Mahakama na wanasiasa wa Tanzania wana la kujifunza kwa Wazambia kuhusiana na kesi za matokeo ya uchaguzi

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,143
22,111
Mwaka huu nimetokea kuvutiwa na siasa za Zambia na kuamua kufuatilia mambo kadhaa kupitia mitandao ya kijamii. Kuna jambo limetokea siku za hivi karibuni ambalo limenishangaza sana na ni somo kubwa sana kwa siasa za Tanzania na mhimili wa mahakama.

Wote tunakumbuka uchaguzi wa wenzetu ulifanyika mwezi wa nane ambapo baada ya matokeo kukatokea washindani ambao waliona uchaguzi haukuwa huru na wa haki waliamua kwenda mahakamani kudai haki. Hilo sio jambo la kushangaza kwasababu hata hapa kwetu kila baada ya uchaguzi kuna kesi hufunguliwa kupinga matokeo.

Kinachoshangaza ni kwamba chini ya mitatu tangu kesi kufunguliwa tayari mahakama za Zambia zimeshatoa hukumu ya hizo kesi. Wabunge watano hadi leo tayari wamepata pigo ya ushindi wao kubatilishwa na mahakama. Wabunge hao na majimbo yao ni;

1. Bowman Lusambo - Kabushi
2. Joseph Malanji - Kwacha
3. Mutotwe Kafwaya - Lunte
4. Sibongile Mwamba - Kasama Central
5. Lukas Simumba - Nakonde.

Binafsi kilichonishangaza zaidi ni wabunge hao kupokea maamuzi ya mahakama kwa heshima bila kutoa maneno ya kuudhi dhidi ya mahakama kama ilivyo kwa CHADEMA hapa Tanzania.

Wanasiasa na Mahakama zina kujifunza toka kwa wenzetu. Kesi zichukue muda mfupi na pia wanasiasa hasa wa upinzani waziheshimu mahakama.
 
Ila kwa hawa wetu wanasemekana kuwa na masikio mithili ya yule jamii ya mjusi. Kujifunza hivi hivi tu? Hilo ondoa.
 
Mtoa hoja huwezi jenga hoja yako mpaka uwahusishe Chadema?au unaona hoja yako haitajibiwa bila kuwepo kwa Chadema?umeelezea vema ila hujatuambia majaji hawa wa Zambia wanateuliwa vipi na unajifanya kuwa hujui wakati ccm ilivuruga huu so called uchaguzi na kuonekana kama uchafu tu,ccm wanaogopa nini to level the playing field halafu wananchi wachague?
 
Back
Top Bottom