Zitto: Nia, Uzalendo na Uwezo wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania ninao!

ilikuaje mpaka akasema yote hayo...nilifikiri leo ilikua ni kutoa hoja kuhusu bajeti ya sayansi na techonology haya ya urais yametoka wapi?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
unajua huyu jamaa ni mpuuzi sana, nimemsikiliza kwa makini baada ya kuchangia na akaishiwa maneno akaanza ohhh, haya yanayosemwa mitaani yatapita , alafu akafumba tena maneno...uwezo , nguvu , yakuwa amiri jeshi mkuu, upo.

Mimi nataka nimwambie wazi ...huyu bwana mdogo, na ninajua ataisoma hii, naungana na mdau mmoja hapa, Siku CHADEMA wakikuchagua kugombea URAISI wa Tanzania, narudisha kadi ya chadema na nitaipigia CCM hata wakisimamisha Jiwe.....
ZITTO kisha jua weak points za mabosi wake na watamkoma. MBOWE na SLAA hawamuezi ZITTO na SHIBUDA sana sana watajikanyaga na mwishoe watanyamaza.

Matumizi mabaya ya fedha za chama, Ukabila na udikteta ndani ya CDM ni mambo ambayo ni bomu ambalo wakiwachezea akina ZITTO watalipuliwa tu.

Hongera sana ZITTO vijana, wasanii, wasomi wote wanajua angalau wewe ndo mwenye dira ya kweli ndani ya CDM.
 
Zitto will go back to Magamba soon or later!! Kama si Magamba basi chama kipya kitaanzishwa na wanasiasa wengi watalundikana huko!! Yote ni kheri isipokuwa civil war tu ndo tutashangaa
 
ZITTO kisha jua weak points za mabosi wake na watamkoma. MBOWE na SLAA hawamuezi ZITTO na SHIBUDA sana sana watajikanyaga na mwishoe watanyamaza. Matumizi mabaya ya fedha za chama, Ukabila na udikteta ndani ya CDM ni mambo ambayo ni bomu ambalo wakiwachezea akina ZITTO watalipuliwa tu.
Hongera sana ZITTO vijana, wasanii, wasomi wote wanajua angalau wewe ndo mwenye dira ya kweli ndani ya CDM.
wewe una matatizo sana maana kama hayo matatizo ya ufisadi, ukabila na mengine yapo CDM mbona Zitto amekaa kimya? au anataka kusubiri ayatumie kama agenda ya kutafuta nafasi ya kugombea urais?? amechelewa sana aende NCCR akagombee kwa tiketi ya chama hicho, CDM hakutakiwi unafiki!!
 
We have to be much smarter than the other organs if you know what m i reffering too! TISS n the likes! Stay focused CDM!
 
unajua huyu jamaa ni mpuuzi sana, nimemsikiliza kwa makini baada ya kuchangia na akaishiwa maneno akaanza ohhh, haya yanayosemwa mitaani yatapita , alafu akafumba tena maneno...uwezo , nguvu , yakuwa amiri jeshi mkuu, upo.

Mimi nataka nimwambie wazi ...huyu bwana mdogo, na ninajua ataisoma hii, naungana na mdau mmoja hapa, Siku CHADEMA wakikuchagua kugombea URAISI wa Tanzania, narudisha kadi ya chadema na nitaipigia CCM hata wakisimamisha Jiwe.

Hivi zito Ikulu unataka nini? Si wewe uliyewahi kusema uliingia kwenye siasa kwa bahati mbaya wala hukupenda kuwa mwanasiasa na huipendi siasa,na unafikiria kutoka?sasa kulikoni ikulu?

Ikulu si pango la vibaka, kila siku unageuka na maneno mnafiki kuliko hata KIKWETE, tukikupa nchi si ndio tumekwisha kama kikwete tu kaaribu kiasi hiki, wewe je?

Na hivi si zito huyu aliyekuwa anatapa tapa jimbo la kugombea uchaguzi uliopita, mara kinondoni, mara sijui wapi...Huu ndio uwezo wa kuwa Amiri jeshi mkuu wa Tanzania? SHAME ON U LITTLE BOY, A PROSPECTED RAIS WA KIGOMA..GO IN HELL BEFORE DAYS SENDS U

pili Hivi zito atakuwa na miaka ya kutosha kugombea urais mwaka 2015 (Sina uhakika wadau ni saidieni hili?

MAKAMANDA wote ni mduda wakusimama na kumwambia ZITO ukiutaka urais kupitia CHADEMA imekula kwako, anyway najua utahama tu kwani unatumiwa.

Iko kampeni ya kushusha miaka katika mchakato wa katiba ili aweze kugombea...wapo vijana wengi tu wanapigania hii ishu irekebishwe kwenye katiba. Wana"refer" umri wa Nyerere alipochukua nchi akiwa 39
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nashangaa watu wanachoona ajabu kwa zitto kusema maneno haya,je katiba haimruhusu?au mnataka kutuaminisha CDM kuna watu maalum katika nafasi ya urais?na Dr Slaa kateuliwa lini kugombea urais wakati CC yakumpitisha haijakaa,kuna ubaya gani kwa zitto kusema hivyo,watu wana weweseka kama angesema ambae wanajua hana mvuto watu wasingetoa povu hivi,
 
unajua huyu jamaa ni mpuuzi sana, nimemsikiliza kwa makini baada ya kuchangia na akaishiwa maneno akaanza ohhh, haya yanayosemwa mitaani yatapita, alafu akafumba tena maneno...uwezo, nguvu, yakuwa amiri jeshi mkuu, upo.

Mimi nataka nimwambie wazi ...huyu bwana mdogo, na ninajua ataisoma hii, naungana na mdau mmoja hapa,alisema, Siku CHADEMA wakikuchagua kugombea URAISI wa Tanzania, narudisha kadi ya chadema na nitaipigia CCM kura hata wakisimamisha Jiwe.

Hivi zito Ikulu unataka nini? Si wewe uliyewahi kusema uliingia kwenye siasa kwa bahati mbaya wala hukupenda kuwa mwanasiasa na huipendi siasa, na unafikiria kutoka? sasa kulikoni ikulu?

Ikulu si pango la vibaka, kila siku unageuka na maneno mnafiki kuliko hata KIKWETE, tukikupa nchi si ndio tumekwisha, kama kikwete tu kaaribu kiasi hiki wewe je?

Na hivi si zito huyu aliyekuwa anatapa tapa jimbo la kugombea uchaguzi uliopita, mara kinondoni, mara sijui wapi...Huu ndio uwezo wa kuwa Amiri jeshi mkuu wa Tanzania? SHAME ON U LITTLE BOY, A PROSPECTED RAIS WA KIGOMA..GO IN HELL BEFORE DAYS SENDS U.

pili Hivi zito atakuwa na miaka ya kutosha kugombea urais mwaka 2015 (Sina uhakika wadau ni saidieni hili?

MAKAMANDA wote ni muda wakusimama na kumwambia ZITO ukiutaka urais kupitia CHADEMA imekula kwako, anyway najua utahama tu kwani unatumiwa na hao makada.
naunga hoja 99%
 
Ile tekniki iliyotumika kwa Shibuda naona ita apply vyema kwa huyu Zitto. CHADEMA uongozi wa juu chonde chonde naomba msimjibu huku mkitafuta a permanent solution to this problem.
Kuna swala la Mdee na Nasari napata shaka kama huu ni mpango uliopangwa toka mwanzo....makanusho pekee hayatoshi, tunataka kujua wazi where you stand.
 
Last edited by a moderator:
Akichangia wizara ya mawasiliano na uchukuzi leo bungeni, mh zitto kabwe ametetea wasanii kuhusu fedha kidogo wanazolipwa kutokana na nyimbo zao kutumika kama ringtones. amesema wasanii wanalipwa chini ya 10% ya mapato ya ringtones. kampuni za simu zinachukua 90%! ameomba serikali iliangalie suala hili kwa ukaribu mkubwa.

Amesema kuwa amesikia maneno mengi baada ya kuwaunganisha wasanii wenye asili ya kigoma. ameendelea kuwa nia yake ni ya kuundeleza mkoa wa kigoma na kutetea maslahi ya wasanii kwa ujumla. "nashangaa watu wanalihusisha na urais!" "Mungu akitaka mtu awe rais hakuna anaeweza kuzuia." kwa taarifa yenu "uadilifu wa kuwa amiri jeshi mkuu wa taifa letu ninao". hata yakisemwa maneno mengi lkn Mungu akitaka hakuna wa kunizuia.


MY TAKE:
niliwahi kuandika hapa jf makala kuhusu hali ngumu ya kinyng'anyiro cha urais chdm. Lissu anautaka, Zitto anautaka, mbowe anautaka na slaa anautaka. slaa ameoa ili 2015 aondoe maneno kuwa hana mke halali. nasikia mbow yuko singapore na japan. inasemekana hakuhudhuria harusi ya slaa japo hili sina ushahidi nalo. wadau mnaweza kunipasha ukweli wa hili.


chdm wasipoangalia, urais utakimega chama vipandevipande. zitto anaungwa mkno na wabunge vijana na anaendelea na uhamasishaji. mtei aliwahi kumuambia kuwa "chama kina wenyewe" hapo chacha!!!!!! kazi ipo wakatabahu: wakuziba
wakuziba hapa JF wakati fulani nishawahi kuhoji upeo wako wa kufikiri, mabandiko ya namna hii yanakudhalilisha kama hujui.
  1. Kwanza SI KWELI kwamba ndoa ya Dr. Slaa imeshafungwa, kwa hiyo kusema Mbowe hakuhudhuria tukio hilo wakati huna hakika kama limefanyika ni KUROPOKA.
  2. Kufikiria kuwa raisi au kuweka nia ya kugombea SI KOSA LA UHAINI hivyo kwamba liwe na athari ya kukibomoa chama kama unavyodai. Kama ni mkongwe kwenye siasa za nchi hii ebu tukumbushe: Wakati Mzee Mwinyi anamaliza uongozi wana CCM wangapi WALICHUKUA fomu za kutaka kugombea? Chama kilikufa?
Kuwania urais si dhambi, ni haki ya kila raia kikatiba; na kwa sababu kila chama kina utaratibu wa kumpata mgombea wao kwa njia za kidemokrasia hakuna tatizo hapo. Tena ni afadhali wajitokeze wengi zaidi ili wanachama wawe na wider choice hivyo kwamba atayepatikana awe kweli ni chaguo la watu na si kuchukua nafasi hiyo kimizengwe.

Ni bora uwe unatafiti mambo kabla ya kujiaibisha.
 
Mwanzo nilikuwa naona kama Zitto ni mtu makini, hata yalipokuwa yakisemwa mabaya yake binafsi sikusapoti, ila kwa hii ya leo naomba kukubaliana na wadau, "ZITTO ANATUMIKA" ili kuivuruga chadema!!

Zitto nilikusapoti sana 2010, nilikuamini na kukutegemea ila naona sasa bahasha za kaki zimeshakuharibu!!

Naomba nikuulize Zitto, hivi wewe kama kijana unatumika kuivuruga chadema ili ccm waendelee kuwanyonya wanyonge, je utapata faida gani baada ya CDM kusambaratika!!?

Zitto tambua pesa si chochote chini ya jua!! Utakufa uziache!! MUOGOPE MUNGU!!
 
Iko kampeni ya kushusha miaka katika mchakato wa katiba ili aweze kugombea...wapo vijana wengi tu wanapigania hii ishu irekebishwe kwenye katiba. Wana"refer" umri wa Nyerere alipochukua nchi akiwa 39

Vijana wote wanaotaka kugombea urais ni wezi hakuna mzalendo kati ya hao wote wanaotaka urais
 
  • Thanks
Reactions: FJM
ZITTO kisha jua weak points za mabosi wake na watamkoma. MBOWE na SLAA hawamuezi ZITTO na SHIBUDA sana sana watajikanyaga na mwishoe watanyamaza. Matumizi mabaya ya fedha za chama, Ukabila na udikteta ndani ya CDM ni mambo ambayo ni bomu ambalo wakiwachezea akina ZITTO watalipuliwa tu.
Hongera sana ZITTO vijana, wasanii, wasomi wote wanajua angalau wewe ndo mwenye dira ya kweli ndani ya CDM.

Chukua LIKE
 
ulikuwa unasubiri ukafinye pilau huku ukidodosa umbea wa kutuletea hapa?? imekula kwako ndugu yangu, chukua jembe ukalime!!

Taratibu Mkuu. Lugha ya kistaarabu haiuzwi. Vyovyote utakavyosema lakini the fact ni kuwa Harusi haikufanyika.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom