Ibambasi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2007
- 9,299
- 4,701
Huna tofauti na mzee Makamba, unataka Zitto ajipendekeze kwa Magu kama wewe?
Zitto ni msaliti au siyo msaliti?
Huna tofauti na mzee Makamba, unataka Zitto ajipendekeze kwa Magu kama wewe?
Zitto huwa hatishiwi nyau.Ushauri kwako kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo!!
Upepo gani wakujifunga makaratasi midomoni,sasa kwa taarifa yako zitto sio mwanasiasa uchwara,.wala sio mwanasesere.Wenzie wenye ufahamu kiasi fulani wamesoma upepo uliopo kwa sasa wakaamua kukaa kimya
Mimi chadema lakini umbea atupendi.siasa ni maisha na maisha uendana na wakati .Zito amekosa nini !!!!???? Au ni wewe huko nyuma ya wakati .Namkumbuka Zitto Zuberi Kabwe wa 2005-2010 na ninamlinganisha na huyu wa sasa mmmmhhh hadi inauma sana tukiendelea kupoteza vijana kama huyu wengine miaka ijayo kuna kazi kubwa sana ya kuja kulikomboa taifa hili!!
Nimekuwa nikijiuliza hivi Zitto ni nini kimempata??
Yuko wapi Zitto aliyeibua sakata la mgodi wa Buzwagi?
Yuko wapi zitto aliyekuwa akipigania masilai ya wanyonge bungeni kupitia ununuzi wa Rada??
Zitto aliyeungana na Dr slaa juu ya Richmond yuko wapi??
Zitto huyu huyu anayetuhumiwa kwa kuwa na mali zisizolingana na kipato chake ??
Zitto huyu huyu ambaye milija yake imezibwa pale NSSF?
Zito amekuwa mtu tena wa kupiga dili na kuakikisha kila kitu amekipata kanunua majumba mazuri ,Magari mazuri,kila kitu kamiliki leo hii kabaki na kazi moja tu ya !!
Kila siku kuiponda selikari ya Rais magufuli!!!
Hivi hakuna mazuri ya kumpongeza Rais magufuli ni kumponda tu ? Hata akipongeza anapongeza kwa unafiki!!
Kama kweli Wewe ni mzalendo unapigania masilai ya watanzania njoo ujibu maswali yafuatayo!!
Wewe si dictator??
Na ulivyo dictator ulipofika tu ACT wazalendo ukapewa cheo cha kiongozi mkuu wa chama hivi uoni kwamba ilo ni tatizo la kupenda madaraka?
Kwani kulikuwa hakuna watu wengine mpaka upewe wewe hicho cheo uligombea na nani?
Sasa hivi professor Mkumbo anawashauri wapinzani mbadilishe njia za kupambana na selikari ya Rais magufuli lakini hata ushauri usikii imekuwa sikio la kufa!
Na juzi tu mama Anna ametofautiana na wewe waziwazi kuusu mwaliko uliotolewa Dodoma !!
Mbili kwanini uliondoka chadema kwa kutaka uwe mwenyekiti uoni hapo kuna tatizo la udikiteta kutaka cheo kwa nguvu? Kwanini ukusema wazi wazi ila ukaanzisha mtandao ndani ya chama?
Ulishamsikia magufuli anagomea cheo ndani ya chama toka amejiunga na CCM hata cha mwenyekiti wa shina??
Leo hii unatoka na kumfananisha rais magufuli na Putin wa Russia hivi hoja yako ya Jana kwamba watu wamsome Putin ina faida gani kwa taifa?
Kuna faida gani kwa wananchi wa Ujiji??
Hivi unafikiri wananchi wa vijijini wanaweza kaa wasome vitabu au wapekue Internet kwa vifulushi vipi hivi hivi vya wanyonyaji Voda,Tigo na Airtel?
Baada ya kuishauri selikari ilifufue shirika letu la TCCL ili tupate affordable bundle wananchi waweze kupata Internet ilivyo bora na kuepukana na makampuni ya wanyonyaji upo tu kukosoa !!
Mkuu Zitto tulikuheshimu sana lakini sasa your politically finished!!
Baada uungane na Magufuli mpeleke kiwanda cha nyavu za kuvulia Dagaa ujiji ??unaangaika eti wananchi wamsome Putin Hivi mwananchi wa kawaida wa ujiji atakuelewa kweli??
Kwanza tu nikufaamishe taarifa nyingi unazozisoma kwenye mitandao kuusu Putin kama hazitoki Russia ni za kupika kutoka nchi za magaribi!!
Nchi za magaribi hazimpendi Putin kwa sababu analeta mabadiliko ya kweli uko Russia!!
Ni kiongozi imara asiyeteteleka kama alivyo Magufuli hivyo vyombo vya habari vya magaribi haviwezi kumpamba hata kidogo Putin ni kiongozi imara kama alivyo Magufuli!!
Ushauri kwako kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo!!
Watu unaotakiwa kubishana nao ni Mkuu wa mkoa Kigoma,Mkuu wa willaya jimboni kwako,Mkurugenzi jimboni kwako na spika wa ubunge Hao ndio size yako!! Hakuna mtu anayeupata Urais kwa kumponda Rais aliyeko madarakani hapa Afrika nikukumbushe lazima tuambiane ukweli!!
Tanzania- Professor Lipumba aliponda ameenda,
Kenya-Raila Odinga aliponda huyo anakwenda,
Uganda-Kiza Besige aliponda anakwenda,
Zimbabwe- Morgan Shangelai aliponda amekwenda !!
Mifano ipo mingi tu ila nikushauri pigania masilai ya wananchi wako wa ujiji na Tanzania!!
Nasikitika tunapoteza nguvu kazi za Taifa hasa vijana tuliokuwa tunawategemea wanatoweka taratibu.
Asanteee.
Ungetambua mwelekeo wa Serilali ya Magufuli, ungeondoa mawazo mgando. Mawazo ya kufanya mambo na kuwaza yaleyale kwa mazoea.Tatizo la Nyie magambaa mnataka kila mtu ajipendekeze kwa magu alafu magu asikosoleweee.....
Sijaona kosowa ya kujenga zaidi ya lawama na manung'uniko. Hii nchi yetu wote na haiwezi kuendelezwa na Rais pekee. Mawazo na maelekezo yake kama siyo sahihi, tumsahihishe kwa hoja na siyo matusi, kebehi na kukata tamaa kwa maneno na mawazo km "hafiki popote"!Kwan magufuli ni Mungu asikosolewe???
Toka lini chadema mumeanza kumkubali Zitto ?Mimi chadema lakini umbea atupendi.siasa ni maisha na maisha uendana na wakati .Zito amekosa nini !!!!???? Au ni wewe huko nyuma ya wakati .
Mkuu asante kwa kulielewa hiliMleta mada ujumbe wako uwafikie viongozi wote wa CCM na kambi ya upinzani kwamba Dr Magufuli anatoa mfano wa kiongozi mzalendo zaidi ya mfano wa Baba wa Taifa.
1) Yeye ana utashi wa kisiasa
2) Hamng'unyi maneno wala kuwa na kigugumizi kutetea haki ya Watanzania
3) Ni mwiba mrefu kwa wanasisa maslahi
WAKATI NDIYO HUU TUJENGE TANZANIA MPYA YENYE NEEMA.
Hivi uchaguzi wa mwenyekiti wa chadema ni lini vile ukinijibu najiunga na chademaMzazi wako alikupa elimu ya kujipendekeza na kushinda hapa jukwaani kukashifu wasiomnyenyekea unayemnyenyekea? Juzi ccm wamefanya mkutano wao wa kumchagua mwenyekiti wenu, cha ajabu ni kama wanaccm wote ni kama maroboti, toka lini mtu akapata kura asilimia mia moja? Katika mazingira kama hayo unataka na watu wenye mtazamo tofauti waunge mkono kila mnachofanya nyie. Kama wanaccm mmeshikiwa akili sio lazima kila mtanzania awe kama nyie. Jaribu kuheshimu mawazo ya wengine hata kama hampendi wala hupendi mawazo yake.
Mwendo wa matamkoZito akome kuchafuachafua rais wetu,kulasiku anakalia kuitisha selikariyetu kwamambo yasiyo natija,ashindwe na alegee
Politically finishedkwel bwan huy jamaa namuelewaga sana bt now dah ananichefua aisee
Kwa taarifa yako baba yangu hana shida yeyote ndo maana alifanikisha shule yangu
Huyo Putin aliyetoka kustaafu Urais akateuliwa kuwa waziri Mkuu baadae akateuliwa kuwa tena RaisMagufuli kufananishwa na putin kuna tatizo gani kwani?.
Putin ni mmoja wa viongozi wazuri sana duniani,maana hana undumilakuwili yule