Zitto na PAC yake waliteleza?

Zitto na PAC yake waliteleza?

Badala ya kushughulikia kupukutisha majani ya mti, tungemwona wa maana kama angeunga na wapiganaji na wanaharakati wa UKAWA kushughulikia kung'oa mizizi ya ufisadi kwa kudai katiba ya wananchi ambayo kama ingepitishwa haya yote yangekuwa yamepatiwa mwarobaini come next year! Lakini sasa anafanya usanii wa kuwasweka ndani vidagaa huku akibeza juhudi za UKAWA. Ni msanii tu kama alivyo propesa jk.
Duu!! sasa ukawa wamefanya nini mpaka sasa? au ndio wameungana, sijui unaitafsir vp harakati ya kweli? ni ile inayoonekana kwa vitendo kama PAC ifanyavyo au ya kufikirika!!!
 
Akili yako nindogo mno!!!
hivi unahisi hao unao ona c wasaliti wana mzidi uwezo wakujenga hoja zitto?
acha ujinga wa kumezeshwa chuki na wajinga ...kaa chini umiza kichwa kutafiti ujuee ukwel..

kipindi kile zitto katangaza kuwania urais kupitia chadema mli mezeshwa sumu eti ana vuruga chama na ni msaliti wapumbavu mka kubali kauli za mazuzu..
hapa juzi Tundu lisu amesema anaweza kugombea uraisi kupitia chadema hakuna mbwa hata mmoja alie sema Lisu ni msaliti..ila ipo sku tuta ujua ukweli.

Lissu si msaliti, hayo a Zitto kuitwa msaliti kwa kutaka kugombea urais umeyaibua wewe hakuna aliyewahi kusema hivyo.
 
Zito ni mzuri sana wa kujenga hoja lakini mara nyingi ni mzushi na mwongo. Na mara nyingi hufanya mambo mengi kwaajili ya personal political gains kuliko faida ya umma.

Hata tukilazimisha vipi, ukweli hubakia kuwa Duniani kote mikataba ya kibiashara huru ni siri kati ya wale wahusika wakuu. Tatizo kubwa hapa kwetu siyo usiri wa mikataba bali uadilifu wa wanaosaini mikataba kwa niaba ya Taifa.


Ndugu yangu,sijawahi ona mimi duniani mikataba yenye maslahi kwa nchi ikafichwa kwa chombo chenye dhamana ya kuisimamia serikali.Embu jipe picha US Senate commitee inahitaji mkataba wa kuchimba mafuta Alaska baina ya serikali ya USA na kampuni fulani,halafu mtumishi wa shirika husika akatae kuwasilisha mkataba?Pata picha kitamkuta nini.

Mkuu tusimjadili ZITTO,mada husika nayo ni ufisadi uliokithiri nchini kwetu mpaka maofisa wanakataa kutoa nyaraka kwa kamati ya BUNGE,hichi ni kiburi na dharau ya hali ya juu kwa Watanzania.Hivi jamani mmeangalia uzito wa hili jambo au chuki yenu kwa ZITTO imewafunika kutizama ukweli.Siasa za USIMBA na YANGA zinaimaliza hii nchi.
 
Mkuu

Nashukuru kwa maelekezo yako.

Lakini naomba nikuweke sawa, mimi sichangii hapa kishabiki, Lakini natambua kwamba msimamo wangu juu ya Zitto ni Negative, na sidhani kama hilo ni Kosa.

Sasa turudi kwenye hoja yako?

Unamaanisha kwamba Mwanasheria wa Bunge aliwapa akina uzito ushauri kwamba wanaweza wakaruka taratibu za kupeleka mahitaji yao kwa speaker ili ayawasilishe serikalini na hata kuruka ngazi zingine za kiserikali na kwenda moja kwa moja polisi? sababu hicho ndio walichokifanya kina Zitto.

Na Je, lengo lao la kuwaitia jamaa polisi ni nini? Wote tunajua polisi ni njia tu ya kufika mahakamani, sasa PAC walikuwa wamechukua maamuzi ya kuwapeleka jamaa mahakamani?

Ndio maswali yangu hayo, labda ungenijibu na mimi, sababu majibu yako kwa mleta mada nimeyaelewa.

Ama sivyo kama issue imeisha, inabidi tujue lengo lilikuwa ni nini? Sababu kama waliteleza Je, wameanzisha mchakato stahili? Kama hawajaanzisha ni kwa nini? au wameishapewa hiyo mikataba?

Sangarara,

Labda kwa kumaliza hilo nilipenda UFAHAMU SHARIA ZA TANZANIA ZINARUHUSU MTU KAMA ANAONA HAJATENDEWA HAKI BASI ANA HAKI KWENDA MAHAKAMANI KUDAI HAKI YAKE.

Sasa kama viongozi hao wanaona hawakutendewa haki sasa tujiulize kwanini mpaka leo hawajaenda mahakamani.

Tuvute subra tuone kama viongozi hao watakwenda kudai haki yao mahakamani ya kudhalilishwa na bunge.

 
Sangarara,

Labda kwa kumaliza hilo nilipenda UFAHAMU SHARIA ZA TANZANIA ZINARUHUSU MTU KAMA ANAONA HAJATENDEWA HAKI BASI ANA HAKI KWENDA MAHAKAMANI KUDAI HAKI YAKE.

Sasa kama viongozi hao wanaona hawakutendewa haki sasa tujiulize kwanini mpaka leo hawajaenda mahakamani.

Tuvute subra tuone kama viongozi hao watakwenda kudai haki yao mahakamani ya kudhalilishwa na bunge.


Mkuu Barubaru

Unanichanganya kidogo.

Kwa nini hautaki kuangalia mstakabali wa chanzo cha tukio husika.

PAC iliwakamatisha polisi wakurugenzi wawili wa TPDC sababu walikuwa wanaleta ubishi na kukataa kukabidhi mikataba 26 kwa PAC.

Kwa nini tusisubiri kuangalia kama kwa maamuzi hayo PAC watapatiwa mikataba badala yake tuangalie kama hao jamaa watakimbilia mahakamani kulalamika kwamba wamedhalilishwa?

au lengo ilikuwa kuwadhalilisha na sio kupatiwa mikataba?
 
Mkuu Barubaru

Unanichanganya kidogo.

Kwa nini hautaki kuangalia mstakabali wa chanzo cha tukio husika.

PAC iliwakamatisha polisi wakurugenzi wawili wa TPDC sababu walikuwa wanaleta ubishi na kukataa kukabidhi mikataba 26 kwa PAC.

Kwa nini tusisubiri kuangalia kama kwa maamuzi hayo PAC watapatiwa mikataba badala yake tuangalie kama hao jamaa watakimbilia mahakamani kulalamika kwamba wamedhalilishwa?

au lengo ilikuwa kuwadhalilisha na sio kupatiwa mikataba?

Nafikiri unajichanganya hapo.

Kumbuka kuwa mikataba ni mali ya Serikali ya JMTz na hilo litabaki kuwa sakata la Serikali na Bunge lake.

Lakin kumbuka waliodhalilishwa kama unavyodai ni viongozi wa TPDC ambao walikataa kutoa mikataba hiyo ima kwa sababu Serikali imewakataza kuitoa au ....

sasa kumbuka wao kama wao binafsi kama waliona hawakutendewa haki na Kamati hiyo ya bunge PAC. Wana haki ya kwenda kudai haki yao mahakamani.

Sasa naomba ulitazame suala hilo katika pande mbili.

Pole sana

 
Back
Top Bottom