Zitto: Nia, Uzalendo na Uwezo wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania ninao!

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Mheshimiwa ZITTO ZUBERI KABWE leo wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Sayansi na Teknolojia amesema anao uwezo wa kuongoza nchi, anao uzalendo kwa nchi yake na anao uwezo wa kuwa amri jeshi mkuu wa Tanzania.
 
Zitto kasema Bungeni sasa hivi hana mashaka kuwa ana uwezo na ni mwadilifu kuweza kuwa Rais alafu hapo hapo anaruka kihunzi kuwa katika tamasha lile alikuwa na makusudi mengine.

Zitto umesomeka wewe ni mnafiki na hustahili. Huwezi kuteuliwa na CCM wala CHADEMA kuwa mgombea maana wanaokuzidi ni wengi sasa naomba ujipime kwa Rissu na Silaa uone unavyopwaya.

CHADEMA achaneni na Zitto mapema aende anapotaka. Na katika CCM ndio kabisa!!!!!! hawezi maana mnyukano wa huko ni wa kufa mtu na wako wengi sana
 
Mh. Zitto Kabwe wakati akichangia hotuba ya Wizara Sayansi na Teknlojia amewananga wale wanao taka asiwe rais wa nchi hii, kwa kutaja mambo matatu ambayo amesema hana shaka nayo hata kidogo kuwa anayo japokuwa watu wengine wamekuwa wakimsaga. Mambo hayo ni :

  1. Uwezo
  2. Uadilifu
  3. Uzalendo

Kazi kwenu wana JF, Zitto amedhamiria kuutaka na kuupata Urais
 
Nyerere alisema hayoooo

Kwani kuwa mzalendo na kulitumikia taifa lazima uwe Rais?

Fanya kazi watanzania tukuone, ikifika wakati tutakuita wenyewe.

Kwani Mwinyi ama Mkapa walipokuwa mawaziri walikuwa wanatamka mambo ya Urais?

Sasa tuangalia huyu aliyeota uraisi na kuunda mtandao? Alikimbilia Ikulu, angalia mambo yanayofanyika!!!!

Nawaonya wananchi wa Tanzania na Wanachama Wa CDM, wale woote wanaotaka uraisi sana, tuwachunguze na kuwaangalia kwa jicho la husuda.
 
Dumela Mbegu

Ni kweli Zitto ni mzalendo halisi hata mazungumzo yake na Jack Zoka wakati wa uchaguzi yanathibisha hilo.

Mh. Zitto Kabwe wakati akichangia hotuba ya Wizara Sayansi na Teknlojia amewananga wale wanao taka asiwe rais wa nchi hii, kwa kutaja mambo matatu ambayo amesema hana shaka nayo hata kidogo kuwa anayo japokuwa watu wengine wamekuwa wakimsaga. Mambo hayo ni :

  1. Uwezo
  2. Uadilifu
  3. Uzalendo

Kazi kwenu wana JF, Zitto amedhamiria kuutaka na kuupata Urais
 
Last edited by a moderator:
Huyo aje CCM tutampa kura. Lakini kule kwa magwanda? magwanda wenyewe ndio wanampinga.
 
Katika kukamilisha kile kinachosemwa na watu wengi juu ya hatima ya Zitto na Urais, muda mchache uliopita wakati akichangia katika hotuba ya wizara ya Sayansi na Teknolojia Mh. Z.Z. Kabwe amesema hana wasiwasi na uongozi kwa nafasi ya uamiri jeshi hana wasiwasi labda mambo mengine...

MY TAKE:

Kweli huyu jamaa anashindwa kuelewa utaratibu uliopo ndani ya CHADEMA juu ya kumpata mpeperushaji wa bendera katika nafasi ya Urais? au anafanya makusudi ya lazima? au ndo utoto? au uchekibob?..........................
 
ww Mheshimiwa Hon. MP acha unafiki naona umetumwa kumchukia ZITTO bila sababu ni aibu kwa nini usigombee na ww? mm kumlinganisha na RISSU au SILAA ni uhayawani
leta mada za kueleweka wabunge wameshazungumzia mitandao inayowachafua Watanzania usisababishe tukafungiwa nakuomba tafuta address ya Zitto, au teamzitto ukamtukane huko kwenye PM yake
 
Zitto atakuwa na mkono wa magamba!!ndiyo maana wanataka awepo mgombea binafsi.ila kachemka mbaya!!!
 
Mh. Zitto Kabwe wakati akichangia hotuba ya Wizara Sayansi na Teknlojia amewananga wale wanao taka asiwe rais wa nchi hii, kwa kutaja mambo matatu ambayo amesema hana shaka nayo hata kidogo kuwa anayo japokuwa watu wengine wamekuwa wakimsaga. Mambo hayo ni :

  1. Uwezo
  2. Uadilifu
  3. Uzalendo

Kazi kwenu wana JF, Zitto amedhamiria kuutaka na kuupata Urais
Hayo yote ni sawa...linapokuja swala la kuwa Rais hafai!!! Jamaa ni ndumilakuwili sana...
 
Kwa viegezo vyake yeye mwenyewe anauwezo, lakini kwa viegezo vya wengi anapwaya. Lakini pia tukiri kuwa anauwezo mkubwa kuliko aliyepo
 
Huyo aje CCM tutampa kura. Lakini kule kwa magwanda? magwanda wenyewe ndio wanampinga.

Labda magamba system! yale makundi mengine hayataki kusikia hata jina lake likitajwa maana wanajua mchonganishi na ana Sura mbili!
 
Back
Top Bottom