Kosa kubwa walilofanya January Makamba, Nape na Zitto

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,353
2,137
Ukifuatilia vuguvugu la kisiasa linaloendelea nchini kwa sasa, hususan ‘mnyukano’ unaoendelea ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), utagundua kwamba kuna shida kubwa mahali fulani na kinachogombaniwa, pengine si hiki ambacho wengi wanakiona kwa nje, bali kitu kingine kikubwa zaidi.

Sitaki sana kuwazungumzia wazee na wastaafu kama Yusuph Makamba, Abdulrahman Kinana au Benard Membe, ni busara kuwaacha wapumzike baada ya kulitumikia taifa na kukitumikia chama kwa kipindi kirefu katika maisha yao.

Mchambuzi mmoja wa masuala ya kisiasa nchini, aliuelezea waraka wa Kinana na Makamba kama picha ya mnyama mkali, ambayo ilikuwa ikitumika kuwatishia watu lakini nyuma ya picha hiyo, kuna wanyama wakali halisi, ambao wameshakaa tayaritayari, wakiwa wamechomoza makucha yao na meno makali, wakisubiri windo lao.

Kadiri muda unavyosonga mbele, tunaanza kuwaona sasa ni akina nani waliokuwa nyuma ya waraka huo na nini ilikuwa dhamira yao! Yawezekana kweli Makamba na Kinana walikuwa na hoja zao kuhusu kile walichokuwa wakikilalamikia, lakini msukumo mkubwa unatoka kwa vijana watatu wanaoonekana kuwa kama ‘think tanks’ ya mpango mzima.

Nawazungumzia January Makamba, Nape Nnauye na Zitto Kabwe. Pengine utashangaa kwa nini namtaja Zitto wakati si mwanachama wa CCM? Ukweli ni kwamba japokuwa Zitto si mwana-CCM, lakini uswahiba wake na January pamoja na Nape, unaonesha watatu hawa wana ‘misheni’ inayofanana.

Yawezekana hii ndiyo sababu iliyomfanya baada ya waraka kutoka na kuwa gumzo kubwa, Zitto aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuelezea mawazo yake, akijitahidi sana kukwepa mtego wa kuonesha mahali alipokuwa ameegamia na kujificha kwenye kivuli cha ‘maslahi mapana ya taifa’.

Yawezekana pia kwamba ni ‘misheni’ hii iliyomfanya Zitto awe mwepesi wa kumkaribisha upya January kwenye kundi lao aliloliita ‘back bencher’ bungeni muda mfupi tu baada ya kuvuliwa uwaziri na Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Ukiwatazama wote watatu, ni vijana, tena wenye ushawishi mkubwa miongoni mwa vijana na Watanzania kwa jumla. Wanasimama kama ‘role models’ wa vijana wengi wenye ndoto za kuingia katika siasa.

Hata hivyo, licha ya umaarufu na ushawishi wao, katika hili linaloendelea, watatu hawa wamefanya kosa kubwa la kifo ambalo litawagharimu kisawasawa.

Yawezekana wengi wakahisi kwamba huenda ‘mission’ yao ni kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020! La hasha! Malengo ya wote watatu, ni uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Zito anataka kuwa rais wa nchi hii baada ya Rais Magufuli kuondoka, January Makamba anaota ndoto hizohizo na Nape Nnayue hali kadhalika.

Ukishalielewa hilo, utaanza kupata picha kwamba kumbe kinachoendelea sasa, ni vita ya madaraka! Power Struggle! Vita ambayo ni mbaya kuliko vita nyingine yoyote!

Mwandishi Mahiri Robert Greene katika kitabu chake cha 48 Laws of Power (Sheria 48 za Madaraka), amefafanua kwa kina sana mambo ambayo wanasiasa wanapokuwa wanahitaji madaraka wanatakiwa kuyafanya, na hata pale wanapokuwa kwenye madaraka, nini cha kufanya ili kuendelea kubaki madarakani.

Katika kitabu chake hicho, Sheria ya Tatu, Greene anaeleza kwamba ‘CONCEAL YOUR INTENTIONS’ akimaanisha ‘Ficha Malengo Yako!’ Unapokuwa kwenye vita ya madaraka, maadui zako hawatakiwi kujua ni nini unachokilenga.

Watu wakiwa hawajui unachokilenga katika mambo mbalimbali unayoyafanya, hawawezi kuandaa mbinu za kupambana na wewe, wakija kushtukia inakuwa tayari wamechelewa na inakuwa rahisi kwako kutimiza kile unachokitafuta; kupata madaraka.

Lakini katika kitabu hicho, Sheria ya Kumi na Tano, Greene anaeleza kwamba ‘CRUSH YOUR ENEMIES TOTALLY’ akimaanisha wavunjevunje kabisa maadui zako.

Mbinu hii imekuwa ikitumika sana na viongozi waliopo madarakani tangu zama za kina Musa (katika Biblia). Tangu enzi hizo, mtu yeyote ambaye alionesha kupingana na Mfalme, aliishia kukatwa kichwa au kunyongwa hadharani. Hali ni hiyohiyo mpaka leo.

Uzuri na ubaya ni kwamba, viongozi karibu wote waliopo madarakani, wamekisoma kitabu hiki na wanatumia falsafa zilizomo ndani yake. Watu wengi waliofanikiwa kupata madaraka, ni wale ambao walificha dhamira zao mpaka dakika za mwisho.

Rais Magufuli kwa mfano, wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya CCM, alikuwa kimya kabisa, hakupewa nafasi na pengine hakuwa akizungumziwa kuwa tishio.

Hata alipokuwa akihojiwa kama ana mpango wa kuchukua fomu, alikuwa akitoa majibu ambayo yaliwafanya wengi wasimuweke kwenye orodha ya watu wanaopewa nafasi kubwa ya kupata tiketi ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha urais.

Alifanikiwa kuficha dhamira yake lakini akaja kuibuka dakika za mwisho na kuchukua fomu, mwisho akaibuka mshindi katika vita ya madaraka na leo ndiyo rais wetu. Wote ambao walishindwa kuifuata sheria hiyo, waliangukia pua na wengi wao hicho kikawa ndiyo ‘kifo’ chao kisiasa.

January, Nape na Zitto, wamefanya makosa makubwa katika sheria hii namba tatu. Wote wanauwania urais wa Tanzania 2025 lakini wameshindwa kuficha dhamira zao, matokeo yake wamejikuta wakishiriki kwenye mambo ambayo yameibua taharuki kubwa ndani ya chama na nchi kwa jumla.

Kwa Zitto hii inaweza kuwa ni mara yake ya pili kufanya kosa la namna hiyo, alifanya hivyo mwaka 2014 kwa kushindwa kuficha dhamira yake na akaishia kufutwa uanachama wa Chadema, bahati yake ni kwamba alianzisha chama kingine cha ACT. Kwa Nape pia hii ni mara ya pili, alifanya kosa kama hilo awali na kujikuta akiishia kuvuliwa uwaziri na Rais Magufuli.

January naye amefanya kosa lilelile, la kushindwa kuzichanga vyema karata zake na mwisho dhamira yake imefichuka, ameishia kutenguliwa kwenye nafasi ya uwaziri aliyokuwa nayo.

Huu unaweza kuwa mwanzo tu wa mwisho wao, Waingereza wanasema The Beggining of The End!

Viongozi waliopo madarakani, dunia nzima huwa wanatumia sana Sheria Namba 15! Ukishaona mtu anajaribu kushindana na wewe au kufanya mambo yanayoweza kutafsirika kama hujuma wakati upo madarakani, Robert Greene anakwambia ‘crush him totally!’ Mmalize kabisa kwa sababu kama utamuacha akiwa japo na nguvu kidogo, anaweza kuanza kujiimarisha tena halafu akawa tatizo siku za baadaye, kwa hiyo dawa yake ni kummaliza kabisa.

Pengine kwa sasa wategemee tu huruma za Rais Magufuli lakini kama akiamua kutumia sheria hiyo, kama wanavyotumia viongozi wengine duniani kote, kosa walilolifanya vijana hawa litamaanisha ‘kifo’ chao cha kisiasa!

Litamaanisha kwamba huu ndiyo mwisho wa ndoto zao walizokuwa wakiziota kwa kipindi kirefu za kuja kuwania urais mwaka 2025 na pengine kushinda na hatimaye kushika hatamu. Ni suala la muda tu.

Hashpower7113
 
As long as ni Watanzania na wana sifa za kikatiba kuwania uraisi basi ni haki yao.

Pia acha kutisha watu,hii ni nchi yetu wote hakuna mwenye uhalali wa kutawala kumzidi mwenzie,wote tunaongozwa na katiba moja tu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
As long as ni Watanzania na wana sifa za kikatiba kuwania uraisi basi ni haki yao.

Pia acha kutisha watu,hii ni nchi yetu wote hakuna mwenye uhalali wa kutawala kumzidi mwenzie,wote tunaongozwa na katiba moja tu ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania.
Kwa hiyo hao watatu wanautaka urais na wameungana
Nani atateuliwa agombee urais hiyo 2025?
 
As long as ni Watanzania na wana sifa za kikatiba kuwania uraisi basi ni haki yao.

Pia acha kutisha watu,hii ni nchi yetu wote hakuna mwenye uhalali wa kutawala kumzidi mwenzie,wote tunaongozwa na katiba moja tu ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania.
Ni sawa Mkuu! Hakuna anayemtisha yeyote, ni mtazamo tu
 
Ukifuatilia vuguvugu la kisiasa linaloendelea nchini kwa sasa, hususan ‘mnyukano’ unaoendelea ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), utagundua kwamba kuna shida kubwa mahali fulani na kinachogombaniwa, pengine si hiki ambacho wengi wanakiona kwa nje, bali kitu kingine kikubwa zaidi.

Sitaki sana kuwazungumzia wazee na wastaafu kama Yusuph Makamba, Abdulrahman Kinana au Benard Membe, ni busara kuwaacha wapumzike baada ya kulitumikia taifa na kukitumikia chama kwa kipindi kirefu katika maisha yao.

Mchambuzi mmoja wa masuala ya kisiasa nchini, aliuelezea waraka wa Kinana na Makamba kama picha ya mnyama mkali, ambayo ilikuwa ikitumika kuwatishia watu lakini nyuma ya picha hiyo, kuna wanyama wakali halisi, ambao wameshakaa tayaritayari, wakiwa wamechomoza makucha yao na meno makali, wakisubiri windo lao.

Kadiri muda unavyosonga mbele, tunaanza kuwaona sasa ni akina nani waliokuwa nyuma ya waraka huo na nini ilikuwa dhamira yao! Yawezekana kweli Makamba na Kinana walikuwa na hoja zao kuhusu kile walichokuwa wakikilalamikia, lakini msukumo mkubwa unatoka kwa vijana watatu wanaoonekana kuwa kama ‘think tanks’ ya mpango mzima.

Nawazungumzia January Makamba, Nape Nnauye na Zitto Kabwe. Pengine utashangaa kwa nini namtaja Zitto wakati si mwanachama wa CCM? Ukweli ni kwamba japokuwa Zitto si mwana-CCM, lakini uswahiba wake na January pamoja na Nape, unaonesha watatu hawa wana ‘misheni’ inayofanana.

Yawezekana hii ndiyo sababu iliyomfanya baada ya waraka kutoka na kuwa gumzo kubwa, Zitto aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuelezea mawazo yake, akijitahidi sana kukwepa mtego wa kuonesha mahali alipokuwa ameegamia na kujificha kwenye kivuli cha ‘maslahi mapana ya taifa’.

Yawezekana pia kwamba ni ‘misheni’ hii iliyomfanya Zitto awe mwepesi wa kumkaribisha upya January kwenye kundi lao aliloliita ‘back bencher’ bungeni muda mfupi tu baada ya kuvuliwa uwaziri na Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Ukiwatazama wote watatu, ni vijana, tena wenye ushawishi mkubwa miongoni mwa vijana na Watanzania kwa jumla. Wanasimama kama ‘role models’ wa vijana wengi wenye ndoto za kuingia katika siasa.

Hata hivyo, licha ya umaarufu na ushawishi wao, katika hili linaloendelea, watatu hawa wamefanya kosa kubwa la kifo ambalo litawagharimu kisawasawa.

Yawezekana wengi wakahisi kwamba huenda ‘mission’ yao ni kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020! La hasha! Malengo ya wote watatu, ni uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Zito anataka kuwa rais wa nchi hii baada ya Rais Magufuli kuondoka, January Makamba anaota ndoto hizohizo na Nape Nnayue hali kadhalika.

Ukishalielewa hilo, utaanza kupata picha kwamba kumbe kinachoendelea sasa, ni vita ya madaraka! Power Struggle! Vita ambayo ni mbaya kuliko vita nyingine yoyote!

Mwandishi Mahiri Robert Greene katika kitabu chake cha 48 Laws of Power (Sheria 48 za Madaraka), amefafanua kwa kina sana mambo ambayo wanasiasa wanapokuwa wanahitaji madaraka wanatakiwa kuyafanya, na hata pale wanapokuwa kwenye madaraka, nini cha kufanya ili kuendelea kubaki madarakani.

Katika kitabu chake hicho, Sheria ya Tatu, Greene anaeleza kwamba ‘CONCEAL YOUR INTENTIONS’ akimaanisha ‘Ficha Malengo Yako!’ Unapokuwa kwenye vita ya madaraka, maadui zako hawatakiwi kujua ni nini unachokilenga.

Watu wakiwa hawajui unachokilenga katika mambo mbalimbali unayoyafanya, hawawezi kuandaa mbinu za kupambana na wewe, wakija kushtukia inakuwa tayari wamechelewa na inakuwa rahisi kwako kutimiza kile unachokitafuta; kupata madaraka.

Lakini katika kitabu hicho, Sheria ya Kumi na Tano, Greene anaeleza kwamba ‘CRUSH YOUR ENEMIES TOTALLY’ akimaanisha wavunjevunje kabisa maadui zako.

Mbinu hii imekuwa ikitumika sana na viongozi waliopo madarakani tangu zama za kina Musa (katika Biblia). Tangu enzi hizo, mtu yeyote ambaye alionesha kupingana na Mfalme, aliishia kukatwa kichwa au kunyongwa hadharani. Hali ni hiyohiyo mpaka leo.

Uzuri na ubaya ni kwamba, viongozi karibu wote waliopo madarakani, wamekisoma kitabu hiki na wanatumia falsafa zilizomo ndani yake. Watu wengi waliofanikiwa kupata madaraka, ni wale ambao walificha dhamira zao mpaka dakika za mwisho.

Rais Magufuli kwa mfano, wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya CCM, alikuwa kimya kabisa, hakupewa nafasi na pengine hakuwa akizungumziwa kuwa tishio.

Hata alipokuwa akihojiwa kama ana mpango wa kuchukua fomu, alikuwa akitoa majibu ambayo yaliwafanya wengi wasimuweke kwenye orodha ya watu wanaopewa nafasi kubwa ya kupata tiketi ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha urais.

Alifanikiwa kuficha dhamira yake lakini akaja kuibuka dakika za mwisho na kuchukua fomu, mwisho akaibuka mshindi katika vita ya madaraka na leo ndiyo rais wetu. Wote ambao walishindwa kuifuata sheria hiyo, waliangukia pua na wengi wao hicho kikawa ndiyo ‘kifo’ chao kisiasa.

January, Nape na Zitto, wamefanya makosa makubwa katika sheria hii namba tatu. Wote wanauwania urais wa Tanzania 2025 lakini wameshindwa kuficha dhamira zao, matokeo yake wamejikuta wakishiriki kwenye mambo ambayo yameibua taharuki kubwa ndani ya chama na nchi kwa jumla.

Kwa Zitto hii inaweza kuwa ni mara yake ya pili kufanya kosa la namna hiyo, alifanya hivyo mwaka 2014 kwa kushindwa kuficha dhamira yake na akaishia kufutwa uanachama wa Chadema, bahati yake ni kwamba alianzisha chama kingine cha ACT. Kwa Nape pia hii ni mara ya pili, alifanya kosa kama hilo awali na kujikuta akiishia kuvuliwa uwaziri na Rais Magufuli.

January naye amefanya kosa lilelile, la kushindwa kuzichanga vyema karata zake na mwisho dhamira yake imefichuka, ameishia kutenguliwa kwenye nafasi ya uwaziri aliyokuwa nayo.

Huu unaweza kuwa mwanzo tu wa mwisho wao, Waingereza wanasema The Beggining of The End!

Viongozi waliopo madarakani, dunia nzima huwa wanatumia sana Sheria Namba 15! Ukishaona mtu anajaribu kushindana na wewe au kufanya mambo yanayoweza kutafsirika kama hujuma wakati upo madarakani, Robert Greene anakwambia ‘crush him totally!’ Mmalize kabisa kwa sababu kama utamuacha akiwa japo na nguvu kidogo, anaweza kuanza kujiimarisha tena halafu akawa tatizo siku za baadaye, kwa hiyo dawa yake ni kummaliza kabisa.

Pengine kwa sasa wategemee tu huruma za Rais Magufuli lakini kama akiamua kutumia sheria hiyo, kama wanavyotumia viongozi wengine duniani kote, kosa walilolifanya vijana hawa litamaanisha ‘kifo’ chao cha kisiasa!

Litamaanisha kwamba huu ndiyo mwisho wa ndoto zao walizokuwa wakiziota kwa kipindi kirefu za kuja kuwania urais mwaka 2025 na pengine kushinda na hatimaye kushika hatamu. Ni suala la muda tu.

Hashpower7113
Makala safi sana ,kuna funzo.Ila kiukweli hawa kwa tamaa zao nahisi wanapotea jumla ,sidhani kama watasimama tena na kuwa na nguvu
 
Back
Top Bottom