commonmwananchi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2011
- 3,377
- 1,957
Ndugu wanabodi,
Nimeona niliweke hili swali hadharani ili kwanza tulijadili kwa sababu linahusu maslahi ya raia wote wa nchi hii.
Lakini pia huenda kuna watakaoweza kutoa majibu kwa kiwango wanachoelewa.
Ni muda sasa tangu ccm walipowapiga Ban wanachama makada waliokuwa wametangaza nia yao ya kuusaka urais wa nchi hii kupitia ccm.
Hilo lilifanyika kwa kudaiwa kuanza kampeni mapema na bila ridhaa ya chama chao.
Lakini sasa..tumeona hivi karibuni january makamba ameendelea na kampeni hizohizo...kwa mbinu ya kuzindua kitabu ambacho kilihaririwa na rais mstaafu wa jamhuri ya tanzania mh.Alli hassan mwinyi.
Na kikaandaliwa na (padri msimamishwa upadri)
Privatus karugendo.
Baadae wasomaji wa magazeti ya mwananchi na Raia mwema nao wakachomekewa kitabu hicho katika matoleo ya magazeti hayo(mwananchi toleo la jumatatu january 19/2015 na raia mwema jumatano 21/2015),
Kabla hiyo haijapoa,tukamuona january huyohuyo kwenye tv station kadhaa za humu nchini kwa mgongo wa kupromote kitabu chake hicho.
Na leo 31/01/2015,mchana wa saa saba na nusu,TBC televisheni imerusha tena matangazo ya TBC radio akihojiwa live studio ya radio.
Wakati haya yote yakifanyika hakuna kada au kiongozi yeyote yule wa ccm aliyetoa tamko.iwe kutoa angalizo au kukemea.
Isipokuwa tumeona mtafuta urais mwingine mwigulu nchemba, akizuiwa hata kufanya mikutano ya kuhamasisha chama pamoja na nafasi aliyonayo ya unaibu katibu mkuu ccm bara inamruhusu kufanya mikutano hiyo.
Wakati fulani tumetaarifiwa na vyombo vya habari kwamba,familia ya Alli hassan mwinyi ina mgogoro kuhusu mgombea urais wa muungano.
Na pia tukaambiwa kwamba kuna maelewano au makubaliano fulani kati ya mmoja wa watoto wa mzee mwinyi kujitokeza nafasi ya mgombea mwenza,bara.ili awe makamu wa rais.
Na baadae kugombea urais wa zanzibar.nafasi ambayo mwanafamilia mwingine pia anaitaka kwa udi na uvumba huko visiwani.
Swali kwa wana ccm...je huyu makamba ndio mpango mzima??