Zitto umewadhalilisha Wabunge wa Viti Maalum CDM; Waombe Radhi


Mkuu binasfi sidhani kama kuna mtu anaweza kuogopa kushindwa kujiunga ga CDM kwa kauli ya ziito kumuitwa mbunge wakuja. Kwangu threat kubwa kwa CDM sio makosa ya syntax ya mtu moja mmoja kuelezea kitu sahihi. bali threat ni tabia kama za huyu mleta mada. tena wengine ni wabunge. Tena wengine wanatumia screen name za kike. What if ni wanaume..... anyway niisiende huko nikajikuta nasema yale ya msekwa "tabia za kike" gaijin na wenzake wakanishambulia . teh teh teh

Ninaweza kupata hoja za msingi kwenye sentensi ya ziito japo z ina makosa ya lugha ya kukubalika lakini Hao wanaomlaumu hupati substance yeyote ya maana . ebu jaribu kungalia big picture ya CDM mkuu. Sometime mtu analeta mda inahusu zittto unajiuliza anajaribu kuachieve nini iwe ni kwa manufaa ya chama au nchi no maater lafudhi nzuri na sarufi atayotumia.

But kama CDM will be clean stable na hatutasikia mipshasho without ziito basi wamfukuze. kwenye footbal tunasema No single player is better than a team. tunachotaka watanzania ni mabadiliko.

Thanks i like politics but am not a politician
 
Labda hujanisoma vizuri. Nimesema wa kuja halina ubishi kwani hata yeye Zitto anaweza kuitwa wakuja na wenyeji wake ktk mazungumzo yanayohusu ujio wake..Hiki ni kiswahili tunachokitumia siku zote na wala sii tusi unless wewe mwenyewe ndio unajihisi Ugeni ni tusi.

Swala ni mtu uliyechini yako na mgeni anaanza kutoa maneno ambayo kiaina yanakosa adabu na zaidi ya hapo mtu huyo hajui undani wakile anachokizungumza zaidi ya kushabikia. Mzee Pius Msekwa anaweza kabisa kuwaita wabunge wa CCM wa kuja kama hao wabunge watamkosea adabu na wataanza kumzungumzia yeye na sii kazi walokabidhiwa. Tena basi huyo mzee wetu pius Msekwa anaweza kutukana matusi ya nguoni acha hii habari ya kuitwa watu wa kuja. Kawaita upinzani wanafiki atashindwa kumwita mtu wa kuja?

Huyu mbunge alozungumza simjui ila Zitto anamfahamu vizuri na kuja kwake hapa JF akipinga matumizi ya lugha ya Zitto kwa kiongozi wake ktk FB hali yeye mwenyewe anarudia uozo ule ule hapa JF, inabidi apigwe kibao cha kerbu na ndio hayo majibu ya Zitto. Kifupi kule tulikotoka Zitto mwenyewe kakubali makosa ktk kusherehesha malalamiko yake, hata huyu mbunge wetu inabidi ajifunze kutumia lugha nzuri unapowakilisha hoja. Kama kuna malalamiko yoyote zipo njia mbadala za kufikisha malalamiko hayo na sii kuvuana nguo hapa JF kama vile Zitto ni baradhuli asiyejiweza..
 
Reactions: EMT

Mwita,

I dont get your point,i mean what is the correlation?

Uko obsessed na chadema?nitaanza kuamini hivyo.....................
 
Acha wivu wewe,vaa sketi nawewe ili uzawadiwe Ubunge kama ubunge unazawadiwa.Wacha Vitimaalum viwepo ili nasisi tunaotaka kuingia tuupate.Abarkiwe aliyeleta wazo la vitimaalum.Mtapiga kelele habari ndio hiyo.Hilo ni takwa la SADC.Wivu tu..


Unaweza kutumbia. Assume uko bungeni leo hii unatoa speech kuchangia hotuba ya bajeti . Chagua wiziara yeyote unayopenda kuilenga.
  • tupe tathmini mambo gani unezungumza mjengoni?
 

Safi sana kwa hili hata mimi asubuhi nilitangaza azma ya kulipeleka hili kamati kuu kwa kudhalilisha wabunge wa viti maalumu kwenye mitandao.hii ni dharau iliyopitiliza.nilishasema hawa wanawachukia kwa sababu walitaka kuchomeka watu wao.kinachoshangaza zaidi kuna tetesi kuwa wana mahawara zao huko huko.Mwone huyu hapa chini nae amejaribu sana kujiweka mbali na hii kashfa lakini amejenga hoja zenye muelekeo wa kufuta viti maalumu.Dharau zao ziko waziwazi.Hebu watuache wasituharbie chama mbelekeni mawazo yenu huko nccr hakuna anayewazuia bwana


 
THANKS! For being fair .
 
Utakapopeleka hoja ya kudhalilishwa viti maalum usisahau na hoja ya kiti maalum mmoja kutamka wazi Zitto kamwe hawezi kugombea urais CDM, ili tupate uhakika kama hoja hyo ilishajadiliwa tupewe na vigezo.
 
Mh inaelekea Chadema ndani yake kuna makundi kama ilivyo CCM. Chadema wasipo angalia wataanza kugeuka replica ya CCM kabla hata ya kushika madaraka. Ubaya wa wao kuwa kama CCM ina maanisha chama kitakua kimeenda kinyume kabisa na ujumbe wao wa kuwa chama mbadala na CCM watahakikisha wananchi wanajua na wananchi hawato sahau.
 

Mfundishe kwanza Zitto halafu uje kwangu,mwisho malizia na kwako.
 
Hatutaki viti maalum/kuteuliwa....It's nonsense and undemocratic!!,let alone cost effectiveness of the whole dumb idea.
 


MKANDARA,
Nami napenda nikuunge mkono bila uficho katika maneno yako yenye ukweli mtupu.
Ila natofautiana na wewe katika kipegele kimoja, hawa wanaojibu matusi na mashabiki wanaojivika gwanda la chadema kwa kujifanya wanajua sana na eti wanauchungu na chama ni watu wenye milengo butu isiyo na maono hai.
Hawa ni wale waishio kwa upepo uvumao kusi-kaskaz, tena ukiwawataka wajadili kitu kwa uhalisia hutapata majibu na ukitaka ukoshe waombe wajadili ushibiki wenye wingi wa porojo utaona mandiko yenye ufundi wa kijuha kabisa.
Nayasema haya bila gubi lolote kwani nimewashauri mara kadhaa wawe wenye kujadili hoja na sio kushambulia kwa matusi, lakini hawashiki mpambanuo huo.
Nami nakazia...UBUNGE VITI MAALUM NI ZAWADI NA HATA WAO WANAJUA WAMEZAWADIWA...NA WANAJUA KABISA NI BAHATI NA SIO KWA VIGEZO VYA UWEZO BINAFSI.
 
Naomba mtu mmoja aweke link ya hiyo thread nimejaribu kuitafuta siioni, nataka na mimi niweke mawazo yangu baada ya kuwa nimeshasoma hayo majibizano.
 
Mwenye majina ya wabunge wote wa viti maalum kupitia chadema/picha zao,namuomba ayaweke hapa
 
THANKS! For being fair .

He's always fair.....

Sio shabiki ndiyo maana utaona baadae watu wataanza kumshambulia ati mbona jana ulikuwa una-oppose mbona leo una-support.Watu wanashindwa kuelewa tofauti kati ya Analysis by intellectual reasoning na political fanatiscism cum personal vendatta.Sio kila mtu JF ni shabiki
 
good!!!!!thanks.

Nyakarungu/Jikedume

Unaatamani na wewe kama ungekuwa mwanamke vile ili upate ubunge wa vitimaalum uache kurandaranda.Hivi kwenye Uongozi wa BAVICHA hakuna vitimaalum ili uteuliwe na wewe?maana ulifanya kazi nzuri sana ya washa taa mchana.hivi mfadhili wako bado yupo?
 

Kama Mh. Zitto hakufurahishwa na aliyosema Marytina, taratibu za JF zinasemaje? Mods hawakuona aliyosema Marytina? I don't know whether or Marytina is also an MP, but if she is then I don't condone what she said either hata kama anajificha kwa ID feki. Similarly, I don't condone Hon. Zitto's response. Angetumia busara zaidi. Otherwise, anaweza kuwekwa kundi moja na Martyana. Kuna njia nyingi za busara za ku address issue kama hii. Badala yake ame-respond in way that tries to justify demarcations of members within the party.

Hon Zitto should have been wise to give thought to Marytina's remarks before responding. If it were you responding to Marytina's remark, as a person holding a public office, you would want to put a little thought into what you are about to post in a forum like this. If people post comments that are critical or even insulting you, you would always maintain an even demeanor. Hon Zitto should not have over reacted in a way which he might come to regret later or which will cast him in a negative light in the same way as Marytina. Condoning Hon Zitto's response is condoning Marytina's remarks and vice versa.
 

hakika kweli huyu ni wa kuja, sio wakuja cdm tu, bali katika siasa huyu ni wa kuja.
Anaamini siasa ni kupigana majungu tu, anaamini hana uwezo wa nguvu za ushawishi bali anatumia njia za aina hii kuwaharibu wenye hoja.
Ninamuomba aende kwa wananchi afanye kazi ya kujenga chama tuone uwezo wake.
Na watu wa aina hii ni hatari sana, kwani watagombania jimbo la viti maalum na mwisho wa siku watawagawa wananchi na hali hii imemponza dada mmoja ni viti maalum sasa.

Kuna mambo yakufanya ili jamii ikuamini na ikupende sio kupiga majungu kila wakati mama.
 
heee makubwa haya kumbe ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni ni kweli. Nijuavyo mimi CDM ni chama chenye watu makini na nilimtegemea Zitto ni mmoja wao lakini kwa hili amesikitisha na kuonesha his true colours! Zitto ndio alikuwa msimamizi mkuu wa Uchaguzi huo kabla haujavurugika na yeye anajua kwa nini hali ilifika pale. Lakini hata baadaye alikuwa kwenye kamati ya kuteua waheshimiwa hao sasa leo inakuwaje aseme haya! Kama si unafiki dhahiri nini? Atueleze ni wapi aliwapa na wale waliokosa waende wapi?
Hii inatuonesha kwamba vigezo vilivyoelezwa na Dr Kitila ni vya uongo?? Tunaomba viongozi wakuu mumfunde huyu maana atakiingiza chama pabaya
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…