Zitto: Serikali ya JK katika hali mbaya kifedha; Mkulo Akanusha!

hii hoja haina mantiki yoyote kwa maana hii nchi imekwishatawaliwa na marais wanne na kili mmoja wao hakuna hata mmoja aliyeweza kuondoa kero za watanzania wote Kwa hiyo mnachosema kuhusu jk ni kama mnamuonea tu na hasa baada ya huyu rusputini wenu kukosa urais

Aise we ni makupa wa GRM au?mana siamini unaweza ongea huu upupu
 
Haraka haraka napendekeza tuwafute wabunge viti maalum,tukomboe zile pesa za mishahara na marupurupu pia magari yao tuyapige mnada,tupunguze wizara ziwe20,
 
Hachana na hizo propaganda za kitoto kabisa katika kila FISCAL YEAR kuna BUDGET ya kukidhi mambo yote uliyoainisha. Acha uwongo wa mchana mchana.
 
Mkuu mawazo yako mazuri but nani anajali washakuambia wanaishi kimjinimjini unategemea nini? Hizo project za flyovers ni Twin tower nyengine kutengeneza mianya ya ufisadi. Kilimo badala ya kuwasaidia wakulima wanapeana tenda wao kwa wao kuleta matrekta mabovu ya powertillers ambayo kabla ya kuanza kutumika yashakufa. Kilimo kwanza mikopo wamechukua watu wasiojulikana ambao si wakulima hata hivyo wakulima wenyewe wameachwa wakifa na njaa tu. Ndio maana sasa ukiangalia wakulima kama Mbeya wameamua kuuza mazao yao Zambia na Malawi kwani wanafaidika zaidi na nchi kwao.

Rais wetu anasema maendeleo ni kuwa na magari amesahau kuwa wakati wenzetu Kenya wameleta viwanda vya kuassemble magari ili kutoa kazi kwa watu wao sisi tunajivunia magari mengi yaliyozagaa nchi ambayo ni second hand. Rais wetu anatakiwa asimame kidete kuondoa tatizo la umeme amasivyo uchumi wa nchi utaporomoka vibaya sana. Vile vile ampumzishe waziri wa fedha kwani hana ufanisi wa kuanisha vyanzo vipya vya hela zaidi ya kutoa majibu ya kisiasa na kuendelea kula bata yeye na watu wake wa karibu. Asipofanya hilo makusanyo ya kodi yataporomoka kila siku. TRA inahitaji kubadilishwa uongozi mzima wa juu kuzuia mianya ya uepukaji kodi na rushwa.

Vile vile JK apunguze gharama za kuendesha serikali yake ambazo zimekuwa mzigo kwa Serikali na pia Bunge lipunguzwe ukubwa kuanzia wafutilie mbali ubunge wa viti maalum ni mzigo mkubwa kwa taifa. Pia marupurupu yapungue kusave pesa kwa ajili ya kuipunguzia mzigo serikali.

Venginevyo nchi hii inauzwa tu mabenki hayo serikali inapokopa interest rate Tanzania iko kati ya 17%- 26% . Fikiria serikali ikikopa Bilioni 500 tukisema Tbills rate sasa iko 9-10% kama sijakosea inamaanisha interest rate ya Billioni 500 ni Billioni 50 - 40 kwa mwaka na inaenda ikikua. Tuombe mungu wasiwe wamechukua overdraft facility ndio kiama kabisa maana deni linakuwa kwa siku. Mwisho nchi itashindwa kulipa deni tutaanza kuuza rasilimali za nchi. Mungu ibariki Tanzania!!!


Mkuu,
Ni kweli unachokiongea na hatua za mwanzo ndo hizo ulizozianisha. Lakini pia serikali lazima iwe na kitu anacho export hata kwa nchi zinazotuzunguka.

Nafikiri, badala yakuwapa wakulima mikopo, serikali yenyewe i-organize project kama 10. Walime na wamwagilie.

Nchi za wenzetu kilimo kimekabidhiwa watu wa uhakika wa kulima sio kila mtu ajilimie tu kwa ka trekta ka mchina ama ng'ombe pilau.

Nanichosema na kuona serikali haiwezi jiendesha kama inategemea kodi ya ndani tu hata ukiikusanya kwa 100%.
 
Kukopa sio dhambi, tatizo ni kama hutarudisha ulichokopa!!!! hata Bill Gates wanakopa! we vipi? nafikiri umefika wakati mada kama hizi zitolewe mapema zinatupotezea muda! IVISIBLE UPO WAPI...au wewe ni CDM pia?
 
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alidai kuwa hali hiyo mbaya fedha kwa Serikali imesababisha watumishi wake pamoja na wabunge kutolipwa mishahara hadi jana Mei 7, 2011.

Akizungumza na wananchi Vwawa katika Jimboni Mbozi Mashariki katika viwanja ya ofisi ya Afisa Mtendaji, Zitto alisema Serikali sasa inatafuta fedha za kuwalipa watumishi wake mishahara ya mwezi Aprili.


"Hata sehemu ya posho za wabunge mkutano uliopita, zikiwemo za kugharamia mafuta ya safari za wabunge majimboni bado hazijalipwa kutokana na Serikali kukosa fedha," alidai Zitto.


Alisema kutokana na hali hiyo Serikali imekwenda kukopa
Sh540 bilioni kutoka benki za ndani ili watu wasijue kuwa inakabiliwa na ukata.

"Serikali haikopi fedha ili ijenge bandari, viwanda au kugharamia miradi ya maendeleo,
bali inakopa ili ilipe mishahara ya wafanyakazi," alisema Zitto.

Angalizo:
Kama ndio mwaka wa kwanza tu mambo yamekuwa hivi, ikifika 2014 itakuwaje? Na kama haina hata hela za kulipa mishahara tu je hiyo miradi itawezekana kweli?

hali ni mbaya najua hata wizara na tasisi zote za serikali tangu januari anu decemba ziliambiwa kukata bajeti zao kwa zaidi ya 40%. Kweli inasikitisha sana pesa zote zilikombwa kupelekwa kwenye uchaguzi bila idhini ya bunge
 
Kwenye Mei Mos JK aliiweka kapuni hii inshu ya nyongeza za mishahara.... I think this is the secret behind!!

Mi hamu yangu kubwa ni kuona wafanyakazi wanagoma!!yaani ikitokea hili, maisha yatabadilika kwa kasi sana!!

I can't wait for this... nadhani mliona SA ilivyokuwa! Mgomo wa wafanyakzi ndio mpango nzima
Wafanyakazi kugoma!! hapana, watatishiwa virungu vya polisi na watashuriwa kuwa mbayuwayu aliyekataa ushauri wa kong'ota na akachanganya na za kwake.
 
Walishaandika barua mara mbili za kuomba pesa toka kwa nchi wafadhili ili kuweza kuendesha Serikali kati ya January - June 2011, inaelekea Wafadhili wamewatolea nje. Walikomba pesa zote hazina kwenda kufanyia kampeni za 2010.
Kuna taifa moja la EU linaloongozwa na lib democracy lilifuatwa likagoma kwa kuwa lilituhumiwa na ccm kuwasaidia cdm, ilibidi serikali iingie kwenye mabenki ya biashara kukopa:phone:
 
Kuna taifa moja la EU linaloongozwa na lib democracy lilifuatwa likagoma kwa kuwa lilituhumiwa na ccm kuwasaidia cdm, ilibidi serikali iingie kwenye mabenki ya biashara kukopa:phone:

Hii nafikiri ni radio mbao, nchi za EU uchumi wao kwa sasa sio mzuri, hakuna kazi maisha yako juu na serikali wanajaribu kukabiliana lakini wapi. Hali ni ngumu EU.
 
Huo ndio ukweli wafanyakazi wengi wamelipwa baada ya tarehe 4 Mei mishahara ya mwezi April. kweli serikali imekwama baada ya matumizi mengi mabaya, kuwakopesha wabunge, kulipia safari za mkulu nje zisizo na tija, kuanzisha mikoa 4 na wilaya kibao bila sababu ya msingi, na hata kulipia mafiuta ya mitambo ya IPTL wakati kuna hela zimewekwa tu zinzsubiri uamuzi wa mahakama. kweli kazi tunayo JK !
 
Nimepita kwenye pub moja hapa MBEYA na kuliona gari lenye namba.....SU_ _ _ _.Kwa matumizi haya mabaya ya mali za umma yakiwemo magari hazina lazima ikauke tu
 
kukopa sio dhambi, tatizo ni kama hutarudisha ulichokopa!!!! Hata bill gates wanakopa! We vipi? Nafikiri umefika wakati mada kama hizi zitolewe mapema zinatupotezea muda! Ivisible upo wapi...au wewe ni cdm pia?




hivi bill gates anakopa ILI akuze mtaji microsoft?au ili anunue gari ya kutembelea!ni hatari kukopa kwa ajili ya matumizi ya kawaida we kilaza
 
Twafa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Utakufa peke yako sisi wengine hii ndiyo opportunity ya kusiamama tuhesabiwe na kuweka legacy zetu! Uchumi kazana ku poromoka ili wananchi ustaarabu uishe walazimishe wang'ang'anizi ku surrender tuonyeshe njia!
 
Halafu tunashangaa riba kuwa juu angali biashara zote, kubwa na ndogo wanashinda na serikali kukopa kwenye mabenki ya ndani.

Baadaye tunambiwa kuna mpango kamambe wa kufufua uchumi na kuleta maendeleo na ajira. Wenye kujua tunaelewa hilo haliwezekani, kwani ni vigumu kupata mikopo ya biashara (1) fedha serikali imekopa kulipa mishahara, fedha chache ndio inayobaki katika mabenki (2) kama ukipewa mkopo inabidi uwe ghali sana, kwani serikali wanakopa katika riba kubwa. That is totally, the demand and supply equation wala sio mazingaombwe.

Halafu baadaye kuna binadamu atakuja na ukweli ulio wazi "at raisi ni mchumi (amesoma), asiyeujua uchumi". Utawasikia akina magamba humu, mara aaaaah, mara ooooh, kama walivyotumwa.

Kuendesha nchi sio kama kucheza kiduku, immeshidwa.

Punguza ukali Ndugu Utakuja ambiwa wewe sio Raia au mdini unataka kuleta machafuko na mwisho Mhaini..
 
Ahaaaaaaa,...
kumbe ndo maana wanavyuo wana cheleweshewa hela kwa
ngonjera za system haifanyi kazi vizuri eh?

sijui week ijayo itakuaje vyuoni
Watachuna magamba yaliyobaki, kisingizio kitakuwa ni CDM kuchochea kumbe ni yenyewe serikali inajikaanga kwa mafuta yake. Hivi mpaka leo baadhi ya watumishi hawajalipwa fedha ya mishahara hii ni aibu ya mwaka. JK alishawahi kutoa kauli ya kisiasa kuhusu kupata mishahara kila tarehe 25 ya kila mwezi lakini sasa hali imekuwa kinyume. Ben Mkapa alimpa kiburi sana JK kipindi anachukua nchi kutokana na hazina aliyoikuta, saizi ni aibu kwa yeye.
 
hii hoja haina mantiki yoyote kwa maana hii nchi imekwishatawaliwa na marais wanne na kili mmoja wao hakuna hata mmoja aliyeweza kuondoa kero za watanzania wote Kwa hiyo mnachosema kuhusu jk ni kama mnamuonea tu na hasa baada ya huyu rusputini wenu kukosa urais
Watu wa system utawajua, yaani majibu yao ya kejeli, dharau tupu kwa sababu yeye ana ahueni kasahau ndugu zake wanakula vumbi tu kijijini! Yanayojiri saizi hata kama CDM ingekuwa madarakani au CUF nisingekosa kulalamika. Hadi mishahara mkakope hiyo nchi maendeleo yatakuja lini halafu unachekea wawekezaji wakikwapua rasilimali hivi hivi, mikataba feki mingi tu inayotuangamiza miaka na miaka kisa eti 10% na ubinafsi kama dunia ndiyo mwisho yaani hakuna kufa.
 
Mbona hayo matatizo hata nyerere aliyapitia.
Kwa hiyo hicho ndicho kigezo, baba yako akioa wake kumi, nawe ukioa wake wengi utaona umefuata nyayo za baba yako hata kama alipotoka? Halafu Nyerere naweza kumtetea alipigana vita ambayo ilichukua rasilimali nyingi kidogo, sasa JK anapigana vita gani inayokausha hazina?
 
Back
Top Bottom