Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,097
- 43,309
Tuna kama miezi miwili tu kabla ya kikao cha Bunge la bajeti kuanza; endapo hoja ya kutokuwa na imani itatolewa sasa na kama Spika atakubali kuitisha kikao maalum ndani ya siku 14 (kwani haiwezi kutolewa kwenye kikao cha sasa) manake ni kuwa hoja kama hiyo haiwezi kuletwa ndani ya miezi sita. Ukishapata kura hizo sabini au zaidi basi unapanga kuleta hoja hiyo kwenye kikao kijacho na kuondoa kuzuiwa na muda kufanya hivyo.
Lakini zaidi watu wasije wakachanganya vitu viwili - kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu na kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu. Ili hoja iweze kuletwa Bungeni zinahitajika asilimia 20 tu ya wabunge (ndipo namba ya kura 70 inapokuja). Kura 70 HAZIWEZI kumuondoa Waziri Mkuu; zinaweza tu kufanya hoja iletwe Bungeni. Baada ya kuletwa bungeni na wabunge kupiga kura inahitajika asilimia 50+1 kwa Bunge kupitisha Azimio la kutokuwa na imani na waziri mkuu.
Hii ina maana ili azimio lipitishwe ZINAHITAJIKA kura 178 na siyo 70!
Sasa haitoshi kufanya hoja iletwe Bungeni tu (kwa kura 70) lakini tunataka inapoletwa Bungeni ni kweli kuna uwezekano wa ku-effect the removal of the Prime Minister. Jambo zuri ambalo limetokea ni kuwa kwa mara ya kwanza Watanzania tunazungumzia njia ya kidemokrasia ya kumuondoa Waziri Mkuu. Kwa hili Zitto amethubutisha watu kufikiria uwezekano huo na hili litaingia kwenye historia vizuri kabisa. Lakini pia linafanya watu wazungumzie juu ya madaraka ya Waziri Mkuu kusimamia serikali yanakoma wapi na kama ni mtu sahihi kumwajibisha.
Ikumbukwe pia kuwa hoja ya kumshtaki Rais chini ya article 46 ni RAHISI zaidi kwani nayo inahitaji kura 70 kuweza kuletwa mezani na sababu za kumshtaki Rais Bungeni ni za chini kidogo - mojawapo ni kuwa amedhalilisha ofisi ya Urais! Nimesema mahali pengine kuwa kutokuwa na imani naWaziri Mkuu ni kutokuwa na imani na rais hivi viwili kwa mfumo wetu havitenganishwi. Wote ambao wameunga mkono kwa kutia sahihi kura 70+ ina maana hawana imani na rais hakuna tafsiri nyingine. Kwa vile hili ni kweli ni muhimu basi kwenda moja kwa moja for the "jugular" yaani kuleta mashtaka dhidi ya Rais katika kikao kijacho!
Kwa kuleta mashtaka dhidi ya Rais na yakathibitika basi rais atajiuzulu na Makamu wa Rais atashika madaraka na atapewa nafasi ya kuunda serikali mpya bila kulazimisha uchaguzi mpya. Lakini kama tunataka mabadiliko ya kweli hadi Bungnei (kwa sababu wengine tunaamini matatizo hayako kwa Waziri Mkuu au Rais peke yake bali hadi Bungeni) basi azimio la kumtaka Rais avunje Bunge litolewe ili WOTE (kuanzia Rais hadi wabunge) warudi kwa wananchi ili kupata ridhaa mpya (a new mandate). Tusitake mabadiliko nusu kwani hakuna mapinduzi nusu (there is no half-revolutions)! Kama tunataka kubadilisha TUBADILI KITU CHOTE KIZIMA!
So, kwa sasa nashauri a strategic withdrawal ya hoja hii!!