Zitto: Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"

Zitto: Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"

Haya si mapambano ya ZZK. Ni mapamabano ya wananchi dhidi ya dhulma. Hakuna cha mbadala, kwani nani alimweka ZZK hadi tuulizwe mbadala. Kwani ZZK ni nani katika mapambano kiasi cha ombwe lake kuonekana.

Lazima tupigane kama wananchi na si jeshi la mtu mmoja.
Tumejifunza, baada ya kupelekwa Uswiss na kuachwa huko bila ticket ya Siwss air kurudi nyumbani.

Haya ni mapambano yetu si ya mtu.

Mapambano ya wananchi ni kutaka Pesa zetu zirudi ,basi, hayo mapambano yenu(yako) dhidi ya ZITTO ni yenu na si ya wananchi
 
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya Kamati ninayoongoza ya PAC kuwasilisha Bungeni Taarifa Maalumu kuhusu ukaguzi maalumu wa akaunti ya Tegeta Escrow, kumekuwa na kampeni za chini chini zinazoendeshwa kwenye korido za Bunge na kwenye mitandao dhidi yangu binafsi na baadhi ya wabunge waliosimama kidete dhidi ya wizi wa fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania akaunti ya Escrow.

Baadhi ya tuhuma nimezipeleka kwenye vyombo vya dola ili zichunguzwe kwani zina vielelezo vya mahala pa kuanzia (kama leseni ya udereva ya mwanamke anajulikana kama Vivian Emmanuel Sirikwa na muhuri wa kampuni ya uwakili inayomilikiwa na Bwana Joseph Mkandege). Baadhi ya tuhuma nitazijibu moja baada ya moja.

Waziri mmoja ambaye ni mtuhumiwa wa wizi wa fedha za Tegeta Escrow anazunguka kwa wabunge akisema tuhuma hizi kupikwa kama njia yake ya kuhamisha mjadala kutoka uporaji wa Tshs 200 bilioni kwenda kwenye masuala binafsi.

Tuhuma hizi zenye kichwa cha habari "Zitto na Filikunjombe wanatumiwa na Kenya na Uingereza kuvuruga na kudhoofisha Uwekezaji nchini mwetu" zinajibiwa hapa chini. Utaona ndugu Filikunjombe ametajwa kwa kichwa cha habari ili kumtaja tu bila sababu yeyote ile.

Tuhuma #1 :

Zitto anaye rafiki yake Mkenya aitwae Rapahel Ongangi ambao kwa pamoja wameanzisha Gombe Advisors Co. Ltd (registered on 24 November 2011, Certificate No 87387) kwa ajili ya kufanya biashara na Makampuni ya Gesi na Mafuta yanayofanya kazi nchini hapa.

Majibu:

Gombe Advisors ni kampuni binafsi isiyofanya faida yaani ‘Company Limited by Guarantee’. Haina kazi na kampuni yoyote ya Gesi na Mafuta na wala yenyewe haijuhusishi na biashara hiyo. Gombe advisors haijafanya kazi yoyote ile na kampuni nyingine zaidi ya kusaidia wasanii wa kundi la Kigoma All stars. Upotoshaji hapa unalenga kupindisha mjadala.

Tuhuma #2 :

Zitto amemsaidia Ongangi kupata uraia wa Tanzania na kwa sasa ni raia wa pasipoti. Zitto na Ongangi walimtafutia CEO wa Shell aitwae Axel Knospe nyumba na gari ya kukodi.

Majibu:

Raphael ni mtu binafsi ambaye anafanya shughuli zake hapa nchini, amesoma hapa nchini na ameoa na ana mtoto. Tuhuma hizi hazina msingi wowote ule maana ni uwongo. Wanaotoa tuhuma hizi waonyeshe hiyo pasipoti ya Bwana Ongangi kuthibitisha madai yao.


Tuhuma #3 :

Mikataba ya STATOIL iliyokuwa inarushwa kwenye mitandao ya jamii na kuchapishwa kwenye magazeti ya Kenya ya hapa nchini (The Citizen na Mwananchi) mwandishi mkuu alikuwa huyo CEO wa Shell.

Majibu:

Mkataba uliovujishwa wa StatOil ulivujishwa na waandishi wa habari wa Norway. Uchambuzi wa mkataba huo nimeufanya mwenyewe kwa kutumia utaalamu wangu niliosomea wa kuchambua mifumo ya kodi kwenye sekta ya mafuta na gesi. Kwa namna yoyote ile, huyo anayetajwa kuwa CEO wa kampuni ya Shell hahusiki. Tuhuma hii wanaoitoa watoe ushahidi usio na chembe ya mashaka.

Ikumbukwe kuwa mkataba wa StatOil utaipotezea Tanzania mapato ya dola za Marekani bilioni 12 (takribani Tshs 20,400,000,000,000/=) katika kipindi cha miaka 15 baada ya gesi kuanza kuchimbwa. Uamuzi wa Kamati ya PAC kutaka mikataba yote ya Gesi kuwa wazi una lengo la kuchambua kuona kama mikataba yote nchini haipotezi mapato kwa nchi. Uamuzi huo umewakasirisha sana baadhi ya waliohusika kuingia mikataba Serikalini maana wanajua kuna madudu kwenye mikataba na wanataka umma wa watanzania usijue!

Tuhuma #4 :

Kampuni ya SHELL imechukizwa sana kucheleweshwa kwa kupata kibali cha kutafuta gesi na mafuta kule Pemba. Vilevile SHELL haina uwekezaji mkubwa Tanzania Bara kwani ilishindwa kwenye tenda zenye vitalu vyenye gesi nyingi upande wa Bara.

Majibu:

Ukweli ni kuwa Kampuni ya Shell ina vitalu 4 huko Zanzibar na tayari ina makubaliano na Serikali ya Zanzibar kuhusu utafutaji mafuta huko katika vitalu namba 9,10,11 na 12. Shell inafanya kazi na kampuni ya Petrobras ya Brazil kwenye kitalu namba 6 na namba 8. Taarifa hizi zipo wazi kwenye tovuti ya TPDC. Tuhuma nyepesi namna hii dhidi ya kampuni kubwa kama Shell zinaonyesha dharau na kiburi kinachotokana na uelewa mdogo wa mambo wa watu wanaotuhumu.

Tuhuma 5:

Ongangi anapokea maelekezo kutoka Serikali ya Kenya kuhujumu uwekezaji nchini mwetu.

Majibu:

Nazifahamu mbinu nyingi zinazotumika kufanya propaganda, lakini mbinu hii imeshindwa ikiwa mapema sana. Ni vema wanaotoa tuhuma hizi wazithibitishe vinginevyo ni mwendelezo wa propaganda zisozingatia diplomasia ndani yake dhidi ya jirani zetu wa Kenya. Hizi ni propaganda hatari ambazo hata hao wanaotuhumiwa wakisikia watatudharau sana.

Tuhuma #6 (juu ya Uingereza):

Uingereza imekuwa inamfadhili Zitto kwa miaka mingi kwa mambo yake ya kisiasa kwa hiyo sasa hivi Ubalozi wa Uingereza unamlipa Zitto na Kafulila kuhakikisha kwamba Standard Chartered ya Uingereza inalipwa deni lake lisilotambulika kisheria nchini mwetu.

Majibu:

Nimetangulia kusema hapo awali kuwa kuna propaganda ambazo haziangalii hata diplomasia; nyingine ni hii. Pamoja na kukanusha uzushi huu, ni vizuri wanaotoa tuhuma za namna hii kuthibitisha. Mimi binafsi sijawahi kufadhiliwa kisiasa na Taifa lolote lile. Inaelekea kuna wanasiasa wanaofadhiliwa na mataifa mengine ambao kwakuwa kwao ndiyo maisha wanaamini na wengine tupo kama walivyo. Kwangu itikadi yangu ni ‘Uzalendo kwa nchi yangu’, ni jambo ambalo halina mbadala wake. Siku zote nasema “Right or wrong, my country first". Kurudia kurusha tuhuma kwa Ubalozi wa Uingereza nchini ni kudhihirisha kwa mara nyingine kiburi cha kuwa na mamlaka (arrogance of power) walicho nacho wanaotuma tuhuma hizi.

Aidha, wanatuhumu kuwa “Kafulila na Zitto wamehaidiwa 15% ya USD 150 million kama deni likilipwa”

Mtanzania anayeweza propaganda dhaifu kama hizi basi anatakiwa ajitafakari. Hata hivyo ni vema wanaotoa tuhuma hizi wathibitishe bila chembe ya mashaka.

Tuhuma #7 :

Mbunge Mkono nae ameshikwa hasira kupoteza kazi ya uwakili pale TANESCO. Kafulila na Zitto wanalipwa na Mkono kuvuruga Serikali kwa hasira za kukosa fedha za kitapeli za TANESCO.

Majibu:

Hizi ni tuhuma ambazo sasa tumezizoea kutolewa. Mambo mepesi hayawezi kujibu mambo ya msingi kama tuhuma za wizi wa fedha zaidi ya Tshs bilioni 200 kutoka Benki kuu ya Tanzania. Kukusanya kila propaganda ili kuuhamisha umma ni kupungukiwa hekima na busara.


Aidha, wanaotuhumu wanadokeza kuwa “Naomba tuwe macho na Wabunge wetu achananeni na madai ya Zitto ya wizi. Huyu mtu anafanya biashara na Kampuni ya SHELL na inasemekana analipwa na Ubalozi wa Uingereza. Serikali ya Kenya na tapeli mkubwa Mbunge Mkono nae anawalipa Zitto na Kafulila”.

Watanzania, haya ni maneno ya hasira ya watu wanaokaribia kukamatwa kwa kushiriki wizi wa fedha katika Benki kuu ya Tanzania. Kamwe tuhuma kama hizi haziwezi kutukatisha tamaa katika kupambana ili ukweli ujulikane. Sisi tutapigana kwa ajili ya Taifa, kwa ajili ya mtanzania na tunachotaka ni umma uujue ukweli wa mambo.

Hasira hizi zinatokana na mambo mawili:

Moja ni uamuzi wa kamati ya PAC kuwasweka ndani baadhi ya watendaji wa TPDC kwa kushindwa kutekeleza maamuzi ya Kamati yanayohusu uwazi wa mikataba ya Gesi na Mafuta.

Pili, ni uamuzi wa PAC kuagiza ukaguzi maalumu wa mchakato mzima wa kuanzishwa na kufungwa kwa akaunti ya Tegeta Escrow ambapo zaidi ya shilingi bilioni 200 ziliporwa na zaidi ya shilingi bilioni 12 zinalipwa na TANESCO kila mwezi kwenda kampuni ya PAP inayomilikiwa na Harbinder Singh Seth (50%) na watu wasiojulikana kupitia kampuni ya Simba Trust iliyosajiliwa na kufichwa nchini Australia (50%).

Ieleweke kuwa PAP inalipwa shilingi milioni 400 kila siku kutoka TANESCO izalishe au isizalishe Umeme! Watanzania, PAP itaendelea kulipwa namna hiyo kwa miaka 20 ijayo. Kwa namna ambayo Seth analindwa na baadhi ya watendaji Serikalini na hasa ndani ya Wizara ya Nishati na Madini. Aidha, kuna fununu kuwa kuna maofisa serikalini wanaomiliki hizo 50% za kampuni ya PAP. Seth pia anamiliki kitalu cha gesi Mnazi bay Kaskazini kupitia kampuni ya HydroTanz.

Hasira hizi walizo nazo wanaonituhumu na Kamati yangu zimewapelekea kugushi nyaraka mbalimbali zinazonituhumu mimi na wenzangu ili kutuogopesha na kutukatisha tamaa katika kutafuta ukweli juu ya suala la uporaji wa fedha kutoka Benki kuu. Lengo lao ni kututoa kwenye mstari. Mimi na wenzangu hatutatoka kwenye mstari, tutashirikiana na wabunge wenzetu kuhakikisha ukweli unajulikana na wezi kuchukuliwa hatua kali.

Harbinder Singh Seth aliiangusha Serikali ya KANU nchini Kenya, sasa anachotaka kukifanya kinaweza kuiangusha Serikali ya CCM wakiendelea kumkumbatia. Watanzania sio mabwege!

Zitto Kabwe
Mwenyekiti PAC

Dodoma, 9 Novemba 2014

Stop looking for sympath, man up & tell us what business did you do in this short period of time that made you to own big?
 
Hapa suala si Zitto. Tena ni makosa kutaja jina la Zitto. Suala ni mada iliyopo mbele yetu ambayo imeandikwa na Zitto na ndipo bahati mbaya anapotajwa. Hatuna tuhuma na ZZK, tunataka majibu ya maswali yetu
Mkuu Nguruvi3, yapi hayo maswali?
 
Last edited by a moderator:
Pesa za Marubeni bilioni 70 inasemekana zimerudi. Je hiyo ndiyo njia sahihi?

Unachotaka kusema ni kuwa katika vita hii watu wachague kurudishwa kwa pesa hata kama kuna mtinange wa pembeni au kuna motive nyingine. Hapana tunataka pesa zirudi lakini pia Zitto afafanue kile alichokiacha katika maelezo yake.

1. Mkandege alitoa mhuri au ulikuwa feki. Hili litasaidia pande zote, za Zitto na wengine kujua ukweli wakati wa mapambano
2. Je ni kweli Ongangi ameshiriki kuanzisha Gombe, na ushiriki wake upoje kama upo. Ni kweli au hapana
3. Gombe na Laketugite zinafanya kazi ya ushauri na zina ushiriki wa Zitto. Je, zinafanyaje kazi hiyo na Ongangi anashiriki au hashiriki vipi
4. CEO wa Shell anadaiwa kutafutiwa nyumba na ZZK. Je, ni kweli au si kweli

n.k.

Tupo pamoja katika mapambano dhidi ya Mafisadi, lakini ni hatari kama tunakwenda vitani kutafuta haki wengine wakitumia vita hiyo kutafuta namna nyingine. Ndivyo tulivyopelekwa Uswiss na labda nikuulize, zile pesa za Uswiss zimerudi zaidi ya political stunt. Hivi na hili lisilo na majibu kwanini tusihoji ili tujue tunakwenda vitani kwa lengo nmoja la kukabiliana na ufisadi.

Nyumba ya bilioni 2.5 ya gavana tuliungana pamoja, mwisho wa siku ni ZZK huyu akasema deal ni safi.
Leo tunajua kuna mengine yanayohusiana na kauli ya 'clean deal''. Tumeachwa njia panda.

Kila siku tunaomba maji njia panda, tutakunywa madafu hadi lini? Kwanini tusitafute ramani kabisa safari hii ili tusijejikuta njia panda tukinywa madafu kwa kiu ya kuachwa na mwenzetu?

Usizidi kujishusha kwa kiwango hiki kama mtoto wa shule ya msingi sasa...ebu anzisha thread nyingine naamini Zitto atakujibu huko.

Shame on you
 
Labda kama kuna Mtu anatumia ID yako, ww sio yule...too low for you
Yaan kuna watu hizi chuki zinawashushia sana heshima.Yaan Nguruvi kageuka akili kama mtoto wa Chekechea?kweli upambe ni mbaya sana.
 
Usizidi kujishusha kwa kiwango hiki kama mtoto wa shule ya msingi sasa...ebu anzisha thread nyingine naamini Zitto atakujibu huko.

Shame on you
Teh teh Kazi kweli kweli Aanzishe thread Nyingine ili iweje?

Kwn hii imewekwa na nani?

Nguruvi3 Kajishushaje wakati hoja zake hazina majibu?

Huwezi kujibu tuhuma kwa kuchagua maswali ya kujibu.
 
Last edited by a moderator:
Kwann usiende kupata hayo majina kwa KUB, badala yake unataka hayo majina kwa msaliti, idiot

Mfyuuuuu

sasa matusi ya nini wewe! Mkikamatwa mnabaki na viroja km hizi siyo

pole zenu
 
Kwann usiende kupata hayo majina kwa KUB, badala yake unataka hayo majina kwa msaliti, idiot

Mkuu Granta unajua maana ya neno KUB,ni Kiongozi wa Uhuni Bungeni
 
Last edited by a moderator:
Wenzako wanasema Zitto ni maskini tu alishindwa hata kuwa na mil.6 za kumtibia mama yake

We unakuja kumtuhumu kuwa ana ukwasi wa kutisha

Hivi chuki zenu zinalisaidiaje Taifa
I told him to man up n come out clean
 
Yapo kwa Godbless Lema

Mkuu naiona Escrow ikienda na wengi tena ilivyowataja na viongozi wawili toka upinzani ndo basi jamaa siku ya pili wanashinda humu kuhakikisha wanambana Zitto ashindwe kuwasilisha ripoti hiyo siku iliyopangwa, si kwa sababu nyingine yoyote isipokuwa kuwalibda viongozi wa upinzanu
 
Mkuu naiona Escrow ikienda na wengi tena ilivyowataja na viongozi wawili toka upinzani ndo basi jamaa siku ya pili wanashinda humu kuhakikisha wanambana Zitto ashindwe kuwasilisha ripoti hiyo siku iliyopangwa, si kwa sababu nyingine yoyote isipokuwa kuwalibda viongozi wa upinzanu

Report isimuache hata mmoja, fisadi ni fisadi tu hata akiwa kijani au kavaa gwanda
 
Back
Top Bottom