Zitto: Serikali ya JK katika hali mbaya kifedha; Mkulo Akanusha!

hivi ndugu yangu unajua Urais au kuwa kiongozi wa nchi unatakiwa kuwa makini na kuwasoma wale walio chini yako na sio kulea watu kwani utavuna mabua kaka. kweli jamani hali ni mbaya na tumwombe mungu atusaidie si kwa mabaya ila ainusuru nchi yetu.
 
habari za kweli zisizo na chembe ya uzushi ni kwamba sirikali ya mtu wa bagamoyo imetembeza bakuli kwenye mashirika ya umma kuomba pesa kwa ajili ya kuendeshea kile kinachoitwa semina-elekezi. hali ni mbaya, na anko zito hakuropoka alipotamka pasipokung'ata maneno aliposema sirikali imeshindwa kulipa mishahara ya watumishi wake.

swali, jeeeeeeeeeeeeeee?

bwana dokta wilbroad peter slaa angekuwa Ikulu angezuia vipi hali hii ama ageepukaje aibu hii?

tafuata hotuba zake wakat wa kampen,mojawapo alisema ni kubana matumizi ya serikal mfano magar ya kifahar,kufuta wakuu mkoa wilaya,kuangalia raslimal za nchi ili ziinufaishe.mfano mkulo anakusanja 4 anatumia 2.95 mishahara,je kibakicho chaweza tosha huduma nyingine?mfano mikopo vyuon,safar za kuzura za kiserikal.Haina haja Dr Slaa kulitolea maelezo.
 
Angeenda Vatican

Kwani Vatcan na hali mbaya ya Serikali kifedha vina uhusiano gani? Sasa kama ni kukimbilia kwa Dr Slaa huko nafikiri karibia tutasikia ****** anaenda Mecca au Madinna. Fikiri kabla ya kutenda kama utashindwa kutatua matatizo yako kwa kufikili walio na imani fulani wana sehemu ya kukimbilia pindipo nchi ikiwa na matatizo, Ni hatari tena hatari kubwa sana.
 
Total crap!! Sio lazima kila mtu apost thread wengine m' baki kuwa wachangiaji.
 
Dr. asingeweza kufika katika hali hiyo,ila kama angeikuta hali hiyo angewasaka wote walioiba fedha na kuzitumia kwenye uchaguzi badala ya maendeleo ya wananchi.
 
u
habari za kweli zisizo na chembe ya uzushi ni kwamba sirikali ya mtu wa bagamoyo imetembeza bakuli kwenye mashirika ya umma kuomba pesa kwa ajili ya kuendeshea kile kinachoitwa semina-elekezi. hali ni mbaya, na anko zito hakuropoka alipotamka pasipokung'ata maneno aliposema sirikali imeshindwa kulipa mishahara ya watumishi wake.

swali, jeeeeeeeeeeeeeee?

bwana dokta wilbroad peter slaa angekuwa Ikulu angezuia vipi hali hii ama ageepukaje aibu hii?[/QUOTE

Huwa unatumia Lubisi ama chang'aa?
 
Subiri Budget mbadala anayoiandaa Zitto Kabwe utapata jibu, Urais ni Taasisi sio mtu mmoja. Ukichagua wasaidizi wako kizawadizawadi matokeo yake ndiyo haya. JKN alishasema Ikulu sio mahali pa kufanyia biashara. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.

Short an clear...ujumbe umefika!!
 
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alidai kuwa hali hiyo mbaya fedha kwa Serikali imesababisha watumishi wake pamoja na wabunge kutolipwa mishahara hadi jana Mei 7, 2011.

Akizungumza na wananchi Vwawa katika Jimboni Mbozi Mashariki katika viwanja ya ofisi ya Afisa Mtendaji, Zitto alisema Serikali sasa inatafuta fedha za kuwalipa watumishi wake mishahara ya mwezi Aprili.

"Hata sehemu ya posho za wabunge mkutano uliopita, zikiwemo za kugharamia mafuta ya safari za wabunge majimboni bado hazijalipwa kutokana na Serikali kukosa fedha," alidai Zitto.

Alisema kutokana na hali hiyo Serikali imekwenda kukopa
Sh540 bilioni kutoka benki za ndani ili watu wasijue kuwa inakabiliwa na ukata.

"Serikali haikopi fedha ili ijenge bandari, viwanda au kugharamia miradi ya maendeleo,
bali inakopa ili ilipe mishahara ya wafanyakazi," alisema Zitto.

Angalizo:
Kama ndio mwaka wa kwanza tu mambo yamekuwa hivi, ikifika 2014 itakuwaje? Na kama haina hata hela za kulipa mishahara tu je hiyo miradi itawezekana kweli?
Kutoka Maktaba ya Mkoa Kigoma.
 
Kutoka Maktaba ya Mkoa Kigoma.
Aaah aah! Asante kwa kufukua hili kaburi.
Ukisoma comments za watu humu ndiyo utajua Nani hasa ni mnafiki!

Vijana wengi wa JF wanaona Kama fashion kukosoa mambo bila kujiridhisha. Awatumii akili zao Bali wanacheza ngoma za wanasiasa bila kujijua! Wanasiasa wana agenda yao, ya kushika madaraka siyo kukuletea maendeleo.

Kelele zoote mlizopiga kwenye uzi huu Magu kazifanyia kikamilifu, Zitto anaendelea kula matapishi yake!
 
@Zitto
 
Back
Top Bottom