Zitto: Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"

Zitto: Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"


Komaeni tu walau ukweli ujulikane hayo mambo sijui hatua za kisheria ni ndoto tu.

Halafu toka lini watanzania wameacha kuwa mabwege?

Acheni kufarijiana,watanzania ni mabwege wa kiwango kisichoelezeka.

R.I.P S.Mwamwindi.
 
MUHONGO alisema watu wanaleta ushahidi wa makaratasi ya kufungia maandazi

MWIGULU akasema wabunge wa upinzani hawajui hata maana ya neno ESCROW

PINDA akasema hakuna fedha iliyoibiwa BOT

BENO NDULU akasema kabla ya kukubali kutoa fedha nilikuwa kwenye PRESSURE kutoka kwa wakubwa wakitaka nitoe izo pesa wakati kulikuwa na zuio la BUNGE La kutokutolewa kwa fedha izo

MASELE HAKUNA HATA SENTI YA WA TZ iliyopoteea ni uzushi wa balozi wa UINGEREZA kutaka bank ya standard chatered ipewe mgao, na kumwambia balozi huyo asiingilie mambo ya TZ

SAADA MKUYA hakuna fedha yetu iliyoibiwa kuna watu wanatumiwa kutaka kutuvuruga

hawa ndio mawaziri wa kikwete kila mtu na lake MUHONGO ni muhongo kama jina lake na kwenye hili sakata achomoki lakini siwalaumu walishatuona sisiwa TZ ni mabwege kwaiyo wanatupeleka watakavyo tunapiga kelele siku 2 tuna kaa kimya
 
Zitto tunakuelewa sana na tunaamini uwezo wako.Ila shida ni moja kila jambo zito unalolianzisha linaishishia katikati na hii hasa ndo inakufanya usihaminike kwa wafuatiliaji wa mambo.Kumbuka ni wewe ulieanzisha yafuatayo na baadae kuyatelekeza;

1.Kuongeza 50% ya gharama halisi za ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kuja Dar

2.Ulianzisha hoja ya watanzania walioficha fedha nyingi nje ya nchi lakini ukaishia njiani.

Yote ni mazito ambayo kama ungeyafikasha mwisho ungekuwa umelisaidia taifa sana.

Sasa umekuja na ili la mikataba ya gesi, wewe na kamati yako mkisimama imara mpaka mwisho watz watakuwa nyuma yenu mwanzo hadi mwisho.

Usituangushe tena simama imara "KAMANDA" ZITTO.
 
ZZK, ninaamini kuwa kiitikadi wapo wengi wanaotofautiana na wewe. Lakini kwenye hili nadhani uko sahihi na hata kama utakuwa na maslahi binafsi the way kamati yako imehandle bado upo sahihi. Keep it up!
 
Binafsi nitafurahi kama jambo hili la Escrow litashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.

Kinachokera hivi sasa ni kutafuta umaarufu wa kisiasa. Kwamba baada ya Zitto kugaragazwa vibaya kisiasa na Chadema kiasi cha kuishi ubungeni kwa msaada wa mahakama na kupoteza mashabiki wengi aliokuwa nao, sasa anataka kuwa-retain waliobaki na kupata popularity upya kupitia matukio.

Wakati Zitto ana deni letu la majina ya walioficha fedha uswisi, anakuja na mbwembwe za kutishiwa maisha bila ushahidi.

Fedha za uswis sisi hatukumtuma aziseme. Ni yeye mwenyewe aliyesema anajua majina ya watu walioficha hizo fedha huko. Akafanya safari mbili tatu akapotea kimyaa lakini ilikuwa ni baada ya mbwembwe kama hizi. Maana ilikuwa kila siku ni Zitto na fedha za uswisi. Ikaja tena hekaya kama ya leo kuwa kutokana na fedha ya uswis kubumbuliwa na yeye eti wanataka kumuua. Fedha za uswis hazijaja na majina hatujayapata na kwenye tume ya Werema Zitto kakanusha kuyajua majina.

Hili la Escrow ni dana dana nyingine ya 'nitoke vipi' Ni mwendelezo ule ule wa Zitto kutaka kujiinua tena kwa visibgizio na mbinu za kizamani tena bila ushahidi.
Asubihi leo, zimepandishwa threads tatu za kumsifia Zitto toka kwa mtu mmoja. Thread zenyewe ukiziona ni kama takataka tu lakini kwakuwa ni mkakati maalum zikaanzishwa. Mara eti Zitto ni Mbunge bora wa November. Wapi walianza kutoa hizo tuzo? Kama Zitto ni mbunge bora wa November, wa February ni nani? Mbunge bora kwa Parameters zipi? Zimekubaliwa na nani hizo parameters hadi tukubali Zitto ni mbunge bora wa November? Wenye akili tulipoona thread zinazomsifia Zitto zimeanzishwa tukajua tu kuna kitu kitaibuliwa.

Sasa Zitto amekuja na hadithi njoo utamu kolea. Sisi hatutaki kujua nani katishiwa nani hajatishiwa. Tunataka fedha za Escrow zirudi kwa watanzania wanaokosa dawa, wanaochangishwa michango ya kishenzi ilhali fedha ipo mifukoni mwa wajanja. Hii move pamoja na Kafulila Mnyika aliwahi kuishikia bango. Sasa PAC mnayo, fanyeni kazi zenu mje na matokeo acheni longolongo kama za fedha za uswis. Na mkome kutaka kupata umaarufu binafsi kwenye ishu yenye national interest.

kaka taratibu issue ya uswis kulikuwa na mizengwe mingi hata hao wazungu hawakuwa tayari sana kusaidia ila ili kwakuwa lipo hapa hapa bongo lazima liende na watu tuweni kitu kimoja jambo hili linaweza kulimaliza hili zimwi linalotumaliza
 
Bravo Zitto! Naona wengine wanachangia kichama zaidi badala ya taifa.
 
Zito, ushauri wangu kwako binafsi. Acha kugombana na wapinzani wenzako. Tengeneza mahusiano mazuri ya kweli na CHADEMA, ukubali unapokosolewa ujirekebishe kweli kwa sabbu hat sisi huku nje tusio na vyama tunakuona una makosa mengi tena makbuwa. Kiburi na undumila kuwili hakukusaidii na karibu unapotea katika anga za siasa.

Jirekebishe tabia zako mbaya, ufanye kazi na wenzako. Huwezi kucheza peke yako ukategemea utazuia magoli.

Tena ufanya haraka maana sasa unazidi kupoteza muda.
 
Bramo asante sana kwa maswali uliyokaukiza haka kajanja janja haka.

Kanataka kutumia matatizo ya kitaifa kujinufaisha kiuchumi na kisiasa.

Kamweka heading kuhusu PAC alafu kanakuja na mambo ambayo ni zaidi ya PAC.

Ceo wa shell

Shell yenyewe

Oginga

Serikali ya kenya.

Hawa wanauhusiano gani na PAC,sababu uharo wote kalioweka hapa ni kuwatetea wao chini ya kivuli cha PAC,au kanadhani PAC ni mali yake.
 
Last edited by a moderator:
Ile milioni sita ulliyotuhumiwa kuchukua kwa ajili ya kutibia mama naona hujaiongelea
 
Zitto unataka kurudisha umaarufu na mara hii ukichemka umekwisha!
_uliteuliwa kamati ya kuchunguza mikataba ya madini ukavuta zako ukapiga kimya
_fedha za uswis oooh una majina ukavuta zako ukapiga kimya !
~sasa hili la escow ukishakula zako utakaa kimya!
~~~kila la heri
 
Last edited by a moderator:
Usimwamini mwanasiasa yeyote at a kama ni upinzani hayo ni maneno yako sasa tatizo Lako ni kutomaliza unachokifanya ungemaliza at a LA uswiss na mengine ulioanzisha ungekuwa umeisaidia nchi Kwa kiasi kikubwa sana kupambana na ufisadi Kwa hili la iptl pambaneni mpka mwisho hofu ni kuishia njiani kama kawaida yako
 
Haujajibu tuhuma hata moja hspo,unapiga kelele tu na unadhihirisha u shalo wako.

Kwanza kwa nini unamjibia huyo ceo wa shell? kwamba sio aliyevujisha mkataba wa statoil balu ni waandishi wa habari?

Na unaizungumzia shell, wewe kana nani shell?

Nilitegemea kama umekuja hapa kujibu tuhuma ujibu tuhuma zako.

Kwa mfano,ungeeleza kwamba matibabu ya marehemu mama yako uliyagharamia kwa pesa zako mwenyewe n.k na haujawahi kuomba pesa directly au in directly kutoka PAP. Na sio kutishia watu na vyombo vya dola.

Wewe ni mtu wa ajabu sana na report itakapo toka utaumbuka! Unaendeshwa na hisia za kichadema na kibavicha kwenye kila jambo! Hauwezi kupambana na Zitto kwa hoja za kitoto namna hii!

Na kuhakikishia Sangarara mtaumbuka kama mnafukiri Zitto ataingia kwenye mtego wenu! Tarehe 27 si mbali!
 
Last edited by a moderator:
PAP wanalipwa milioni 400 kila siku, wazalishe umeme wasizalishe.

Aiseee!! Roho inaniuma hadi inataka kuchomoka kibaya zaidi ati watalipwa kwa miaka mingine 20 ijayo!? Haki ya nani baada ya uchaguzi mkuu ujao naamini tutachinjana sana. Na nina uhakika wagombea wengi wa ccm ambao wana vyeo kwa sasa matokeo watakua wanayasikiliza wakiwa nje ya Nchi.
 
Bravo Zitto! Naona wengine wanachangia kichama zaidi badala ya taifa.
Utaifa gani kaweka hapo?

Muongo mkubwa huyu,kanasema kanashambuliwa kwa sababu ya kuwasweka jamaa wa TPDC ndani, ni namna gani wale jamaa wa TPDC wame anzisha jambo lolote la kukashanbulia.

Au kamesikia wanafikiria kukapeleka mahakamani kwa kuwadharirisha ndo kanaanza kujamba jamba.

Kasema PAC inashambuliwa,unaweza kunionyesha popote pale kwenye huu uchafu wake kalipoonyesha PAC inashambuliwa.

Kanafikiri PAC ni mwanvuli wa kufichia upuuzi wake?

Eti kazelendo.
Watu wanasema oginga anaichafua tanzania kwa niaba ya serikali ya Kenya, kenyewe ksnakuja hapa kumtetea oginga, ndio uzalendo huo?

Think my comrade.
 
Tunaamini mafisadi watatatumia kila mbinu chafu kufanikisha azma yao. Mambo yako wazi
 
Wewe ni mtu wa ajabu sana na report itakapo toka utaumbuka! Unaendeshwa na hisia za kichadema na kibavicha kwenye kila jambo! Hauwezi kupambana na Zitto kwa nhoja za kitoto namna hii!

Na kuhakikishia Sangarara mtaumbuka kama mnafukiri Zitto ataingia kwenye mtego wenu! Tarehe 27 si mbali!
Sizungumzii report mimi,nazungumzia haya aliyoandika hapa.

Kwa nini unafikiria juu ya report ambayo wewe mwenyewe haujaiona.isiposomwa je?

Unaweza kunionyesha ni wapi kwenye post yake ya utetezi kaonyesha namna PAC inavyoshambuliwa kama heading inavyosema.

Oginga ni member wa PAC.
 
Last edited by a moderator:
Zitto Hongera sana kazi unayo Fanya ni kubwa Sana na usitegemee watu wote kuipenda! Mimi huwa nakuombea kila Leo Mungu aendelee kukulinda!

Wewe ni mtu makini sana na tunu kwa taifa kupitia wewe huwa naamini vijana wana uwezo wa kuongoza taifa!
 
Last edited by a moderator:
Zitto kabwe,
kwanza umefanya vema kujitokeza kujibu tuhuma zinazokukabili lakini unaonekana kutumia akili pana sana kujibu tuhuma zako hasa kwa kutumia maneno ya kulaghai badala ya kumibu hoja asilia,ninashaka na maneno yako hasa kwenye maeneo haya,

kwanza,umesema kampuni ya shell haifanyi biashara hivi kunakampuni ambayo inaweza kuanzishwa siyo kufanya biashara? Kama haifanyi biashara inafanya kazi gani sasa.

Pili utakumbuka kwenye tuhuma zako unatuhumiwa kuazimwa au kukopeshwa kiasi cha milioni sita na kampuni moja wapo hapa nchini pesa hiyo ilitumika kwenda kumtibia mama yako kwanini hujasema hiyo pesa ulipewa kwa makubaliano gani au ulipewa kama msaada au kama mikopo mingine ili urudishe.

suala lako la kupewa hela na ubarozi wa uingeleza siyo jipya hata wakili wako ambaye sote tunamjua anayetokea mkoa wa kaskazini unamtumia sana kwenda kuchukua pesa zako za madili kutoka kwenye makampuni kadhaa unachofanya pesa nyingi huchukui wewe unatuma watu kwaniaba yako.

zipo sehemu mbili ambazo wakili wako amechukua pesa kwa maelekezo yako na amesainishwa siku moja hiyo document utawekewa hapa ila mnamuaibisha sana wakili wako japo hapendi unavyofanya lakini wewe unasema huwezi kuacha kuwasaidia waingeleza umetoka nao mbali.

jambo lingine ni wewe kutumiwa na nimrod mkono kiukweli hili unavyokataa binafsi mimi nakuona kituko mkono hajaanza leo kukutumia mpaka anakununulia ile gari ambayo kwasasa umeikodisha ni katika makubaliano yenu ya baadhi ya kazi unazomfanyia za kutumika kiukweli zitto nilikuwa shabiki wako sana tangu nijue kuwa wewe mla rushwa nakuweka kundi moja na wachumia tumbo wengine na hii tabia ya rushwa na wizi sasa umemfundisha hata deo filikunjombe.

ushauri wangu kwako fanyeni yote mnayofanya watanzania wasije kuwajua lakini siku moja wakijua mtachomwa moto mchana kweupe.

Uwe na AIBU mda mwingine,wanachopigania kina ZITTO ni jambo la Taifa,mimi NI mwana CCM,na kadi yangu nalipia mwenyewe,silipiwi na mtu yoyote,ficha upumbavu wako usifiche busara
 
Back
Top Bottom