Zitto: Waliohusika Escrow wamepewa Bandari ya Tanga!

Zitto: Waliohusika Escrow wamepewa Bandari ya Tanga!

Zitto mtu wa ajabu huyu, frankly speaking.. Hebu niambieni kosa moja la rugemalira katika escrow, aliuza hisa zake, akalipwa chake, akalipa kodi. Sasa ni kitu gani amefanya rugemalira kibaya mpaka aitwe fisadi? Au zitto anaendelea na umbea wake kama ule alipeleka kwa Jk kuhusu mengi..
 
Sijapata kuona mwanasiasa mnafki kama Zitto Zuberi Kabwe.

Sasa ndiyo nagundua hawakufanya makosa kumtema CDM
 
Tz bado tunakazi sana! yaan ccm na cdm wanaungana kutetea uovu na mikataba yenye harufu ya ufisadi! kisa tu aliyoyasema hayo ni ACT, sitashangaa kumbe kuona ccm na cdm wameungana kusimamisha mgombea mmja wa ubunge! swala kama hili inapaswa kuliangalia ukweli wake na si kuropoka tu kwakua amesema mtu flani!

Cdm wametoa tamko lini mkuu kuunga kupingana na hii kauli ya Zitto?
 
Kama Mbowe na Dr Slaa sio vibaraka wa CCM kwanin wao basi wasiyataje hayo majina?
maana kama Zitto anaweza kuyajua hayo majina kwanin Mbowe na Slaa wasiyajue?

Kama hawayajui maana yake unamaanisha kuwa Zitto ana uwezo mkubwa wa kuona madudu ya serikali kuliko wao,sasa kwanin tupoteze muda kuwaitaja kuwa ni viongozi wakuu wa upinzani kama hawana uwezo wa kuona?kama Zitto anaweza kuona yaliyojificha kuliko wao?basi ni viongozi wakuu wa upinzani vipofu, dhaifu na wasio na sifa ya kuitwa hivyo.

Bila kujijua kauli yako hiyo inamaanisha kuwa Slaa na Mbowe hawana uwezo wa Zitto, maana viongozi wakuu wa upinzani ndio walipaswa wajue kuliko Zitto, sasa kumbe hawajui??hivyo bila Zitto ndio basi tena hatuwezi kujua, shame!

Tunahitaji viongozi wakuu wa upinzani wenye uwezo wa kuona, watchdogs, mabadiliko ni sasa!!

Mbowe na Dr Slaa hawafanyikazi Serikalini, huyo Kiongozi Mkuu -------- anashirikiana na TISS ndiyo maana details nyingi anazo! Sasa wewe unapowang'ang'ania tuelewej
 
ni kweli aliyosema zitto ila ameliongelea hilo swala juu juu kwani hapo ndio ytajua kwanini dr bukuku aliwekewa pesa benki kwani ndie anayehusika na hiyo miradi ya ppp nafikiri alitakiwa kumuumbua bukuku na kuwauliza takukuru kwanini mpaka sasa hawajamchukulia hatua hata hivyo hiyo taarifa ilishaandikwa na gazeti la citizen
 
Zitto Ni kibaraka Wa CCM na haya kama anauchungu na taifa hili atutajia majinga ya walioficha matrilon huko uswiss
Zitto + Bakary Kikwete + usalama+chikawe=?

Kapwela Mkuu aliyesema ana majina ya walioficha mabilioni uswizi ni nani? mabilioni ilikuwa Zitto na sisi wananchi tunapenda kusikia nini kilijiri baada ya yeye kufuatilia

Kwahiyo kumbe akina Mbowe na Dr Slaa hawajui?maana wangejua tusingemsubiri Zitto, wao ndio jukumu lao haswa kama viongozi wakuu wa upinzani, lakini labda uwezo wao wa kuona ni mdogo ndio maana masula makubwa, yenye akili ni mpaka tumsubiri ZItto ayaanzishe.

Hii ni ishara kuwa Zitto ana kitu ambacho hao hawana.

Kama Mbowe na Dr Slaa sio vibaraka wa CCM kwanin wao basi wasiyataje hayo majina?
maana kama Zitto anaweza kuyajua hayo majina kwanin Mbowe na Slaa wasiyajue?

Kama hawayajui maana yake unamaanisha kuwa Zitto ana uwezo mkubwa wa kuona madudu ya serikali kuliko wao,sasa kwanin tupoteze muda kuwaitaja kuwa ni viongozi wakuu wa upinzani kama hawana uwezo wa kuona?kama Zitto anaweza kuona yaliyojificha kuliko wao?basi ni viongozi wakuu wa upinzani vipofu, dhaifu na wasio na sifa ya kuitwa hivyo.

Bila kujijua kauli yako hiyo inamaanisha kuwa Slaa na Mbowe hawana uwezo wa Zitto, maana viongozi wakuu wa upinzani ndio walipaswa wajue kuliko Zitto, sasa kumbe hawajui??hivyo bila Zitto ndio basi tena hatuwezi kujua, shame!

Tunahitaji viongozi wakuu wa upinzani wenye uwezo wa kuona, watchdogs, mabadiliko ni sasa!!
 
Hapa kazi ipo. Kwani wewe unajua ni vigezo gani utumika kukiita chama kuwa ndio kiongozi wa upinzani? Kama huvijui hivyo vigezo, basi kwa bandiko lako ili umejiacha uchi.

Tiba

Haa ha ha, bila shaka hujui kwanin inaitwa kambi rasmi ya upinzani na kwanin tuna nafasi ya kiongozi mkuu wa upinzani na kwanini bajeti ya ofisi yake(upinzani bungeni) tunaigharamia kwa pesa zetu, wananchi wa Tanzania, lengo ni ili afanye kazi hii vizuri, aweze kuona pasipoonekana, kushauri, na kukosoa kwa maslahi yetu na kwa faida yetu, Kwa namna nyingine yeye ndiye mlinzi wetu mkuu juu ya yote yanayofanywa na serikali!tunamlipa kwa hilo, maana yake investment tunayoweka kwake(kifedha) ataturudishia na faida juu(kwa utumishi huo)

Sasa labda kama viongozi hao wakuu ni weupe, na ni vipofu wasio na macho ya kuona, labda ndio maana ya matokeo haya, badala ya kuwasubiri wao tunamtegemea huyu mtu mmoja, Zitto, sole player, anayejituma mwenyewe.Hii ni shara nyingine kuwa ana kitu ndani yake ambacho hawa wengine hawana.

Maneno haya yanapaswa kuwa wimbo kwetu sote.
..................................................................
Kutambua usichojua ni fungu la mwenye akili

kutambua uwezo wa watu wake ni wajibu wa jamii

kuwaweka watu kwenye nafasi wanazozimudu ni msingi wa maendeleo.
...................................................................................................

Kashfa hii inatukumbusha kuwa kama nchi hatuna udhaifu wa serikali tu bali pia udhaifu wa viongozi wakuu wa upinzani.Tunahitaji mabadiliko!

Zitto Ni kibaraka Wa CCM na haya kama anauchungu na taifa hili atutajia majinga ya walioficha matrilon huko uswiss
Zitto + Bakary Kikwete + usalama+chikawe=?

Kama Mbowe na Dr Slaa sio vibaraka wa CCM kwanin wao basi wasiyataje hayo majina?
maana kama Zitto anaweza kuyajua hayo majina kwanin Mbowe na Slaa wasiyajue?

Kama hawayajui maana yake unamaanisha kuwa Zitto ana uwezo mkubwa wa kuona madudu ya serikali kuliko wao,sasa kwanin tupoteze muda kuwaitaja kuwa ni viongozi wakuu wa upinzani kama hawana uwezo wa kuona?kama Zitto anaweza kuona yaliyojificha kuliko wao?basi ni viongozi wakuu wa upinzani vipofu, dhaifu na wasio na sifa ya kuitwa hivyo.

Bila kujijua kauli yako hiyo inamaanisha kuwa Slaa na Mbowe hawana uwezo wa Zitto, maana viongozi wakuu wa upinzani ndio walipaswa wajue kuliko Zitto, sasa kumbe hawajui??hivyo bila Zitto ndio basi tena hatuwezi kujua, shame!

Tunahitaji viongozi wakuu wa upinzani wenye uwezo wa kuona, watchdogs, mabadiliko ni sasa!!
 
Tiba mama, majitu mengine hapa ni mapoyoyo kichwani hakuna kitu. Yanaandika na kutoa mifano irrelevant ili mradi tu yanaharisha.

Lengo lao ni distractions na dawa yao ni kuyadharau.

Kama kitu hujui,ficha upumbavu wako!!hujui wajibu wa upinzani ni nini!!upinzani usio na macho ni upinzani dhaifu, haya yote yalipaswa wa kwanza kuyajua na kuyafichua awe Mbowe na Dr Slaa, lakini kwa kuwa hivi vitu vinahitaji uwezo binafsi pia ndio maana tunawasubiria akina Zitto.
 
Kwa wasiojua, Zitto ilikuwa aibue pia kashfa ya gesi lakini akaona kwa sababu Mbowe alitaka atoke nayo basi Zitto akaamua kuachana nayo.Matokeo yake mpaka bunge linaishia Mbowe hajafika popote, sio kila mtu anaweza haya mambo, yanahitaji uwezo binafsi, yanahitaji kusoma, yanahitaji kujifunza, na yanahitaji upeo!!

Hata kama hatutaki moyoni tunatambua kuwa tuna udhaifu sio kwa serikali tu bali mpaka kwa upinzani wenyewe.

Zitto akirudi bungeni itabidi atusaidie kukamilisha hili pia!!

Tujikumbushe.

Zitto: Nitamuunga mkono Mbowe

zitto.jpg

Mtwara. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe pale atakapowasilisha hoja yake bungeni kuhusu ufisadi wa zaidi ya Sh1 trilioni katika mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.

"Najua bado mnalia kuhusu bomba la kupeleka gesi Dar es Salaam, machozi yenu yatafutika kwani tayari habari za ufisadi mkubwa katika ujenzi wa bomba hili zimeanza kuchomoza.

"Kiongozi wa Upinzani Bungeni (Mbowe) ametamka mara kadhaa kuwa atatoa hoja kuhusu ufisadi katika ujenzi wa bomba la gesi. Pale atakapohitaji msaada wetu tutamsaidia, tunaamini gharama za mradi huu zimezidishwa mara mbili na inawezekana kabisa kuwa zaidi ya Dola ya Marekani 600 milioni (zaidi ya Sh1 trilioni) zimegawanywa kwa watu kama rushwa kuanzia China mpaka hapa Tanzania. Machozi yenu wana Mtwara yatafutwa kwa uwezo wa Mola," alisema Zitto.

Zitto: Nitamuunga mkono Mbowe - Kitaifa

Sasa labda aliona aibu kuomba msaada na matokeo yake ndio haya, hoja imepotea hewani!kuutambua uwezo wa mtu ni jambo muhimu sana.

Tz bado tunakazi sana! yaan ccm na cdm wanaungana kutetea uovu na mikataba yenye harufu ya ufisadi! kisa tu aliyoyasema hayo ni ACT! swala kama hili inapaswa kuliangalia ukweli wake na si kuropoka tu kwakua amesema mtu flani!

HII NI AKILI, hongera ndugu!!
 
Mbowe na Dr Slaa hawafanyikazi Serikalini, huyo Kiongozi Mkuu -------- anashirikiana na TISS ndiyo maana details nyingi anazo! Sasa wewe unapowang'ang'ania tuelewej

Duh kumbe unajua kuwa hawajui?sasa wapinzani gani wakuu wasio na macho ya kuona?wataisimamiaje,wataikosoaje serikali kama hawajui lolote?basi tuna upinzani wa dhaifu na wasio na faida, na pesa tunayowalipa kufanya kazi hiyo basi inapotea bure.

Hili ni miongoni mwa matatizo makubwa tuliyonayo kama taifa,mabadiliko ni sasa!!
 
Kama kitu hujui,ficha upumbavu wako!!hujui wajibu wa upinzani ni nini!!upinzani usio na macho ni upinzani dhaifu, haya yote yalipaswa wa kwanza kuyajua na kuyafichua awe Mbowe na Dr Slaa, lakini kwa kuwa hivi vitu vinahitaji uwezo binafsi pia ndio maana tunawasubiria akina Zitto.

Kwahiyo we ulitaka Dr. Slaa aende Uswisi akapekenyue huko?? Sasa yeye ataenda kama nani??
 
Kwahiyo we ulitaka Dr. Slaa aende Uswisi akapekenyue huko?? Sasa yeye ataenda kama nani??

Kwahiyo unamaanisha Dr Slaa uwezo huo hana?kwanin Zitto aweze yeye ashindwe?

Msingi wa kwanza ni kujenga mtandao wa kimataifa wa kupambana na fedha chafu, wameshindwa??sasa tutawahitaje kuwa ni viongozi wakuu??
 
Unazijua sheria za kibenki za Uswisi??
 
Unazijua sheria za kibenki za Uswisi??

Zipi hizo ndugu ambazo zitamzuia Mbowe na kumruhusu Zitto?masuala ni matatu tu
1.UWEZO 2. UPEO 3. USHAWISHI

Tujikumbushe!!

.................................................................................................................................................................
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alifanya mazungumzo na Serikali ya nchi hiyo ambayo imemweleza kuwa imebadili sheria zake ili kuwadhibiti wageni wanaoficha fedha nchini humo.

Zitto alisema amepata taarifa hizo juzi baada ya kukutana na Waziri wa Fedha wa nchi hiyo ambaye alimwandalia mazungumzo na watalaamu wake.

"Jana nilikutana na Waziri wa Fedha na akatuacha na mazungumzo na wataalamu wake. Wamesema hadi sasa, Tanzania haijasaini mkataba wa kubadilishana taarifa za kikodi (Multilateral convention on administrative assistance in tax matters)," alisema Zitto na kuongeza;

"Kwa kutosaini, Tanzania inajinyima haki ya kupata taarifa hizi na kutoza kodi kwa watu walioficha fedha huku (Uswisi), maana Sheria ya Kodi ya Tanzania inataka kila Mtanzania popote anapopata kipato halali lazima alipe kodi."

Zitto alieleza kuwa kitendo cha Serikali ya Uswisi kubadili sheria zake, kinaiwezesha nchi hiyo kutoa taarifa za benki za watu walioweka fedha nchini humo wakiwamo Watanzania, ambao sasa watatakiwa kuthibitisha kama fedha hizo ni safi au la.

"Kiufupi, Tanzania haijaomba taarifa yeyote kutoka Uswisi. Ila Uswisi wamebadili sheria yao na sasa mmiliki wa fedha ndiyo anapaswa kuthibitisha kwamba ni safi, na ikithibitika kuwa hazina mwenyewe wala maelezo, zitarudishwa nchi husika," alisema.

Zitto alisema mbali na kukutana na watendaji hao wa Serikali amezungumza na Umoja wa Mabenki wa nchi hiyo uliobainisha kuwa Uswisi ina Watanzania wachache wenye fedha.

"Wamesema Watanzania wengi wana fedha Uingereza, Jersey, Cayman Islands na Mauritius. Dubai pia imetajwa sana," alisema Zitto.

Zitto alielezea kuwa umoja huo wa benki za Uswisi umeanzisha mkakati wa kusafisha fedha uitwao ‘clean money strategy', na wamegundua watu wengi ambao ni wanasiasa, wamezuia akaunti zao na kupeleka majina kwenye Serikali zao.

"Tanzania haijafanya maombi rasmi hapa Uswisi na hivyo wao kama benki hawawezi tu kutoa taarifa bila kuombwa.

Sheria yao imerekebishwa ambapo sasa ni wajibu wa mwenye akaunti kusema kama fedha zake ni halali au hapana," alisema Zitto na kuongeza.
................................................................................................................................................................................
Kwa kifupi:

1. Alikutana na Waziri wa Fedha wa Uswiss

2. Alikuwa kiongozi wa uchunguzi juu ya masuala ya uwazi katika kodi wa shirika la kimataifa la mtandao wa ulaya wa madeni na maendeleo (Europena Network on Debt and Development)

3. Alikutana na maafisa wa mabenki na asasi zisizo za kiserikali zilizopo jijini Geneva.

4. Zitto alihudhuria mkutano wa Kamati ya Umoja wa Mataifa katika kampeni yake ya kuzuia unyonyaji wa nchi za Kiafrika unaofanywa na Makampuni makubwa ya Kimataifa.

5. Alitembelea Luxembourg na Brussels kabla ya kwenda Norway ambapo alikutana na Jopo la Wataalamu wa masuala ya kodi na Maendeleo kuandika taarifa maalumu yenye mapendekezo kuhusu kuzuia utoroshaji wa fedha kutoka Afrika.

6. Alikwenda jijini London kutoa mada kuhusu uwazi katika kodi kimataifa katika mkutano wa Uwazi (Open Government Partnership), na kuendelea kusisitiza juu ya uwazi wa sheria za fedha kimataifa.

7. Kaandika barua kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Cameroon juu ya kusaidia kubana serikali juu ya haya

8.Kakutana na Wabunge wa Uingereza, chini ya mwenyekiti wao, Bi Margaret Eve Hodge, Lady Hodge MBE, PC, MP kuhusu kuendeleza wito wake kwa makampuni ya kimataifa kulipa kodi zao barani Afrika na kuacha tabia ya kutumia ‘Tax Havens' kukwepa kodi na kufukarisha nchi za Kiafrika.
.............................................................................................................................................................................
Wao wamefanya nin?SIFULI!!Unadhani data zinapatikana kwenye magazeti ya Shigongo?lazima uwe na uwezo wa kujenga mtandao wa kimataifa.

TUKUBALI TU, TOFAUTI YAO NA YEYE SIO SHERIA BALI NI UWEZO, UPEO NA USHAWISHI!

Tukubali tu kuwa kuna vitu Zitto anaweza ambavyo hawa wengine hawawezi, ata lile la gesi itabidi Zitto akirudi bungeni alimalizie mwenyewe maana Mbowe ni wazi kuwa limemzidi kimo.
 
Back
Top Bottom