Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,869
- 20,051
Umeamkia kutoka kilabu gani leo hii ndugu yangu wakati swala hili bado linashughulikiwa na timu ya kimataifa ya arbitration na wala hawajatoa uamuzi wao? Kumbuka kuwa kuna sheria ya kimataifa iliyo wazi kabisa kuhusu definition ya mpaka unaohusu maji yalioko mipakani kuwa siku zote maji hayo yatagawanywa baina ya nchi mbili husika. Mipaka ya nchi haiwekwi kwa kingo za maziwa au mito; ama ziwa/mto wote pamoja na ardhi inayolizunguka iko chini ya nchi moja au nchi mbili zinagawana maji ya ziwa au mto huo. Angalia miaka ya nchi hizi ambazo ama iko kwenye maziwa au mitoni.Sote tunajua kuwa Malawi wamesema ziwa Nyasa, ambalo kwa Malawi linaitwa Ziwa Malawi, ni mali yao na Tanzania haina hata tone moja la maji. Mazungumzo yanayoratibiwa na Tanzania yameshindwa kubadili msimamo wa Malawi. Malawi imejiandaa kwenda mahakamani ya kimataifa, ICJ, kutafuta suluhu ya kile wakisemacho. Uwezekano wa kushinda kesi ni mkubwa, tena mkubwa sana.
Malawi ina ushahidi wa kutosha kuhusu wasemalo: mkataba wa Heligoland 1890 kati ya Mjerumani na Mwingireza uliipa Uingereza (Malawi kwa sasa) ziwa lote. Mjerumani (Tanganyika/Tanzania) iliachiwa Heligoland na makoloni mengine Afrika ya Magharibi.
Kuna ushahidi wa kutosha pia kuwa waziri mkuu wa Tanzania, kwa wakati huo, Kawawa, aliwahi kutoa matamko Bungeni, mara nyingi tu, kuwa Tanganyika/Tanzania haina hata tone moja la maji katika ziwa Nyasa/Malawi. Kwa maneno mengine ziwa Nyasa au Ziwa Malawi ni mali ya Malawi.
Ni mhimu kujua kuwa maneno/matamko yanayotolewa na viongozi wa serikali ya nchi husika, kwa sheria za kimataifa, yanahesabiwa kuwa ni sera ya nchi na hivyo huibana nchi anakotoka kiongozi aliyetoa maneno/matamko hayo. Kwa wafuatiliaji wa mambo, angalia kesi zilizoamuliwa na mahakama ya mbalimbali za kimataifa hasa ICJ. Kuna kesi tatu mhimu kwenye hili: Tamko la Ihleni (Ihlen Declaration), kesi ya Peninsula ya Bakassi na Matamshi ya mwakilishi wa Marekani katika WTO. Kesi mbili za mwanzo ziliamuliwa na mahakama ya kimataifa ya ICJ.
(Pakua na Soma zaidi....liliandikwa siku nyingi)
Canada- USA
Uruguay-Brazil
Uruguay-Argentina
Argentina-paraguay
Paraguay-Brazil
Bolivia-Peru
Estonia-urusi
Turkmenistan-Uzbekistani
Switzerland- Ufaransa
Iwapo wasipogawana maji hayo basi yanakuwa ni international waters kama ambavyo ilivyo Black sea. Mojawapo kati ya mifano michache ambapo maji yote karibua na mpaka huchukukiliwa na nchi yote ni pale maji hayo yanakuwa yamenzungwa na nchi hiyo kama ilivyo Ziwa Nicaragua mpakani mwa Nicaragua na Costa Rica, ziwa lote limezungukwa na Nicaragua ingawa liko mpakani.