mimi nilishangaa sana yaani unamkamata mtu aliyeteuliwa na mkuu wakati all the instruction anazipata kutoka juu
Nasikia Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati E. Maswi aliingilia kati na kusema kua Zitto na kamati yake hawana mamlaka ya kuwaweka ndani kwa hiyo ni makosa kuwaweka ndani.
Tanzanian. Mko busy kutizama weaknesses za individuals, badala ya kuangalia masuala muhimu. Inshu sio kukamatwa, Inshu ni MIKATABA iwasilishwe kwenye kamati ya PAC. Nadhan swali la kujiuliza ni kwann inafanywa siri kiasi hicho? Wanaficha nn na kwann?
Wananchi nadhan tungewapokea wajumbe wa PAC, Kwa kudemonstrate na kushinikiza serikali iweke wazi hiyo mikataba, ili Mafisadi wajukikane... Tuache kushambuliana, we r Loosing the Big Target here... Halafu, humans tunakosea, we deserve second Chances, Let us not Loose hope completely kwa Mh. Zitto, Mimi binafsi naona anafanya kazi nzuri... Tumpe support. Tuache Ujuaji, Na unabii wa kijinga.
Hata kama wameteleza kwangu ni sawa. Kwa kiburi na ukaidi wa watendaji wa serikali ni bora tu mtu uzivuke taratibu kuwakomesha wapuuzi wanaolinyonya taifa. Mtu mikataba ni ya rasilimali za nchi sio document za ndoa zao kwanini hawataki wawakilishi wetu sie wenye nchi wazione? Ni nini wanaficha kwenye hiyo mikataba? Wameshazoea kutumia uzoefu wao kwenye mapungufu ya hizi sheria kutufunga midomo. Hii ndo dawa yao.
Pinda alipotoa kauli kuwa watu wanaowaua zerezeru nao pia wauliwe tulipiga kelele ajiuzulu! Pinda aliposema wapinzani nwanasumbua wapigwe tu, tukamtaka ajiuzulu. Sita na ndugu zake wanapovunja sheria bunge la katiba tunalalamika hadi hamu ya kula hatupati Leo zitto na kamati yake wanavunja sheria tunamwona mashujaa, wametumia udikteta kulinda mali ya umma ehheeee?
Juzi makamba (na wengine) wmesema tunahitaji raisi dikteta kila mtu humu kalia naye hadi CCM wenzake wamelia!!!! Zito na kamati yake ni wakosaji kwa hili na wanapaswa kuoma radhi kwa udhalilishaji na uvunjifu wa sheria.
Sheria haziendeshwi na mapenzi na ushabiki hata siku moja. sio sahihi kumshabikia zito hata kama nia njema, afuate sheria.
Kingmairo kalijibu vizuri swali unalouliza. Mbona wale punda wa unga kule China wanaozea jela wao wenyewe baada ya kushikwa na si wale waliowatuma??
Kamati imeshughulika na waliopewa dhamana full stop! Ndiyo maana kwenye haya mawizara wakurugenzi na viongozi makini ni wale wanaopokea maelekezo in writting, hata kama ni kimemo cha maandishi ya mkono!! Wale wachumia tumbo ndo wanapokea maelekezo nyeti kwa simu na saa hiyo hiyo anakurupuka kutekeleza, mambo yakibuma aliyempa instructions anamruka maili mia!!
kwanza inaonyesha kila dalili kuwa wale jamaa waliandaliwa kiaina kabisa kwamba watapelekwa polisi then wataachiwa, inaonyesha huo mpango uliandaliwa mahsusi tangu awali ili kuanza kuliinua jina la msaliti juu, bahati mbaya halijainuka,
Pinda aliyatoa hayo baada ya sheria kuvunjwa, kwa utetezi wake akazidi kuvunja sheria. Kina sita wamevunja sheria kuhalalisha maslahi ya kikundi chao tena ya watu wachache, viongozi wamekuwa wakivunja sheria kwa namna nyingi na tofauti tofauti kwa maslahi yao au ya familia au mitandao yao sio kwa manufaa ya nchi. Kote huko hakuna hatua yoyote tangible mloichukua. Kibaya zaidi wataendelea kuvunja sheria hizi tena kwa maslahi yao na hamtawafanya chochote. Leo hii zitto anapindisha taratibu kwa kutetea maslahi katika rasilimali zenu, mnamuona scrapegoat?Pinda alipotoa kauli kuwa watu wanaowaua zerezeru nao pia wauliwe tulipiga kelele ajiuzulu! Pinda aliposema wapinzani nwanasumbua wapigwe tu, tukamtaka ajiuzulu. Sita na ndugu zake wanapovunja sheria bunge la katiba tunalalamika hadi hamu ya kula hatupati Leo zitto na kamati yake wanavunja sheria tunamwona mashujaa, wametumia udikteta kulinda mali ya umma ehheeee?
Juzi makamba (na wengine) wmesema tunahitaji raisi dikteta kila mtu humu kalia naye hadi CCM wenzake wamelia!!!! Zito na kamati yake ni wakosaji kwa hili na wanapaswa kuoma radhi kwa udhalilishaji na uvunjifu wa sheria.
Sheria haziendeshwi na mapenzi na ushabiki hata siku moja. sio sahihi kumshabikia zito hata kama nia njema, afuate sheria.
siku hizi maagizo au malalamiko ni kwa njia ya email na barua,hii inafuta utata,njia kama simu au maneno ya ana kwa ana hayana ushahidi,sijuh lini watakuwa smart
Wakuu hii hoja tumsimtazame Zitto as Zitto but tuntazame Zitto kama mwenyekiti wa PAC, ili hoja iende vizuri.
Back to topic: kwangu mimi naona kama suala hili endapo litapelekwa mahakamani basi ndio utakuwa mwisho wa mjadala huu kwa kisingizio cha kulinda uhuru wa mahakama, by conclude hapa kamati ya PAC itakuwa haijasaidia kitu zaidi ya kuizamisha hoja hii shimoni.
Mimi sina tatizo kabisa na ilicho fanya Kamati ya Zitto Kabwe. Kama Polisi na Vyombo vya Mashtaka vimeshindwa kuchukua hatua hilo ni tatizo la Sheria zetu na Uwajibikaji. Ni mwendelezo wa siasa zetu za kijinga. Ni mwendelezo wa ujinga wa Waziri na Katibu wake Mkuu wa Wizara ambao wamejenga kiburi kama hiyo ni Ofisi yao binafsi! Ni mwendelezo wa ujinga wetu kulalamikia mtu wa pembeni badala ya mhusika! Ni udhaifu wa utawala wa Kikwete umesababisha hawa wasilale ndani na wanao wazuia wasitoe Mikataba wakatimuliwa
Pinda aliyatoa hayo baada ya sheria kuvunjwa, kwa utetezi wake akazidi kuvunja sheria. Kina sita wamevunja sheria kuhalalisha maslahi ya kikundi chao tena ya watu wachache, viongozi wamekuwa wakivunja sheria kwa namna nyingi na tofauti tofauti kwa maslahi yao au ya familia au mitandao yao sio kwa manufaa ya nchi. Kote huko hakuna hatua yoyote tangible mloichukua. Kibaya zaidi wataendelea kuvunja sheria hizi tena kwa maslahi yao na hamtawafanya chochote. Leo hii zitto anapindisha taratibu kwa kutetea maslahi katika rasilimali zenu, mnamuona scrapegoat?
Well said mkuu, kula likes zangu. Hili ndilo tatizo letu kuu, tumeacha hoja kuu ya TPDC kugomea mikataba ya rasilimali za nchi tumeng'ang'ana na Zitto as if hiyo kamati ni yeye peke yake!
Nchi ina hali mbaya sana shauri ya mambo haya haya badala ya kuendesha mijadala humu mitandaoni na kwingineko kuiunga kamati mkono na kuibana serikali mikataba itolewe ili tujue wanaotuhujumi tuko bize kulumbana wenyewe kwa wenyewe.
Kama akina Chenge walipewe mabilioni kwenye dili la rada ni nini kitazuia hawa watendaji wa TPDC na wizara wasihongwe ili kuingia mikataba isiyo na maslahi na nchi yetu?? Jiulize kwa nini wanaifanya siri hata kwa kamati za bunge?? 2 yrs now hawataki kabisa kuitoa why??
/