Kwa ziwa malawi labda kweli ni lao lakini kwa ziwa nyasa linamilikiwa na sote Tz na Nyasaland
Hii mikataba ya kina sultan mangungo wa msovero na Karl Peters bado inatambulika ? haina tofauti na ule wa kutokutumia maji ya mto nile huyu bwana sijui lengo lake nini ?Kama umetumwa nenda kawaambie tunasema, wacha ziwa tu, tutaichukuwa Malawi yote iwe himaya ya Tanzania na kama mnabisha mwende mkawaulize Uganda.
Naona mnamjaribu homeboy, tutalihamisha ziwa lote tulipeleke Chatle.....acha wajipendekeze kwa homeboy. Tutawamiliki wao na ziwa Nyasa [HASHTAG]#BringbackZiwaNyasaFully[/HASHTAG]
Kua mtulivu basi, ndugu zenu tunao hapa kwa maelfu! Binafsi nawafahamu wengi tu! Sidhani kama ni busara sana kutumia lugha mnayotumia?? Halafu wale ndugu zetu mliowakamata muwaachie bila masharti yoyote!Kua munatembea kuna wa Bongo kibao Mozambique, Zambia,Malawi n.k atlarge ....respect freedom of expression archaic people nyie
Uingereza ni kisiwa tu, lakini alitawala dunia! Unajua kwanini?? Muingereza ndio baba na mama wa fitna dunia hii!
Mito yote inayoingia Ziwani inatoka Tanzania. Tuweza kuikausha kiana. Ni kuanzisha irrigation schemes za kufa mtu kutoa maji mto Songwe, Lufilyo na Mbaka.
Malawi waangalie upande wa pili
Hembu mnisaidie nasikia mlima ulikuwa wa jirani sasa enzi hizo sie tulikuwa na bahari kuanzia Tanga mpaka ile ya mombasa ilikuwa yetu ikabidi wakae wazee wakombozi wa hizi nchi mbili ikabidi wa kwetu ampe kipande cha bahari kinachoitwa mombasa kwa sasa na sie wakatupa mlima hii maneno iko na ukweli ndani yake ? Nauliza tu nipate kujua manake wengine vitukuu humuWaachie tu maana hata mlima ule mlefu unatushinda mpaka majirn nao wanaotangaza ulaya kuwa wao sasa mshikaa mawili moja humponyoka tukomae na tunachoweza
Hivi siku zote hizo mbona hiyo nyonyo ilikuwa haisumbui?Wamepatwa na nini?Hiyo nyonyo itabakia kama ilivyokuwa siku zote wasilete mchezo.[HASHTAG]#Hatupendagi[/HASHTAG] ujinga sisi#
Kama munauwezo wakuwadhibiti wapinzan kutumia maji washa, kuwasweka rumande bila sababu n.k siju mbinu zenu mutafanikiwa hata kuisubulu inchi nzima.Halafu ziwa likikauka tunachukua ardhi! Bahati mbaya pombe hajui international pilitics wal diplomacy. Tutapiga tu!
Mhh wataongea mengi ila bahari ni yetu na mlima ni wetu.Bye bye Kenya.Hembu mnisaidie nasikia mlima ulikuwa wa jirani sasa enzi hizo sie tulikuwa na bahari kuanzia Tanga mpaka ile ya mombasa ilikuwa yetu ikabidi wakae wazee wakombozi wa hizi nchi mbili ikabidi wa kwetu ampe kipande cha bahari kinachoitwa mombasa kwa sasa na sie wakatupa mlima hii maneno iko na ukweli ndani yake ? Nauliza tu nipate kujua manake wengine vitukuu humu
Kitangiri seriously [emoji23] ?Na vipi kuhusu haya maziwa
Rukwa
Natron
Manyara
Kitangiri
Wallah nimewahi kuona watu wanafiki lakini hawa watu weupe ni wanafiki mpaka shetani anawaogopa watakuchekea mpaka jino la mwisho huku wakiwasha moto kwa mlango wa nyuma pumzika kwa amani Gadafi, na Mungu akujaalie maisha marefu Rais Robert Mugabe Mungu mpe afya njema Rais wetu baki hapa hapa tusukume gurudumu la maendeleo mwenye shida aje tu hapa tuzungumze.Nimesikia kuna mafuta wa Waingereza ndiyo shinikizo usiniulize source.
Sote tunajua kuwa Malawi wamesema ziwa Nyasa, ambalo kwa Malawi linaitwa Ziwa Malawi, ni mali yao na Tanzania haina hata tone moja la maji. Mazungumzo yanayoratibiwa na Tanzania yameshindwa kubadili msimamo wa Malawi. Malawi imejiandaa kwenda mahakamani ya kimataifa, ICJ, kutafuta suluhu ya kile wakisemacho. Uwezekano wa kushinda kesi ni mkubwa, tena mkubwa sana.
Malawi ina ushahidi wa kutosha kuhusu wasemalo: mkataba wa Heligoland 1890 kati ya Mjerumani na Mwingireza uliipa Uingereza (Malawi kwa sasa) ziwa lote. Mjerumani (Tanganyika/Tanzania) iliachiwa Heligoland na makoloni mengine Afrika ya Magharibi.
Kuna ushahidi wa kutosha pia kuwa waziri mkuu wa Tanzania, kwa wakati huo, Kawawa, aliwahi kutoa matamko Bungeni, mara nyingi tu, kuwa Tanganyika/Tanzania haina hata tone moja la maji katika ziwa Nyasa/Malawi. Kwa maneno mengine ziwa Nyasa au Ziwa Malawi ni mali ya Malawi.
Ni mhimu kujua kuwa maneno/matamko yanayotolewa na viongozi wa serikali ya nchi husika, kwa sheria za kimataifa, yanahesabiwa kuwa ni sera ya nchi na hivyo huibana nchi anakotoka kiongozi aliyetoa maneno/matamko hayo. Kwa wafuatiliaji wa mambo, angalia kesi zilizoamuliwa na mahakama ya mbalimbali za kimataifa hasa ICJ. Kuna kesi tatu mhimu kwenye hili: Tamko la Ihleni (Ihlen Declaration), kesi ya Peninsula ya Bakassi na Matamshi ya mwakilishi wa Marekani katika WTO. Kesi mbili za mwanzo ziliamuliwa na mahakama ya kimataifa ya ICJ.
(Pakua na Soma zaidi....liliandikwa siku nyingi)