Zitto: Membe karibu upinzani

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
430
1,000
Na Mwandishi Wetu, Kilwa

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema sasa ni wakati mwafaka kwa Benard Membe kujiunga na upinzani rasmi hapa nchini.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kilwa, Zitto alisema mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa mbunge na waziri wa wizara nyeti hapa nchini ana fursa ya kuunganisha Watanzania wenye kiu ya mabadiliko kupitia vyama mbadala vya siasa.

"Ndugu yangu Benard Membe kafukuzwa uanachama wa CCM. Ninajua bado anatetea haki yake ya uanachama huko. Ni hatua sahihi.

"Hata hivyo muda wa kuleta mabadiliko katika nchi umewadia, ninamsihi afanye maamuzi ya kuunganisha nguvu kupitia vyama mbadala ili kuwapa Watanzania Mabadiliko wanayoyataka," alisema.

Kiongozi huyo wa ACT ambaye yuko katika ziara ya kichama ya mikutano ya ndani Kusini mwa Tanzania, alisema anaelewa mwanasiasa huyo bado anapambana kubaki ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini muda huu anahitajika zaidi kwenye upinzani.

Membe, mmoja wa wanasiasa mashuhuri nchini, alifukuzwa uanachama wake CCM miezi michache iliyopita na hali yake kwa sasa iko kwenye sintofahamu.

Akizungumza na redio moja ya kimataifa hivi karibuni, Membe alisema ingawa kwa sasa bado anaangalia hatma yake ndani ya CCM, upo uwezekano wa kuwania Urais kupitia vyama vingine mbadala.

Lakini, katika mkutano huo wa Kilwa; Kusini mwa Tanzania anakotokea Membe, Zitto alisema historia itamhukumu vibaya mwanasiasa huyo endapo hatafanya uamuzi wa kujiunga na upinzani sasa.

"Mimi najua Membe anaipenda Tanzania na ni Mwana demokrasia.
Adhihirishe mapenzi yake kwa nchi yetu kwa kuongeza nguvu wa vyama mbadala.

"Kama kuna kosa la uhaini basi itakuwa ni kwa Membe kutofanya maamuzi ya kuwatumikia Watanzania nje ya CCM. Ninamsihi kuwa afanye tafakari na kufanya maamuzi sahihi na wananchi," alisema Zitto huku akishangiliwa na umati uliohudhuria mkutano huo.

Membe amegeuka kuwa mmoja wa wakosoaji wa utawala wa Rais John Magufuli, akikosoa hadharani mambo anayodhani hayako sawa kiutawala.

Ukosoaji huo umemjengea umashuhuri mkubwa kiasi kwamba sasa anatajwa kuwa mmoja wa wanasiasa wanaotajwa kuweza kuwania Urais wa Tanzania kupitia upinzani ( vyama mbadala) mwezi Oktoba mwaka huu.

Zitto anaendelea na ziara yake ya mikoa ya Kusini.

Mwisho
 
G4rpolitics

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
3,744
2,000
Nilitabiri hii na lazima itimie kuwa Membe to Act then Act na Chadema mezani halafu kidedea atakuwa ni BM kuwania katika tiketi ya muungano wa upinzani, ila mtakuwa mmemsaliti Lissu.
 
PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
10,198
2,000
nilitabiri hii na lazima itimie kuwa Membe to Act then Act na Chadema mezani halafu kidedea atakuwa ni BM kuwania katika tiketi ya muungano wa upinzani....ila mtakuwa mmemsaliti Lissu.
Kitu ambacho CHADEMA hakitaruhusu kutokea ni kuunga mkono mgombea urais wa ACT WAZALENDO.

Kufanya hivyo itakuwa ni tiketi ya moja kwa moja kuwa kimeiruhusu ACT kukua kupitia mgongo wake na CHADEMA kusinyaa kupitia ACT.

It will never happen.
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
4,549
2,000
Na Mwandishi Wetu, Kilwa

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema sasa ni wakati mwafaka kwa Benard Membe kujiunga na upinzani rasmi hapa nchini.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kilwa, Zitto alisema mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa mbunge na waziri wa wizara nyeti hapa nchini ana fursa ya kuunganisha Watanzania wenye kiu ya mabadiliko kupitia vyama mbadala vya siasa.

"Ndugu yangu Benard Membe kafukuzwa uanachama wa CCM. Ninajua bado anatetea haki yake ya uanachama huko. Ni hatua sahihi.

"Hata hivyo muda wa kuleta mabadiliko katika nchi umewadia, ninamsihi afanye maamuzi ya kuunganisha nguvu kupitia vyama mbadala ili kuwapa Watanzania Mabadiliko wanayoyataka," alisema.

Kiongozi huyo wa ACT ambaye yuko katika ziara ya kichama ya mikutano ya ndani Kusini mwa Tanzania, alisema anaelewa mwanasiasa huyo bado anapambana kubaki ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini muda huu anahitajika zaidi kwenye upinzani.

Membe, mmoja wa wanasiasa mashuhuri nchini, alifukuzwa uanachama wake CCM miezi michache iliyopita na hali yake kwa sasa iko kwenye sintofahamu.

Akizungumza na redio moja ya kimataifa hivi karibuni, Membe alisema ingawa kwa sasa bado anaangalia hatma yake ndani ya CCM, upo uwezekano wa kuwania Urais kupitia vyama vingine mbadala.

Lakini, katika mkutano huo wa Kilwa; Kusini mwa Tanzania anakotokea Membe, Zitto alisema historia itamhukumu vibaya mwanasiasa huyo endapo hatafanya uamuzi wa kujiunga na upinzani sasa.

"Mimi najua Membe anaipenda Tanzania na ni Mwana demokrasia.
Adhihirishe mapenzi yake kwa nchi yetu kwa kuongeza nguvu wa vyama mbadala.

"Kama kuna kosa la uhaini basi itakuwa ni kwa Membe kutofanya maamuzi ya kuwatumikia Watanzania nje ya CCM. Ninamsihi kuwa afanye tafakari na kufanya maamuzi sahihi na wananchi," alisema Zitto huku akishangiliwa na umati uliohudhuria mkutano huo.

Membe amegeuka kuwa mmoja wa wakosoaji wa utawala wa Rais John Magufuli, akikosoa hadharani mambo anayodhani hayako sawa kiutawala.

Ukosoaji huo umemjengea umashuhuri mkubwa kiasi kwamba sasa anatajwa kuwa mmoja wa wanasiasa wanaotajwa kuweza kuwania Urais wa Tanzania kupitia upinzani ( vyama mbadala) mwezi Oktoba mwaka huu.

Zitto anaendelea na ziara yake ya mikoa ya Kusini.

Mwisho
Kamanda Membe atatueleza mengi siku za usoni na ana kazi yake kubwa upinzani.
 
paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
1,521
2,000
Ningekuwa Membe, Wakati huu ndio ungekuwa Wakati wa kupumzika kisiasa, kwani si rahisi Kwa mtu kama Membe Kwa siasa alixokuwa amefikia halafu Leo arudi chekechea, hizi siasa ndizo zilizowashusha hadhi kina Sumae na wengine,

Lakini Kwa kuwa huenda tena ikawa na siasa zilezile za CCM na ujasusi wake, Membe nenda kama ulivyotumwa na CCM kafanye yako, na temu hii hili bomu likiwalipukia hawa vichwa maji labda watakoma kushobokea vitu vizuri vizuri vilivyotegwa barabarani vikitafuta wajinga wasio ridhika na vyao

2015 nililazimika kukikacha Chama changu pendwa Kwa vitu hivihivi vya kijinga
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
24,256
2,000
nilitabiri hii na lazima itimie kuwa Membe to Act then Act na Chadema mezani halafu kidedea atakuwa ni BM kuwania katika tiketi ya muungano wa upinzani....ila mtakuwa mmemsaliti Lissu.
Chadema hawawezi kumkubali membe hata iweje,huku wao wana chaguo la Mbowe,lissu au Nyalandu
 
Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
22,722
2,000
Kama ACT ikamsimamisha Membe halafu chadema wakaungana na ACT halafu mgombea awe Membe basi chadema na upinzani kwa jumla hatuna la kujifunza,ni kuwakosesha wananchi imani ,lowasa na kina sumaye walikuja wakarudi halafu leo membe tena,upinzani wa nchi hii utakuwa hauaminiki hamna hata haja ya kuwa na wapinzani.

Heri kama mgombea anakosekana wasisimamishe wajenge chama huku chini hadi mda wa kumsimamisha mgombea wao ufike
 
mr chopa

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
4,660
2,000
Zitto Mwaka 2015 alikuwa mtu wa kwanza kumsema Membe juu ya ufisadi wa pesa za LIBYA alipotangaza kugombea kupitia ccm leo anamsafisha! shame.

Membe hawezi kutoboa na uwenda akauzika upinzani zaidi ya fisadi lowassa alivyofanya.
Ndio maana wakaitwa wapinzani njaa hata mbowe na lisu walimuita lowasa na sumaye kila jina baya halafu wa kawasafisha na lowasa akawa mgombea uraisi, Tanzania hakuna wapinzani ni wachumia tumbo tu
 
mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
3,968
2,000
Zitto Mwaka 2015 alikuwa mtu wa kwanza kumsema Membe juu ya ufisadi wa pesa za LIBYA alipotangaza kugombea kupitia ccm leo anamsafisha! shame.

Membe hawezi kutoboa na uwenda akauzika upinzani zaidi ya fisadi lowassa alivyofanya.
Katika siasa hamna adui wa kudumu au rafiki wakudumu kichopo ni maslahi ya kudumu......kwahiyo hiyo sio issue
 
paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
1,521
2,000
Ujenzi wa Chama Imara ni kazi inayohitaji uvumilivu, muda wa kutosha, jasho na damu pia, ni kazi inayohitaji kutumia akiri nyingi na Hekima na Neema za Mungu!
Kiwango ambacho kilifikiwa na Chadema, kukakosekana kitu kidogo tu, Interejensia ya kung'amua ujasusi wa Chama tawala,

Si kila mti wa tunda utakaoupanda eti uote,ukue na Kisha uyale wewe matunda yake! Kuna kazi zingine ni za mtu kukumbukwa tu Kwa misingi aliyoiweka

Kwa mwenendo huu, natabiri, hiki Chama cha ACT kama kispobadiri namna ya siasa zake, muundo wake na kiuongozi, hiki ndicho Chama ambacho hakitakaa Kwa muda mrefu kwenye siasa za Taifa la Tanzania
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
28,842
2,000
Kitu ambacho CHADEMA hakitaruhusu kutokea ni kuunga mkono mgombea urais wa ACT WAZALENDO.

Kufanya hivyo itakuwa ni tiketi ya moja kwa moja kuwa kimeiruhusu ACT kukua kupitia mgongo wake na CHADEMA kusinyaa kupitia ACT.

It will never happen.
This is well calculated by chadema! Hawana mbavu za kupimana na jpm, wao watamteua lissu ila lisu atajitoa. Watamuunga mkono membe.
 
EZZ CHEZZ

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
739
1,000
Ningekuwa Membe, Wakati huu ndio ungekuwa Wakati wa kupumzika kisiasa, kwani si rahisi Kwa mtu kama Membe Kwa siasa alixokuwa amefikia halafu Leo arudi chekechea, hizi siasa ndizo zilizowashusha hadhi kina Sumae na wengine,

Lakini Kwa kuwa huenda tena ikawa na siasa zilezile za CCM na ujasusi wake, Membe nenda kama ulivyotumwa na CCM kafanye yako, na temu hii hili bomu likiwalipukia hawa vichwa maji labda watakoma kushobokea vitu vizuri vizuri vilivyotegwa barabarani vikitafuta wajinga wasio ridhika na vyao

2015 nililazimika kukikacha Chama changu pendwa Kwa vitu hivihivi vya kijinga
Umenikumbusha namna 2015 ulivyokuwa mwaka wangu mgumu kisiasa. Chama nilichokiamini kilisaliti harakati kimiujiza ujiza. Naona zile tikitaka zinajirudia. Acha waendelee kujivuruga.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
23,363
2,000
Ndio maana wakaitwa wapinzani njaa hata mbowe na lisu walimuita lowasa na sumaye kila jina baya halafu wa kawasafisha na lowasa akawa mgombea uraisi, Tanzania hakuna wapinzani ni wachumia tumbo tu
Kinachowindwa na Zitto kwa Membe sio yeye kama yeye inawindwa pesa yake waibomoe kama walivyobomoa ya Lowasa

Wanaiwinda hela yake
 
Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,247
2,000
Hahahaha Membe ana kwenda kugombea Urais kupitia ACT na hii ilijulikana toka zamani sema tuu huyu Zitto ana tufanya sisi watoto hahahaha
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,313
2,000
Ndio maana wakaitwa wapinzani njaa hata mbowe na lisu walimuita lowasa na sumaye kila jina baya halafu wa kawasafisha na lowasa akawa mgombea uraisi, Tanzania hakuna wapinzani ni wachumia tumbo tu
Nyie mliemtukana EL kwenye kampeni mbona aliporudi CCM mlimpokea kama mfalme?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom