Zitto nakupa wiki moja uondoke CHADEMA

Zitto nakupa wiki moja uondoke CHADEMA

We Mkandara nadhani ubongo wako una mkanda wa jeshi. Hivi Zitto aondolewe mara ngapi Chadema. Jina limeshafutwa kwenye orodha ya wanachama wa Chadema, ila kupitia mahakama. Nikukumbushe, Zitto ni mwanachama wa chadema kwa amri ya mahakama. Yeye ndiyo anaye ng'ang'ania kubaki chadema. Mkandara anza kula mbegu kabla mambo kuwa mabaya.
Ahahaha mbona mkali? sasa ikiwa Zitto ni mwanachama wa Chadema kwa amri ya mahakama sii bado mwanachama? nachokisema mimi akiondoka rasmi na kujiunga na chama kingne cha moto kitatokea ni mtazamo wangu mimi kwa yanayokuja hivyo usiwe na hasira maana sio mimi nayepanga bali nakisia yajayo!. na CCM akondoka Lowassa itasambaratika japo watu hawa hawafanani.

Kifupi Lowassa anaweza kuwa mbaya lakini ukweli utabakia kuwa ni jembe la CCM, vile vile Zitto anaweza kuwa mbaya kwako na wengine wote lakini ndiye mbegu stawi ya umoja wa Chadema na wanachama wake, Lissu anapendwa lakini sidhani kama ni kiungo kikubwa cha wanachama Chadema.
Ni mtazamo wangu usitokwe na povu buree...
 
Hata kama hana uwezo mmezidi sana mdomo kiasi kwamba sasa mnachosha. Ni sawa na mtu alolewa pombe anaongea hovyo usiku kucha.
Na nawaambieni kabisa kwamba Zitto akijiondoa rasmi Chadema na kuingia ACT, moto wa kisiasa utaripuka na utaona jinsi Chadema itakavyosambaratika maana sasa imefikia kuwa Chadema ina watu wake wanaoaminika - Chama cha Mpira, mnachosha sana hata kuwasikiliza!

Kama ccm imeshindwa , ataweza mwakilishi wa kutumwa ? Ngoja nikuulize kitu , kwani zitto ni mwanachama wa cdm ? Utasubiri sana mjomba , usaliti ni laana !
 
Zitto kwisha habari yake.

akuna anae mwamini tena.
Nasikia hata yule "mupenzi" wake wa Clouds FM naye kammwaga baada ya kushtuka kuwa jamaa ana kaelement ka utapeli tapeli hivi. Demu kaona isiwe taabu, kwa nini jamii ifikie mahali ikucheke kwa kuwa na mshikaji msaliti wa jamii? Mwepesi kununulika? Yaani mtu anayetembea na price tag shingoni.
Mwana mume wa shoka hawi hivyo, basi akamwagwa.
 
Kama ccm imeshindwa , ataweza mwakilishi wa kutumwa ? Ngoja nikuulize kitu , kwani zitto ni mwanachama wa cdm ? Utasubiri sana mjomba , usaliti ni laana !
Mkuu maneno haya waliyasema hata CUF mwaka 2009 tena hadi karibia uchaguzi wa mwaka 2010 wakitudharau, na niliwaambia haya haya kuhusu Rashid Hamad hawakusikiliza, nikaambia ya muafaka na CCM wakaona wamepiga bao wao wakiamini hawawezi kushuka ati ni chama rasmi cha Upinzani na wana msomi Lipumba!. Wako wapi leo? Kiburi mara zote hakilipi mkuu wangu, kwani toka lini mtu akayajua mapungufu yake? sii mpaka uambiwe ndio utajua...
 
Ushauri wako hauna malengo mazuri na cdm , ni kipi usichokijua kuhusu hawa wasaliti unaowapigania kufa na kupona ? Unataka cdm ifanye nini zaidi ya hatua zilizoChukuliwa ? Huku hatuchezi na mamluki.
 
Kiukweli nayachukia maccm lakini kwa ubaguzi huu wa chagadema dhidi ya zitto ni bora hayo maccm yaendelee tu....mbaya zaidi wafuasi wa chadema wanaonekana kuwa wamezaji wa lolote kutoka kwa viongozi hata kama ni pumba.

Tuliyapokea maisha bora kwa kila mtanzania kwenye gunia. Ahsante ccm kwa usanifu huu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom