Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

Status
Not open for further replies.
Duh mbona kakuingia kichwani mno?
utaweza pata usingizi kweli?

huwezi kum ignore?
 
Duh mbona kakuingia kichwani mno?
utaweza pata usingizi kweli?

huwezi kum ignore?

Nadhani hukustahili hii thread..utakuwa umekosea njia.Jiulize kwanini Zitto awachukie waliomzidi na si kujifunza walivyofika hapo ,akiwafikia ndipo afikiri kudhindana nao.
 
Mkuu unamaanisha peter selukamba? maana ujaweka bayana maswali ni mengi juu ya uzi wako!

HUyo mbunge badala ya kuwaambia wana kigoma kajifunza nini kwa wengine ili nao wajikwamue km wenzao..anakwenda waambia jinsi alivyopambana na kuwafanya maadui.

Hembu jiulize wachaga wangekuwa wanauza mbinu zilizowafikisha hapo..Zitto si ndio angeshindwa kabisa kuwa sehmu yao, na kigoma angekuwa manaharakati zaidi ya kiongozi....badala ya kuwaongoza wenzake kwa alichojifunza anawaongoza kuchukia na kupigana na walio mbali.
 
hii inanikumbusha akina karamagi,chenge,lowasa,ngeleja walivyotimuliwa walipokelewa kwa mbwembwe kwelikweli lakini leo hii wako wapi.
 
ZZK unaleta ukabila Tanzania ?

Tukueleweje, wachagga wamekukosea nini ?

ni vema ukawaombe msamaha wachagga. Hujawatendea haki.
 
Hawa watu ni wengi na nadhani wamempa nguvu ya kuamini kwamba hata akitoka CDM bado anaweza kwenda chama chochote na akapata support ya kutosha kumwezesha kuwa mbunge.
 
Ukiweka ukabila na udini huwezi kujifunza kitu. Angalia waislam walioenda kusoma seminari za kikristu na wale wa dini moja. Wamchanganyiko ni rahisi kuchangamana na wenzake
 
Huyu jamaa sasa,, kashajiandaa liwalo na liwe.. na hadi anafanya haya yote... kashaona hana chake tena chadema, na naona chadema wametumia akili sana kukaa kimya baada ya siku 14, na hapa naamini huenda hata hii ziara imeandaliwa na makao makuu bila hata zitto kujua lengo likiwa ni kuzidi kupima busara zake.. haiwezekani leo ndio ufanye mikutano ya aina hii isyo na itikadi za chama chako huku sisiemu wakiiratibu.. hajawahi kufanya hivi.. hana bendela ya chama,.. anakisema chama chaee vibaya.. hana uvumilivu wala staha.. naona kamati kuu haitamuacha..

mimi nadhani namshauri ushauri wa bure atangaze kujitoa tu rasmi chadema mapemaa aungane na wakina kafulila, muhamed rashid, wakina kaburu etc waunde chama chao wao si wanaamini wanaushawishi na chadema hakina ushawishi Chama cha kikanda na kikabila...

LAKINI NAUONA MWISHO MBAYA KABISA WA KISIASA KWA KIJANA HUYU HADI MWAKANI MWEZI KAMA HUU SIJUI KAMA ATAKUWA NA CHA MAANA TENA... JULIUS MALEMA ALIKUWA MASHUHURI KWELI ANC NA VIJANA WALIMPENDA HASWAA LEO YUKO WAPI?? ETI WATU WANAMFANNANISHA HUYU NA MANDELA KWELI?? MANDELA NI LINI ALIWAHI KUKISEMA VIBAYA CHAMA CHAKE, ZITTO AMEPATA MISUKOSUKO GANI YA POLISI AU JESHI, MANDELA HAKUWAHI KUWA NA MIKAKATI YA SIRI DHIDI YA VIONGOZI WAKE, ALIIKUTA ANC NA KAICHA.... HESHIMA NA BUSARA NI VITU MUHIMU SANA KATIKA MAISHA HAYA.... WANAOKUSIFIA LEO KESHO HATA SALAMU HAWAKUPI WAKISHAKUONA UMETEPETA KAMA MKATE WA BOFLO KWENYE CHAI.
 
Zitto na lowassa ni zaidi ya vyama vyao, hawa mabwana wakiungana wakaingia sehemu kama nccr hivi, hii nchi, mikoa, wilaya na viunga vyake vitachimbika nasema.

Duu!! Sasa hivi tena kwa Lowassa, huchoki kutumiwa namna hiyo au ndiyo starehe kwako??
 
Zitto hajengi chama anabomoa chama hafai kabisa
[h=5]Zitto Kabwe
[/h]Nitapambana kutetea uanachama wangu.

Kwa upinzani ni lazima tufanye tofauti na CCM. Tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma kwa upinzani ni mbaya zaidi kuliko. Hivyo uwajibikaji kwa wote bila kujali vyama. Uwajibikaji sio msamiati kwa watawala tu bali kwa viongozi wote. Namna tunavyotaka nchi iendeshwe ndivyo hivyo tuendeshe vyama vyetu. Tuhuma dhidi ya Kiongozi wa Upinzani kuhusu masuala ya uadilifu zinapaswa kuhukumiwa kwa namna ile ile wanayohukumiwa watawala.
Ninarudia kuwaambia ndugu zangu kwamba sitoki CHADEMA. Chama kina jasho langu na nitapambana mpaka dakika ya mwisho kutetea haki ya uanachama wangu.
Mimi ni CHADEMA toka ujana. Niliingia CHADEMA kwa kuchagua na sio wengine walioingia kwa Mazingira Ya kupata fursa za kugombea. Wengine wangepitishwa na chama walichokuwa kuwa wagombea Leo wasingekuwa upinzani na inawezekana wangekuwa mawaziri mizigo au waendesha operesheni tokomeza!

usemayo kweli mkuu naona kaanza ligi tu .. muda utatuambia.. sidhani kama atabaki maana hata shonza nae alsema bado ni makamu mwenyekiti bavicha.. ngoja tuone...
 
Zitto has nothing to loose,wakimfukuza uanachama,anakwenda mahakamani,mpaka 2015,anaingia chama kingine halafu anagombea,CHADEMA WATAPOTEZA MAJIMBO MENGI SANA 2015
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom