Ziwa Duluti, Arusha

Ziwa Duluti, Arusha

Like really?pale Lowasa alifanya mkutano wa kwanza baada ya kujiunga CHADEMA?
hahaha
inasemekana
kuna mzungu na farasi wake walizama pale tindigani kimandolu
siku mbili baadaye wakaja kuibukia yeye na farasi wake ziwa Duluti siku ...
 
Kwa mujibu wa taarifa za kusadikika, inamaanika neno "Duluti" ni jina la mwanamke aliyekuwa akiishi kule ukanda wa meru

Mwanamke huyu alipotea katika mazingira ya kutatanisha, watu walimtafuta kila mahali lakini hawakumpata

Miezi michache baada mwili wake ulionekana katika ziwa hili akiwa amekufa,

Kumbuka hakuna mto au mfereji unaomwaga maji yake kwenye ziwa hili, Maji yanaingia chini kwa chini na yanatokea chini kwa chini

Tukio hili liliwashangaza watu wengi na kubatiza jina la ziwa hili "Duluti"

....

Ziwa hili linapatikana nje kidogo ya mji wa Arusha, kabla ya kufika soko la tengeru ukielekea Moshi... Ni kilometa mbili adi tatu kutokea barabara kuu

Kiingilio kwa mtanzania ni shilingi Elfu mbili, malipo yanafanyika kwa mtandao

Pia kuna utalii wa kuvua samaki na utalii wa kupanda mabehewa (malipo yake ni tofauti na kiingilio)

Pia kwa wale wanaopenda ndege, kuna ndege wa aina nyingi zaidi ya species 200 (aquatic birds pia wapo)

Karibuni sanaView attachment 1162974View attachment 1162975View attachment 1162976
Asante sana though ilianza kama story tamu lakini ikaishia kuwa tangazo
 
Niliwahi enda hapa,tena Ilikuwa siku ya jmosi tulikuwa shopping sokoni.Nitafika tena siku za usoni
 
wanasema lina chunusi alizama siku nzima ikabidi walinzi wa hapo wawaondoe wenzetu kinguvu sababu waligoma kutoka mpaka wauone hata mwili ajabu alikuja ibuka kesho yake
Kumbe na wewe Madame S watokea Arachuga?
 
Leo huku Meru kuna baridi si ya kitoto.Hapa napiga mahesabu ya kuchomoka kwenye blanketi!
 
Sasa mimi nimezaliwa hapa na nimesoma hapa....,,,,nasema hakuna kituo kinachoitwa Duluti Bali ukitokea Moshi waweza shukia Tengeru pale stand ukachukua boda ukiwaambia unafika Duluti watakupeleka ni buku tu Pia ukitokea Arusha Mjini unaweza shukia Sang'si pale ulichukua boda unapelekwa pia kwa buku hiyo hiyo

Then kuhusu suala lakuogelea unaruhusiwa kabisa ila watu huogopa kuogelea kwasababu ya Historia ya Nyuma ila sisi ma Baharia hatuogopagi na kila jpili utatukuta pale hapa mwanzo (Forest) tunapiga mbizi na Wazungu mana weekend pale ni kama wote ase karibuni


Chonde chonde ukitaka kuogelea uwe na mwenyeji pia bot zipo full kuzungushwa ziwa zima ukitaka
Asante mkuu kwa marekebisho madogo
 
Back
Top Bottom