Zitto: Nitagombea Ubunge 2010

Zitto: Nitagombea Ubunge 2010

Watu mnachuki binafsi na Zitto mmmh!

zitto HANA LOLOTE LA MAANA!he is full of politics!hamna kitu kabisa,ngoja amalizie zile mil 100 za RA halafu tuone.........
 
zitto HANA LOLOTE LA MAANA!he is full of politics!hamna kitu kabisa,ngoja amalizie zile mil 100 za RA halafu tuone.........

Duuh! Wapiga kura wataamua kama ana/hana kitu kabisa. Uki-substantiate
allegations zako, watu watakusapoti zaidi lakini zikiendelea kuwa base-less basi na wewe utakuwa unafanya politicking.
 
Kwa mawazo yenu ya harakaharaka mlifikiri Zitto anaweza kuachia ulaji ule 'kihovyohovyo tuu'Zitto lazima awepo na kutia uzito pale mjengoni,hongera kijana.
 
...ntarudia tena na tena: "sijapata kuona binadamu wanaogombea nafasi za uongozi ili wawatumikiye wananchi,bado kuona."
 
Kama kweli Kulikoni waliandika kuwa Zitto atagombea "Jimboni mwake" (wakimaanisha Kigoma Kaskazini) basi watakuwa wamekosea, si huko tena! Lakini, muda muafaka ukifika atakuja 'mwenyewe' ndani ya JF kuwafahamisha ni Jimbo gani atagombea na sababu hasa za maamuzi yake.

Anataka jimbo la Ubungo lakini bado Mnyika nae analitaka
 
Yah!!! Zitto Kabwe ni mbunge chipikizi ambaye ametoa wa kuigwa Bungeni kushinda wale wabunge vikongwe ambao wanatumia nafasi yao Bungeni kuuchapa usingizi na kushtushwa na makofi ya kinafiki. Cha msingi kama Zitto umeamua kugombea tena 2010 ni vema ukafanya hivyo kwa jimbo lako la Kigoma na si vinginevyo. Ukiamua hasa kurudi majimbo ya Dar au kwingineko utaanguka vibaya sana Kisiasa tena kwa kishindo. Kama kuna mtu anakushauri ugombee Dar huyo atakuwa ametumwa purposely kukumaliza kisiasa, na itakuwa ni furaha na kicheko kwa mafisadi na vibaraka wao. Be very carefully and stand on your decisions, avoid influences. However, keep it up!!! In comparison, you have done it.
 
Kijana unatakiwa kuwa na msimamo, kama ulikujua hujui wengi wa vijana wanakuona wewe kama role model wao sasa kama hueleweki misimamo yako unataka kujenga taswira gani? Mi nafikiri ugombee usigombee ni vema ukakaa kimya ili upime upepo. Kuna usemi wa kizungu husema "Silence is the best weapon" adui yako hupata shida sana unapokuwa kimya au asipojua nia yako. Kwa mtindo unaoenda nao...sijui kama mwakani utapata mteremko. Tuko nyuma yako ila ukianguka tuko mbele yako.
 
mimi pia nilisikitika sana niliposikia hagombei tena, lkn sasa nimefarijika. wanaosema hajafanya lolote nawashangaa, angalieni mjengoni akisimama yeye kuchangia wabunge wote no stories no kusinzia wanamsikiliza yeye, big up zitto. halima mdee nae anakuja kuja
 
Nilitegeme hilo hasa baada ya kupata majibu kuwa hajachuja kisiasa baada ya ishu ya Dowans. Ni sawa kwa hilo kwani aendelee kumpa chati mzee Zitto kule Kigoma na Ujiji pia. Kwetu wana JF ni kuja na mkakati mpya kama wa Politician Star Search ili tupate vijana shupavu katika siasa za Tanzania tuitakayo na kumpa support wawe ili wawe wengi mjengoni. hatuna pa kwenda zaidi ya Tanzania tuipendayo, ni vema tukapaboresha walau kwa kiwango cha kuboresha utendaji na uzalendo
 
nazani kama anagombea ni jambo jema ila inabidi atoe taarifa rasmi na aje na hoja ya kwanini ameamua kurudi? ili watu wamuelewe kuwa anamsimamo, inawezekana pia ni pressure anapewa ili abadilishe mawazo kwahiyo yeye kama member aje tu hapa atoe taarifa...anajua wengi tunamsupport kama atagombea...
 
Hii kitu bado ,ikithibitishwa kulingana na maelezo marefu aliyoyatolea kuunga mkono hoja yake hiyo ya kuachana na ubunge na kwenda kusoma sijui kuendeleza utaalam wake mimi nitasema tu kwa ufupi YAMETIMIA.Nasubiri kwa sasa kuufahamu ukweli wenyewe na halisi.
 
Nilitegeme hilo hasa baada ya kupata majibu kuwa hajachuja kisiasa baada ya ishu ya Dowans. Ni sawa kwa hilo kwani aendelee kumpa chati mzee Zitto kule Kigoma na Ujiji pia. Kwetu wana JF ni kuja na mkakati mpya kama wa Politician Star Search ili tupate vijana shupavu katika siasa za Tanzania tuitakayo na kumpa support wawe ili wawe wengi mjengoni. hatuna pa kwenda zaidi ya Tanzania tuipendayo, ni vema tukapaboresha walau kwa kiwango cha kuboresha utendaji na uzalendo

Kila kijana ni shupavu ila tofauti tu wa ushupavu unaupima kutoka wapi na huo ushupavu unamaslahi gani binafsi na mpimaushupavu wa mwingine.
 
...mshahara 10m na gari zaidi ya mbili za 100m naye anajiona mtetezi wa wananchi,ni sehemu ya mafisadi tuu hana lolote,angekuwa na uchungu angekataa na kupinga kwa nguvu hiyo mishahara ya wizi wanayojipa hao mafisadi!
 
amen my brother! Kuna thread alitaja hela anayolipwa...sijui 200,000 kwa siku katika kamati moja na 320,000 kwa siku katika nyingine. Hii sijui inaishia wapi. anyway....Chadema isingeweza kukubali kupoteza kiti bungune. Ile ruzuku ya mil 60 ingepungua mbaya sana. Chama kingekufa.
 
teh teh teh teh teh nimeipenda hiyo, na hapo ndipo msingi mkuu wa vyama vinavyojiita vinatetea wanyonge
 
Back
Top Bottom