Nia na lengo la swali nadhani ilikuwa ni kupima IQ ya waziri. lakini pia nadhani swali lililenga kumjua kama atakuwa na mawazo sawa na wazanzibari wengine wanaodai kwamba wanaonewa na serikali ya muungano kwa kutoa fursa nono ikiwemo vyeo kwa wabara alhali wazenj hawapewi kipaumbele katika fursa hizo nyeti. Kimsingi waziri alikuwa ameanza vizuri ktk kujenga hoja na kujibu swali ila kuunganisha hoja ya swali lake kwa kusema mbona M/kiti CHADEMA hajawahi kutoka kigoma ni Silly thinking. Alipaswa ajibu kwa mujibu wa utamaduni wa kijeshi,maadili ya kijeshi,taaluma ya kijeshi n.k ukizingatia kwamba jeshi huwa halisajili /haliajiri kwa misingi ya kikabila, ukanda,udini wala kwa nguvu ya kulazimisha watu wajiunge(unless kuwe na sababu ya msingi hususani ya kuwalazimisha watu). Kwa hiyo swali la zitto halikuwa baya kwani ilikuwa ni aptitude test ndani ya bunge. na waziri angejikoroga tu akasema ``kama waziri najaribu kulishughulikia ili kuleta uwiano ................."kama walivyozoea kukurupuka na kujibu nagekuwa amejipalia mwenyewe mkaa ndani ya bunge,jeshini na umma kwa ujumla. Awe makini na baadhi ya maswali kwani yanaweza kumporomosha au kumpandisha.zitto *****! Afu utamsikia anabana pua "nina masters"