Nimesoma kwa makini sana post ya Mh. Lema iliyosema "Unafiki wa Zitto Kabwe na suala la posho" pia nimesoma kwa makini majibu ya Mh. Zitto yaliyowekwa na JF nikagundua Zitto amejibu hoja 1 tu kati ya hoja/tuhuma 3 za msingi za Mh. Lema kama ifuatavyo; 1. Kukataa kupokea posho ndogo ya bunge wakati huohuo anachukua posho kubwa ya vikao katika mashirika. 2. Msimamo/hoja ya kukataa posho haikuwa yake bali ni maamuzi ya kambi rasmi ya upinzani (walijadili pamoja). 3. Anatumia vyombo vya habari kupotosha ukweli na kutafuta sifa ambazo kimsingi hana".
Namwomba Mh. Zitto atoe ufafanuzi kama msimamo wa kukataa posho ulikuwa wake binafsi au wa chama kama Lema alivyo mtuhumu? kama ni hoja ya chama kwanini alijitokeza kutoa hoja kama yake binafsi?, Je ni kweli anatumia media kutafuta sifa; nawasilisha.