Zitto Naibu katibu Mkuu hata vikao vya chama anaadimika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto Naibu katibu Mkuu hata vikao vya chama anaadimika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Sep 10, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Katika operation ya vuvuvuvu la mabadiliko, Zitto Kabwe haonekani kuandamana na makamanda wenzake, wakati akiwa Kaimu Katibu Mkuu ambaye ndiye kijana wa kuwa mstari wa mbele katika mapambano.

  Isitoshe hata kikao hiki kilichofanyika Jijini Dar alitazamiwa kuwa katika picha, labda imekatwa alikaa pembeni, tukumbuke yeye ni kiongozi mwandamizi, lakini naona yuko makini kutokea katika picha za misafara ya kumsindikiza Kikwete kutalii. Hii imekaaje?

  Tunahitaji Zitto aje kujibu haya, ndio uwajibikaji tunaohitaji sasa hivi. Tunahitaji viongozi wa chama wanaowajibika kwa chama na wananchi chama tunachotegemea kuchukua dola, na hivi kujihakikishia viongozi watakaowajibika kwa wananchi na wananchi wawe na haki ya kuwajibisha wasipowajibika kiutendaji.

  Kiongozi anayefanya kazi kwa ujanjaujanja na kukwepakwepa magumu ni hatari kwamba siku yakitokea magumu anaweza kuwatelekeza wenzake na hata kukitelekeza chama chake.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Jamani Zitto yuko nje ya nchi kama mwakilishi wa bunge la Tanzania CPA.
   
 3. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Zitto unafiki wake haufikichiki na kila kiongozi chamani anamjua. yuko tofauti na viongozi wote hapo pichani. Ni kama chagulani wa mwanza, kiama chake kinakaribia
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hivi Zitto kawafanya nini? FJM anatuhabarisha kwamba Zitto yupo Ughaibuni akiwakilisha Bunge la Tanzania lakini sisi tunamtafuta kwenye mikutano ya CC ya CDM.

  Hivi kumbe CDM ina warangi rangi hadi kwenye CC? Au ni mwakilishi wa Chama Rafiki?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Mh Zitto haitowezekana kuacha kikao cha CC bila sababu ya msingi.
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Naona Mh. Freeman Aikael Mbowe ameketi kwa mamlaka ati kisha aishie Uenyekiti tu asipate Mamlaka ya juu? Hilo alilikubali Nyerere na kumachia Kawawa sijui wanasiasa wetu wa sasa wanaweza kufanya hivyo.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Kimbunga, Tunashukuru kuhabarishwa kwamba yuko safarini nchi za nje, lakini ukweli haupingiki kwamba Zitto huwa na udhuru katika mikutano na majukumu ya Chadema, lakini hata siku moja sijasikia akitoa udhuru kwa shughuli za bunge au kumsindikiza Kikwete kwenye misafara yake.

  Mabadiliko tunayotaka si ya kushika dola tu, ila wananchi tuwe na haki za kuhoji uwajibikaji wa viongozi wetu katika masuala muhimu ya uwajibika, ndicho tunachokifanya. Hilo linaloongelewa mara kwa mara kuhusu Zitto ni uthiitisho kwamba kuna kitu ambacho wengi hawaridhika na mwenyendo wake katika uwajibikaji wa pamoja kama viongozi chamani, yeye akiwa kiongozi mwandamizi.

  Ikitokea uchaguzi ujao akiachwa nje ya CC kuna wanatakaolalamikia uamuzi huo, lakini kwa sasa wanajenga utetezi wa kumtetea. Tuwe wazi jamani, na kama anasikia malalamiko haya anatakiwa kuyafanyia kazi zi kuyadharau na kufanya mambo kiujanjaujanja.

  Jukumu la uongozi si la ujanja ujanja, ndio maana tunaona yanayoendelea nchini mwetu sababu ya huu mtindo wa kuongoza nchi kiujanjaujanja.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tuna mengi ya kujifunza toka kwa Mzee Madiba, kwani wachache sana wenye kuwa na moyo huo wa kuona nafasi zao kwa sasa zinawatupa mkono na kinachotakiwa ni kushika kipindi kimoja kuonyesha njia ya kupita ili wanaomfuata wasipotee njia.

  Naamini kizazi cha leo inawezekana tu kama mfumo wa uongozi unabadilika kwa kutanguliza zaidi uwajibikaji na kujitolea badala ya kuzidi kuongeza mianya ya ulaji kivutio kinachokuwa urimbo kwa wengi hata kuwa tayari kuua ili mradi kulinda nafasi katika kiti chake.
   
 9. m

  mmwaisoba JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 434
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na hawa wakoloni mgongoni mwa slaaaa wanasubiri nini kama si kutupiga mnada?? Wao wana kwao watuachie nchi yetu
   
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Swali la kuuliza ni je, katika mkutano wa kamati kuu Godbless Lema anakaa meza kuu kama nani?
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Zitto Zuberi Kabwe.
   
 12. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #12
  Sep 10, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Anasubiri apewe deaal ya kulipua ili liwe azimio serikali itekeleze na kumpatia umaarufu yeye...sasa akishiriki kwenye CC ya leo na maamuzi yake yasitekelezwe unadhani atakuwa maarufu....!
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  FJM, Umenikumbusha kwamba kamati hii ipo kikazi sehemu fulani nje ya nchi, pamoja na ukweli huo, ukiangalia picha hii utagundua kuwa pamoja na kuwa marafiki, Filikunjombe ni wa kujituma kwa sana tu bila kujibakisha hata yuko makini kuelezea uozo kwa uwazi wa chama chake yeye akiwa mfano wa wazi katika utendaji jimboni mwake, hii ni tofauti na Zitto ambaye anapima kutoka kifua mble mahali ambapo hakuna matatizo yanayoweza kumpata.

  Huu si ujasiri tunaotegemea vijana wa leo, ni ujanja ujanja kama alivyowahi kumwambia Speaker Anne Makinda kwamba hatamweza kwani atatumia ujanja wa chuoni hata ashindwe kumwajibisha kuhusu kutotia kitabu cha mahudhurio bungeni.
   
 14. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #14
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Gamba lingine hili ndani ya cdm
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kama mmoja wa wahusika katika meza kuu hayupo, kiti hakiwezi kubaki kitupu, kuna mmoja ataitwa kuja kiti kutokana na heshima yake aliyojijengea katika chama.

  Wakumbuka maneno haya katika misahafu kwa lugha ya kilatini: "amice ascente superio" tafsiri yake (unapoalikwa usikae kiti cha mbele arusini hadi mwenye kukaribisha wageni atakapokuambia, rafiki yangu njo huku mbele zaidi, ndipo utakapokuwa na heshima mbele ya watu).
   
 16. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #16
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  kuna mtu aliwaulizia humu ndani.CDM haiishi wasurprice watu pessimistics.who knows next time ataumbuliwa, mukama alishaonja adha ya umbea.
   
 17. Piere. Fm

  Piere. Fm JF-Expert Member

  #17
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,194
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Zitto Kabwe msubirini 2015 atakapokuja kuchukua form ya kugombea urais nyie pigen kazi kwanza.
   
 18. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #18
  Sep 10, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Unajua chuki, majungu na unafiki vimekujaa hadi hueleweki unachokisema. Tulia wewe.
   
 19. nzitunga

  nzitunga Senior Member

  #19
  Sep 10, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acheni kuchonganisha watu! Waacheni CDM wenyewe waseme kuhusu Zitto! Kuna vikao halali vya kusema hivyo. Kamati kuu wenyewe hawajasema kukosekana kwa Zitto, na inawezekana kabisa aliwapa baraka akisema I agree and Support whatever you decide!
   
 20. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #20
  Sep 10, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Lijitu hata kuandika halijui, si upite tu kama huna hoja?? Ptuuu.
   
Loading...