Zitto, Makamba wautaka urais?

Joblube

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
369
151
Wana JF

Mimi ni miongoni mwa wale wanao amini kuwa siasa kati ya vyama na vyama si uadui bali ni kutofautiana kwa hoja katika kusukuma gurudumu la maendeleo. Hivyo ni muhimu kwa wanasiasa wetu wapingane kwa hoja lakini yanapokuja katika kusimamia maslahi ya taifa wayasimamie kwa pamoja bila kujali itikadi zao. Pia si vibaya kwa wanasiasa wetu kushirikana iwe kwa wale wa upinzani na wa chama tawala.

Bada ya kusema hayo nataka kutoa angalizo kwa CHADEMA juu ya ushirikiano wa kisiasa kati ya Makamba na Zitto niseme tuu huu ni mtazamo wangu naweza kuwa sahii au laa. Ukitazama kwa sasa juu ya harakati za kisiasa za hawa mabwana ni kama vile utadhani wako chama kimoja,huoni wakipingana kwa hoja wao kwa wao pia utaona kuwa vyombo vyote vya habari vile vinavyoshabikia propaganda mbovu kwa CHADEMA kama Jombo leo, TAZAMA, na Clauds FM vipo mstari wa mbele katika kuwashabikia hawa wawili kwa mfano ukiridi kwenye suala la posho za wabunge utaona kuwa CHADEMA na wabunge wake wote wamekuwa wakipinga hoja ya poshao za wabunge hadharani sijawahi kumwona Januari akipinga jambo hilo nje ya vikao vya bunge lakini imejengwa dhana na vyombo hivi vya habari kuwa hawa tuu ndio wapingaji wa suala la posha katika msingi huo ndipo ninapojenga hisia na angalizo kwa CHADEMA kuwa makini na urafiki huu yawezekana ukawa ni mkakati maalumu wa CCM kumbuka wamesema wamefungulia mbwa kwa sasa na hakuna kulala mpaka 2015.Nirudie tu niseme huo ni mtazamo wangu naweza kuwa sahihi au kinyume chake na hili ni angalizo tuu.
 
Kwanini angalizo hili tusilielekeze CCM kwamba yawezekana ukawa ni mkakati maalum wa CHADEMA?
What you see is what you get.
 
Uxkonde......! Kila ki2 kpo poa but makamba ni mpiganaji zasy hata Mbowe alimkaribisha ajiunge na CDM pale bungeni so ni lazima ashikamane na mpiganaji mwenzake zitto.
 
Jamani wadau mimi ninawasiwasi sana na ukaribu na utendaji kazi wa Zito Kabwe yaana urafiki aliokuwa nao na wanamagamba unatia wasiwasi suala moja lakujiuliza kwanini asishirikiane na watu


kamaMnyika,lema,msigwa,kasulumbayi,mbilinyi na makamanda wengine huu ukaribu wake na wakina January na kigwangala hatusemi wawe maadui ila tu kisiasa ukifanyakazi na watu mnaotofautiana itikadi hasa ikiwa wapo wenzako ambao mnaitikadi sawa wengi tu unaoweza kufanyanao kazi inatia sana mashaka lakini pia kuna dalili ya agenda ya chinichini kuunganisha nguvu hii ni kwa maslahi ya naani? NAWEKA WAZI MASHAKA YANGU ILI KUWEKA KUMBUKUMBU VIZURI JUU YA HILI


 
Zito anajibagua sana na wana mabadiliko wenzake,tulisha mzoea yule,nafikiri udini unamsumbua sijui kwa nini asirudi ccm
 
Hakuna ubaya wowote Zitto kufanya kazi Janauri, kinachotakiwa ni kuwa mzalendo na nchi yako kwa mustakabali wa taifa letu.

Kwa mara ya kwanza leo umeandika pointi mkuu wangu.Tukutane Arumeru lakini
 
Nashangaa anashndwa kuwa karbu na hata a smart boy mh mnyika. Zittophobiasis inamsumbua
 
Enzi zake zitto, Huyu na mwanasiasa uchara

images
 
Waanza kampeni ya kupunguza umri wa urais
headline_bullet.jpg
Wataka sasa upunguzwe hadi miaka kufikia 35



Umri(1).jpg

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (kushoto), akisisitiza jambo wakati akichangia mada katika kongamano la kuelimisha vijana kuhusu Katiba lililoandaliwa na Femina Hip. Kulia ni Mbunge wa Bumbuli, January Mmakamba. (Picha na Omar Fungo)


Mbunge wa Bumbuli (CCM), January Makamba, ameshauri katiba mpya inayotarajiwa kuundwa nchini iwe na mabadiliko yatakayoupunguza sifa ya umri wa mgombea kiti cha urais toka miaka 40 ya sasa hadi kufikia miaka 35 ili kutoa nafasi kwa vijana kugombea.

Msimamo wa Makamba uliungwa mkono na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ambaye alikwisha kusema kwamba mwaka 2015 hatagombea tena ubunge ila atajitosa katika urais.

Makamba alisema kwa kufanya hivyo kutawawezesha vijana ambao ni zaidi ya asilimia 65 ya idadi ya Watanzania kuwa na fursa ya kugombea nafasi hiyo ya juu nchini na hatimaye kushiriki moja kwa moja kwenye maamuzi yanayohusu mustakabali wa nchi yao.

Aidha, Makamba, aliyezaliwa Januari 28, 1974 alipendekeza katiba mpya iwe na mabadiliko yatakayoruhusu sifa ya umri wa raia kupiga kura upunguzwe kutoka miaka 18 ya sasa hadi miaka 16 kwa lengo la kupanua wigo wa vijana kushiriki katika maamuzi ya kumchagua rais na wakilishi wanaowataka.

Makamba aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akishiriki kwenye warsha ya Vijana na Katiba iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Femina na kuwashirikisha vijana wa kada mbalimbali pamoja na mabalozi, wabunge, wanaharakati, maofisa wa serikali na wanafunzi.

“Pamoja na mambo mengine ya msingi, tutakayokubaliana kama taifa, ningependelea zaidi katiba ijayo iwe na mabadiliko hayo niliyoyataja hapo juu, na hili ninawaasa tulipiganie,” alisema na kuongeza:

“Wakati umefika kwa vijana kushiriki kwenye ngazi zote za maamuzi kwa ajili ya kuhakikisha mambo yanayotuhusu yanaingia kwenye mipango ya utekelezaji na si wakati wa kukaa pembeni na watu wengine kutufanyia maamuzi.”

Ingawa Makamba na Zitto hawakutaka kusema wazi wazi kwamba wanataka marekebisho hayo ya sheria yafanyike ili wajitose kwenye urais, walisema kuwa warsha ya jana haikuwa kwa ajili ya kutangaza nia ya kuwania urais, ingawa walijenga hoja ya marekebisho ya sheria ili vijana wapate fursa hiyo.

Ingawa Makamba hajatangaza kokote kuwa atawania urais mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu, kauli yake inakuwa kama mwangwi wa habari ambazo zimekuwa zikielezwa kwamba ni miongoni mwa vijana wanaotamani urais ili kuwakilisha maslahi na hisia za vijana.
Naye Zitto akijenga hoja ya vijana kuruhusiwa kuwania urais kwa kushusha umri unaoruhusiwa kisheria kutoka miaka 40 hadi 35, alisema kuwa nchi zote za maziwa makuu, kama Uganda, Kenya, Burundi na Rwanda umri wa kuwani urais ni miaka 35 na kuhoji ni kwa nini Tanzania ni tofauti.

Kauli ya jana ya Zitto inazidi kuthibitisha nia yake ya kuwania urais ambayo alianza kuitoa mwaka 2010 wakati wa kuwania ubunge.

Akihutubia moja ya mikutano ya kampeni za uchaguzi wa ubunge wa mwaka 2010 katika jimbo lake, aliwaambia mamia ya wananchi waliokuwa wamekusanyika kumsikiliza kwamba mwaka 2015 atakaporejea tena kuwaomba kura hazitakuwa za ubunge ila ni za urais.

Zitto aliingia bungeni mara ya kwanza mwaka 2005 akiwa ni mbunge kijana kuliko wote walioingia katika chombo cha wawakilishi mwaka huo akiwa na umri wa miaka 29. Alizaliwa Septemba 24, 1976.

Kadhalika, Zitto, aliwaasa vijana kuachana na siasa za kulalamika bila ya kutoa majawabu ya matatizo wanayoyalalamikia na kwamba enzi hizo zimepitwa na wakati.

“Siasa za vijana wa sasa ni za kutoa masuluhisho ya kukabiliana na changamoto zilizopo bila ya kuangalia itikadi za kivyama, kama ambavyo tumekuwa tukifanya mimi na Makamba katika mambo ya msingi yenye maslahi kwa nchi. Ni lazima palipo na maslahi ya nchi, tusimame pamoja kwa kuwa bila ya kufanya hivyo, watu wengine watatusemea,” alisema.

Aidha aliwaasa vijana kutowaachia wanasiasa suala la katiba mpya kwa kuwa wao wanaangalia maslahi yao, badala yake wahakikishe kwamba wanashiriki kikamilifu kwenye mchakato huo kwa kutoa mawazo na mapendekezo yao ili yawe sehemu ya katiba mpya.



CHANZO: NIPASHE
 
Jamani wadau mimi ninawasiwasi sana na ukaribu na utendaji kazi wa Zito Kabwe yaana urafiki aliokuwa nao na wanamagamba unatia wasiwasi suala moja lakujiuliza kwanini asishirikiane na watu
kamaMnyika,lema,msigwa,kasulumbayi,mbilinyi na makamanda wengine huu ukaribu wake na wakina January na kigwangala hatusemi wawe maadui ila tu kisiasa ukifanyakazi na watu mnaotofautiana itikadi hasa ikiwa wapo wenzako ambao mnaitikadi sawa wengi tu unaoweza kufanyanao kazi inatia sana mashaka lakini pia kuna dalili ya agenda ya chinichini kuunganisha nguvu hii ni kwa maslahi ya naani? NAWEKA WAZI MASHAKA YANGU ILI KUWEKA KUMBUKUMBU VIZURI JUU YA HILI


''MGENI AMANI'' Kwanza napenda kusema Mungu akubariki kwa kuwakumbusha wadau hofu uliyo nayo!!! Kama umekua ukifuatilia vizuri mimi ni mmoja wapo wa watu wanaomtilia shaka ZOTTO KABWE....Nilishawahi kuonya kwamba Mtu atakaye vuruga CHADEMA wasipokuwa makini ni ZITTO KABWE....Nawaomba viongozi wa Chadema wawe makini na huyu mtu!!!! Hata kama ni mchapa kazi na mjenga hoja mzuri Tukumbuke hata SHETANI wakati mwingine alikuwa na uso wa malaika!!!! Chonde chonde wapenda haki muwe makini na ZITTO!!! Nilikuwa namkubali sana Zitto Lakini toka Magamba wamteke nimekuwa na mashaka naye
 
hapana si busara kumshambulia zitto kwa kila jambo hata katika mambo yasiyokuwa ya msingi, zitto ana ratiba zake kama ambavyo myika, sugu na wengine wanazo hivyo kufanya kazi pamoja inategemea ratiba zao. pili mnyika na zitto walikuwa tanga pamoja kwa muda wa wiki nzima sijaona shida. tatu, malengo ya mapambano haya ni kupigana na udhalimu, kutokuwajibika, uonevu na kadhia nyingine zinazofanana na hizo, ikiwa anashirikiana na wanaopigana vita hivyo mbona shida hakuna.
 
Hakuna ubaya wowote Zitto kufanya kazi Janauri, kinachotakiwa ni kuwa mzalendo na nchi yako kwa mustakabali wa taifa letu.

kausake kwanza uadilifu kwa makinda, ndugai, kashilila, msekwa, jk, tendwa, chatanda, chiligati, lukuvi, manyanya, ngedere sorry simba······································ kabla hujafikiria kuja chadema na wingineko.
 
Back
Top Bottom