Zitto na PAC yake waliteleza?

Zitto na PAC yake waliteleza?

Pinda alipotoa kauli kuwa watu wanaowaua zerezeru nao pia wauliwe tulipiga kelele ajiuzulu! Pinda aliposema wapinzani nwanasumbua wapigwe tu, tukamtaka ajiuzulu. Sita na ndugu zake wanapovunja sheria bunge la katiba tunalalamika hadi hamu ya kula hatupati Leo zitto na kamati yake wanavunja sheria tunamwona mashujaa, wametumia udikteta kulinda mali ya umma ehheeee?

Juzi makamba (na wengine) wmesema tunahitaji raisi dikteta kila mtu humu kalia naye hadi CCM wenzake wamelia!!!! Zito na kamati yake ni wakosaji kwa hili na wanapaswa kuoma radhi kwa udhalilishaji na uvunjifu wa sheria.

Sheria haziendeshwi na mapenzi na ushabiki hata siku moja. sio sahihi kumshabikia zito hata kama nia njema, afuate sheria.

Mkuu mbona skuelewi?
hebu nifumbue macho mwenzio kipofu hivi nisheria ipi inasema mikataba ya rasilimali za nchi ni siri ya serikali?.
 
Uko smart mkuu ile ni drama huyu msaliti anatumia kila njia kujibua lakini ndio keshapima kina cha tope kwa miguu miwili, atajaribu kila aina ya u-senge lakini hataweza kujiokoa.

Akili yako nindogo mno!!!
hivi unahisi hao unao ona c wasaliti wana mzidi uwezo wakujenga hoja zitto?
acha ujinga wa kumezeshwa chuki na wajinga ...kaa chini umiza kichwa kutafiti ujuee ukwel..

kipindi kile zitto katangaza kuwania urais kupitia chadema mli mezeshwa sumu eti ana vuruga chama na ni msaliti wapumbavu mka kubali kauli za mazuzu..
hapa juzi Tundu lisu amesema anaweza kugombea uraisi kupitia chadema hakuna mbwa hata mmoja alie sema Lisu ni msaliti..ila ipo sku tuta ujua ukweli.
 
Pinda aliyatoa hayo baada ya sheria kuvunjwa, kwa utetezi wake akazidi kuvunja sheria. Kina sita wamevunja sheria kuhalalisha maslahi ya kikundi chao tena ya watu wachache, viongozi wamekuwa wakivunja sheria kwa namna nyingi na tofauti tofauti kwa maslahi yao au ya familia au mitandao yao sio kwa manufaa ya nchi. Kote huko hakuna hatua yoyote tangible mloichukua. Kibaya zaidi wataendelea kuvunja sheria hizi tena kwa maslahi yao na hamtawafanya chochote. Leo hii zitto anapindisha taratibu kwa kutetea maslahi katika rasilimali zenu, mnamuona scrapegoat?

We kweli akili hazikutoshi....kama anapindisha sheria kwa maslah ya nchi we unaumia nn?
Au ulitaka apindishe sheria kwa maslah binafsi ndo umuone mzuri?...yaan kuna mijitu mingine huwa c ielew ni mitanzania au mikenya...hayana jema hhata sku mmoja kila linalo fanywa na zitto kwao ni nongwa afanyej ili mlizike?
 
Ni ukweli ulio dhahiri kuwa mambo haya yanafanyika maksudi na wanaofanya hivi wanafanya maksudi kwa sababu wamezoea kutumika,lengo nikutupoteza katika swala ka msingi la katiba,ndio maana huwez kusikia yule jamaa akizungumzia swala la katiba...
 
Na huo ndo ukweli Zitto alikuwa anatafuta "comeback" imegoma!

Unatuhamisha kiboyo Aiseeee... Ishu ni Mikataba, na sio Ujio wa Zitto... Tunapoteza Energy kubwa kujadili MTU mmoja, badala ya Kuumiza kichwa kwenye Mambo Ya Msingi, Huu Ni Ujinga.
 
kwanza inaonyesha kila dalili kuwa wale jamaa waliandaliwa kiaina kabisa kwamba watapelekwa polisi then wataachiwa, inaonyesha huo mpango uliandaliwa mahsusi tangu awali ili kuanza kuliinua jina la msaliti juu, bahati mbaya halijainuka,

Hivi watu kama huyu ni Great Thinker au ndio ......!!!
 
Akili yako nindogo mno!!!
hivi unahisi hao unao ona c wasaliti wana mzidi uwezo wakujenga hoja zitto?
acha ujinga wa kumezeshwa chuki na wajinga ...kaa chini umiza kichwa kutafiti ujuee ukwel..

kipindi kile zitto katangaza kuwania urais kupitia chadema mli mezeshwa sumu eti ana vuruga chama na ni msaliti wapumbavu mka kubali kauli za mazuzu..
hapa juzi Tundu lisu amesema anaweza kugombea uraisi kupitia chadema hakuna mbwa hata mmoja alie sema Lisu ni msaliti..ila ipo sku tuta ujua ukweli.

Sisi hatuangalii anachokisema huyo mjinga wenu tunaangalia anachokifikiria.

Jipangeni.
 
Ni Kweli waliteleza ...walitakiwa kupata Kibali cha spika ...kabla ya kuwatia ndani wale Jamaa ...,Sioni kwanini hawakuomba kile kibali ..week Moja kabla ..unless walikuwa na mashaka kuwa spika angepitisha wakamatwe ..
Wamefanya kazi nzuri though Jamaa wanaweza KUDAI fidia...UJUMBE umefika .....though Kisiasa wanaweza Kuiweka Kama vile wajumbe walitaka kupata faida ya kisiasa

Mkuu mikataba alisaini prof KJ alipokuja prezidaa wa China kama unakumbuka,sasa kama wanaitaka c wangemuuliza mukulu ametunza wapi?au prof muongo?hao jamaa wameonewa sababu wanauwezo wa kumbana waziri wa nishati na madini bungeni!
 
Tanzanian. Mko busy kutizama weaknesses za individuals, badala ya kuangalia masuala muhimu. Inshu sio kukamatwa, Inshu ni MIKATABA iwasilishwe kwenye kamati ya PAC. Nadhan swali la kujiuliza ni kwann inafanywa siri kiasi hicho? Wanaficha nn na kwann?

Wananchi nadhan tungewapokea wajumbe wa PAC, Kwa kudemonstrate na kushinikiza serikali iweke wazi hiyo mikataba, ili Mafisadi wajukikane... Tuache kushambuliana, we r Loosing the Big Target here... Halafu, humans tunakosea, we deserve second Chances, Let us not Loose hope completely kwa Mh. Zitto, Mimi binafsi naona anafanya kazi nzuri... Tumpe support. Tuache Ujuaji, Na unabii wa kijinga.

Mkuu kwani hujui TPDC wako chini wa wizara ya nishati na madini na maelekezo yanatoka huko?kwanini waziri mwenye dhamani asibebeshwe mzigo wa kuleta mikataba bungeni?mikataba alisaini mkuu wa kaya alipokuja prezidaa wa china na mwanasheria Mkuu alikuwepo kwanini hao wasiiweke wazi kwa wananchi tukaijua?Napinga hao watu kukamatwa sababu wenye mikataba wanajulikana!
 
Hivi Wadau , ktk katiba inayopendekezwa suala la mikataba limewekwaje? Maana mikataba ya rasilimali ya nchi inabidi iridhiwe na Bunge kwa niaba ya wananchi.
 
Mkuu kwani hujui TPDC wako chini wa wizara ya nishati na madini na maelekezo yanatoka huko?kwanini waziri mwenye dhamani asibebeshwe mzigo wa kuleta mikataba bungeni?mikataba alisaini mkuu wa kaya alipokuja prezidaa wa china na mwanasheria Mkuu alikuwepo kwanini hao wasiiweke wazi kwa wananchi tukaijua?Napinga hao watu kukamatwa sababu wenye mikataba wanajulikana!

Nimekuelewa Mkuu..
 
Mkuu mikataba alisaini prof KJ alipokuja prezidaa wa China kama unakumbuka,sasa kama wanaitaka c wangemuuliza mukulu ametunza wapi?au prof muongo?hao jamaa wameonewa sababu wanauwezo wa kumbana waziri wa nishati na madini bungeni!

So wamefanya Ze comedy show ....kuchukulia Kiki wakijuwa wazi mikataba ufunguo kwa baba
 
Ahsante mkuu. Kama watu wangekuwa wanachangia kama wewe, this way, jukwaa hili lingekuwa na maana maradufu. Ahsante sana kaka. Sina la kuongeza

"POOR WE". Twiga wanasafirishwa, wanauzwa nje kama karanga, Tupo kimya. Madawa ya kulevya, Bangi, Pembe za Ndovu, kucha za Simba n.k vinakamatwa kila iitwayo LEO lakin, sijawahi kusikia Serikali inazifanyia nn hizo vitu? Je watavichoma? Ama wataviuza? Wanajua Mpaka bei, lakin hatujui wamejuaje? Soko ni lipi? Wapi?.... Kuna Ujinga Mwingi Serikali inafanya. Na tumenyamaza kabisa.... Sasa wanapeana nchi ki ndugu, Tumenyamaza, Tsh inazidi ku depreciate tupo kimya. Wanapandisha nauli Bei ya mafuta ikipanda, Yakishuka bei wanakausha... Yakipanda tena kwenye rate ile ile ya mwanzo, ama yakizidi kidooogo tuu, wanapandisha tena Nauli... Tunaumia mimi na ww, Yet bado Tunashabikia Ujinga. "POOR WE"...

Nadhani WaTz hatuko sawa Mentally....
 
Nakumbuka zitto aliomba mwongozo kwa mwakilishi wa katibu wa bunge ambae wakiambatana nae kuhusu hili swala. Na huyo mwakilishi wa katibu wa bunge alisema PAC ina haki ya kuzipata hizi nyaraka zilizoombwa.
 
Mwanasheria wa Bunge alisemaje? Kwa nini tusubiri hao jamaa waende Mahakamani badala ya kusubiri Polisi wawafikishe mahakamani? Kwani kazi ya Polisi inaishia kuwakamata watu na kuwapeleka Polisi?

Tunachosubiri ni PAC iwafikishe mahakamani hao Jamaa, na ni update ya hatua hiyo ndio iliyonifanya leo niutembelee uzi huu.

Ama sivyo, Bunge linapaswa kukachukulia hatua ka Zitto kwa kujibebesha mamlaka ambayo PAC haina.

umenielewa?

Sangarara,

Acha kukurupuka, unatakiwa usome mwanzisha uzi huu amejadili nini na mimi nimemjibu nini.

Kama umemsoma vizuri mtoa mada amesema akina Zito na PAC hawana mamlaka ya kuwafikisha wale viongozi wa Polisi na akatoa mpaka na kifungu cha sharia.

Mimi nimemjibu hata PAC wana mamlaka hayo kwani hawakukurupuka bali walipokea maelekezo hayo toka kwa wanasharia wa bunge na mmoja wa wanasharia hao alitoa ufafanuzi hapo.

Sasa kumbuka kila mtu ana haki kwa maana PAC au Bunge na watuhumiwa waliodhalilishwa kama alivyobainisha mtoa mada.

Mimi nikatoa hitimisho kuwa kama hawakuridhia na maamuzi ya PAC ambayo hatima ya kuwafikisha mahakamani ipo kwa SPIKA basi na wao wana haki ya kulishitaki Bunge (PAC ni kamati ya Bunge) kwa kuwadhalilisha.

nafikiri nimekupa mwanga kidogo wa muradi wa andiko langu.

Usikubali kuongozwa na chuki wala ushabiki utateteleka kiumsimamo.

Pole sana

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zikiwemo Kamati zake mbalimbali za Kudumu, linaongozwa na Katiba, Sheria na Kanuni za Kudumu za Bunge hilo. Kila jambo Bungeni husimamiwa na sheria tajwa. Hivi karibuni, kumetokea sintofahamu kati ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Mashirika na Taasisi za Umma (PAC) na viongozi wa TPDC.

Iliripotiwa kuwa viongzi husika waliagizwa na Kamati ya Zitto kuwasilisha nyaraka mbalimbali mbele ya Kamati hiyo. Ikaripotwa tena kuwa kufuatia kukaidi kwa viongozi hao kuwasilisha nyaraka,walikamatwa na polisi na baadaye kuachiwa baada ya kuhojiwa.

Bunge linapewa nguvu kupitia Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge ya 1988 iliyofanyiwa Marekebisho mwaka 2004 kupitia Sheria Nambari 3 ya 2004. Binafsi nimevutiwa na kifungu cha 17(2) cha Sheria tajwa ya 1988 ambacho hakikuguswa na marekebisho ya 2004. Sakata la viongozi wa TPDC linahusiana nacho.Kifungu kinasomeka hivi:

17 (2) Where any person ordered to attend or to give evidence or produce any document before any committee refuses to answer any question that

may be put to him or to produce any such document on the ground that. the same is of aprivate nature and does not affect the subject of inquiry,

the chairman of the committee may report such refusal to the Speaker with the reasons therefor; and the Speaker may thereupon excuse the

answering of such question or the production thereof.

Ni wazi, kama ilivyoripotiwa kuwa viongozi wa TPDC waliagizwa na Kamati ya Zitto kuwasilisha nyaraka.Pili, kwa maneno au matendo hawakuwasilish na hivyo kuonekana wamekataa. Mwenyekiti wa PAC angeweza kuripoti kwa Spika wa Bunge akiainisha sababu za kuripoti kwake na mwisho mwishoni Spika angeweza kusamehe kutolewa kwa nyaraka hizo.Yaani, Spika angeweza kulazimsha au kusamehe uwasilishwaji wa nyaraka husika.Hapo nimetafsiri kifungu cha hapo juu pamoja na kilichoripotiwa.

Hivyobasi, PAC haina na haikuwa na mamlaka ya kuwakamata au kusababisha kukamatwa kwa viongozi wa TPDC. Kama ilifanyika kinyume na utaratibu uliowekwa na Sheria, PAC iliteleza.

Kisa zitto roho mbaya itakua
 
Sangarara,

Acha kukurupuka, unatakiwa usome mwanzisha uzi huu amejadili nini na mimi nimemjibu nini.

Kama umemsoma vizuri mtoa mada amesema akina Zito na PAC hawana mamlaka ya kuwafikisha wale viongozi wa Polisi na akatoa mpaka na kifungu cha sharia.

Mimi nimemjibu hata PAC wana mamlaka hayo kwani hawakukurupuka bali walipokea maelekezo hayo toka kwa wanasharia wa bunge na mmoja wa wanasharia hao alitoa ufafanuzi hapo.

Sasa kumbuka kila mtu ana haki kwa maana PAC au Bunge na watuhumiwa waliodhalilishwa kama alivyobainisha mtoa mada.

Mimi nikatoa hitimisho kuwa kama hawakuridhia na maamuzi ya PAC ambayo hatima ya kuwafikisha mahakamani ipo kwa SPIKA basi na wao wana haki ya kulishitaki Bunge (PAC ni kamati ya Bunge) kwa kuwadhalilisha.

nafikiri nimekupa mwanga kidogo wa muradi wa andiko langu.

Usikubali kuongozwa na chuki wala ushabiki utateteleka kiumsimamo.

Pole sana

Mkuu

Nashukuru kwa maelekezo yako.

Lakini naomba nikuweke sawa, mimi sichangii hapa kishabiki, Lakini natambua kwamba msimamo wangu juu ya Zitto ni Negative, na sidhani kama hilo ni Kosa.

Sasa turudi kwenye hoja yako?

Unamaanisha kwamba Mwanasheria wa Bunge aliwapa akina uzito ushauri kwamba wanaweza wakaruka taratibu za kupeleka mahitaji yao kwa speaker ili ayawasilishe serikalini na hata kuruka ngazi zingine za kiserikali na kwenda moja kwa moja polisi? sababu hicho ndio walichokifanya kina Zitto.

Na Je, lengo lao la kuwaitia jamaa polisi ni nini? Wote tunajua polisi ni njia tu ya kufika mahakamani, sasa PAC walikuwa wamechukua maamuzi ya kuwapeleka jamaa mahakamani?

Ndio maswali yangu hayo, labda ungenijibu na mimi, sababu majibu yako kwa mleta mada nimeyaelewa.

Ama sivyo kama issue imeisha, inabidi tujue lengo lilikuwa ni nini? Sababu kama waliteleza Je, wameanzisha mchakato stahili? Kama hawajaanzisha ni kwa nini? au wameishapewa hiyo mikataba?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom