Zitto Vs Spika

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Zitto awasha moto
Halima Mlacha
HabariLeo; Tuesday,December 25, 2007 @00:01

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameliomba Bunge kuipitia upya adhabu ya kumsimamisha, akidai kwamba imesababisha adhalilike na kushushiwa hadhi ndani na nje ya nchi. Zitto pia anataka Spika na mawaziri wengine kadhaa wachukuliwe hatua, kwa madai kwamba walinukuliwa na vyombo vya habari wakisema yeye ni mwongo bila madai hayo kuthibitishwa.

Kwa mujibu wa barua aliyomwandikia Spika wa Bunge jana (nakala yake gazeti hili inayo), mbunge huyo ametoa ombi hilo kwa kuwa anaamini adhabu hiyo haikuwa halali kwake kutokana na kutofuata kanuni za Bunge na pia kutopewa nafasi ya kujitetea. Mbunge huyo alisimamishwa kazi za Bunge kwa mikutano miwili Agosti 14, mwaka huu, kwa madai ya kusema uwongo dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kuhusiana na mkataba wa madini uliosainiwa nje ya nchi.

Adhabu hiyo imekwisha na anatarajiwa kuanza kuhudhuria vikao vya Bunge baadaye mwezi ujao. Zitto alifika katika ofisi ndogo za Bunge binafsi jana majira ya mchana kuwasilisha barua hiyo kwa Spika ambaye yuko safarini. “Adhabu niliyopewa iliniweka katika wakati mgumu sana na hata kunishushia heshima si tu katika jamii ya Tanzania, bali katika jamii ya kimataifa. Nimekuwa nikionekana ni Mbunge mwongo…

“Mheshimiwa Spika licha ya kwamba nina nafasi na haki ya kuomba chombo kingine cha dola kama Mahakama kupitia adhabu hii, nimesita kufanya hivyo ili kulipa Bunge nafasi ya kujikosoa,” ilisema sehemu ya barua hiyo ya Zitto. Katika barua hiyo, ambayo Zitto alikiri kuiandika, pia aliomba Bunge hilo kupitia vifungu vyote vya Kanuni za Bunge, ikiwamo kumsikiliza katika kikao cha kamati, kauli za viongozi wa Bunge na wa Tawi la Utendaji kuhusu adhabu aliyopewa ili kuona kama kanuni za Bunge na Sheria namba 3 ya mwaka 1988 hazikuvunjwa.

Alisema kama chombo hicho kikiridhika kuwa viongozi waliotajwa pamoja na hatua ya mbunge huyo kupewa adhabu ilikuwa ni kinyume na kanuni na sheria zilizopo za Bunge basi, chombo hicho kiombe radhi. Alisema Bunge lina taratibu za kuleta hoja bungeni ambazo zimeshafafanuliwa katika kanuni za chombo hicho na kuainishwa wazi kwamba hoja haiwezi kutolewa juu ya hoja nyingine.

“Kanuni zetu zimesema wazi kabisa katika kifungu cha 59-3 kuwa iwapo mbunge anashutumiwa uongo bungeni au kutoa lugha ya kuudhi, atapewa muda ili kuthibitisha analoshutumiwa mheshimiwa Spika….sijawahi kupewa muda wa kuthibitisha chochote,” alisema Zitto katika barua hiyo.

Alisema muda wa kuwasilisha hoja yake, viongozi wa Bunge waliueleza kama ndio muda aliopewa kuthibitisha maneno yake, muda ambao aliouomba kikanuni kuleta hoja yake binafsi na haukuwa wa kuthibitisha jambo lolote.

Alisema maamuzi ya kumsimamisha kwa kusema uongo bungeni yalimdhalilisha binafsi na mbele ya jamii na kudunisha utu wake. “Adhabu niliyopewa iliniweka katika wakati mgumu sana na hata kunishushia heshima si tu katika jamii ya Tanzania hata kimataifa.”

Copyright @TSN 2006 All Rights Reserved
 
Quotes:-

""Kanuni zetu zimesema wazi kabisa katika kifungu cha 59-3 kuwa iwapo mbunge anashutumiwa uongo bungeni au kutoa lugha ya kuudhi, atapewa muda ili kuthibitisha analoshutumiwa mheshimiwa Spika….sijawahi kupewa muda wa kuthibitisha chochote," alisema Zitto katika barua hiyo."

Hii ni Fact, ahsante mkuu Zitto, barua nzima maneno yako hapa tu kwenye hii qoute, sasa Spika ni kunyoa au kusuka! Sasa ngoja tuwasikie viongozi vinyonga mabao majuzi walikuwa wakukuunga mkono waseme public kukuuunga mkono sasa tuone!
 
Quotes:-

""Kanuni zetu zimesema wazi kabisa katika kifungu cha 59-3 kuwa iwapo mbunge anashutumiwa uongo bungeni au kutoa lugha ya kuudhi, atapewa muda ili kuthibitisha analoshutumiwa mheshimiwa Spika….sijawahi kupewa muda wa kuthibitisha chochote," alisema Zitto katika barua hiyo."

Hii ni Fact, ahsante mkuu Zitto, barua nzima maneno yako hapa tu kwenye hii qoute, sasa Spika ni kunyoa au kusuka! Sasa ngoja tuwasikie viongozi vinyonga mabao majuzi walikuwa wakukuunga mkono waseme public kukuuunga mkono sasa tuone!

Viongozi wa CCM ni wagumu sana kutamka neno samahani. Hili linasababishwa na wao kujiona wanayoyatamka au kuyafanya hayana kasoro zozote kwa sababu wao ni Miungu watu. Binadamu hatuko perfect tunafanya makosa kila kukicha na unaonyesha ubinadamu wako pale ambapo utakuwa tayari kusema samahani pindi utakapobaini kwamba ulikosea. Hata wanasiasa wamarekani wamegundua jinsi wamarekani wanavyoappreciate pale wanavyotamka "I am sorry, I was wrong."

Zitto katika barua yake kaonyesha kwamba akiombwa samahani basi sakata hili litakuwa limekwisha, lakini CCM watataka kupindua pindua maneno ili waonekane hawakukosea chochote. Tusubiri tuone CCM ( Sitta and company) wataifanyia kazi vipi barua hii toka kwa Zitto.
 
Tusubiri tuone,
Wanatakiwa wawe makini na kile watakachokisema au kukipindisha. Wananchi wengi wanamuunga mkono zitto na ukizingatia mkataba wa Buzwagi ulipatikana na ukathibitisha nani alikuwa muongo.

Faulu watakayochezwa na bunge itasaidia kuzia safari ya kuelekea mabadiliko 2010.
 
Kwanza Hongera Zitto kwa kufanya mambo kwa utulivu . Mimi nilikuwa nasema na mnene mmoja yuko karibu sana Chief Whip wa Bunge akasema wanadai unakurupuka na kutaka umaarufu na wao wanakuzima kwamba huna hoja . Mimi nika tofautiana naye sana .Tena juzi tu hapa Mwigobero .Nikawahakikishia kwamba kijana yule ni simati sana .

Leo umeibua mgogoro mzito .Lakini hapa kuna watu walipigia misumari sana akiwemo Mzee Dr.Malecela .Hawa ndiyo tunawategemea wasimamia ukweli sina hakika kama wataamua kuwa wakweli na wa wazi maaana Nchi hii ni yetu sote . Hongera kwa hili na nategemea kwamba hawatakaa kimya kama kawaida yao .
 
Quotes:-

"“Kanuni zetu zimesema wazi kabisa katika kifungu cha 59-3 kuwa iwapo mbunge anashutumiwa uongo bungeni au kutoa lugha ya kuudhi, atapewa muda ili kuthibitisha analoshutumiwa mheshimiwa Spika….sijawahi kupewa muda wa kuthibitisha chochote,” alisema Zitto katika barua hiyo."

Hapa patamu kabisa,
Washa moto Kijana Zitto, Mheshimiwa Mudhihili upo??

Mzee SAM mwiba huo unaona sasa?? jiandae tende linanyemelea

Mheshimiwa six busara zako?

Naam, ''Damu mpya kilele cha mawazo mgando''
 
Huyu anahitaji ushauri nasaha tu... iweje kesi ya Nyani aipeleke kwa Ngegedere?
 
Hongera sana ZITTO.

Hii ndio dawa yao tutaona kama je walikuwa wanaangalia suala la maslahi ya taifa ua itikadi za chama hapo ndio wenyewe watagawanyika wenyewe na ninafikiria sana ulishikilia bango hadi mwisho watakubali walifanya makosa.

Keep it up....
 
This is a game of cat and mouse, who will blink first?

Go on Zitto, so far so good, you are playing your cards very well.
 
Hongera sana zitto.

Kwa hili sasa ngoja tusubiri upande wa mweshimiwa SPIKA, kama kweli ataruka kihunzi hiki.

Sijui atakuja tena naibu wake?

Huu ni Mzigo mzito sana kwa Spika kumurudisha alipokukuwa akiomba asirudishwe.

Pia ubuzwagi-buzwagi unaweza kurudia tena hapa. Maana kila kitu adharani.
 
Kwa akili yako Masatu wewe ulitaka bwana Zitto amwandikie nani ambaye anaweza kutoa maamuzi ya busara? Nadhani kitu alicho kifanya ni sahihi kabisa kwamba huwa wanaamua kwa jazba na sasa watafanya reflection na Watanzania watajua ukweli ni upi hasa kulingana na lile saga . Zitto ni Mtanzania na Mbunge wa Tanzania hawezi kwenda kupeleka malalamiko yake US kama vile Mkulu afanyavyo kuongelea maswali ya Nchi yake akiwa US
 
Heri ya Noeli,

Nimeona ni bora niwawekee barua hapa ili muione yote badala ya habari za magazeti tu.

Lengo langu ni kutaka kuweka rekodi sawa. Ninajua walionihukumu ndio hao hao ninawapelekea kesi tena. Hapo ndio tutaona uungwana wa viongozi wetu. Nadhani hii ni hatua muhimu sana kwangu kisiasa. Nimefikiria hatua hii kwa muda mrefu sana. Nikatumikia adhabu mpaka imeisha. Ninakutana na wabunge wenzangu tunaingea na wanaona kilichotokea ni suala la kawaida tu. Eti ni siasa tu. Kwa kweli nikasema ngoja tuone kama asasi zaweja kujikosoa. Tusubiri Januari maana kanuni inasema, kamati ya kanuni itakutana mara moja kujadili shauri kama hili. Hoja ipo katika public, lazima ijadiliwe!

Nawatakia kila la kheri.
 
Dar es Salaam.
24/12/2007



Spika wa Bunge,
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dar es Salaam.



BUNGE KUPITIA UPYA ADHABU DHIDI YANGU

Tarehe 14/8/2007 Bunge lilipitisha azimio la kunisimamisha kazi za Bunge kwa jumla ya mikutano miwili.

Kwa mujibu ya kanuni za Bunge, wewe mheshimiwa Spika ndio unapaswa kuhakikisha kuwa utaratibu Bora unafuatwa Bungeni.

Kanuni ya 58(1) ya kanuni za Bunge, Toleo la mwaka 2004 (ambazo ndizo zinafanya kazi mpaka ninapoandika barua hii) inasema ifuatavyo:

Bila kuathiri masharti ya kanuni ya 4(2), Spika, atawajibika kuhakikisha kuwa utaratibu bora unafuatwa Bungeni, na uamuzi wake kuhusu jambo lolote la utaratibu utakuwa ni wa mwisho.

Msingi wa kanuni hii ni Kanuni ya 4(2) na 4(3) ambayo inasema

Kanuni ya 4

4(2) Spika ataongoza kila kikao cha Bunge na ndiye mwenye mamlaka ya kuamua mambo yanayoweza kuzungumzwa Bungeni.

4(3) Spika atawajibika kutilia nguvu Kanuni zote za Bunge, na endapo Mbunge yeyote hataridhika na uamuzi wa Spika anaweza kuwasilisha sababu za kutoridhika kwake kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni za Bunge ambayo itatakiwa ikutane mara moja kufikiria na kutoa uamuzi wake kwa Spika juu ya jambo hilo, na Spika atalijulisha Bunge uamuzi uliotolewa……….

Mheshimiwa Spika, kwa misingi ya kanuni zetu nilizozinukuu hapo juu ninaleta kwako maombi ili Kamati ya Kanuni za Bunge ipitie upya adhabu niliyopewa na Bunge ambayo mimi ninaamini haikuwa halali, haikufuata kanuni za Bunge, haikuzingatia tamaduni za Bunge (maamuzi ya Bunge yaliyopita) na kubwa zaidi haikunipa nafasi ya kujitetea.

Mheshimiwa Spika, mimi kama Mbunge katika Bunge lako ninaamini ya kwamba adhabu niliyopewa ilifikiwa kwa shinikizo la kiitikadi na hata kufikia kundi moja la wabunge kutumia vibaya wingi wao Bungeni (abuse of majority) na kuniadhibu bila kufuata kanuni za Bunge.

Nimeona, kwa kuwa demokrasia inakua nchini kwetu, ni vema niliombe Bunge kupitia upya adhabu ile na kama Bunge kupitia kamati ya Kanuni za Bunge likiona Kanuni za Bunge zilifuatwa nitaridhika na adhabu ile. Vile vile kama Bunge likiona kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni za Bunge, kwa bahati mbaya au kwa makusudi, basi niombwe radhi.

Mheshimiwa Spika, ombi langu hili mbele yako ni muhimu sana katika kulifanya Bunge lijiangalie na kurekebisha, kama inabidi, pale ambapo litakuwa limekosea. Hii itasaidia kuepuka makosa kama haya siku za usoni.

Mheshimiwa Spika, Kanuni za adhabu zimeanishwa katika Kanuni za Bunge Toleo la mwaka 2004. Kanuni husika ni kanuni namba 58, 59, 60, 61 na 62. Lakini pia kanuni hizi msingi wake, pamoja na masuala ya amani na utulivu Bungeni ni kanuni inayokataza kusema uongo Bungeni. Kanuni hii ni kanuni namba 50 ya kanuni za Bunge letu tukufu.

Mheshimiwa Spika, Bunge lina taratibu za kuleta hoja Bungeni. Taratibu hizi zimefafanuliwa kinagaubaga katika Kanuni za Bunge na zimeanisha wazi kabisa ya kwamba hoja haiwezi kutolewa juu ya hoja nyingine na kwamba muda wa kutoa taarifa za hoja umewekewa taratibu ndani ya kanuni za Bunge.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, kanuni zetu zimesema wazi kabisa (59-3) kuwa iwapo Mbunge anashutumiwa kusema uongo Bungeni, au kutoa lugha ya kuudhi atapewa muda ili kuthibitisha hilo analoshutumiwa. Mimi mheshimiwa Spika, sio tu sikuwahi kushutumiwa kusema uongo bali pia wewe binafsi unajua sijawahi kupewa muda kuthibitisha chochote.

Muda wa kuwasilisha hoja yangu, ambao kwa masikitiko makubwa, viongozi wa Bunge mmeueleza kama ndio muda niliopewa kuthibitisha maneno yangu, ni muda wa kikanuni ambao niliomba mimi ili kuleta hoja binafsi na wala sio muda niliopewa kuthibitisha jambo lolote.

Mheshimiwa Spika maamuzi ya Bunge ya kunisimamisha kwa kusema uongo Bungeni (uongo ambao haujawi kusemwa ni upi) yalinidhalilisha mimi binafsi mbele ya jamii na kudunisha utu wangu. Adhabu niliyopewa iliniweka katika wakati mgumu sana na hata kunishushia heshima sio tu katika jamii ya Tanzania bali katika jamii ya kimataifa. Nimekuwa nikionekana ni Mbunge mwongo.

Mbaya zaidi baadhi ya Viongozi wa Bunge, ukiwemo wewe mheshimiwa Spika, Naibu Spika na Katibu wa Mbunge mliendelea kuonyesha kuwa adhabu ile ni sahihi na kuwaaminisha wananchi kuwa mimi ni Mbunge Muongo.
Vile vile viongozi wa upande wa serikali akiwemo Waziri Mkuu, Mawaziri na Manaibu mawaziri wamenukuliwa na kurekodiwa na vyombo vya habari wakisema mimi ni Muongo kufuatia adhabu hiyo.

Adhabu niliyopewa na Bunge, ambayo naomba Kamati ya Kanuni za Bunge iipitie, imenidhalilisha sana kama mtu binafsi. Lakini pia adhabu hii ni ishara mbaya sana kwa demokrasia ndani ya Bunge let tukufu.

Mheshimiwa Spika, licha ya kwamba nina nafasi na Haki ya kuomba chombo kingine cha dola kama Mahakama kupitia adhabu hii, nimesita kufanya hivyo ili kulipa Bunge nafasi ya kujikosoa.

Ninaliheshimu sana Bunge na mimi kama Mbunge ningependa kuona Bunge likiheshimika mbele ya jamii, tena chini ya uongozi wako. Hii imethibitishwa kwa kuitumikia adhabu yote na kutotoa kauli yeyote iliyoingilia mamlaka ya Bunge kuhusiana na adhabu niliyopewa.

Ninawasilisha kwako, kwa unyenyekevu kabisa maombi yafuatayo

1. Bunge, kupitia Kamati ya Kanuni za Bunge, lipitie adhabu niliyopewa na Bunge tarehe 14/8/2007 na lijiridhishe kama Kanuni za Bunge zilifuatwa.

2. Bunge, baada ya kupitia vifungu vyote vya Kanuni za Bunge, ikiwemo kunisikiliza katika kikao cha Kamati, lipitie kauli zote za viongozi wa Bunge na wa Tawi la Utendaji (Serikali) kuhusu adhabu niliyopewa na kuona kama hawakuvunja kanuni za Bunge na sheria namba 3 ya mwaka 1988.

3. Kama Bunge likiridhika kuwa matamshi ya viongozi niliowataja katika namba 2 hapo juu, yanakiuka kanuni za Bunge kwa hali yeyote ile, basi wapelekwe katika kamati husika ya Bunge.

4. Bunge liniombe radhi kwa kunipa adhabu isivyo halali.

5. Bunge lijutie (repent) maamuzi iliyoyachukua na kuahidi mbele ya jamii ya Watanzania ambayo ndio inayotoa mamlaka ya utawala (Ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano) kuwa halitarudia kuvunja kanuni za Bunge kwa makusudi na kumuadhibu mwakilishi wa wananchi mwingine yeyote bila makosa.

6. Bunge liahidi kuwa kamwe haitotokea Mbunge kuonewa kwa sababu za kiitikadi au kukomoa na kupiga marufuku vikao vya kamati za vyama vya siasa ndani ya Bunge kupanga njama za kuadhibu Wabunge bila makosa.

Mheshimiwa Spika, Ninaleta kwako maombi yangu haya nikiamini kabisa kuwa yatafanyiwa kazi kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na hasa Kanuni namba 4(3) inayotoa mamlaka kwako kutilia nguvu matumizi ya Kanuni za Bunge na inayonipa nafasi mimi kama Mbunge kukata rufaa na kuonesha kutoridhishwa kwangu na maamuzi ya Bunge.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kanuni zetu maamuzi ya Bunge ni maamuzi ya Spika na vile vile maamuzi ya Spika (anapotekeleza mamlaka yake) ni maamuzi ya Bunge. Hivyo nimejiridhisha kabisa ya kwamba Kamati ya Kanuni za Bunge ina mamlaka ya kujadili suala hili.

Nakutakia kila kheri katika kuimarisha demokrasia ndani ya Bunge.

Wako mtiifu,




Kabwe Zuberi Zitto (Mb)
Mbunge wa Kigoma Kaskazini.


Nakala

1. Katibu wa Bunge
2. Kiongozi wa Upinzani Bungeni
 
Kwa akili yako Masatu wewe ulitaka bwana Zitto amwandikie nani ambaye anaweza kutoa maamuzi ya busara? Nadhani kitu alicho kifanya ni sahihi kabisa kwamba huwa wanaamua kwa jazba na sasa watafanya reflection na Watanzania watajua ukweli ni upi hasa kulingana na lile saga . Zitto ni Mtanzania na Mbunge wa Tanzania hawezi kwenda kupeleka malalamiko yake US kama vile Mkulu afanyavyo kuongelea maswali ya Nchi yake akiwa US

Mawazo ya busara? nani Six huyu huyu au mwingine?

Hapa hakuna lolote ni wastage of time and resources Zitto ushaona mtaji wako wa umaarufu unafifia umeona bora uufufue upya!!

Good try mate....
 
Mheshimiwa Zitto,

Barua yako inagusa na ina mantiki kabisa kabisa. Kweli unatupa fahari kubwa vijana. Kazi unayoifanya ni kubwa sana, ujenzi wa demkrasia unahitaji watu wenye moyo huu; wasiokatishwa tamaa na mfumo fisadi.
Tuko wengi tunakutakia kila la heri katika kazi hii ngumu ya kuijenga demokrasia.Tunamuomba Mungu atujalie nasi wengine tukuunge mkono kwa vitendo, japo yahitaji kujitoa..lakini mtaka cha uvunguni sharti ainame. Tunatarajia bunge litatimiza wajibu wake ipasavyo bila kufuata ushabiki wa kiitikadi na kusahau jukumu lake.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mawazo ya busara? nani Six huyu huyu au mwingine?

Hapa hakuna lolote ni wastage of time and resources Zitto ushaona mtaji wako wa umaarufu unafifia umeona bora uufufue upya!!

Good try mate....

JF members ignore Masatu, he is either an old crap or one of the fisadis.
 
Quote:-

"Hapa hakuna lolote ni wastage of time and resources Zitto ushaona mtaji wako wa umaarufu unafifia umeona bora uufufue upya!!"

Mkuu Masatu,

Heshima mbele mkuu, kuna wakati wa kila kitu katika maisha na hata siasa pia, huu sio wakati wa kumkatisha tamaa mwanamapinduzi wa kweli na wa kwanza katika historia ya taifa letu, Mheshimiwa Kijana Zitto,

In fact, sasa hivi tunashuhudia our national political History in the re-making, single handed by Zitto, a merely 30 something years old kid, Mungu akubariki kijana Zitto, standing tall katika nchi yenye wananchi zaidi ya Millioni 40, tena wengi wetu tukiwa na umri mkubwa kuliko wa kwako, wengine tukiwa na elimu kubwa kuliko yako, wengine tumeona mengi kuliko uliyoyaona, uhuru wetu wa taifa miaka karibu 45, ilibidi uje wewe kuja kutuamusha na kuiamusha serikali yetu uchwara,

In the wake ya habari depressing kama za kina Mama Mongella, Now here comes the Masatus, maana ni wengi sana hawa kwenye taifa letu, kina do nothing lakini criticize everything wasichoweza kufanya, God bless you Zitto,

Remember one thing mkuu Zitto, tuko wengi nyuma yako, stand up mkuu utusaidie kusimama na sisi wanyonge wa Mungu.
 
Quote:-

In the wake ya habari depressing kama za kina Mama Mongella, Now herer comes the Masatus, maana ni wengi sana hawa kwenye taifa letu, kina do nothing lakini criticize everything wasichoweza kufanya, God bless you Zitto,

]



Mkuu huu ni ujumbe maridhawa wa kufunga mwaka! wale ambao hatuwezi hata kujaribu si tuwaachie wenye moyo wajaribu? Umaskini ni mbaya lakini wa fikra ni mbaya zaidi!
 
Mimi naangalia katika pande mbili,wana JF sijui ni kwanini Zitto amechelewa kuwasilisha hoja zake Bungeni za malalamiko haya anayoyaleta leo?Je hakuna kanuni ya Bunge ambayo inatoa mwisho wa Mbunge kulalamika kutokana na Adhabu?Unaweza ukawa unadai haki yako sawia lakini ukapotoka katika taratibu.Ni wenyewe kwa wenyewe tu wanaweza lindana na si kwa mtu kama Kabwe.
Lakini pili kama tunategemea Bunge litatoa jibu fulani kama baadhi ya wana JF walivyosema kunasababu gani kwa Kabwe kurudi tena Bungeni,Bunge ambalo haliangalii maslahi ya Taifa.
Nionavyo mimi Kabwe alitakiwa aende kwenye muhimili uliobakia ambao ni Mahakama.Kama umaarufu alishapata sasa atafute haki.
Nawasilisha.
 
I
n the wake ya habari depressing kama za kina Mama Mongella, Now here comes the Masatus, maana ni wengi sana hawa kwenye taifa letu, kina do nothing lakini criticize everything wasichoweza kufanya, God bless you Zitto,

ES Hii ndio kensa kubwa inayotumong'onyoa kila uchao mitazamo hodhi! Mitazamo kama yako haina nafasi ktk harakati za kumkomboa Mtanzania.

Hili suala lipo crystal clear ni upotezaji wa muda. Hivi tunategemea nini kutoka ktk Bunge lenye kutawaliwa na over 90% CCM? Huhitaji kuwa rocket scientist kujua hili.

Niliuliza mapema tunataraji kuwa Mzee Six aungame na kusema wamekosea? hata siku moja. The bigger picture here is kamati/tume zitakaa posho zitawaliwa na majibu yatakuwa yale yale "yasiyoridhisha" kwa wengi wetu humu, sasa anachokifanya Zitto ni kutupeleka katika ufisadi-wakati maana anajua kabisa hakuna la maana atakalo achieve kwenye hili (umaarufu?)

Mimi nadhani ile mbinu ya Dr Slaa ni nzuri zaidi yeye kakataa hata kwenda mahakamni kwani anajua fika hatopata kitu huko na akaamua kupeleka suala kwenye mahakamani ya wananchi pale Mwembe Yanga na kwingineko, Zitto nae amefanya vivyo hivyo mwanzoni lakini all over suddenly now anaturudisha kule kule kwenye "busara za Spika"

Zitto labda kama una jipya kwenye "ushiriki" wako wa kamati/tume ya madini lakini ktk hili mwaya umechemsha na kwa bahati mbaya JF imekuwa blind folded hawataki constructive criticism bado wapo na zidumu fikra za Mwenyekiti.

Natusubiri Sitta alipeleke suala hili kwenye kamati walichambua (huku wakila posho) na majibu yatakuwa more or less busara zangu zinanituma!

Only in Tanzania......
 
Back
Top Bottom