano mikoa yenye waislam wengi kama pwani,wananchi wengi hawataki ata kuliskia..na shekhe ponda ndo huyo wanamsikiliza..sasa serikali ingeanza na kumuelimisha kwanza sheikh ponda alafu ili atumie nguvu aliyonayo kuwashawishi waislam, kwasababu yeye mwenyewe elimu kidogo tatizo ndo maana haelewi maana ya sensa..ni maoni tu.
 
Wajumbe, tupeni taarifa toka maeneo mbali mbali mliko ili tuikomboe hela ya watanzania. Hii kitu kwa nchi yetu hufanyika mara moja na ni kila baada ya miaka 10 au tukishindwa ni zaidi ya hiyo miaka. Tulifanyie kazi tusaidie wale waliopewa majukumu alafu wakaamua kulala.
 
Nimewasiliana na marafiki zangu sehemu mbali mbali mbali kwa hapa Dar wanakiri kuwa zoezi limefunikwa na utata. Rafiki yangu aliyepo kata ya Buyuni Dar amesema kule si rushwa tu ya 20 elf bali posho ni makubaliano. Amesema kuwa hali hii ni ya kwaida kwani ata kwenye uchaguzi huwa ndo muda wa watendaji kata kuvuna na anakupa nafasi alafu mnagawana pasu. Hii ni hatari na itatuletea balaa kwenye zoezi hili muhimu.
 
Mh Tanzania na marushwa sijui inakuwaje kila kitu ni issue ma CCM na watendaji wao wa kata ni issue sana
 
serikali yetu bhana sijui watu wa usalama wanatusaidiaje kama nchi?
Hii ni kuchezea fedha ya wafadhili na kuharibu mambo ya msingi ya kitaifa! Zoezi hili ni lazima lifanywe kwa uangalifu na si kitu cha kufanyia mzaha! Angalia, ungekuwa mwenge ungeona kuwepo umakini lakini zoezi muhimu ambalo hadi shule zinafungwa na la muda mfupi linafanyiwa mzaha! Tunaomba kupewa taarifa ya kuwaondoa wale wote walioingia kwa kutokuwa na vigezo na wale waliolipishwa hela wajulikane na waseme wamempa nani na amekusanya kiasi gani kwakuwa tunajua na kwakujiamini kuwa RUSHWA imetembea na bado inaendele kutembea.
 
Habari wakuu wa jf,muda c mref 2metoka halmashaur ya manispaa ya shy kuchek majina ya mawakala wasaidiz wa kusimamia sensa,aisee wote waliochaguliwa ni walimu hakuna mwanafunzi hata m1.
NB:kama serikali ilikuwa inajua itachukua walimu tu ingesema sifa ya mwombaj n awe mwalimu,kuliko kupotezea watu muda.nawasilisha wakuu
 
Nilitegemea walimu kutowekwa katika sensa ila nikahisi nafasi yao itachukuliwa na wananchuo waliohitimu juzi tu lakini kata yetu ya ubungo(pengine nahisi ndo kata yenye wanafunzi wengi hapa tanzania)...wanachuo waliochaguliwa hawafiki hata 20 ni jumla ya watu 356, asilimia kubwa ya waliochaguliwa wameandikwa kuwa ni form 4's, ikiwa pia sio kweli kwani nahisi hao ni std sema tu wameamua kutuzuga..
 
Mwalimu Nyerere ktk kitabu chake, Nyufa, cha mwaka 1995 alisema "sasa Tanzania inanuka rushwa..... tunataka kiongozi anayejua hivyo, ambaye atasema rushwa kwangu ni mwiko, mwaminifu kabisa kabisa hawezi kugusa rushwa na ... watoa rushwa watamjua hivyo" yale aliyokuwa anazungumzia Mwalimu leo yanaonekana wazi wazi mchana kweupe viongozi wa ccm wanakula rushwa kuliko rushwa yenyewe. Mungu ibariki Tz utuepushe na adhabu hii kwetu sisi wanyonge wa Tz kwani nchi inamilikiwa na wachache na watanzania umewapa uwoga mwingi mno.

Heri shujaa aliyekufa Kuliko mwoga anayeendelea kuishi. Mtanzania usikate tamaa
 
Waislamu nao walishagoma kuhesabiwa.Swali langu: Je watapata nafasi ya kuwa makarani wa Sensa?
 
leo asubuhi nilimpigia simu rafik yangu ambaye aliomba usimamizi wa sensa huko lindi katika halmashauri ya kilwa ameniambia amekosa japo kuwa ana diploma na degree ya procurement cha kushangazi wamechukuliwa waalimu ambao wengi wao n form 4 wenye certificate
 
Katika hali ya kushangaza watendaji wanapiga simu kwa watu na kuwauzia nafasi. Kinachotia shaka ni jinsi UZEMBE huu unavyoachwa kwenye zoezi hili muhimu. Mambo ya sensa katika eneo muhimu sana ni hili la ukusanyaji taarifa (Data Collection). Iwapo eneo hili litaaribika basi maeneo yote yanayofuata yatakuwa yamehariba pia! Yaani maeneo ya Data Organization, Data Analysis, Data Interpretation and Report Writing. Tusubiri kupata data zisizo sahihi kwa uzembe huu.

kwani hizo data sahihi zimetusaidia nini? Mbond barabarani foleni, madarasa hayatoshi, zahanati hazitoshi, nakazalika!
 
Nimewasiliana na marafiki zangu sehemu mbali mbali mbali kwa hapa Dar wanakiri kuwa zoezi limefunikwa na utata. Rafiki yangu aliyepo kata ya Buyuni Dar amesema kule si rushwa tu ya 20 elf bali posho ni makubaliano. Amesema kuwa hali hii ni ya kwaida kwani ata kwenye uchaguzi huwa ndo muda wa watendaji kata kuvuna na anakupa nafasi alafu mnagawana pasu. Hii ni hatari na itatuletea balaa kwenye zoezi hili muhimu.

kwani kuna shida gani wajameni? Ukitaka kula shurti uliwe! Na pia hauwezi kuvuna bila kupanda.
 
Ni wazi pia waislamu wameshakwamisha sensa. Nashangaa sana kwanini siku zote Serikali inawaogopa hao jamaa. Ingekuwa wakristo saa hii tayari hotuba kali ya kuwadhalilisha kwa kutumia Biblia ingeshatolewa na watawala. Lakini kwa hawa jamaa wanaotaka kuingiza nchi pabaya viongozi wako kimya. Ni lazima katiba ifuatwe katika kuendesha nchi na tusiruhusu watu wachache wenye maslahi yao ya kidini kuharibu nchi. Hata kama kipengele cha dini kikiingizwa itakuwa ndio mwanzo wa lawama maana wakijikuta wako wachache kuliko wanavyoaminishwa wataanza kusema ni hujuma na uchakachuaji na kuzusha migogoro zaidi. Wailamu mliosoma waelimisheni wenzenu waache jazba na kufuata sheria za nchi.
 
Back
Top Bottom