Zitto: Nia, Uzalendo na Uwezo wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania ninao!

Ukweli husemwa:

Ni haki yake kikatiba na fikra ni za kwake bila kujali ametumia kigezo gani kujua kama anazo hizo sifa anazozitaja na kama ndizo pekee zinatosha kwa Mtanzania kuwa Raisi wa Tanzania.

Kama ilivyo CCM, pia katika CHADEMA, kulitaja swala la URAISI ni taboo au kwa lugha nyingine 'NO GO ZONE' achilia mbali kusimama na kusema unataka kuwa Raisi. Sababu kuu ni fikra za wapenzi na wanachama wa vyama hivi kuwa na imani na tumaini kuwa Raisi ajaye lazima atatoka tu katika chama chao. Fikra hizi zimezaa makundi na misuguano ndani ya vyama hivyo.

Zito anapata mashambulizi makali siyo tu kwa sababu anaonekana ni tishio na kizingiti katika makundi mengine ndani ya chama chake bali pia kwa vyama vingine vinavyoinyemelea hii ofisi kuu nchini

Itanishangaza kama Mzee Mapesa (John Cheyo) akisimama na kusema anataka kuwa raisi kama atapata mashambulizi makali kama haya anayoyapata Zito Kabwe kwa sababu jamii katika makundi hayo inamuona kama siyo kizingiti kikubwa kufikia lengo lao.

Tutasikia na kuona mengi na Zito Kabwe hatakuwa wa kwanza na wa mwisho kutamka kama anaitaka hii ofisi kuu nchini kabla ya michakato ya kumtafuta huyo mwanachama ndani ya vyama kuanza.

Yetu Macho na Masikio.
 
Zitto kayasema maneno hayo kwa kuwaumiza wabunge wa CDM, uongozi wa juu CDM na mashabiki wa CDM.
Na si kuwa ameyasema hayo kwa kutaka kuwakwaza CCM....huu mzigo mzito unaoitwa Zitto CDM utawateseni
sana kichwani na hamjui sehemu ya kwenda kuutua ili nanyi mupumzike. Poleni sana!
 
Sasa kweli nime amini unafiki wa zitto. Sasa mbona halikataa? Kweli mnafiki hajifichi!

Chama kinataka kujijenga wewe unatangaza kuwania urais.
 
Another silly season for Zitto. Plz zitto usipime upepo kisiasa namna hiyo...tungetegemea ujikite kuleta vyanzo tangible vipya vya kuboresha maisha ya mtanzania than urais unaoutaka kupitia CDM. Think of synergism. Avoid being Contraversial. Very soon you wil be Shibuda part 2.
 
Kwa viegezo vyake yeye mwenyewe anauwezo, lakini kwa viegezo vya wengi anapwaya. Lakini pia tukiri kuwa anauwezo mkubwa kuliko aliyepo

100%. Vigezo vyake mwenyewe, anajpigia debe mwenyewe na kuungwa mkono na maadui wa Tz na CHADEMA. Typical individualist

He's apparently (Zitto) proved unfit for any sensitive public office. Of coz Kikwete kachangia watu wenye uwezo mdogo, wabinafsi na wasiofaa kudhani wanafaa/wanawwza kuwa marais wa Tz.

Kwa nini wana ccm humu huwa wanamuunga sana mkono? swali jepesi hilo.
 
Hata akisema na bajeti ya serikali ya miaka 5 atatoa yeye hakuna chama kitakacho mpendekeza yeye. Watu wote makini wanajua kuwa mtu yeyote mwenye uchu wa madaraka kama yeye ni hatari kwani ama ametumwa au ana agenda ya siri.CHUNGUZENI URAIA WAKE.

Hili ndiyo nilisubiri mseme.Hakika lazima pana mushkeri na uraia wake, ukichimbua zaidi utabaini.Anzeni mtabaini kuna siri hapo
 
​umetumwa na nape maana anamuogopa huyu ile mbaya
unajua huyu jamaa ni mpuuzi sana, nimemsikiliza kwa makini baada ya kuchangia na akaishiwa maneno akaanza ohhh, haya yanayosemwa mitaani yatapita , alafu akafumba tena maneno...uwezo , nguvu , yakuwa amiri jeshi mkuu, upo.

Mimi nataka nimwambie wazi ...huyu bwana mdogo, na ninajua ataisoma hii, naungana na mdau mmoja hapa, Siku CHADEMA wakikuchagua kugombea URAISI wa Tanzania, narudisha kadi ya chadema na nitaipigia CCM hata wakisimamisha Jiwe.

Hivi zito Ikulu unataka nini? Si wewe uliyewahi kusema uliingia kwenye siasa kwa bahati mbaya wala hukupenda kuwa mwanasiasa na huipendi siasa,na unafikiria kutoka?sasa kulikoni ikulu?

Ikulu si pango la vibaka, kila siku unageuka na maneno mnafiki kuliko hata KIKWETE, tukikupa nchi si ndio tumekwisha kama kikwete tu kaaribu kiasi hiki, wewe je?

Na hivi si zito huyu aliyekuwa anatapa tapa jimbo la kugombea uchaguzi uliopita, mara kinondoni, mara sijui wapi...Huu ndio uwezo wa kuwa Amiri jeshi mkuu wa Tanzania? SHAME ON U LITTLE BOY, A PROSPECTED RAIS WA KIGOMA..GO IN HELL BEFORE DAYS SENDS U

pili Hivi zito atakuwa na miaka ya kutosha kugombea urais mwaka 2015 (Sina uhakika wadau ni saidieni hili?

MAKAMANDA wote ni mduda wakusimama na kumwambia ZITO ukiutaka urais kupitia CHADEMA imekula kwako, anyway najua utahama tu kwani unatumiwa.
 
USHAURI WA BURE KWA ZITTO

Mzee Mtei ambaye ni muasisi wa chadema, aliwahi kukuwekea pingamizi usigombee uenyekiti wa chadema. Ulikua umshinde mbowe kwa kupata 70% ya kura. Mtandao wako wa akina kafulila ukasambaratishwa na kufukuzwa. Una maadui wengi chadema. pole sn kwa hilo! siasa ndivyo ilivyo.

Siyo siri wewe ndiyo ulionivutia kuipenda chadema. naamini wapo wengi ambao uliwavutia kwa kujenga hoja nzuri bungeni na wakajiunga au kuipenda chdm.
...

Hata mzee Malecela alikamia sana kuwa rais wa nchi hii, lakini CCM ina wenyewe kama cdm ilivyo, pamoja na kuahidiwa pesa na nchio ya Iran kwa ajili ya kamppeni hadi kufikia kubadili dini, chama chake kiliendelea kusema CCM ina wenyewe.Nakubaliana kuwa zitto tayari amepigwa charter na wazee wa CHADEMA haitatokea apatwe nafasi yoyote ndani ya CHADEMA.

The same na EL haya maneno mtakuja kunikumbusha siku moja.Wote wale wako kwenye BLACK LIST kwenye vyama vyao.Kwa wanaodhani EL ataukwaa wanota CCM ina wenyewe na wenyewe ndiyop wao
 
tatizo liko wapi naona ccm wanamuogopa huyu maana zile siasa za ukanda watakuwa hawana hoja,ukanda hakuna hoja,wala dini hakuna hoja kikubwa zaidi wanaelewa kuwa huyu sio zao la akili ndogo kuongoza akili kubw naona ccm wanpwaya sana wakisikia zito ana nia hiyo mnashangaa nini mnataka awe membe ambaye hajaoteshwa usingizini naona to tactics za ccm za kukiogopa kiumbe makini zito namuunga 100% ni kijana ni mchapa kazi kidogo juzi amuondoe waziri mkuu kwa uzembe wake bungeni anazo sifa zope za kuwa kiongozi people's power forever.
 
Hana lolote huyu na wala hafai na unafiki wake. Eti rais? Uadilifu upi ulionao. Wana CDM tusikubali huyu mtu hata kidogo. CDM mkimpitisha 2015 mimi kama kijana na kada wa chama nahama rasmi na kurudi CCM! Tuna watu wana akili na uwezo mzuri sana kama Lissu na Mnyika lakini wao bado. 2015 ni Dr. Slaa tu na baada ya hapo Dr. Slaa utusamehe tupate nafasi ya kuwafikiria na wengine na hapa ndo Zitto anaweza kujaribu kama tu ameacha unafiki a.k.a undumilakuwili. NDOTO ZA MWENDAWAZIMU HIZO WE ZITO HATA SISI VIJANA WA CDM TULIO WENGI HATUKUKUBALI NA TUNAFAHAM UNATYMIKA KUKIHUJUM CHAMA.
 
Hivi kuna uhusiano wowote katika kutajwa huyu Mtesaji wa Dr. Ulimboka na maneno ya Zitto bungeni?

Inashangaza kuwa tangu jana, harufu ya Zitto kulipuka imekuwepo hapa JF na leo kalipuka.

Ila ni leo hii hii, Mwanahalisi imemtaja Ramadhani Ighondu (kumbe ni huyu walisema anaitwa RAMA) wa Usalama wa Taifa kuwa ni yeye alisimamia kuteswa kwa Ulimboka. Hizi habari zilianza kuelezwa siku nyingi kidogo na leo zimefumuka.

Na leo hii hii, inawezekana baada ya kujua kinachopikwa na Kubenea, Zitto akaanza na yeye kupika chake.
Ngongo naona usemi wako wa kumuhusisha Jack Zoka na Zitto yana ukweli fulani. Inawezekana kabisa katika kutupotezea mwelekeo wetu wa kujua kilichompata Ulimboka na hasa baada ya kutajwa Ramadhani Ighondu, basi Jack kamwambia Zitto kuwa muda wake wa malipo umefika na amwage cheche za kutaka Urais.

Kuna uwezekano Zitto akafanya jambo kali zaidi ya hili ili kuvuta akili, masikio na macho ya Watanzania kusahau jambo muhimu litakalotokea nchini na hasa linaloiabishia Serikali.

Sitashangaa hata kumuona akirusha NGUMI au kutoa matusi kwani anajua Serikali itamlinda.

Lazima nikiri kuwa hawa akina Jack Zoka kwa kweli WANA AKILI sana ila kuna sehemu wamepotea kidogo.....

acha kua na fikra dhaifu na nyonge wewe kipi kinakupoteza muelekeo kisa gazeti au kauli ya zito bungeni?
inaonyesha wazi kua wewe ni mshabiki wa habari zats all.
 
Tunaletewa movie mpya ya zitto kabla hatuja maliza za ulimboka, mwigullu, MV skagit na ya pamba kwa shs.660 TAYARI TUME-LOOSE TRACK
 
Mheshimiwa ZITTO ZUBERI KABWE leo wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Sayansi na Teknolojia amesema anao uwezo wa kuongoza nchi, anao uzalendo kwa nchi yake na anao uwezo wa kuwa amri jeshi mkuu wa Tanzania.
Siku Zitto atakapopitishwa na CDM kugombea urais, watu wote niliowashawishi wahamie chadema mwaka 2010 nitaungana nao kuwashawishi wengine waipigie ccm hata kama ccm wataweka haja kubwa kugombea urais
 
Kwa kujinadi tayari alisha ji disqualify kwani siku zote kiongozi bora ni yule anayependekezwa na si anayejipendekeza na kujipigia chepuo kufa na kupona. Zitto umekosa hekima sana naomba ulewe mchumba huchumbiwa na kamwe hajichumbii
 
Agombee tu urais ila atafute chama kama UPDP cha Faham Nassor ndio kinamfaa....si Chadema wala CCM
 
mda na kipaumbele kwa wananchi walio wengi tu ndo kigezo kwake cha kumfanya asubiri mpaka hapo baadae labda mnamo miaka ya 2025 na kuendelea richa ya kuwa uwezo,uzalendo na kuwa amiri jeshi mkuu vyote anavyo.lakini kwa sasa wananchi tuliowengi Slaa is our best option in the country in the couple of few years to come.believe it Or not ,that remains as an objective truth to all revolutionarists across the territory.for further help zitto should go round and do a simple research on this.my take:people should always devote much of their time and cogitate before they leap.To my opinion,kabwe still have a long way journey to go on this saga.being a minister is what can suit u at this point in time.pl'se observe political tolerance !!!!

Kinachomtofautisha Zitto na wengine wote wanaofikiriwa kugombea nafasi ya Urais kupitia CHADEMA ni busara na hekima. Wengine wote wanaonekana kuwa na hekima isipokuwa Zitto.
 
Nyie mnaotukana mnataka nani awe Rais,Zitto anaweza na uwezo wake ni mkubwa na anawaacha mbali Slaa na Mbowe!
 
Mbona CDM mnahaha juu ya ishu ya Zitto na urais?
kwani kusema hayo ndo kupita mnataka kupinga hilo kamati kuu ndo inapitisha jina lake so watampiga chini kama kweli hana uwezo wa kua raisi kama mnavyo lalamika.
coment zot zinaonyesha Zitto alivyo na nguvu kubwa na tishio kwa vigogo CDM uraisi 2015.
mngejua ndo mnampa coverage.
Go go goooo Zitto tunahitaji mabadiliko
 
Siku Zitto atakapopitishwa na CDM kugombea urais, watu wote niliowashawishi wahamie chadema mwaka 2010 nitaungana nao kuwashawishi wengine waipigie ccm hata kama ccm wataweka haja kubwa kugombea urais

Kama ikatokea chama chochote kikamteua Zitto kugombea nafasi ya Urais, litakuwa ni jibu tosha kuwa ndani ya chama hicho hakuna wenye hekima, na nchi isikubali kuongozwa na chama cha siasa chenye viongozi wasio na busara.
 
Back
Top Bottom