Mohamed Abubakar
JF-Expert Member
- Jun 26, 2014
- 915
- 1,113
Tamko la Maimamu Tanzania kwa Ummah kufuatia kikao cha dharura kilichofanyika leo tarehe 27, Oktoba 2024.
Lifuatayo ni TAMKO LA AZIMIO LA MAIMAMU KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.
TAMKO: Waislam Hawatoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa iwapo tutakinai kulikosekana Uadilifu na udanganyifu katika zoezi zima la Uandikishaji.
Kwa mujibu wa takwimu za TAMISEMI takribani Watanzania 31,282,331 wamejiandikisha kupiga kura katika zoezi lililoanza Oktoba 11 mpaka Oktoba 20,2024.
Kwa takwimu hizi zikiliganishwa na takwimu za Sensa ilizofanyika mwaka 2022 ambapo zilionesha watu wenye umri wa miaka kumi na sita na kuendelea walikua 32,988,131, kitakwimu kama tukipunguza idadi ya vifo na wale ambao mpaka wakati wa uchaguzi bado watakua na miaka 17, basi kuna uwezekano mkubwa Wizara ya TAMISEMI imeweza kuwasajili Watanzania wote wenye sifa za kupiga kura.
Kwa ushahidi wa kimazingira uwezekano huo haupo bali kuna kila dalili za Udanganyifu umefanywa. Uislam unakataza kila aina ya udanganyifu. Na mbaya zaidi udanganyifu huo ufanye kupigania itikadi au imani ambazo zinapingana na uwepo wa dini na uwepo wa Mungu.
Katika uchaguzi waislam hatuzingatii kufata sera za chama bali itikadi na mrengo wa chama.
Serikali yetu ni yenye kufata imani ya Ujamaa.
Kama kuna udanganyifu unafanywa na watendaji wa serikali katika zoezi ya kuandikisha daftari la wapiga kura. Ni wazi udanganyifu huo una lenga kutaka imani ya Ujamaa iendelee kutawala.
Wale wanadhani Ujamaa umekufa, wajue hali hii ya kuendelea kudhibiti makundi mengine ya imani ni ishara kuwa imani ya Ujamaa bado inafanya kazi. Kwani katika nchi za kibepari huwezi kukuta kudhibitiwa kwa makundi ya imani nyingine.
Kwa hiyo Ujamaa bado unaishi.
Kwa ufupi muislam hapaswi kufa kutetea imani ya Ujamaa. Na kwamba tukikinaishwa kuwa kuna udanganyifu katika zoezi la uandikishaji katika daftari la wapiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Sisi maimamu na waumini wetu hatutoshiriki uchafuzi huu.
Maimamu Tanzania
27 Oct 2024