Zitto ni maporomoko ya mto Nile - hayazuiliki kwa kifusi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto ni maporomoko ya mto Nile - hayazuiliki kwa kifusi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUNTEMEKE, Aug 1, 2012.

 1. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Nimeshawishika kuandika uzi huu kumfananisha ndugu yangu kabwe zuberi zitto na maporomoko ya nile ambayo maji yake husafiri kwa nguvu ya ajabu sana.
  katika vipindi tofauti tofauti na kwa sababu tofauti tofauti, zitto amekuwa akishambuliwa na maadui zake hasa kutokana na misimamo yake, kwa kipindi kirefu watu wengi walishawishika kuamini kuwa uzalendo wa zitto umetoweka.

  kadri siku zinavyoenda na kadri mtiririko wa matukio unavyoonyesha ni dhahiri nyota ya kijana huyu haiwezekani kuzimwa kwa majungu kama ilivyotakiwa iwe. mtiririko wamatukio unamfanya zitto aonekane kuwa ni shujaa na mzalendo wa kweli katika taifa hili.

  pamoja na kuwa anasimama kidete bungeni kuwatetea masikini na walala hoi wenzetu lakini amekuwa akiyafanya mengi zaidi na zaidi. leo nitataja machache tu.

  1. ni zitto ndiye aliyekuwa mbunge wa kwanza Tanzania tangu mwaka 2000 kupeleka hoja binafsi bungeni ambapo alipeleka hoja ya BUZWAGI ILIYOMLETEA MISUKISUKO

  2. ni zitto ndiye mbunge wa kwanza tanzania tangu kuanzishwa kwa dunia kusimamishwa kushiriki bunge kwa madai ya kusema uwongo bungeni kisa kufichua siri ya waziri wa nishati na madini kwenda kusaini mkataba nje ya nchi kipindi ambacho rais ametangazab marekebisho ya sheria za madini.

  3. ni zitto huyu huyu aliyelishauri taifa kuinunua mitambo ya dowans ili kunusuru nchi isiingie kwenye mgao wa umeme, wakati huo mitambo hiyo ilikuwa ikiuzwa kwa dola elf 40 tu. lakini kwa unafiki wa wanasiasa wetu na wanafiki wachache walishirikiana kuupotosha umma na kusema zitto amehongwa. kitu cha kusikitisha miaka mitatu baadae mitambo ile ile sasa imeuzwa kwa dola mil120 na wanafiki wote wameufyata hakuna tena mzalendo hapo. kwenye hili zitto leo ni shujaa. na mitambo imebadilishwa jina inaitwa symbions na inatuuzia umeme kila kukicha na serikali imeshindwa kesi mahakamani na inatakiwa kuwalipa dowans zaidi ya dola mil50

  4.ni zitto ndiye aliyeongeza ushawishi wa kuwavutia vijana wengi hapa nchini washiriki kikamilifu siasa na kujiona kuwa nao wanaweza na mpaka leo wamepatikana wabunge wengi wa chadema ambao ni vijana. wabunge kama wenje, silinde, highness na sugu ni mfano wa wabunge walioshinda kati ya vijana wengi waliogombea.

  5. ni zitto pekee ndiye kiongozi wa kitaifa wa chadema aliyezunguka sehemu kubwa ya nchi kipindi cha uchaguzi mkuu kwenda kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo mbali mbali-ukiondoa slaa aliyekuwa mgombea urais. mbowe yeye alijifungia hai na maeneo machache ya mkoa wa kilimanjaro.

  6. ni zitto ndiye aliyeasisi operesheni ya wabunge kukataa kupokea posho ya kushiriki vikao bungeni ambapo amekutana na vipingamizi vingi na upinzani mkali kutoka kwa wabunge wa upinzani na ccm.

  7. ni zitto pekee ambaye ndio mbunge peke yake asiyepokea posho za vikao hapa tanzania kati ya wabunge wote wanaojidai leo hii ni wazalendo.

  8. ni zitto aliyeasisi na kulisimamia sekeseke la uwajibikaji la kukusanya sahihi 70 za kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu na kumlazimu rais avunje baraza la mawaziri.

  9. ni zitto aliyewaunganisha wasanii wa bongo fleva na injili kuvunja mikataba yao na kampuni za simu ili waongezewe malipo kutoka 7% ya sasa wanayolipwa.

  10. ni zitto pekee aliyetangaza hadharani kuwa anataka kuwa rais wa taifa hili na kwamba uwezo wa kufanya hivyo anao, uzalendon wa kufanya hivyo anao na uadilifu wa kufanya hivyo anao. zitto ndio mwanasiasa pekee ambaye hafanyi siri dhamira yake ya kuutaka urais, na wala hasubiri ajitokeze kwa kushtukiza hapo baadae, lakini pia inaonyesha haitaji mfumo wa kizamani wa kubembeleza uombwe ili kugombea urais. kwa hili nina hakika amejiongezea maadui wengi ndani ya chama chake na nje ya chama chake.

  kwa hayo niliyoyataja na yawezekana mengine mengi nimeyasahau. kuna kila sababu ya huyu jamaa kuundiwa mazengwe mbalimbali ili kuondoa credibility yake.

  imefahamika pia wapinzani wake wa ndani ya chama chake wameanzisha kikundi maalumu walichokipa jina na OPERESHENI CHAFUA ZITTO..

  kwa hayo machache nawatakia mjadala mwema wakuu.
  narudia tena:- zitto ni maporomoko ya nile hayazuiliki kwa kifusi.
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mbona Waziri kasema MIGAO ya Umeme siku zote inapangwa? Umejitahidi kidogo ila kajipange upya.

  Naona kweli wewe umeingia JF 24 July, 2012.... Karibu sana JF, Kuku mwenye kamba yake Mguuni.
   
 3. Kagwina

  Kagwina Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: May 1, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizo ndiyo zinakupa upofu wa kutokuona mabaya yake! Huyo Kijana tunamfahamu uzuri! Amechenga katika mengi na kutumia CV yake ya umaarufu mwepesi wa kukataa posho sasa hivi kwa sababu ya rushwa kubwa kubwa. Katika hili haponi, hana "moral authority" tena. Mbona anaweweseka sana na tuhuma. Unataka tutoe ushahidi wa msg zake. Hopeless kabisa acheni kuchezewa akili na wanasiasa uchwara wanaotumia matatizo yetu kuapata umaarufu huku wakituumiza kwa kuwaamini.
   
 4. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Nimekuwa nikusubiri kwa hamu sana kusikia majibu ya Mbunge wa kigoma kaskazini Mh.Zitto zuberi. dhidi ya tuhuma za kuhususishwa na rushwa. Mbunge huyu kwa majibu yake ninauhakika atakuwa amewajibu watanzania walio wengi kwamba yeye ni mtu makini,msafi na anajiamini na misimamao yake.

  Kwa yeyote mwenye dukuduku kwamba Ooohhh zitto nimla rushwa ameambiwa aende mahakamani,au aungane na chama chake,au afanye chochote kama kuunda tume aende akamchunguze kwamba yeye ni mla rushwa.Otherwise ni uzushi wapuuzi flani walioamua kupandikiza chuki ili washushe hadhi yake kisiasa.

  Moja kwa moja kwenye Hoja,mwenendo wa CHADEMA kwa siku za karibuni unaonekana kwenda mrama hasa katika maamuzi na kenye utendaji kazi pamoja. Mh.zitto kabwe amekuwa ni moja wa viongozi wa juu pale CHADEMA ambaye amekuwa akianagaliwa kwa jicho la husuda na viongozi wa juu wa chama,hasa jicho hilo limekolea mara baada ya kutangaza nia kuwania urais mwaka 2015.

  Viongzoi hawa licha ya kutuhumiwa na kashfa kama hivi ambazo ni hatari kwa mstakabari wa chama na taifa kw aujumla kama watanzania tutakuja kosea tukawapa nafasi za kuongoza nchi yetu.mfano wa kashfa ambazo majibu yake yalkishawahi tolewa hapahaopa jf ni kama

  KATIBU MKUU WA CHAMA_TAIFA
  Anakashfa zifuatazo ambazo majibu yake yapo(ikibidi kuyaleta yafika) na amewahi kukili hapa JF kipindi flani alipobanwa na wadau hapa Jf.

  1.Kumlipa posho ya tsh;280000 mfanyakazi wa ndani kila siku anaopokwenda kwenye kesi arusha..pesa hiyo ni ruzuku ya chama.
  2.Kujikopesha fedha za kujengea nyumba Kunduchi( nyaraka tunazo na majibu alishatolea hapa-bahati mabyaa sana waliokopeshana mmoja wao ameshamfukuza).
  3.Kulipa kodi kwa mwezi zaidi ya Millioni Moja kupitia ruzuku ya chama pale kijitonyama alipokuwa naishi awali(Abla apartment)
  4.Kukopeshana pesa za uchaguzi na mbunge wa iringa(viti maalumu) na kupanga matokeo ya uchaguzi huo..mgogoro hadi leo haujaisha pale iringa
  5.kumufukuza/kwafukuza viongozi wa mbulu na Shunyanga kwa sababu tu walmeonekana wakiunga mkono sera za ZZK
  6.Kufukuza kazi wakurugenzi bila kufuata kanuni ilimradi nafasi hiyo akabidhiwe Joseophine(mama Joniour)
  7.Anakashfa ya kujilipa mshahara wa Million 7 kwa mwezi,ili hali katibu mkuu wa mkoa,wilaya,kata hapewi hata cent moja ya posho wala mshahara.

  MWENYEKITI
  Yeye anakashfa ya kukiuzia chama magari mabovu kwa bei ya dukani,Pia kujikopesha Million 300 kwaajili ya matumizi yake,Kuchelewesha na kupitisha vifaa vya chama bandari ya kenya vikitokea china,Nabaada ya hapo nusu hushuka Arusha na Kiasi kusambazwa mikoa iliyobaki hali inayosababisha kuishiwa kwa vifaa upande mmoja wa nchi.

  Pia kukwepesha pesa iliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa chuo kibaha. (ikumbukwe majibu ya kashfa hizi yapo na katibu mkuu alikili wazi hapa JF kwamba ni kweli).

  Kutokana na uchafu kama huu ni dhahiri si rahisi kwa watu hawa kupikika chungu kimoja,Kilichotokea ni kwamba wabunge na baadhi na viongozi hawa wameunda mtandao ambao umelenga kujiimarisha kisiasa na kuzika siasa za kijana huyu wa kigoma.
  ZITTO Alipotangaza nia ya kugombea urais,ameukwa akiwekewa vikwazo vya kila namna juu ya kufanya mikutano ya hadhara.

  Ndio maana unaona Zitto hapewi nafasi ya kufanya mikutano ya hadhara kwa sabau ya kwamba hakuna pesa, lakini wakati huohuo kunawatu wanazunguka na CHOPPER nchi nzima kwa lengo moja la kuimarisha na kutafuta wajumbe wa mkutano mkuu watakao kuwa upande wa kaskazini.

  Sasa kwa mazingira kama haya wala usishangae akina Nassari wanavyosimama Bungeni na kumuomba spika wa bunge aivunje kamati ya zitto kwa madai kwamba imejawa na rushwa.

  Zitto anafanya siasa za kishujaa kicha ya maadui wake kuwa wengi,lakini YEYE ANASEMA HATO SALIMU AMRI MBELE YA WATU WAOVU KAMA HAWA.MWISHO WA SIKU ZITTO ATAFUNGA MLANGO THEN TUZUNGUMZE KWA VITENDO

  NI hatari kwa chama kama kweli wabunge wa ccm na chadema wanafikia hatua ya kuungana kwa lengo la kumdhalilisha zitto kwa sababu tu haivi na top head's.
  Jf Jukwa huru nawasilisha.
   
 5. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  ulipenda nijiunge lini?...chambua hoja nilizoziweka usinichambue mimi
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Kazi imeanza tutasikia mengi kuelekea uchaguzi mkuu.
   
 7. M

  Mpwechekule JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imeandikwa huwezi kumsafisha mtu kwa matope zito anachezea matope ili apate ujira wa mwiha kwa wakoloni weusi, ni sawa na wabunge wengi wa ccm wanaopitisha bajeti ambayo haina miradi ya maji na barabara halafu wakati wa kuchangia wanataka maji na barabara, zito ni mnafiki nimeamini hilo, sasa nanyie wafuasi wake hampendi zito ndio maana mnamtuma kazi ambayo nyie imewashinda, mtaweza kugombana na wakati?
   
 8. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  wewe mbona unafahamika kuwa ni wale wale wabunge wanaolilia posho hahahaha aibu yako ndugu yangu...nimechunguza kwa kirefu na nimekubali kuwa zitto ni kiboko japo anawachoma sana
   
 9. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  kamwe chadema haiwezi kuungana na ccm kufanya siasa za maji taka kwa wanachama wake.Chadema mwanachama akikosea kuna vikao halali vitamuita na kumhoji and then maamuzi ya kikao yanawekwa wazi.Siyo ccm miaka nenda rudi vinara wa ufisadi wanaojaulikana waziwazi ndo wanazidi kukumbatiwa ccm
   
 10. B

  Bob G JF Bronze Member

  #10
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Inahitajika akili ya kiwenda wazimu kutakatisha kaniki, utachubuka mikono bure haitatakata nenda kwenye Poll majibu yatakutosha
   
 11. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  jadili hoja nilizoweka hapo.
  wabunge wako wasio wanafiki wamesimamia nini tangible mpaka hivi leo?
   
 12. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,972
  Likes Received: 37,537
  Trophy Points: 280
  Mbona hakuna hata mmoja wenu aliethubutu kumtaja hadharani na kuonyesha ushaidi.Hizi tuhuma za kupanga ndio mtaji mzuri kwa Zitto maana ukweli utajidhihirisha tu tena siku si nyingi.Ni sawa na kumpiga teke chura ukazani unamkomoa kumbe umemsaidia kufika anakoenda.
   
 13. c

  chasuzy JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 449
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  tuhuma katika kamati ya zito azijaanza juzi ni tangia kipindi waziri wa fedha mustafer mkulo,zito ahandamwi na viongozi wa chadema bali ni wabunge wa bunge la jamuhuri ya muungano tanzania,hoja si yy kutaka urais kwani:-

  1.muda wa kuchukua form bado,na JK ndio kwanza ana miaka miwili tu
  2.kikatiba umri wa zito 2015 atkuwa bado ajatimiza sharti la umri

  Zitto ajanyimwa fursa ya kufanya mikutano, pengine ww kutokana na mapenzi makubwa uliyonayo kwake unashindwa kuona jongo unang`ang`ania ni kengeza,katika jimbo lake kafanya mikutano mingapi?kigoma mjini?mkoa wa kigoma?au pesa hakuna?.Pia inaonekana masuala ya pesa ndani ya chadema uyajui ndio maana unarejea ushaidi wa kusadikika waulize wahusika utajua ukweli.Rushwa ni tatizo lilopo bungeni leo zito kaongea na waandishi wa habari kafafanua vizuri sana nahisi ujamsikia
   
 14. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  mtapambana lakini hamtashinda. Aliyekutangulia amekutangulia tu. Zitto amewaacha mbali sana wagaza
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Hakuna anae bisha kuwa Zitto
  ana karama au kipaji au uwezo wa kisiasa ambao
  ni above average ...

  tatizo ni honesty.....

  is he honest enough?
  can he be trusted?
   
 16. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #16
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  chasuzy mimi sijakuelewa kwa kweli
  fafanua kidogo unachomaanisha tafadhali
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #17
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwenye mada unapewa alowernce sh ngapi kusafisha kaniki? Au unapigaga kishoka kwenye hama? Ohh sorry au umeahidiwa kuwa fist lady wetu 2015?
   
 18. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #18
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  i trust him
  he is my next president. No doubt
   
 19. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,628
  Likes Received: 2,049
  Trophy Points: 280
  JF ni zaidi ya burudani hasa ukisoma comment za watu, napita tu no comment
   
 20. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  The next president zitto zuberi kabwe
   
Loading...