Zitto: Serikali ya JK katika hali mbaya kifedha; Mkulo Akanusha!



"Serikali haikopi fedha ili ijenge bandari, viwanda au kugharamia miradi ya maendeleo,
bali inakopa ili ilipe mishahara ya wafanyakazi,"


kaka zitto nilikuambia (nilipokuwa natumia akaunti ya Jerusalem, kabla sijapigwa ban) kuwa anko JK ni msanii. Amewaahidi wanakigoma Paradiso a.k.a Dubai ya Tanzania, kumbe hawezi hata kulipa mishahara!? Looooooooo!

Zitto wewe ni mwanamapinduzi. Kama kuna tatizo ndani ya chama chetu yamalizeni kiutu uzima muendeleze mapambano. ni aibu kwa kijana smart kama wewe kusaliti mapambano muliyoyaanzisha na wenzako.

Wamarekani wamemtafuta Usama kwa miaka kumi. Ndani ya mapambano kulikuwa na friendly-fire kibao, lakini hatimaye wamefanikiwa kummaliza.

CCM must go!!

Achana na huyo laghai wa Bagamoyo.
 
kazi njema CDM, ahsanteni kwa kuleta uamsho kwa wananchi Wadanganyika. Go go! go! go! gooooo Chadema our saviour.
 
hali halisi inaonyesha kwamba uchumi wa tanzania unaangukia mikononi mwa mchumi. Mishahara hailipiki, kodi inadorora, waalimu hawana future, askari rushwa mtindo mmoja

hali halisi inaonyesha kwamba uchumi wa tanzania unaangukia mikononi mwa mchumi.
kusoma uchumi siyo kigezo cha kuitwa mchumi.

Mishahara hailipiki,
atalipaje wakati anategemea misaada, na watoa misaada walishatonywa kuwa alichakachua?

kodi inadorora,
mgawo wa umeme kila leo unategemea wenye viwanda watapata wapi bidhaa za kuuza hata waweze kulipa hiyo corporate tax?

waalimu hawana future,
hao wanajitakia wenyewe. acha maisha yawacharaze. ndiyo wanatumika sana kuweka serikali feki madarakani kwa ujira wa 30 000 kipindi cha uchaguzi. tena hao natamani wawe omba-omba tu.

askari rushwa mtindo mmoja
makamanda sina noma nao. kila mtu na ale kwa urefu wa kamba yake. serikali badala ya kupanua barabara kama mandela road yenyewe imejenga bonge la mtaro ambalo ni useless. sasa mtu akatanua hapo kwa nini askari wasimgeuze dili?
 
hali halisi inaonyesha kwamba uchumi wa tanzania unaangukia mikononi mwa mchumi. Mishahara hailipiki, kodi inadorora, waalimu hawana future, askari rushwa mtindo mmoja
acheni kumwonea jemedari wetu mheshimiwa kikwete matatizo yaliyopo aliyakuta na atamaliza muda wake nyie endeleeni kupiga domo tu
 
Vpi mwajiri mkuu mwaka huu anaweza kuajiri ama vjana wajiandae kukaa vijiweni?vpi wanavyuo wapya sept wataweza kupewa mikopo wote ama itakuwaje??....hakika katiba na muungano vitahtimisha utawala wa huyu msanii wa Bantu group

kuna law moja inasema hivi;If something can go wrong possibly,it will go wrong.

kuna msemo mmo wa kihaya unasema hivi;Alafa.. omubona

tutafakari pamoja!
 
kwa hiyo wewe Makupa unaona mambo yanaenda vizuri tu kwako, au unapinga tu ili uonekane na wewe upo? Kama nchi imemshinda tumpe mtu mwingine kama vp, hata huyo unaemsema kama vp tujaribu kumpa.
 
jk bwana yaani hana tofauti na yule mc maarufu wa dar ambae pia ni mtangazaji.....akilizao ziko sawa
 
Ni kweli lakini hawajalipwa mishahara yao? lakini na hii akili ya kutegemea kodi kundesha nchi.mhhh
 
Kuongoza nchi si sawa na kupiga soga vijiweni ambapo issue kubwa ni kufurahishana. We don't have a serious President, and our past mistake for electing him should save as a lesson tu us all.
 
hali halisi inaonyesha kwamba uchumi wa tanzania unaangukia mikononi mwa mchumi. Mishahara hailipiki, kodi inadorora, waalimu hawana future, askari rushwa mtindo mmoja

wewe upo katika kundi gani? kuhusu JK kushindwa sasa unaonaje uchukue wewe?
 
Lakini sasa ndio tujifunze jinsi ya kuchanganua mbivu na mbichi, kama vile naiona miradi yote ya maendeleo itakavyokwama!!!

hatukuwachagua hawa. waliteuliwa na tume ya uchaguzi kwa uangalizi wa mashushushu. watz tulilijua hili ndo maana tuliwakataa. inasikitisha sisi hao hao tunaumizwa na watu ambao hatukuwataka
 
Hivi Malaria Sugu yupo wapi pamoja na wenzake waje wajibu hii hoja!!!?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom