Zitto: Sijengwi na Kikwete, najijenga mwenyewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto: Sijengwi na Kikwete, najijenga mwenyewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lukolo, Jul 11, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Katika facebook wall yake, Zito Kabwe amelilaumu gazeti la Tanzania daima kwa kuandika habari inayohusu Zitto kujengwa na Kikwete. Binafsi sina shida na lawama alizolitupia gazeti, kwa kuwa kiuhalisia kwa kuandika hivyo kunawapotezea imani wapinzani dhidi ya Zitto. Hilo naungana naye kwa asilimia nyingi, kwamba Tanzania Daima haikupaswa kuandika hivyo.

  Lakini kilichonisikitisha ni kitenda cha Zitto kuweka hoja zake kwa kulihusisha gazeti la Tanzania Daima na Mbowe (mwenyekiti wa CHADEMA). Sidhani kama mhariri wa gazeti anapoihariri habari huwa anampelekea Mbowe aangalie kama habari hiyo inakubalika au haikubaliki. Kwahiyo sioni mantiki ya kuihusisha habari ile moja kwa moja na Mbowe. Na kwa namna nyingine naona kama kauli ya Zitto imelenga kuibua mgogoro mwingine na viongozi wenzake ndani ya chama.
  Nawasilisha.
   
 2. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  bwana mdogo analishwa sumu bila yeye kujua!!
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ila hapo hukumuelewa Zitto vizuri. Siyo kwamba Zitto anamshutumu Mbowe kutumia au kuachia gazeti lake limchafue. Zitto alicho kuwa anasema ni kwamba si mara ya kwanza gazeti hilo kufanya hivyo na Mbowe kama mmiliki ana nafasi ya kuwaambia wahariri wake waache kuandika yasiyo ya kweli haswa juu ya mwanachama mwenzake. Tatizo inaelekea kwamba nje ya chama Chadema ni wamoja ila ndani ya chama kuna power struggle kubwa sana imeanza kutokea.
   
 4. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #4
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Suali kujiuliza kabla ya kujadili hilo,je wamiliki wa vyombo vya habari kwenye nchi changa ama zilizodumaa kidemokrasia kama Tanzania wana influence kwa kile kinachoandikwa au kuripotiwa?
   
 5. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  dah jamani siasa za bongo ni kichwa cha mwendawazimu maana watu hawaeleweki ila kabwe ninachojua amewasaidia sana wanakasulu ktk harakati za maendeleo ya kijamii kama elimu na miundo mbinu ata kwa kujikomba lakini amefanikisha adhima ya kuleta maendeleo jambo ambalo ndyo maana halisi ya mbunge
   
 6. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Pale Tanzania Daima pana Banzi ndani ya jicho, bila kuishughulikia hiyo mapema watajikuta vipofu
   
 7. M

  Marytina JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Zitto anabomolewa na Kikwete!!!!
   
 8. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sijafurahia kitendo cha Zitto kusema eti 'anajijenga mwenyewe'; kwani kukua kwake kisiasa sio kama anajijenga au anajengwa na mtu. Of course atakuwa ana 'mikakati' anayotumia kutafuta njia ya kwenda juu; na hapaswi kutuambia kwamba kuna mikakati anayoitumia. Suala la kujivuna huwa linamuondoshea mtu utashi na charisma
   
 9. ARUSHA01

  ARUSHA01 Member

  #9
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Halafu kuna sub-heading eti MMOJA ANAMHARIBIA MWENZAKE kati ya Jk and Zito cjaelewa This means who is distructing who?
  Something big is coming 4 sure I sense!
  Kila EL anapogain power Zito comes out with backout picture it!
   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ben, hapa jibu linaweza kuwa Yes or no!! Siamini na sitaki kuamini kwamba kabla ya gazeti kutoka, mhariri wa gazeti analipeleka kwa mmiliki ili aone ni nini kimeandikwa. Though ninaamini kwamba mmiliki wa gazeti anao uwezo wa kumwagiza mhariri aandike kitu fulani. But kwa mhariri makini hatakubali kuandika iwapo anajua kinachoandikwa hakimtendei haki mtu fulani.

  Lakini nikigeukia katika kile ambacho Zitto amekiandika, ninafikiri kwamba kabla ya kukiweka kwenye public, angeweza kumpigia simu Mbowe na kumweleza dukuduku yake. Sasa kuondoka na kwenda kumshitaki mwenyekiti wako kwa wananchi kwamba yeye ni tatizo, ndipo tatizo linapoanzia. Na kwa kuzingatia miiko ya uongozi, hapo Zitto ni tatizo, akubali akatae, na hapo ninapata wasiwasi kama anafaa kushika nafasi ya juu ya uongozi katika nchi kama hawezi kureconcile na watu wake ndani ya system.

  Zitto kama kiongozi anayo nafasi ya kujadiliana na viongozi wenzake kwa namna nyingi, na ninafahamu fika kwamba Zitto na Kibanda (mhariri wa Tz Daima) ni watu wa karibu. Kwa nini wasiyamalize huko? On the other hand, wakati Zitto leo analishutumu gazeti la Tz Daima pamoja na Mbowe, amesahau kwamba gazeti hilohilo limetumika sana kumjenga Zitto siku za huko nyuma kabla hajaamua kuanzisha ligi na Mbowe.

  Binafsi namshauri Zito afuate miiko ya uongozi na ajaribu sana kumaliza tofauti za chama ndani ya chama. Haya anayoyafanya, yanamjengea umaarufu kwa kundi fulani la watu lakini yanamshusha sana kwa kundi lingine la watu.
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Una maana gani?
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Inategemea na msimamo wa mhariri. Kuna baadhi ya vyombo hapa nchini vuinaandika habari kwa matakwa ya mwenye mali. lakini wapo baadhi ya wahariri ambao hawakubaliani na hali kama hiyo na ni nadra sana kuwakuta wakifanya kazi katika vyombo vya aina hiyo. Mara nyingi wahariri hao, kama hawafanyo kazi zao binafsi, basi wanakuwa wameajiriwa na magazeti ambayo wamiliki wake wanatoa uhuru kamili kwa mhariri kufanya kazi zake kwa mujibu wa taaluma yake
   
 13. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Mtapinga weeeeeeeeeeeeeeeeeeee lakini Zitto ni tatizo ndani ya Chadema. Wether Tanzania Daima litamwandikaje lakini Zitto ni tatizo kubwa. Mbona yeye Zitto amewanunua waandishi wa Mwananchi wanamsifia hata pale asipopaswa kusifiwa? Kama yeye Zitto ana busara na anaona gazeti limemharibia anashindwa nini kuwaambia viongozi wenzie ndani ya chama kuwa anachotendewa si haki? Zitto anabore sana
   
 14. Bollo Yang

  Bollo Yang JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 440
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Chuki ya akina Mbowe dhidi ya Zitto inazidi kujidhihirisha! Kweli mwisho wa ubaya ni aibu!
   
 15. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  rostam aziz anapelekaga story za kuwachafua wapinzani wake kwenye magazeti yake,na inasemekana kabla ya kuchapishwa anaipitia tena kujiridhisha haiawa sugarcoated....this is what i hear,the street is talking
   
 16. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #16
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Je,waliwasiliana na Zitto kupata maoni yake kabla hawajachapisha?Je,jamii imetendewa haki?Je, Zitto ametendewa haki?

  Kama hawakufanya hivyo,huo uwezo wa kuandika heading na subheading zenye mwelekeo huo zinatoa taswira gani?Hebu tujaribu kuwa analytical kidogo
   
 17. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #17
  Jul 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Zito kaka yangu usha nunuliwa na mafisadi hata umeachia nafasi yako bungeni ile tuliyokuwa tumekuzoea kuwa questionable..

  Mafisadi wananguvu chini ya anga kinoma!
   
 18. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #18
  Jul 11, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Binafsi sijaisoma habari ya Tz Daima na wala hayo malalamiko ya Mh Zitto. Lakini kwani suala la kujengwa (au kubomolewa for that matter) kisiasa ni voluntary kwa kiasi gani? Kama mtu anakufanyia vitu fulani (ambavyo unavikubali) na vitu hivyo vinakupa/kuongezea credentials (political or politically), then suala 'kujengwa' (public opinion) naamini linakuwa involuntary kwa muhusika.

  Btw, tatizo hapa ni 'kujengwa' (vs kujijenga) au ni nani anakujenga (in this case JK, a CCM Chairman)? Yaani kama ingeandikwa kwa mfano, Mh Mbowe anamjenga Mh Zitto, bado lingekuwa ni Tatizo?
   
 19. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #19
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Good! Kulingana na mfululizo wa aina ya uandishi Je,unaamini ndani ya Gazeti la Tanzania Daima kuna aina hiyo ya waandishi na wahariri wa aina hiyo?
   
 20. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #20
  Jul 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Zitto alishalalamikia suala hilo hapa JF na kusema kuwa Mbowe anajua. Hakufafanua kuwa walizungumza nae makhsusi au alijuaje.

  Lakini gazeti linalomilikiwa na mwentekiti Wa chama linaonekana kuwa credible kwenye mambo yake inayowahusu wanachama hata kama hakuna ukweli huo.

  Ikiwa Zitto ameshajadiliana na Mbowe lkn hakuna hatua zilizochukuliwa, kutakuwa na tatizo kubwa na labda ameshindwa njia za kutatua hilo na akaona awaachie wananchi
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...