Zitto nakupa wiki moja uondoke CHADEMA

Zitto nakupa wiki moja uondoke CHADEMA

pole sana kaka CDM ilikuepo na itakuepo kwa sapoti ya watz na co MSALITI ZITTO

bila zito chadema ingeshakufa kitambo, huo usaliti ni wa huko kwenu ufipa , kwa watanzania zito ni shujaa
 
Malengo yake yalikuwa kukiua chama,''nitakuwa wa mwisho kuondoka'' ili aondoke.
Kwa sasa kapigwa ganzi kwa jinsi chama kinavyopeta.
Akiangalia mafanikio kwenye uchaguzi wa ndani anagundua kuwa anaelekea kuwa wakwanza kuondoka.
Zitto ondoka kabla hatujakutolea vyombo kwa nguvu wakati unasubiri mahakama
 
Yes. Tumfukuze kwanguvu.

Kiukweli nayachukia maccm lakini kwa ubaguzi huu wa chagadema dhidi ya zitto ni bora hayo maccm yaendelee tu....mbaya zaidi wafuasi wa chadema wanaonekana kuwa wamezaji wa lolote kutoka kwa viongozi hata kama ni pumba.
 
Kiukweli nayachukia maccm lakini kwa ubaguzi huu wa chagadema dhidi ya zitto ni bora hayo maccm yaendelee tu....mbaya zaidi wafuasi wa chadema wanaonekana kuwa wamezaji wa lolote kutoka kwa viongozi hata kama ni pumba.

Kaa pembeni humjui Zito wewe. Nenda huko huko ccm
 
Zitto kwisha habari yake.

akuna anae mwamini tena.
 
Mnataka asipate pensheni yake ya ubunge? nyie watu vipi? yaani aziachie zaidi ya 40m ?
 
Zitto Zuberi Kabwe aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini CHADEMA(sasa Mbunge wa Mahakama) nampa ‘‘grace period’’ ya wiki moja ya kufungaisha chochote alichobakisha katika ofisi yeyote ya CHADEMA(sijui kama vipo) na kuondoka. Upo CHADEMA ili iweje,hatukutaki!
Ulivyovimba kichwa ulidhani bila CHADEMA ungekuwa mwenyekiti wa PAC, ungekuwa mbunge wa Bunge la Katiba, ungejulikana kimataifa.
Tunazo sababu za kukulazimisha kuondoka CHADEMA kinguvu. Mbali na mikakati unayoifanya vichakani, lakini yapo haya ya wazi:-

1.Umehusishwa na njama za kutungua helkopta iliyotumiwa na katibu kipenzi chetu Dr.Slaa. Madiwani wa Shinyanga wamekuumbua. Hujakanusha ‘‘Silence means YES’’

2.Umehusishwa na mipango ya kubambikiza wanachama ugaidi. Kwa macho na masikio yangu nimekushuhudia Star TV ukiwa na Mwigulu Nchemba mkitangaza kuwa mna mkanda wa video ukionyesha vigogo wa CHADEMA wakipanga ugaidi. Nasema mkitangaza kwa kuwa yalipotamkwa haya na Mwigulu wewe ulikuwa pembeni yake, ukiwa kama Naibu Katibu Mkuu hukukanusha wala kuonyesha kukerwa na propaganda hizo zilizovuka mipaka. ‘‘Silence means YES’’

3.Katika mwendelezo wa kubambikiza kesi za Ugaidi ukaendeleza unafiki wako wakati Kamanda Lwakatare ‘‘Lwax’’ akiwa sero wewe ulikiandikia barua chama kwamba kijiweke mbali na kesi ya Lwakatare, bishaaa. Nikuulize wewe Msaliti Mkuu yupo wapi Lwakatare?

Kama hutaki kufungaisha virago tupe sababu za msingi kwa nini unaona ubaki kuwa mwana CHADEMA. Imebidi nifikishie ujumbe wangu kwa MM na ACT nzima
My Take:-Makamanda na wapenda mabadiliko wote niungeni mkono katika hili. Mods msifute, kama inawauma muiteni aje ajibu kwa nini tusimfurumushe

Kutumika kubaya sana, Mwl. Nyerere aliwahi kusema umasikini kuliko wote ni umasikini wa fikra! Wewe ndugu yangu naona unatumika vibaya na uwezo wako wa kufikiri ni mdogo.

Kwanza wewe ni nani mpaka umwambie ZZK kwamba aondoke ndani ya Chama? Kati yako wewe na ZZK ni nani amekijenga chama na kukifikisha hapo kilipo?
Na kwa nini unamambia aondoke kwa kutaja tuhuma bila kutoa ushahidi, ni wapi umewahi kusikia mtu akihukumiwa adhabu kwa tuhuma bila kuthibitishwa?

Acha kutumika kama toilet paper, kama ni tuhuma tu mbona Mwenyekiti wa CDM ana tuhuma kibao hujamwambia aondoke?
Anatuhumiwa kuchukua rushwa kwa Nimrrod Mkono ili asipige kampeni jimboni kwake na yeye Mkono apite bila kupingwa na Mkt hajawahi kukanusha, kupokea rushwa siyo kosa? Akipewa nchi si ndio itakuwa balaa!
Mwenyekiti pia alibadilisha safari ya mbunge ili akale nae bata saari Dubi kwa hela ya serikali, huo si ufisadi?

Kama mtu anahukumiwa kwa tuhuma tu, Dr. Slaa si anatuhumiwa kumtelekeza mke wake na kwenda kupora mke wa mtu? Huo ndo mfano wa kiongozi bora, mbona hujamwambia walau ajiuzuru nafasi ya katibu mkuu wa chama?
 
Kiukweli nayachukia maccm lakini kwa ubaguzi huu wa chagadema dhidi ya zitto ni bora hayo maccm yaendelee tu....mbaya zaidi wafuasi wa chadema wanaonekana kuwa wamezaji wa lolote kutoka kwa viongozi hata kama ni pumba.

Hapo wanatupa picha jinsi watakavyokuwa endapo wakikamata dola.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom