Zitto vs Waziri wa ulinzi bungeni leo

aliye mjibu hivyo ni mtu asiyefikiria na hapendi kufikiria...maana hayo ni majibu ya kwenye siasa za maji taka na siyo majibu ya mwenye kutumia ubongo au ni wassira nini? au nchimbi kama ni kiongozi bac kipimo cha IQ kinatakiwa vinginevyo nchi itakuwa masikini kwa miaka yote mpaka watu kama hao wasipate fursa ya kushiriki katika panel ya washauri wa mstakabali wa maendeleo ya nchi

Hivi watu wanafikiri Emmanuel Nchimbi,Dr.Fake ni mtu makini??? Basi kwa taarifa tu Emmanuel Nchimbi ni mmoja wa Mawaziri walio DHAIFU sana kwenye Baraza la Kiwete. Huyu anabebwabebwa tu kwa vile tangu zamani alikuwa kada wa UVCCM na hatimaye kaibukia kwenye Uwaziri. Wewe msikilize tu hata anapoongea utajua ni mtu mbambaishaji asiye mbele wala nyuma.

Zitto was very right kuhoji hilo swali kwa vile tunajua kuwa katika mambo ya MUUNGANO TUNAYOSHIRIKIANA YAMO LA ULINZI NA FEDHA. Kwa hiyo Mhe Zitto alitaka kujua kwanini kama tunashirikiana KIULINZI kwanini hata mara moja Mkuu wa Majeshi akatoka Zenji? Kuna kosa gani hapo.

Kwa akili finyu za Nchimbi badala ya KUJIBU SWALI AKAANZA KAMPENI ZA KIJINGA ZA WANA MAGAMBA! Hivi spika leo alikuwa nani kumruhusu mpuuzi huyu kuanza kampeni za ukanda??? Kwanini wabunge wa kambi ya upinzani hawakuomba mwongozo wa spika kuhusu majibu rejareja na Waziri kihiyo kama Nchimbi???

...Nakubaliana 100% na Waziri, hilo lilikuwa swali lilihitaji jibu lililolingana na level ya upuuzi wa swali lenyewe...

...Kwa mtu asiyewafahamu na akasikiliza Bunge angepata picha kuwa Waziri ni mtu makini sana,mwenye ufahamu mkubwa sana, sasa kwa kuwa ameulizwa swali la kitoto kabisa na Mbunge mmoja mdogomdogo hivi ambaye bila shaka ana ufahamu mdogo sana wa mambo, ikapelekea Waziri aamue kutumia lugha ambayo yule muuliza swali angeweza kumuelewa....

...Zitto next time usiulize swali la kipuuzi kama hilo,haliendani na uwezo wako wa ubongo...
 
Mh. waziri yupo sahihi; Z'bar ni mkoa sawa tu na Kigoma (muulize Pinda)
Hivyo Zito alitakiwa kujua viongozi hawachaguliwi kutokana na mikoa wanayotoka but uwezo wao
 
Hivi watu wanafikiri Emmanuel Nchimbi,Dr.Fake ni mtu makini??? Basi kwa taarifa tu Emmanuel Nchimbi ni mmoja wa Mawaziri walio DHAIFU sana kwenye Baraza la Kiwete. Huyu anabebwabebwa tu kwa vile tangu zamani alikuwa kada wa UVCCM na hatimaye kaibukia kwenye Uwaziri. Wewe msikilize tu hata anapoongea utajua ni mtu mbambaishaji asiye mbele wala nyuma.

Zitto was very right kuhoji hilo swali kwa vile tunajua kuwa katika mambo ya MUUNGANO TUNAYOSHIRIKIANA YAMO LA ULINZI NA FEDHA. Kwa hiyo Mhe Zitto alitaka kujua kwanini kama tunashirikiana KIULINZI kwanini hata mara moja Mkuu wa Majeshi akatoka Zenji? Kuna kosa gani hapo.

Kwa akili finyu za Nchimbi badala ya KUJIBU SWALI AKAANZA KAMPENI ZA KIJINGA ZA WANA MAGAMBA! Hivi spika leo alikuwa nani kumruhusu mpuuzi huyu kuanza kampeni za ukanda??? Kwanini wabunge wa kambi ya upinzani hawakuomba mwongozo wa spika kuhusu majibu rejareja na Waziri kihiyo kama Nchimbi???

...Kama Swali la Mkuu wa Majeshi kwa akili zako unaliona ni sahihi basi kwa level hiyohiyo ya fikra ulipaswa utambue pia kuwa Mwenyekiti wa Chadema anaweza akatokea mkoa wowote wa Tanzania, Kigoma ikiwemo...

...Sasa je tuwe tunateua viongozi hawa kwa kubadilishana kuzingatia eneo analotoka kiongozi huyo??jibu ni hapana,sasa kwa kuwa Zitto anaifahamu vizuri Chadema,akaamua kutumia mfano ambao ataweza kuuelewa, kuwa japo Mwenyekiti wa Kwanza wa Chadema alitokea Kilimanjaro lakini bado Mbowe wa Kilimanjaro alichaguliwa tena kuwa Mwenyekiti na Zitto wa Kigoma ambayo haijawahi kutoa Mwenyekiti lakini pamoja na hilo bado alilazimika kujitoa, kwa sababu nafasi hizo hazitolewi kwa mzunguko wa maeneo bali kwa "Uwezo" unaofuatiwa na "Uamuzi wa Mteuzi/Wateuzi", hii ndiyo hekima iliyopo kwenye jibu la Waziri.

...Sijui mnafikiria nini, hivi ulitaka Waziri aseme Mkuu wa Majeshi anateuliwa kulingana na sifa zake,bila kujali anatoka upande gani wa Muungano, na kuwa katika kipindi chote cha Muungano, hatukumpata Mzanzibar mwenye sifa stahiki kuweza kuteuliwa kushika nafasi hiyo??ulitaka kweli Waziri ajibu hivyo?ni mpumbavu pekee anayeweza kupeleka mweleko wa mjadala huko...
 
aliye mjibu hivyo ni mtu asiyefikiria na hapendi kufikiria...maana hayo ni majibu ya kwenye siasa za maji taka na siyo majibu ya mwenye kutumia ubongo au ni wassira nini? au nchimbi kama ni kiongozi bac kipimo cha IQ kinatakiwa vinginevyo nchi itakuwa masikini kwa miaka yote mpaka watu kama hao wasipate fursa ya kushiriki katika panel ya washauri wa mstakabali wa maendeleo ya nchi
Nafikiri wewe ndiye usiyependa kufikiria na unatakiwa kufanyiwa kipimo cha IQ kwa sababu umeshindwa kuona ukweli uliyo wazi katika swali na jibu lililotolewa.

Hivi kuna sababu kwa mtu kama Zitto tunayemwamini kuuliza swali kama hili? Kwa faida ya nani? angechaguliwa Mzanzibar angekuongezea nini katika maisha yako? Watu tuna mambo magumu katika maisha wewe unamshabikia mtu anayekaa mjengoni analipwa fedha kibao halafu anapoteza muda wa bunge kuuliza vitu visivyo na kichwa wala miguu. Kujipendekeza kwa Wazanzibari ili wamsaidie nini? Au asifiwe kwamba aliibua hoja iliyoleta mgogoro? Hivi ulishawahi kujiuliza kwa nini tuna mawaziri kwenye Serikali ya mwungano lakini hakuna watu wa bara ambao wanaweza kupata uwaziri Zanzibar!!!!!!!! Utasema hii ni serikali ya muungano na ile ni ya Zanziba, kama ni hivyo basi, kwa nini tuwe na serikali ambayo ina double standard? Sisi wawe na nafasi ya kutuongoza na kujua siri zetu lakini sisi hatuna nafasi ya kuongoza na kujua siri zao. Inakuingia akilini? Tuache kushabikia mambo kabla ya kufikiri vema. Mind you, you are a great thinker and not a hooligan. Sitaki kusema kila kitu hapa lakini jaribu kuchunguza kama kuna mantiki ya swali hilo katika mazingira tuliyo nayo.
 
Hivi watu wanafikiri Emmanuel Nchimbi,Dr.Fake ni mtu makini??? Basi kwa taarifa tu Emmanuel Nchimbi ni mmoja wa Mawaziri walio DHAIFU sana kwenye Baraza la Kiwete. Huyu anabebwabebwa tu kwa vile tangu zamani alikuwa kada wa UVCCM na hatimaye kaibukia kwenye Uwaziri. Wewe msikilize tu hata anapoongea utajua ni mtu mbambaishaji asiye mbele wala nyuma.

Zitto was very right kuhoji hilo swali kwa vile tunajua kuwa katika mambo ya MUUNGANO TUNAYOSHIRIKIANA YAMO LA ULINZI NA FEDHA. Kwa hiyo Mhe Zitto alitaka kujua kwanini kama tunashirikiana KIULINZI kwanini hata mara moja Mkuu wa Majeshi akatoka Zenji? Kuna kosa gani hapo.

Kwa akili finyu za Nchimbi badala ya KUJIBU SWALI AKAANZA KAMPENI ZA KIJINGA ZA WANA MAGAMBA! Hivi spika leo alikuwa nani kumruhusu mpuuzi huyu kuanza kampeni za ukanda??? Kwanini wabunge wa kambi ya upinzani hawakuomba mwongozo wa spika kuhusu majibu rejareja na Waziri kihiyo kama Nchimbi???

Hivi wewe umelogwaaaaaaa??????????? Akitoka Zanzibar ndio bei ya unga inapungua? au bei ya mchele, maharage, mafuta, nauli za daladala zinapungua???????? Mbona mnakuwa hivi ninyi!!!!!!!!!! Watu wanakula tena kwa taabu mara moja kwa siku wewe unashabikia mswali yasiyo na tija kwa mtanzania!!!!!!!!! Au mwenzetu ni kati ya................ Sisi tunataka kusikia habari za ahueni ya maisha yetu sio mkuu wa majeshi atoke bara au Zanzibar. Mbona huuluzi mwenyekiti au katibu wa cdm hajawahi kutoka Zanzibar????????? Au mwenyekiti wa ccm au katibu kutoka Zanzibar???????? Hebu tuachane na hizo habari leteni story nyingine.
 
Zitto is immatured super politician. Nahodha is a useful Z'barian.

Mimi Ron nakifahamu sana CCM, toka enzi TANU mpaka sasa, sijawahi kuona mwenyekiti akitoka kaskazini! Why? Hata katibu wake mkuu sijawahi sikia akitokea kaskazini satirically uchaggani, why?

Nilitaka muone wanabodi jinsi hoja za udini, ukabila na ukanda zilivyo dhaifu na shenzi
 
Kweli tunakoelekea siyo, kingozi anapo acha kujibu hoja za maana anaanza mambo ya chadema ya ukanda,Zito kauliza katika muungano wa Zanziba na TZ sijawahi kusikia mkuu wa majeshi ametoka Zanzibar,kambiwa tunajiandaa lakini hata mimi sijawahi kusikia Mwenyekiti wa Chadema ametokea Kigoma.CDM kazi mnayo.

It was so sad to hear such useless utterance from Nahodha. A person, one could have thought is very innocent or not associated with cheap politics championed by his party, CCM. Loh! Kumbe gamba ni gamba tu, mpaka livuliwe na kuvalishwa gwanda ndo linakoma kuwa gamba.

Mkuu Kitero

Si bora angesema Mkoa wa Kigoma. Hakusema hivyo. Alisema "(u) Kanda ya Kigoma". Kudhihirisha imani ya ukanda, sasa ni sera iliyoko ndani ya vichwa na akili za wana CCM wengi kuliko watu wanavyofikiri. Hawa jamaa ni hatari. Kama alivyosema Mwenyekiti Mbowe jana. Wataliangamiza taifa kwa propaganda zao za udini, ukabila na ukanda. Huwezi kuamini kuwa mtu kama Nahodha naye muda wote anafikiri kikanda kanda tu kama wana CCM wengine limbukeni. Mnawajua vyema.

Hii CHADEMA-phobia itawaathiri wengi aisee. Poleni Magamba. Hatutawaruhusu nchi hii muifikishe huko. Akili kama za yule mbunge wa Lindi, badala ya kuona namna ambavyo serikali yake ya CCM inalea mtandao wa ufisadi ambao CHADEMA ilishausema siku nyingi na imeendelea kuupigia kelele, kila uchao, yeye akawaona na kuwatazama wezi hao kwa dirisha la kabila, aisee. What a myopic mind! If not stereotype or narrow mindend.
 
Hayo mambo ya majeshi bora wayashike wenyewe wabara, nani anapenda suluba?
 
...Nakubaliana 100% na Waziri, hilo lilikuwa swali lilihitaji jibu lililolingana na level ya upuuzi wa swali lenyewe...

...Kwa mtu asiyewafahamu na akasikiliza Bunge angepata picha kuwa Waziri ni mtu makini sana,mwenye ufahamu mkubwa sana, sasa kwa kuwa ameulizwa swali la kitoto kabisa na Mbunge mmoja mdogomdogo hivi ambaye bila shaka ana ufahamu mdogo sana wa mambo, ikapelekea Waziri aamue kutumia lugha ambayo yule muuliza swali angeweza kumuelewa....

...Zitto next time usiulize swali la kipuuzi kama hilo,haliendani na uwezo wako wa ubongo...

wewe na waziri wako wote ni walewale, mpo kwa maslahi yenu binafsi na chama lenu
 
Swali la Mh Zito la leo la kuhusu mkuu wa majeshi kutowahi kutoka Zanzibar, limeigharimu CDM, baada ya Mh Nahoza kulijibu kisiasa kuwa hata Mwenyekiti wa CDM hajawahi kutoka Kigoma. Swali hilo kiukweli halikuwa na mantiki yoyote zaidi ya Mh Zito kutaka kutafuta umaarufu binafsi au kukubalika zaidi Zanzibar.
 
nahodha ndiye aliyekurupuka .. si haki kufananisha znz na kigoma.. znz ni nchi...!
 
hata mimi kwa upande wangu naona Zito ameanza kupoteza zile siasa za utaifa badala yake anaegemea kwenye ujiko zaidi..eg suala la mkuu wa majeshi kutokea au kutotokea Znz halina dili kwenye maendeleo ya pande zote..kwa kweli hapa amechangia pumba
 
Hili swali la Zito halina maana..inamaana anataka mtu ateuliwe tu kwa kuwa ametokea sehemu fulani. Haya ni mawazo angamizi na ubaguzi..Zito sijui alikuwa anawaza nini mpaka kuuliza ujinga kama huu. Yaani bado mnawazia kumchagua mtu kwa kuwa ni Mzn au Tang,,,shameful Zito...
 
Back
Top Bottom