Zitto: Nia, Uzalendo na Uwezo wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania ninao!

ilikuaje mpaka akasema yote hayo...nilifikiri leo ilikua ni kutoa hoja kuhusu bajeti ya sayansi na techonology haya ya urais yametoka wapi?
 
Reactions: FJM
ZITTO kisha jua weak points za mabosi wake na watamkoma. MBOWE na SLAA hawamuezi ZITTO na SHIBUDA sana sana watajikanyaga na mwishoe watanyamaza.

Matumizi mabaya ya fedha za chama, Ukabila na udikteta ndani ya CDM ni mambo ambayo ni bomu ambalo wakiwachezea akina ZITTO watalipuliwa tu.

Hongera sana ZITTO vijana, wasanii, wasomi wote wanajua angalau wewe ndo mwenye dira ya kweli ndani ya CDM.
 
Mkuu, unao uhakika kuwa Harusi ya Dr. Slaa na Josephine ilifanyika?

ulikuwa unasubiri ukafinye pilau huku ukidodosa umbea wa kutuletea hapa?? imekula kwako ndugu yangu, chukua jembe ukalime!!
 
Zitto will go back to Magamba soon or later!! Kama si Magamba basi chama kipya kitaanzishwa na wanasiasa wengi watalundikana huko!! Yote ni kheri isipokuwa civil war tu ndo tutashangaa
 
wewe una matatizo sana maana kama hayo matatizo ya ufisadi, ukabila na mengine yapo CDM mbona Zitto amekaa kimya? au anataka kusubiri ayatumie kama agenda ya kutafuta nafasi ya kugombea urais?? amechelewa sana aende NCCR akagombee kwa tiketi ya chama hicho, CDM hakutakiwi unafiki!!
 
We have to be much smarter than the other organs if you know what m i reffering too! TISS n the likes! Stay focused CDM!
 

Iko kampeni ya kushusha miaka katika mchakato wa katiba ili aweze kugombea...wapo vijana wengi tu wanapigania hii ishu irekebishwe kwenye katiba. Wana"refer" umri wa Nyerere alipochukua nchi akiwa 39
 
Reactions: FJM
Nashangaa watu wanachoona ajabu kwa zitto kusema maneno haya,je katiba haimruhusu?au mnataka kutuaminisha CDM kuna watu maalum katika nafasi ya urais?na Dr Slaa kateuliwa lini kugombea urais wakati CC yakumpitisha haijakaa,kuna ubaya gani kwa zitto kusema hivyo,watu wana weweseka kama angesema ambae wanajua hana mvuto watu wasingetoa povu hivi,
 
naunga hoja 99%
 
Ile tekniki iliyotumika kwa Shibuda naona ita apply vyema kwa huyu Zitto. CHADEMA uongozi wa juu chonde chonde naomba msimjibu huku mkitafuta a permanent solution to this problem.
Kuna swala la Mdee na Nasari napata shaka kama huu ni mpango uliopangwa toka mwanzo....makanusho pekee hayatoshi, tunataka kujua wazi where you stand.
 
Last edited by a moderator:
wakuziba hapa JF wakati fulani nishawahi kuhoji upeo wako wa kufikiri, mabandiko ya namna hii yanakudhalilisha kama hujui.
  1. Kwanza SI KWELI kwamba ndoa ya Dr. Slaa imeshafungwa, kwa hiyo kusema Mbowe hakuhudhuria tukio hilo wakati huna hakika kama limefanyika ni KUROPOKA.
  2. Kufikiria kuwa raisi au kuweka nia ya kugombea SI KOSA LA UHAINI hivyo kwamba liwe na athari ya kukibomoa chama kama unavyodai. Kama ni mkongwe kwenye siasa za nchi hii ebu tukumbushe: Wakati Mzee Mwinyi anamaliza uongozi wana CCM wangapi WALICHUKUA fomu za kutaka kugombea? Chama kilikufa?
Kuwania urais si dhambi, ni haki ya kila raia kikatiba; na kwa sababu kila chama kina utaratibu wa kumpata mgombea wao kwa njia za kidemokrasia hakuna tatizo hapo. Tena ni afadhali wajitokeze wengi zaidi ili wanachama wawe na wider choice hivyo kwamba atayepatikana awe kweli ni chaguo la watu na si kuchukua nafasi hiyo kimizengwe.

Ni bora uwe unatafiti mambo kabla ya kujiaibisha.
 
Mwanzo nilikuwa naona kama Zitto ni mtu makini, hata yalipokuwa yakisemwa mabaya yake binafsi sikusapoti, ila kwa hii ya leo naomba kukubaliana na wadau, "ZITTO ANATUMIKA" ili kuivuruga chadema!!

Zitto nilikusapoti sana 2010, nilikuamini na kukutegemea ila naona sasa bahasha za kaki zimeshakuharibu!!

Naomba nikuulize Zitto, hivi wewe kama kijana unatumika kuivuruga chadema ili ccm waendelee kuwanyonya wanyonge, je utapata faida gani baada ya CDM kusambaratika!!?

Zitto tambua pesa si chochote chini ya jua!! Utakufa uziache!! MUOGOPE MUNGU!!
 
Iko kampeni ya kushusha miaka katika mchakato wa katiba ili aweze kugombea...wapo vijana wengi tu wanapigania hii ishu irekebishwe kwenye katiba. Wana"refer" umri wa Nyerere alipochukua nchi akiwa 39

Vijana wote wanaotaka kugombea urais ni wezi hakuna mzalendo kati ya hao wote wanaotaka urais
 
Reactions: FJM

Chukua LIKE
 
ulikuwa unasubiri ukafinye pilau huku ukidodosa umbea wa kutuletea hapa?? imekula kwako ndugu yangu, chukua jembe ukalime!!

Taratibu Mkuu. Lugha ya kistaarabu haiuzwi. Vyovyote utakavyosema lakini the fact ni kuwa Harusi haikufanyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…