Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Nimeamini Zitto anauwezo mkubwa wa kufikiria. Chadema hawatamkubali mwaka 2015, na akienda chama kingine ataonekana msaliti miongoni mwetu tulio wengi. Ila mwaka 2020/25 tuhuma hizi zitakuwa zimekufa au zimedhoofika. Zitto atakuwa amejitafakari vyakuyosha na atakuwa na nguvu mpya + tumaini jipya

Hakuna mtu aliyemkamilifu. Zitto akijirudi na kupunguza kiburi kidogo tu, bado ni mtu anayeweza kuiongoza nchi hii vema.
Endapo atatekeleza kauli hii atakuwa amefanya jambo la hekima sana. Naamini mwaka 2020/25 zitto atakuwa nyota tena si ya chadema pekee, Bali nchi kwa ujumla.

pumzika siasa ukiwa ndani ya chadema. muda huo utumie kutatua tofauti zako na chama. umeona mbali.
 
Acheni upimbi ninyi wanafunzi mbona mnajadili siasa kila wakati mnapiga kura ndicho mlichotumwa? Tunalipa kodi ndizo wengi wenu mnasomeshewa kwa nn msitulie darasani na kufanya tafiti za matatizo tuliyonayo, pumbafuuuuu:what:
 
Uamuzi huu wa Zitto siuoni kama ni wa ajabu. Amesoma alama za nyakati tu!
Taarifa za kuaminika ni kuwa Zitto alitarajiwa kuhama jimbo lake na kuelekea Kigoma mjini (kwa Peter Serukamba) ambaye anahamia jimbo la sasa la Zitto.
Kutokana na maridhiano na Mgombea urais wa chama tawala yaliyofanyika Zimbabwe (???), Zitto alitarajiwa atapata nafasi nzuri baada ya kupatikana katiba isiyolazimisha Rais nani wa kumchagua. Kutokana na kuzorota kwa upatikanaji wa katiba, Zitto anaona ni vigumu kuwania nafasi ya ubunge kutokana na kuanguka kisiasa.

Assessment
Inaonekana kushuka kwa Zitto kunaweza kumuathiri sana baadae. Hii inatokana na ukweli kuwa amefanya kosa la kisiasa kutokana na ushabiki wa nje ya chama chake, CDM. Ki siasa huu ni usaliti ambao unamfanya asiaminike hata kwa wanasiasa wengine. Huu ni ukweli usiopingika kutokana na siasa za kuwania nafasi kwa tamaa badala ya kuangalia matakwa ya walio wengi.

Anjo
 
You people have given Zitto Kabwe too much publicity. He is inebriated with his own verbosity.
 
Tuamke sasa tuende kujenga uchumi wa nchi yetu.

Nikiwa napitia magazet asb hii, jana tuliona habar ya wapambe walimfitini mh.zitto kwa mh. mbowe ndani ya mwananchi, leo anasema hivi juu nimejaribu kupitia ndani habari hii ni muendelezo either wakujuta kwa mh huyu au kutoelewa maneno yake juu ya kuachana na ubunge nakwenda kufundisha.
================================================


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anaonekana yuko njiapanda kati ya nia yake ya kugombea urais au ubunge, lakini kwa jinsi mwenendo wa kuandika Katiba Mpya ulivyo, ni dhahiri ataendelea kugombea nafasi kuingia bungeni.

Hata hivyo, mbunge huyo kijana hatarudi Kigoma Kaskazini ambako ameongoza kwa vipindi viwili; atagombea jimbo la Kigoma Mjini.

Septemba 23 mwaka huu, Zitto atakuwa akitimiza umri wa miaka 38, lakini Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano, ambayo hakuna shaka kuwa ndiyo itatumika kwenye Uchaguzi Mkuu mwakani, inaruhusu mgombea mwenye miaka kuanzia 40, umri ambao Zitto hatakuwa ameufikia mwakani atakapokuwa na miaka 39.

"Kama Katiba haitaniruhusu nitafanya kitu ambacho kitanifanya niendelee kufanya siasa na possibly (uwezekano ni kwamba) ninaweza kugombea ubunge Jimbo la Kigoma mjini," alisema Zitto katika mahojiano na Mwananchi wiki iliyopita.

"Suala la umri wa urais limekuwa likihusishwa sana na Zitto, hii siyo sahihi. Hili suala lipo katika Rasimu ya (Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Jaji Joseph) Warioba. Wengine hawataki suala hili libadilishwe ili tu nisipate nafasi, lakini ukweli ni kwamba zaidi ya nusu yaani asilimia 53 walipendekeza umri wa kugombea urais upugunguzwe… siyo mimi ni wananchi.

"Tuangalie nchi zinazotuzunguka kiwango cha umri wa kugombea Urais, Kenya umri ni miaka 35, Uganda miaka 35, Rwanda, Burundi, Senegal, Mozambique, Zimbabwe ni miaka 35. Uingereza wao hawana hata umri. Mtu yoyote anayegombea ubunge anaweza kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza," alisema.

Zitto alionya kuwa ujana siyo sifa pekee ya kuutaka urais. Anaona zipo nyingine za kikatiba, kihaiba na za kijamii.

"Kama mna sifa mmezipanga, zote zipo pale. Sasa kama kuna kijana mwenye sifa, kwa nini azuiwe?" anahoji kwa ukali kidogo.

Hata hivyo, Zitto bado ana nia ya kushika nafasi hiyo ya juu nchini, akisema haoni mtu mwenye sifa zaidi yake.

Zitto alisema nia yake ya kugombea urais ni kutaka kukamilisha ndoto yake ambayo ni kuona kila Mtanzania anafaidika na rasimali zilizopo.

"Simwoni mwingine anayeweza kuiongoza nchi hii kwa sasa zaidi yangu. Nchi hii kwa sasa inahitaji mtu mwajibikaji hata kama jambo hilo litamletea madhara, mwenye uadilifu usio na shaka, anayeyajua matatizo ya wananchi na awe na uwezo wa kuwaunganisha Watanzania," alisema Zitto.

"Sina shaka na uwezo wangu na uzalengo wangu. Mfano nilipotoa hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu watu waliamini ni Chadema tu ndiyo watakaotia saini zao, lakini wapinzani wote walisaini na watano kutoka chama tawala."

Mapema mwaka huu, Zitto alivuliwa nyadhifa zake zote Chadema na mustakabali wake kwa sasa unasubiri uamuzi wa mahakama, hali ambayo inafanya uwezekano wa kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho kuwa mgumu.

Lakini hilo si tatizo kwake.

"Nategemea kuendelea kuifanya kazi ya siasa. Nitakuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa, lakini siyo CCM," alisema Zitto alipoulizwa atagombea urais kwa chama gani kutokana na hali kuwa tete kwake ndani ya Chadema.

Licha ya tuhuma nyingi kwamba alikuwa mbioni kujiunga na CCM, Zitto alisema hawezi kujiunga na chama hicho tawala kwa kuwa ndoto yake ni kuona demokrasia ya mfumo wa vyama vingi nchini inakua kwa kuuimarisha upinzani.

Alisisitiza kuwa ndoto yake ni kuona Tanzania ikiongozwa na Rais kutoka upinzani.

"Kama nikikosa nafasi ya kuwania urais, nitawapima waliopo na nitamfanyia kampeni ninayeona anafaa. Ninapenda kuona mgombea wa upinzani anashinda," alisema Zitto.
 
Tuamke sasa tuende kujenga uchumi wa nchi yetu.

Nikiwa napitia magazet asb hii, jana tuliona habar ya wapambe walimfitini mh.zitto kwa mh. mbowe ndani ya mwananchi, leo anasema hivi juu nimejaribu kupitia ndani habari hii ni muendelezo either wakujuta kwa mh huyu au kutoelewa maneno yake juu ya kuachana na ubunge nakwenda kufundisha.

Source: MWANANCHI FRONT PAGE.

wadandiaji wa siasa mtakoma mwaka huu, mbowe kujiunga na chama kingine cha upinzani endapo atakosa uenyekiti.
 
Tuamke sasa tuende kujenga uchumi wa nchi yetu.

Nikiwa napitia magazet asb hii, jana tuliona habar ya wapambe walimfitini mh.zitto kwa mh. mbowe ndani ya mwananchi, leo anasema hivi juu nimejaribu kupitia ndani habari hii ni muendelezo either wakujuta kwa mh huyu au kutoelewa maneno yake juu ya kuachana na ubunge nakwenda kufundisha.

Source: MWANANCHI FRONT PAGE.
Curiosity killed the cat!!
 
anachofannya zitto ni kujaribu ku spin uchaguzi wa chadema ili yeye awe ajenda na watu wasiwaze uchaguzi unaoendelea. huyu mtu haeleweki. kila baada ya saa moja anabadililka.
 
Back
Top Bottom