Mzito Kabwela
Platinum Member
- Nov 28, 2009
- 18,908
- 7,752
Kwahiyo JK ametulia na ndivyo anavyoipeleka nchi hivi...?
Umdhaniaye ndie kumbe sie...! mnaweza kumpa nchi mtu msietarajia akafanya mambo ya maana kuliko hawa ambao mnaowatarajia.
Kwanza ni zamu ya Wakristo. So long as Zitto ni mjahidina asubiri mpaka 2025
Kwa ushauri wa bure epuka sana hizi siasa zenye mlengo wa kugawa watu.Nadhani kwa nilivyofuatilia mjadala huu na hao wanaokutuhumu kuwa wewe unashirikiana na Zitto katika hiyo mipango yenu mnaoijua wenyewe soon itafumuka na mtaabika vibaya sana.Hawa wanaojadili humu na kutokumuunga mkono Zitto sio kwamba hawamkubali ama sio wafuasi/wanachama/wapenzi wa chadema,la hasha! hawa ni watu wanajadili kwa kina athari za maamuzi ya kamanda wao kimtazamo zaidi.Bitabo,
Naona sasa mjadala unaanza kuwa balanced.watu wameanza kuelewa kuhusu hii debate..........!
Kuna watu wanapima upepo utawaona watakavyokuja hapa kujifaragua na kujifanya weledi lakini watajenga hoja nje ya mantiki.Kuna wengine watakuja watajenga hoja basid on logic
Zaidi,tusubiri vijigazeti uchwara na siku hizi viko vingi.Anyways,Mwanahalisi halitabaki nyuma katika kujaribu kurudisha imani ya weledi.................!
Hakika wewe una utindio wa Ubongo. ZITTO ndiye anafaa kuwa Rais wa 2015, hayo uliyoyasema kuwa ZITTO hanayo sijui umempinga kwa kutumia nini? binafsi mimi naona kama unawalamba miguu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Chama kuwa ndo wanafaa, jambo ambalo naona kama bado ni mawazo mgando ambayo yanahitaji mapinduzi. ZITTO amekafanya kazi chini ya SLAA na MBOWE kwa muda muda mrefu sasa hawezi kukurupuka kutangaza kugombea Urais bila kujua udhaifu wa viongozi wake. Tusisahau pia kuwa CHADEMA ina watu wengi maarufu ambao kwa namna moja au nyingine baadhi yao watakuwa wamemshauri ZITTO kutangaza nia yake ya kugombea urais. Nashauri ZITTO ashindwe kugombea kwa hoja na siyo kusimama jukwaani na kusema hana sifa wakati vijana wenzake tunaona ndiyo mtu muafaka.Wana jf hii nimeinasa kwenye blog iitwayo yerickonyerere.wordpress.com
Nimeshangaa kuona kumbe wengi wanamuogopa zito kiasi cha kusema sana.
25 Mar 2012
Tanzania ni nchi iliyo mithiri ya karia hivi leo na ni nchi yenye lasilimali adhimu duniani,
Jambo la kujiuliza ni je watanzania ni watu wa aina gani? wanaendana na Tanzania ilivyo?
Ukweli ni kuwa watanzania ni wanafiki wakutisha zaidi ya baraza la Sanhedrin, unafiki wetu unatisha kwakuwa umechanganyika na ujinga, Hatuendani kabisa na wasifu wa taifa, Jambo hili ni hatari kwa mstakabali wa taifa kwakuwa kati yetu wajinga na wanafiki kumeibuka kundi la wahuni
Wahuni hawa ambao mbegu yake ni ujinga na unafiki wamekuwa hatari kuliko kawaida, haimithiriki hata kuwatazama kwa jicho la makengeza tu.
Watu hawa wahuni, wanafiki na walanguzi wa fikra wamefanikiwa kuvunja mlango wa siasa za Tanzania na kujikita humo wakiliyumbisha taifa watakavyo, Wanatumia mwito wa utandawazi msonge kujidukiza kisiasa.
Ninavyoamini taifa halijengwi na mwanasiasa bali mwanasiasa ana nafasi kubwa ya kulivunja taifa! Sasa tukiacha siasa hizi za kinafiki zitamalaki ndani ya ardhi ya Tanzania, vitukuu wetu watakuja kuyachapa viboko makaburi yetu. Watanzania kila mmoja kwa imani yake turudi uwalii.
Nashangaa namna siasa za majitaka zilivyoshamiri, magazeti na wanaoitwa waandishi tegemezi nao hawana tofauti, magazeti yamejaa taarifa ambazo hazina msaada wowote kwa watanzania, hatusikii juu ya Mafuta yetu, juu ya dhahabu yetu, juu ya ardhi yetu, juu ya kilimo chetu, juu ya afya zetu, juu ya utamaduni wetu, juu ya tunu za taifa, juu ya mustakabali wa taifa na utaifa wetu.
Heshima yetu imepotea mbele ya walimwengu, utu na nafasi yetu imedharaulika, wengine wanatuamulia mambo yetu, Kenya imetutawala, imetuzuia kujenga barabara serengeti, tumefyata mkia, wazalendo mkowapi? wapiganaji mkowapi? Wenye nchi mkowapi? Arumeru ni kitu kidogo sana ndani nchi, mama zetu, baba zetu, dada zetu, kaka zetu, wadogo zetu vijijin wanalia hawana afya, magonjwa, njaa umasikini vimewazonga, tunafanya nini mijini? Ni hili la Pamela Lowassa, Siyoi Sumari, na Nassari?
Nashindwa kuelewa, nchi imebaki na Wasira tu? Nape? Ndio policymakers wetu? Mwigulu? Slaa? Zitto? Kweli jamani? Usalama wa Taifa mnabeba dhamana kubwa sana ndani na nje ya ya Tanzania, fanyeni kazi kwaajili ya taifa la leo na lakesho si kwa kikundi fulani wala chama furalani, rasilimali zetu zinatoroshwa na magenge mumiani laki taasisi hii ipo na inatajwa kuwa kila palipo na watu watano basi mmoja wao ni Usalama wa taifa, lakini kwanini hali iwe hivi?
Tutumie fikra machipuko kwa upinde wa kijana, japo kuwa vijana wengi wanaakili za kuku, lakini kwa sauti ya mangamuzi ya hekima watafunguliwa na kuacha utegemezi wa fikra,
Mimi ni muamini wa mtandao wa Twitter nikihudumu kwa njia ya @YerickoNyerere Niseme wazi, nimefadhaishwa na baadhi ya wanaoitwa wanasiasa vijana, hasa kijana mwenzangu mbunge wa Kigoma Kaskazini ndugu Zitto Zuberi Kabwe
Nimemtaja Zitto Kabwe kwakuwa anatumia ujinga na unafiki wa watanzania hasa vijana kujidukiza kisiasa kwa hoja dhaifu ya umri wa uraisi, na amefanikiwa kuteka mioyo ya wakware wa fikra kinyume na haki ya fikra huru.
Ukifuatitia vijana wengi wanaojadili na kuunga mkono juu ya hoja hiyo ya Umri wa Urais utabaini kuwa ni waumini wa upepo wa Zitto, Hawasemi faida ya hoja yao, wala hasara ya umri utumiwao kwa sasa, bali kwa jicho la tatu wamekuwa ni mashabiki wamuangaliao Zitto tu bila kujua mstakabali wa taifa lao.
Zitto ninamwamini sana kiutendaji ndani ya chama chake na nje ya chama, kupingwa kwa hoja yake hakutafsiriwi kuwa si kijana mtendakazi bora laa hasha, bali ni ashirio la kengele imwamshayo toka usingizini, tena usingizi wa ulevi mtawalia wa sifa za kisiasa.
Urais ni taasisi nyeti sana, tena hii ni nchi yoyote duniani huheshimu sana taasisi hii, Nimestushwa sana kuona kijana wetu Zitto aliyeonyesha dalili nzuri za kujengeka kisiasa na kiuongozi, akiwahi kuopoa nyama hata kabla ya kunawa mikono, anasema ndio ninautaka urais Hii ni kauli rahisi sana kisiasa lakini inabeba ujumbe wa aina mbili kwa mwanasiasa na raia wa kawaida.
Anawaarifu wanachama wake na wapambe wake kuwa uchaguzi ujao atagombea urais
Anawaonya viongozi wenzeke ndani ya chama kuwa yeye sasa ndiye lulu pekee ya urais.
Zitto bado hajafikia kuwa kiongozi wa juu zaidi kitaifa ndani ya chama chake achilia mbali kuwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Urais unahitaji hekima, Zitto hana kwa sasa, Urais unahitaji busara, Zitto hana kwa sasa, Urais ujasiri wa kweli Zitto hana kwa sasa,Urais unahitaji mtu wa kutafakuri, Zitto hana kwa sasa, Urais hauhitaji mtu mnafiki, Zitto kwa sasa ni mnafiki, Kwa ujumla Urais unahitaji mtu aliyepevuka, na Zitto bado hajapevuka.
Zitto anarubuniwa na kundi la wenye mtindio wa ubongo hasa vijana, wanaomuaminisha kuwa kapevuka na aweza kuongoza kizazi hiki cha nyoka ilihali bado safari yake ni ndefu.
Nimsihi kijana mwenzangu Zitto Kabwe, kuwa ni kweli anautaka urais lakini avute subira na kauli yake imeweka kovu ktk safari yake kisiasa, ambapo atumie muda uliopo kuliziba kovu hili. Ajitahidi kuwa na kifua kigumu chenye kuhifadhi magumu ya kisiasa, Si kila hoja imuhusuyo ni lazima aijibu na akiamua kujibu awatumie washauri wa masuala ya kisiasa.
Turekebishane ili kujenga taifa lenye uchumi imara, demokrasia imara, na siasa safi!
Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki afrika!
Hakika wewe una utindio wa Ubongo. ZITTO ndiye anafaa kuwa Rais wa 2015, hayo uliyoyasema kuwa ZITTO hanayo sijui umempinga kwa kutumia nini? binafsi mimi naona kama unawalamba miguu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Chama kuwa ndo wanafaa, jambo ambalo naona kama bado ni mawazo mgando ambayo yanahitaji mapinduzi. ZITTO amekafanya kazi chini ya SLAA na MBOWE kwa muda muda mrefu sasa hawezi kukurupuka kutangaza kugombea Urais bila kujua udhaifu wa viongozi wake. Tusisahau pia kuwa CHADEMA ina watu wengi maarufu ambao kwa namna moja au nyingine baadhi yao watakuwa wamemshauri ZITTO kutangaza nia yake ya kugombea urais. Nashauri ZITTO ashindwe kugombea kwa hoja na siyo kusimama jukwaani na kusema hana sifa wakati vijana wenzake tunaona ndiyo mtu muafaka.
Wanajf ebu tupevuke, tutakosa thamani ya kuwa great thinkers, hakuna anayemwonea wivu zito, so what ila huu ndo ukweli, zito analewa sifa, kiongozi wa watu hajioni anafaa ila huonekana anafaa na kuambiwa afanye nini. Zito you have lost my brother naomba ufuate ushauri wa huyu mwandishi na wanajf tuache ulimbukeni tuseme ukweli na si kushambuliana kwa matusi ila tujadili hoja, tukiwa hivi jf haitakuwa tofauti na Facebook.
Kwanza ni zamu ya Wakristo. So long as Zitto ni mjahidina asubiri mpaka 2025
Mkuu utatoka povu sana lakini siwezi kuficha hisia zangu wala ninachoamini.Dr Slaa atakuwa Rais bora mwaka 2015 kuliko mtu yeyote ndani ya CD M.Huu ni mtazamo wa wengi ndani ya CDM kwa sasa.Slaa anaungwa mkono na wazee na vijana ndani ya chama.Huu ndio ukweli.Kina Mbowe,Zitto na Lissu tunawahitaji wawe wabunge ili Slaa apate serikali imara.Mimi siwezi kuficha ninachoamini.Anayeibuka sasa kubishana na Slaa anapoteza muda wake na anataka kujiangamiza kisiasa mwenyewe.
Mkuu nisome vizuri utambue nilichokimaanisha!! Hakuna nilipotaja umri!!
Pia mkuu kuifananisha Tz na huko kisiasa binafsi naona unakosea, siasa za wenzetu na demokrasia vimekomaa nchi inajiongoza, tofauti na hapa home ambapo nchi inahitaji kuongozwa!! Tz inahitaji mtu ambaye amekomaa kiuongozi, kisiasa na kidemokrasia!
Binafsi sina tatizo na Zitto kutangaza nia, isipokuwa naangalia je, ni mda muafaka kufanya hivo, Amekomaa?
Kiongozi unakiwa KUONWA sio KUJIONA!!
Najua kitakachomtokea ZITTO kama ataendelea na msimamo wake ndani ya CHADEMA...wanaweza kum HAMAD RASHID au kum KAFULILA. Haya bana ngoja tuone mwisho wake.
siku ile ya msiba wa regia huyu zitto alikuja na bonge la article ambalo ndani yake kwa jicho la tatu limejaa unafiki na uzandiki.....sikufurahishwa na ile article hasa aliposema hivi '' Regia Alishinda kura za maoni katika mchakato wa ndani ya chama. Katika kikao cha Kamati Kuu mmoja wa Wakurugenzi wa Chama akasema tunaye mgombea mwingine mzuri sana, Mwanasheria. Regia akaombwa kukaa pembeni. Akakubali. Kamati Kuu ikampitisha mtu ambaye hakwenda kwenye kura za maoni na wala hatukuwa tunamjua maana tuliambiwa na mtu tunayemwamini kwamba ni mgombea mzuri. Regia hakufurahishwa na uamuzi ule lakini kwa heshima na utiifu wa hali ya juu akakubali kutogombea. Siku za kurejesha fomu za kugombea zilipokuwa zinakwisha yule mgombea akatoa nje. Hakuonekana, kwa sababu mbalimbali ambazo sisi tuliokuwa mbali na Dar es Salaam na Morogoro hatuzijui. Chama hakikuwa na namna isipokuwa kurudi kwa Regia kumwomba aokoe jahazi. Regia hakusita. Akaendesha kampeni za uhakika akiwa hana mali wala jina kisiasa''........haya ni mambo ya ndani na siri za chama hakupaswa kuyasema....
leo tena katika makala yake hiyo yenye kichwa cha habari ''ndiyo nautaka uraisi'' kna mahali anasema ilikuwa ni vigumu sana kumshawishi mnyika kujiunga chedema tena alikuwa haipendi kabisa....haya sio manoeno mazuri ya kusema...
all in all zitto hafai kuwa rais kwa sasa...ajenge chama then chama kikishika dola huko mbele atajikuta anakubalika tu kugombea huo uraisi na wananchi ndio watasema kwa zitto anafaa lakini sio kuja na kauli za kirafi hapa '' NDIO NAUTAKA URAIS''..... huu ni urafi