Zitto: Waliohusika Escrow wamepewa Bandari ya Tanga!

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
[h=3][/h]

KIONGOZI wa Chama cha (ACT) Wazalendo, Zitto Kabwe amesema ameibua hoja nzito na kushangazwa na hatua ya Serikali kuwapa kazi ya ujenzi wa Bandari ya Mwambani mkoani Tanga watu waliokuwa wakituhumiwa katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.

Aidha (ACT) Wazalendo, kimemtaka Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, afanye uchunguzi kuhusu mradi huo wa Mwambani na achukue hatua kwa kile alichodai kuwa utapeli wa watu wa Escrow.

Alisema pamoja na kupewa kazi hiyo kupitia mradi wa Mwambani Economic Corridor Project (MWAPORC), ambao utagharimu Sh trilioni 54 huku kukiwa hakuna taratibu za utangazaji zabuni zilizofutwa na Serikali.

Zitto alitoa kauli hiyo katika mikutano wa hadhara uliofanyika miji ya Mafinga na Iringa mjini katika Uwanja wa Mwetogwa mjini.

Kiongozi huyo wa (ACT) Wazalendo alisema hatua ya Serikali ya kuwapa kazi ya ujenzi Mwenyekiti wa Kampuni ya VIP Engineering and Management, James Rugemalira.

Mwambani Economic Corridor Project. Hapakuwa na zabuni yeyote iliyotangazwa na huu Mradi umekuwa ukiandaliwa na Serikali. Sheria ya Private Public Partnership ( PPP) imeweka utaratibu wa zabuni kwa miradi ya ubia na Serikali.

Taratibu hazijafuatwa, hakuna zabuni iliyotangazwa kuhusu Mwambani miradi mikubwa kama hii Serikali hutakiwa kutoa Guarantee kwa mikopo ambayo inachukuliwa. Hivyo kuhusika kwa Rugemalira wa Escrow na mwanasheria Cathbert Tenga wa Richmond kwenye mradi huu ni muendelezo wa miradi ya kitapeli, alisema Zitto.

Zitto, ambaye pia alikuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema uzito wa mradi huo wa bandari ambao unakwenda na reli ambayo itafika hadi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Waziri Sitta na atoe taarifa kwa umma kwa Taifa limechoka na miradi aliyodai ya kitapeli.

Mwigamba na umaskini

Naye Katibu Mkuu wa (ACT) Wazalendo, Samson Mwigamba, alisema kuwa hali ya umaskini nchini imezidi kuongezeka huku viongozi wakiendelea kuponda maisha.

Wakati Rais Jakaya Kikwete, anaingia madarakani mwaka 2005 hali ilikuwa mbaya lakini bado watu walikuwa na matumaini ya kurekebishiwa hali zao, leo anakaribia kumaliza kipindi cjake cha uongozi uchumi bado unamilikiwa na watu wachache.

"Tanzania ni nchi pekee inayochimba madini ya Tanzanite, mazao yao Mirerani ni madini lakini bado Serikali ilichukua ule mgodi na kuwapa makaburu kutoka Afrika Kusini huku Watanzania wakibaki wazamaji. Pia walikuwa wakichimba huku wakiweka maji yenye sumu huku Watanzania wakiendelea kufa kwa Ukimwi na njaa, alisema

Katibu Mkuu huyo wa (ACT) Wazalendo, alisema pamoja na madini hayo kuchimbwa nchini lakini nchi ya Afrika Kusini imekuwa ya kwanza katika soko la dunia kwa kuuza madini ya Tanzanite ikifuatiwa na Kenya huku Tanzania ikishika nafasi ya tisa.

Mwigamba aliongeza ujio wa chama kipya cha (ACT)Wazalendo ni ukombozi kwa Watanzania hivyo wanachotakiwa ni kukiunga mkono kwa kuhakikisha wanapigania misngi ya kizalendo iliayoanishwa katika azimio la Arusha ambalo liliweka miiko na maadili ya uongozi.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 
Zitto Ni kibaraka Wa CCM na haya kama anauchungu na taifa hili atutajia majinga ya walioficha matrilon huko uswiss
Zitto + Bakary Kikwete + usalama+chikawe=?
 
Hivi wamebadili sera yao namba moja ya kupambana na CDM?
 
Zitto Ni kibaraka Wa CCM na haya kama anauchungu na taifa hili atutajia majinga ya walioficha matrilon huko uswiss
Zitto + Bakary Kikwete + usalama+chikawe=?

Kama Mbowe na Dr Slaa sio vibaraka wa CCM kwanin wao basi wasiyataje hayo majina?
maana kama Zitto anaweza kuyajua hayo majina kwanin Mbowe na Slaa wasiyajue?

Kama hawayajui maana yake unamaanisha kuwa Zitto ana uwezo mkubwa wa kuona madudu ya serikali kuliko wao,sasa kwanin tupoteze muda kuwaitaja kuwa ni viongozi wakuu wa upinzani kama hawana uwezo wa kuona?kama Zitto anaweza kuona yaliyojificha kuliko wao?basi ni viongozi wakuu wa upinzani vipofu, dhaifu na wasio na sifa ya kuitwa hivyo.

Bila kujijua kauli yako hiyo inamaanisha kuwa Slaa na Mbowe hawana uwezo wa Zitto, maana viongozi wakuu wa upinzani ndio walipaswa wajue kuliko Zitto, sasa kumbe hawajui??hivyo bila Zitto ndio basi tena hatuwezi kujua, shame!

Tunahitaji viongozi wakuu wa upinzani wenye uwezo wa kuona, watchdogs, mabadiliko ni sasa!!
 
Kapwela Mkuu aliyesema ana majina ya walioficha mabilioni uswizi ni nani? mabilioni ilikuwa Zitto na sisi wananchi tunapenda kusikia nini kilijiri baada ya yeye kufuatilia
 
Last edited by a moderator:

Hapa kazi ipo. Kwani wewe unajua ni vigezo gani utumika kukiita chama kuwa ndio kiongozi wa upinzani? Kama huvijui hivyo vigezo, basi kwa bandiko lako ili umejiacha uchi.

Tiba
 
Aiseeee
 
Tiba mama, majitu mengine hapa ni mapoyoyo kichwani hakuna kitu. Yanaandika na kutoa mifano irrelevant ili mradi tu yanaharisha.

Lengo lao ni distractions na dawa yao ni kuyadharau.

Hapa kazi ipo. Kwani wewe unajua ni vigezo gani utumika kukiita chama kuwa ndio kiongozi wa upinzani? Kama huvijui hivyo vigezo, basi kwa bandiko lako ili umejiacha uchi.

Tiba
 
I used to like Zitto but not any more, jamaa ni mwongo na mnafiki na anayepoteza muda wa watu,hata hicho anachojifanya kukipigia kelele unadhani anakipigia makelele kutoka moyoni?hapo anaigiza tu ili mradi anatimiza wajibu,anajua mwenyewe anatimiza wajibu gani.Tangu atupige changa la macho kwenye ishu ya mabilioni ya Uswisi na ESCROW simwamini tena.Msanii sana huyu jamaa,yeye na mwenzie Mbowe wote lao moja.
 
Kwani Rugemarila anakosa gani kwenye escrow yeye anakosa gani zitto mjinga sana hana hoja msanii tu.
 
I used to like Zitto but not any more, jamaa ni mwongo na mnafiki na anayepoteza muda wa watu,hata hicho anachojifanya kukipigia kelele unadhani anakipigia makelele kutoka moyoni?hapo anaigiza tu ili mradi anatimiza wajibu,anajua mwenyewe anatimiza wajibu gani.Tangu atupige changa la macho kwenye ishu ya mabilioni ya Uswisi na ESCROW simwamini tena.Msanii sana huyu jamaa,yeye na mwenzie Mbowe wote lao moja.
Hawa jamaa wahuni sana hawana la maana hata moja,

siku zote wanaishi kijanja tu kikubwa ni kupotoshà watu.
 
Rugemalila hawezi akakagawa fedha kwa viongozi wa serekali na viongozi wa dini halafu zikaenda bure lazima zitalipwa na mlipaji ni mwananchi wa kawaida ambae hakufaidika na chochote kwenye mgao.
 
Tz bado tunakazi sana! yaan ccm na cdm wanaungana kutetea uovu na mikataba yenye harufu ya ufisadi! kisa tu aliyoyasema hayo ni ACT, sitashangaa kumbe kuona ccm na cdm wameungana kusimamisha mgombea mmja wa ubunge! swala kama hili inapaswa kuliangalia ukweli wake na si kuropoka tu kwakua amesema mtu flani!
 
Kapwela Mkuu aliyesema ana majina ya walioficha mabilioni uswizi ni nani? mabilioni ilikuwa Zitto na sisi wananchi tunapenda kusikia nini kilijiri baada ya yeye kufuatilia

Majina zito anatembea nayo kwenye pochi yake baada ya kupewa 10%.akapiga kimyaaaa
 
Last edited by a moderator:
Kama Mbowe na Dr Slaa sio vibaraka wa CCM kwanin wao basi wasiyataje hayo majina?
maana kama Zitto anaweza kuyajua hayo majina kwanin Mbowe na Slaa wasiyajue?

Kama hawayajui maana yake unamaanisha kuwa Zitto ana uwezo mkubwa wa kuona madudu ya serikali kuliko wao,sasa kwanin tupoteze muda kuwaitaja kuwa ni viongozi wakuu wa upinzani kama hawana uwezo wa kuona?kama Zitto anaweza kuona yaliyojificha kuliko wao?basi ni viongozi wakuu wa upinzani vipofu, dhaifu na wasio na sifa ya kuitwa hivyo.

Bila kujijua kauli yako hiyo inamaanisha kuwa Slaa na Mbowe hawana uwezo wa Zitto, maana viongozi wakuu wa upinzani ndio walipaswa wajue kuliko Zitto, sasa kumbe hawajui??hivyo bila Zitto ndio basi tena hatuwezi kujua, shame!

Tunahitaji viongozi wakuu wa upinzani wenye uwezo wa kuona, watchdogs, mabadiliko ni sasa!!

hivi ni nani anaweza kuona rangi ya chupi ya mtu aliyevaa bila yeye mwenyewe kumuambia? sanasana labda mumewe au mkewe
 
Back
Top Bottom