Zoezi la abunge kuapishwa laendelea, Je kesi za kupinga matokeo ya ubunge zina maana?

Mwinjilist mtume nabii

JF-Expert Member
Feb 21, 2015
2,437
1,097
Jamani Ikiwa Zoezi La Kuapishwa Kwa Wabunge Linaendelea, Je Sheria Inasemaje Kuhusu Wabunge Ambao Kwenye Majimbo Yao Kesi Zipo Mahakamani Za Kupinga Matokeo Kwamba Hayakuwa Ya Haki??

Kutakuwa na uwezekano Tena Kwa Mbunge ambaye Tayari Amekwishaapishwa Kufutwa Kutokuwa Mbunge Tena??

Karibuni
 
Una muda gani unafuatilia siasa na masuala ya Uchaguzi?

Ndiyo Mara ya kwanza kupiga kura?
 
Hilo sio tatizo anaweza akaapa akishindwa kes aut analetwa alieshindwa anaapishwa anaendelea na kazi
 
Una muda gani unafuatilia siasa na masuala ya Uchaguzi?

Ndiyo Mara ya kwanza kupiga kura?

Taaluma Yangu Mimi Ni "Mchungaji" Nadhani Unanijua Nauliza Ili Niweze Kujua Kama Sheria Ya Nchi Inasemaje. Maana Sisi Tunaongozwa Na Sheria Za Mbinguni. Mungu Akubariki
 
Kwa sheria ilivyo mbunge ni mbunge halali akishatangazwa na msimamo wa uchaguzi awe ameiba kura au vinginenyo. Akishakabidhiwa Cheti cha ushindi huenda nacho ofisi za bunge akiwa ni mbunge mteule. Anapoapishwa huwa mbunge kamili.

Mtu yeyote mwenye kupiga matokeo ya Ubunge au urais sheria imetoa fursa ya kupiga kesi mahakamani. Kesi za matokeo ya Ubunge zinatakiwa kusikilizwa ndani ya Miaka 2
 
Vipi kuhusu ela wanazopewa ikiwemo mill 200+ Za Magari????

Akishindwa case zinarudi? Au ndo matumizi mabaya ya Serikali????
 
Kwa sheria ilivyo mbunge ni mbunge halali akishatangazwa na msimamo wa uchaguzi awe ameiba kura au vinginenyo. Akishakabidhiwa Cheti cha ushindi huenda nacho ofisi za bunge akiwa ni mbunge mteule. Anapoapishwa huwa mbunge kamili.

Mtu yeyote mwenye kupiga matokeo ya Ubunge au urais sheria imetoa fursa ya kupiga kesi mahakamani. Kesi za matokeo ya Ubunge zinatakiwa kusikilizwa ndani ya Miaka 2

Ndani Ya Miaka2 Huyu Mbunge C Anapata Mshahara?Na Posho Kama Kawaida? Sasa Je, Mshahara Huo Utahesabika Wa Nani Ikiwa Mbunge Aliyeshtaki Kesi Ameshinda?
 
Taaluma Yangu Mimi Ni "Mchungaji" Nadhani Unanijua Nauliza Ili Niweze Kujua Kama Sheria Ya Nchi Inasemaje. Maana Sisi Tunaongozwa Na Sheria Za Mbinguni. Mungu Akubariki

Mchungaji mwenye kondoo mtiifu Junior. Cux
 
Last edited by a moderator:
Joseph warioba si tu aliapishwa kuwa mbunge , bali aliteuliwa na kuapishwa kuwa waziri mkuu na mzee ruksa , lakini ubunge wake ulitenguliwa mahakamani na akapoteza uwaziri mkuu .
 
Jamani Ikiwa Zoezi La Kuapishwa Kwa Wabunge Linaendelea, Je Sheria Inasemaje Kuhusu Wabunge Ambao Kwenye Majimbo Yao Kesi Zipo Mahakamani Za Kupinga Matokeo Kwamba Hayakuwa Ya Haki??

Kutakuwa na uwezekano Tena Kwa Mbunge ambaye Tayari Amekwishaapishwa Kufutwa Kutokuwa Mbunge Tena??

Karibuni

Usijali, umbunge hutenguliwa anytime. Kama pana kesi, ubunge unavuliwa ndugu, wala usihofu.
 
Dah! kuna mahali nimeona pastor nae ni muumini wa PM tena topic yenyewe ilikua na ukakasi kidogo nikasema naaaaam.

Yeah pastor anaendesha huduma zake pm... ila ni kwa watoto wazuri tu muda huu, wengine mtajulishwa mabadiliko yakitokea 😊😊😊
 
Ndani Ya Miaka2 Huyu Mbunge C Anapata Mshahara?Na Posho Kama Kawaida? Sasa Je, Mshahara Huo Utahesabika Wa Nani Ikiwa Mbunge Aliyeshtaki Kesi Ameshinda?

Elewa kwamba atakuwa mbunge halali mpaka siku kesi inaamuliwa na kushindwa. Hivyo jimbo lake bado linakuwa likiwakilishwa vyema bungeni na huyo mbunge husika. Akishindwa mshahara wake na marupurupu hukatikia hapo.
Usijali mkuu, halipwi nyongeza ila marupurupu yao ya kawaida tu
 
Sheria ipo palepale tu kama kwenye issue zingine yaani kwa sasa ni mbunge halali kabisa mpaka hapo mahakama itakapoamua vinginevyo na ndipo ubunge wake utatenguliwa (kwa mtaji huu anasimama kama mtuhumiwa tu)
 
Kwa sheria ilivyo mbunge ni mbunge halali akishatangazwa na msimamo wa uchaguzi awe ameiba kura au vinginenyo. Akishakabidhiwa Cheti cha ushindi huenda nacho ofisi za bunge akiwa ni mbunge mteule. Anapoapishwa huwa mbunge kamili.

Mtu yeyote mwenye kupiga matokeo ya Ubunge au urais sheria imetoa fursa ya kupiga kesi mahakamani. Kesi za matokeo ya Ubunge zinatakiwa kusikilizwa ndani ya Miaka 2

Sio miaka miwili
Ni miezi 6
 
Back
Top Bottom