Zitto ni maporomoko ya mto Nile - hayazuiliki kwa kifusi!



... yawezekana mengine mengi nimeyasahau. kuna kila sababu ya huyu jamaa kuundiwa mazengwe mbalimbali ili kuondoa credibility yake.

imefahamika pia wapinzani wake wa ndani ya chama chake wameanzisha kikundi maalumu walichokipa jina na OPERESHENI CHAFUA ZITTO..

kwa hayo machache nawatakia mjadala mwema wakuu.
narudia tena:- zitto ni maporomoko ya nile hayazuiliki kwa kifusi.
Mkuu "Magindu" Kwanza kabisa, nakugongea "LIKE". Naungana na wewe 100%, na naendelea kulaani wote ambao wanaendelea kuhukumu, kabla ya uthibitisho. Hii inaonesha dhahiri kuwa ipo nia ya ndani ya chuki binafsi kwa kamanda Mpiganaji ambaye amekuwa akihatarisha hata maisha yake kupigania haki, usawa na utu wa watanganyika walio wengi, ambao kwa njia moja au nyingine, wameshindwa au hawawezi kupaza sauti zao kutetea utu wao. Wengi wa hao vibwetere wana utashi wao binafsi na wanaingiwa nyongo kwa kamanda huyo kutangaza nia yake ya kikatiba ya kugombea uraisi. Kama hoja yao ni hiyo, basi washindwe na walegee. na Iwapo, chama hicho kitaendelea na chuki za namna hiyo, Nipo tayari kumshawishi kamanda, ahame chama hicho, na kwa gharama yoyote, tuko tayari kushawishi umma, kuunga mkono mageuzi ndani ya chama kipya. Ila, Iwapo, na Ikiwa, Mkuu atakutwa na kashfa ya kula rushwa, nita withdraw statement yangu. "MUNGU ATUHURUMIE"
"MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI ZANZIBARI, RIP TANZANIA"
 
Zzk for president 2015.,mwandishi wa hii thread amefanikiwa kunifungua macho ,hivi ingekua ni zitto ndie katamka maneno kama yale ya mkurupukaji nassari yakujitangazia wakaskazi kujitenga ingekuaje,?chadema acheni kuwa biased
 
Zzk for president 2015.,mwandishi wa hii thread amefanikiwa kunifungua macho ,hivi ingekua ni zitto ndie katamka maneno kama yale ya mkurupukaji nassari yakujitangazia wakaskazi kujitenga ingekuaje,?chadema acheni kuwa biased
 
Hakika zitto Kweli ni wembe anawanyima usingizi Watu humu ndani poleni.Mungu akipanga kitu Hakuna binadamu atakae pangua subirini muone nguvu ya mungu na majungu yenu yote mnayompikia soon mtaaibika
 
Zzk for president 2015.,mwandishi wa hii thread amefanikiwa kunifungua macho ,hivi ingekua ni zitto ndie katamka maneno kama yale ya mkurupukaji nassari yakujitangazia wakaskazi kujitenga ingekuaje,?chadema acheni kuwa biased


judith kushaba,hasheem, magindu et al ...nk..nk..( dugu moja au mutu moja hiyo...joining forms walichukua wote 30th July,2012)

join date ...one day before monthly speech...safi sana
 
Ama kweli wewe ni kipofu yaani azungumze wa ccm alafu kashfa upeleke chadema. wapi na wapi huoni unavyopotea hata mtoto mdogo haimwingii akilini.

Tafakari Zito apigwe vita na nani. Mimi ni mwanachama wa kawaida wa chadema lakini simwamini Zito, pili kazi inayofanywa na viongozi wa chama ni kubwa katika kujenga chama na si kumjenga mtu kama anavyopenda Zito sasa apewe choper ili ajinadi anagombea urais. wakati robo tatu ya bunge ni ccm hiyo ni akili au matope.

Ukumbuke Slaa kugombea urais aliombwa, akujinadi sasa nadhani tofauti unaiona.
 
Umeeleweka mkuu ni ukweli usiopingika ni kweli zitto huwezi kumlinganisha na mwanasiasa yoyote hapa nchini,mwenye kumchukia zitto basi halitakii mema taifa letu..mungu amlinde na ampe maisha marefu zitto
 
Huyo Zito hana nidhamu wala hekima. Ndo maana anapenda kupayuka hovyo na ndiyo yanamcost. Inaonekana haheshimu hata viongozi wenzake.

Tunajua Mbowe ndiye kamjenga Zito hadi kawa maarufu lakini yeye anataka kuwa maarufu kuliko hata chama na kuwa selfish. Kwani kuchafuliwa ni nini? Mbona wanasiasa wengi tu wanachafuliwa lakini wanadunda tu. Dr. Slaa alichafuliwa mara ngapi na hajawahi kujitetea pamoja na kwamba anasemewa uongo?

Lowassa pia lakini yupo kimya. Lakini huyo dogo ameshatekwa na mafisadi anapigapiga mayowe kila wakati. Mwambieni akipenda sana kuandikwa na kusifiwa atachuja mapema yeye afanye kazi yake kama mbunge na kuitetea chama chake. Ona sasa hao CCM waliokuwa wakimpa kichwa leo wanamsakama kuwa amekula rushwa.

Ukiwa rafiki wa mwizi watakuita mwizi tu na wewe vivyo hivyo ukiwa rafiki wa mafisadi na wewe hatutakosea kukuita fisadi au fisadi mtarajiwa.
 
Zitto ni mla rushwa na ni fisadi kuliko hata hao wabunge wa ccm walioko katika hizo kamati za bunge na huyu ni bora angeenda huko kwa magamba mapema maana ameshapoteza uzalendo na chama chake.
 
Wengi ktk GTs hapo coloured mnachemka! unadhani ni sahihi kumhukumu mtu kwa kuangalia join date ndani ya JF? unadhani wote wanaojiunga sasa hawakuwapo/hawakuijua JF kabla? TAFAKARI!!
NB; ZITTO NI JEMBE, 'HUWEZI KUINAJISI ASALI KWA KUITA MAVI YA NYUKI'

Mbona Waziri kasema MIGAO ya Umeme siku zote inapangwa? Umejitahidi kidogo ila kajipange upya.

Naona kweli wewe umeingia JF 24 July, 2012.... Karibu sana JF, Kuku mwenye kamba yake Mguuni.
 
Mbona Waziri kasema MIGAO ya Umeme siku zote inapangwa? Umejitahidi kidogo ila kajipange upya.

Naona kweli wewe umeingia JF 24 July, 2012.... Karibu sana JF, Kuku mwenye kamba yake Mguuni.

sikonge hujielewi wewe kama vp rudi kwenu ukalime viazi.
 
Hizo ndiyo zinakupa upofu wa kutokuona mabaya yake! Huyo Kijana tunamfahamu uzuri! Amechenga katika mengi na kutumia CV yake ya umaarufu mwepesi wa kukataa posho sasa hivi kwa sababu ya rushwa kubwa kubwa. Katika hili haponi, hana "moral authority" tena. Mbona anaweweseka sana na tuhuma. Unataka tutoe ushahidi wa msg zake. Hopeless kabisa acheni kuchezewa akili na wanasiasa uchwara wanaotumia matatizo yetu kuapata umaarufu huku wakituumiza kwa kuwaamini.

kagwina wewe ni mpuuzi tu,umetumwa.
 
Una maana wewe ni mmoja wa watu wenye ID kibao......

Mnaandika na kujijibu na mtu akiwashambulia, mnakuja na ID nyiingi na kujibu na mwisho kujipa LIKE.

JF ni Upepo tu, utapita. Malecela alisema, vita inapiganwa chini ya ardhi na si angani au kwenye MTANDAO.

Kama unaona Zitto ni Jembe, si mchukue umpelekeke kwako na umwachie nyumba? Ikishindikana, tundika picha yake.

Tuna macho na masikio tunaona. AKibadilika huyo Zitto wako na arudi UPINZANI, tutamsoma tu na kumpa support.
Wengi ktk GTs hapo coloured mnachemka! unadhani ni sahihi kumhukumu mtu kwa kuangalia join date ndani ya JF? unadhani wote wanaojiunga sasa hawakuwapo/hawakuijua JF kabla? TAFAKARI!!
NB; ZITTO NI JEMBE, 'HUWEZI KUINAJISI ASALI KWA KUITA MAVI YA NYUKI'
 
ZITTO keep silent, we will speak on your behalf. water and fuel are immisible. we will stand with you to end.
 
Back
Top Bottom