Zitto na Halima wamwita January Makamba mnafiki

Status
Not open for further replies.
Ni nguruwe tu mwenye uwezo wa kuvitafuna vitoto vyake akiwa na njaa na wala si Jmakamba kwa kuwa hana uwezo huo ni sawa kusema Jmakamba ni EMPTY SET
 
1.JANUARY ni mjumbe wa sekretarieti ya CCM ambayo ni think tank ya Chama,akiwa mmoja wa waandaaji wa Ajenda za Mkutano wa KAMATI KUU.Yaelekea bado ile dhana ya 'Chama Kushika Hatamu' haijapoteza maana kwa wana CCM wengi,ikiwemo kwake.Aidha ni mwajiriwa wa CCM ,kwa hiyo kikanuni,anawajibika kwa CCM.Tofauti kabisa na FILIKUNJOMBE.
2.Tumekwisha achana na an old paradigm,maana imeshindwa kujibu maswali yetu tena ,na sasa,tuna embrace a new paradigm, inayo promise kutoa baadhi ya maduku duku yetu.Paradigm hiyo sasa ni 'Bunge Kushika Hatamu'.Hapa utaona January ni mwajiriwa wa wana-Bumbuli na WATANZAINIA kwa ujumla wao,kwa hiyo anawajibika kwa wananchi.
Unaweza kuelewa ugumu unaomkabili kama ukijiweka katika nafasi yake.
Hali hiyo hiyo itamkabili mama Makinda.
 
JMakamba amepotea njia hapo bora atulie ila akitaka kwenda deep ataaibika tu kinachofuata.

UBUNGE WENYEWE KAUPATA, SHUKRANI YA MAFISADI. TUNAJUA NINI KILICHOTENDEKA KUMFITINI SHELUKINDO, NA HATA KUHONGA WABUNGE NJAA WA UPINZANI. SIKU ZENU Ni Za mwisho.
 
Your the clear example of "POVERTY OF INTELECT".

The power of intellect has never been a common property under the sun, you have yours and I do posses mine.......its possible to go through the same intellectual tunnel and come out of it with different mental capacities and qualities......and possibly different paradigms as well, by the way the sort of yours are so many out here..............the ones who think of a bread instead of a bakery itself

Topics on personal attack and point missing were not my favourites during my old school days.........

Mytake; The alternative could be for you to come out loud on the topic requirements so that (we) members could see the smartness of your mental gymnastics instead of highlighting the poverty of my verry intellect!!!!!!!!!!!

Harness the thread IlongaIlunga
 
Hivi kwani ni lazima vijana wote wa Tanzania waunge mkono matakwa ya vijana wa CHADEMA?
Kigarama, hivi matakwa ya vijana wa Chadema ni yapi.

Wapo vijana hawafaidiki chochote kutokana na serikali iliyopo madarakani lakini nao wanayaona yanayotokea kama ni makosa ya kiutendaji na wala si uhalifu.
Kwa hiyo hawa vijana wanaamini;

  • EPA haikuwa uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
  • KAGODA haikuwa uhalifu, ni makosa tu ya utendaji!
  • KIWIRA haikuwa uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
  • MEREMETA haikuwa uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
  • RICHMOND haikuwa uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
  • WIZI si uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
  • UFISADI si uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
  • RUSHWA si uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji
  • UHALIFU si uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji, duh!
Hawa wasichukuliwe kama ni mambumbu bali ni vijana wenzetu wenye mitizamo tofauti na sisi!!
Kwa hiyo kuwa na mtizamo tofauti ni pamoja na kufumbia macho uozo unaotuzunguka. Sasa jamani hapo tutakuwa tunajenga taifa la namna gani? Kama hawa vijana wenzetu wenye msimamo tofauti si mbumbumbu kama unavyodai, tuwaiteje? Mbuni?

Ostrich_head_in_sand.jpg


Hapana Kigarama, naomba kutofautiana na wewe.​
 
Hii ndio JF,
kila mnayepishana mawazo MNAFIKI.
Kazi kweli kweli tanganyika

Ndugu yangu Tume ya Katiba,

Kuna mambo ambayo mnaweza kupishana kama priorities ya nini kianze na kianzie wapi. Hapo hakuna unafiki wala nini ni namna mtu anavyojenga hoja yake na utetezi wa hoja hiyo.

Kwenye hili swala approach iko open; kwamba pelekeni hoja binafsi yenye sahihi 70 za wabunge then mnatoa options 2, kama alizotoa Zitto, kwamba piga kura ya kutokuwa na imani au mawaziri husika wajiuzulu au wakigoma Rais awatimue. Sasa hapa kigumu kiko wapi ambacho kinahitaji caucus ya CCM?

Watu tunasema Makamba ni mnafiki kwa kuwa njia wanayotumia wao haimbani JK kufanya mabadiliko ambayo wabunge wote wa CCM na Upinzani wanataka. Kama wabunge wa CCM wasingekwenda kufanya lobbying kwenye caucus uchwara yao, sasa hivi hadithi ingekuwa ni nyingine.

Mnafiki ni yule ambaye akiwa Bungeni hasemi kitu lakini akiingia kwenye caucus anafungulia mdomo. Januari Makamba baada ya uchaguzi wa EALA alijinasibu kwamba anachukia rushwa. Pia kila siku anajinasibu kwamba anachukia ufisadi. Huwezi ukachukia ufisadi, halafu ukawa unawabembeleza mafisadi waondoke. Njia wanayotumia wabunge wa CCM ni kuwabembeleza mafisadi wajizulu. Njia hiyo ilishashindikana, maana walishaagiza Ngeleja na Jairo waachie ngazi, bado mpaka leo hakieleweki. Sasa kitendo cha kuendelea kutumia njia hiyo ni ku-admit failure, kuwa na hidden agenda (unafiki), ghiliba kwa wapiga kura au umbumbumbu.

Viongozi wote wa CCM ni WANAFIKI, kwenye majukwaa wanapiga kelele wanachukia ufisadi lakini hawawachukulii sheria mafisadi hata pale ambapo ushahidi upo. Ukitaka kujua unafiki wa wana CCM, msikilize JK akiwa anawatetea watumishi wa umma ambao wanatuhumiwa na ufisadi, utamsikia anasema "unajua kuna sheria na taratibu za kazi ajira ambazo zinatakiwa kufuatwa kabla hujamfuta mtu kazi". Uwaziri siyo ajira na haina mkataba, kwanini anasita kuwatimua?

KAMA WANACHUKIA UFISADI WAFANYE KWELI, VINGINEVYO TUTAWAITA WANAFIKI au wanafanya usanii wa kudanganya wapiga kura.
 
  • EPA haikuwa uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
  • KAGODA haikuwa uhalifu, ni makosa tu ya utendaji!
  • KIWIRA haikuwa uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
  • MEREMETA haikuwa uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
  • RICHMOND haikuwa uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
  • WIZI si uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
  • UFISADI si uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
  • RUSHWA si uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji
  • UHALIFU si uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji, duh!
Kwanza Mag3 wengi wenu humu mnachanganya mambo na kutoka nje ya mada. Hapa hoja ni kuhusu ripoti ya CAG na wala si hayo ya Meremeta au Richmond na mengineyo. Kwa mfano hawa mawaziri si wao waliohusika moja kwa moja kwenye kuchota hizo fedha ila yametokea na kufanywa na watu wa chini yao.

Wakati DR. Hibrahim Msabaha alipokuwa anatoa taarifa yake ya kujiuzulu bungeni alisema "kama tusipobadili mfumo hata aje nani naye mtamsulubu", na alitumia neno "bangusilo" kuonyesha kwamba ametolewa kafara badala ya mfumo kurekebishwa.

Hata Mzee Mwanakijiji kwenye hoja yake ya Zitto kupeleka hoja ya kumng'oa Waziri Mkuu amesema tatizo si Waziri Mkuu bali ni Rais Mwenyewe. Kama mfumo unawaruhusu kufanya hivyo walivyofanya. Basi tatizo si wao bali ni mfumo na sisi wengi wetu ni waoga wa kubadili mfumo kwa sababu kwa namna moja au nyingine tunafaidika nao.

Umewahi kujiuliza itachukua muda gani kurekebisha mfumo? unadhani miezi kumi na nane iliyotolewa na Kikwete inatosha kutafuta muafaka wa kitaifa kuhusu Katiba? Narudia tena wapo ambao wanaamini hawa mawaziri hawakutenda uhalifu bali ni makosa ya kiutendaji. tusijifanye vipofu kutokuona kwamba watu kama hao watakuwepo na hakuna njia ya kuwaondoa kwetu kwani ndiyo maumbile yalivyo. Na sijasema wako sahihi kufikiri wanavyofikiri.

Kuna watu wanaamini Ushoga ni jambo la kawaida KABISA na wengine wanaona ni laana ya KUTUPWA. Kati ya haya makundi mawili moja likishinda kwa wingi wake lisijifanye kwamba kundi jingine halina haki ya kufikiri linavyofikiri kwa sababu ni wachache. HOJA YANGU NDIYO HII!!

 
Kwa kifupi J Makamba anajipendekeza ili akitoka Ngeleja awekwe yeye kama ilivyokuwa kwenye ile Email ya kipindi kile kutoka kwa dada yake kwenda kwa Mpenzi wake yule kigogo wa Barick.

Kwa hiyo mimi sishangai kuona hilo linatokea, maana anataka aingie pale na kwenye ukweli anataka kuupindisha hapa mwishoni.

Kingine ni kumbuka Januari ni mwiongoni mwa wabunge wa kuteuliwa na si wakuchaguliwa na wananchi kama kina Filikunjombe anajua kura za wananchi alizipataje, ila kwa huyu dogo alitengenezewa mazingira ya kupita bila kupingwa.

Kingine ni kwamba hii ni Dalili nzuri kwa CDM kuitoa madarakani, kwa sababu kila kona ya nchi hii kila raia alijua wale wabunge 8 wanaondoka kwahiyo kama JK amekataa ni opportunity Nzuri kwa wapinzano kwenda kwa wananchi.

Kama bungebi tu kwa haraka haraka tumepata wabunge watano kutoka CCM maana yake wananchi wa Jimbo lake tunao upinzani na kwa hesabu ndogo tu ni kwamba upinzani umejiongezea Nguvu..
 
Like father, like son.
Kama baba alikua bichwa maji, unategemea mtoto atatoa wapi akili?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom