Zitto, Makamba wautaka urais?

Maikitika kusema kuwa vijana hawa wawili ZITTO na JANUARY wana lao jambo......Naweza kusema kuwa wana uchu wa madaraka...HIVI JAMANI ikulu kuna nini? Mbona kila mtu anataka kukumbilia pale? ZITTO anampango wa kuibomoa CDM ndio maana ameona aanze mkakati wa kuingiza suala la umri wa uraisi kwenye katiba. Tukumbuke ni ZITTO huyu huyu aliwahi kuwaambia wapiga kura wake kule Kigoma kuwa mwaka 2015 hatagombea tena Ubunge bali Urais. Hivi ni nani amemuakikishia kuwa CDM watamteua yeye kuwa mgombea wao wa Urais ? Kwanza kwa umri wake alio nao kama katiba mpya isipo afiki swala la umri wa miaaka thelathini na tano kwa mgombea urais hatan kidhi vigezo maana atakuwa na miaka 39 tu!!! Tujiulize sasa je? Hakuna mkono wa mtu hapo!!! KUONAO nasema KUNAO!!! Mtizame anavyoshirikiana na Magamba Sikatai kushirikiana ila tujiulize mbona ukaribu wake na magamba ni mkubwa kuliko hata wake na Makamanda wenzake wa CDM??? ''''' HILO ANGALIZOooooooooooooooooooooooooooooooooooo''''

Umesema kama nilivyokuwa nawaza
 
MNATUPOTEZEA MUDA NA THREAD ZA KIPUUUZI NANI KATIKA NCHI HII ATAMPA ZITTO URAISI NANI??HATA CDM HATUWEZI KUMCHAGUA SIO TUU KUGOMBEA URAISI HATA UBUNGE 2015 HATUMTEUI LABDA AENDE NCCR KAMA SHEMEJI YAKE KAFULILA ILA CDM HATUMTEUI HATA KUGOMBEA UBUNGE

TOENI MADA ZA KUPOTEZA MUDA TUNAFANYA KAZI KUSOMA UPUUUZI,ETI ZITTO NA MAKAMBA ,MAKAMBA KWANZA SI MGONJWA 2015 ATAFIKA KWA AFYA YAKE UNADHANI??MWANGALIE VIZURI MTU ANATEMBEA KAMA ATAANGUKA KESHO

MASABURI NYiE
 
MNATUPOTEZEA MUDA NA THREAD ZA KIPUUUZI NANI KATIKA NCHI HII ATAMPA ZITTO URAISI NANI??HATA CDM HATUWEZI KUMCHAGUA SIO TUU KUGOMBEA URAISI HATA UBUNGE 2015 HATUMTEUI LABDA AENDE NCCR KAMA SHEMEJI YAKE KAFULILA ILA CDM HATUMTEUI HATA KUGOMBEA UBUNGE

TOENI MADA ZA KUPOTEZA MUDA TUNAFANYA KAZI KUSOMA UPUUUZI,ETI ZITTO NA MAKAMBA ,MAKAMBA KWANZA SI MGONJWA 2015 ATAFIKA KWA AFYA YAKE UNADHANI??MWANGALIE VIZURI MTU ANATEMBEA KAMA ATAANGUKA KESHO

MASABURI NYiE

Samahani kama nimekuudhi ili ni vizuri tukapingana kwa hoja
 
nawashangaa wanaoshangaa ukaribu wa Zitto na Makamba January, hawa wote si walichaguliwa ili watusaidie isitoshe serikali imewachagua kwenye kamati mbali mbali bila kujali tofauti zao, wamegundua madudu mengi kwenye mawizara na kuokoa pesa nyingi zilizokuwa zinapotea, hivyo wako wako sahihi
 
Kapotezwa na mnyika na tundu lissu bungen,,,kujiamin kumeisha hao jamaa wana fikir sana ndo maana amegeukia upande mwingine
 
nawashangaa wanaoshangaa ukaribu wa zitto na makamba january, hawa wote si walichaguliwa ili watusaidie isitoshe serikali imewachagua kwenye kamati mbali mbali bila kujali tofauti zao, wamegundua madudu mengi kwenye mawizara na kuokoa pesa nyingi zilizokuwa zinapotea, hivyo wako wako sahihi
baada ya kugundua?
 
Mimi nilidhania kuwa siasa ni uwanja wa mapambano ya fikra na si uadui!
Kupishana mitazamo hakuna maana ya udhaifu, na badala yake ni ukomavu.
Kama lipo linalofanyika kwa masilahi ya taifa kuna tatizo gani kukaa meza moja?
Suala hilo tusiliangalie kwa akina Zitto, nimeliona hapa JF. Watu hawapambanishi hoja bali hoja zinawapambanisha hadi kurushiana maneno machafu. Siasa haiendi hivyo.

Kuhusu umri, hili tumelijadili mara nyingi. Mimi sipendi kubaguana kwa kigezo cha ujana au uzee.
Kwanini watu tusiangalie mambo haya wakati wa kumtafuta au kuchagua kiongozi.
1. Mtizamo wake kuhusu jamii 2. Uelewa wake wa jamii 3. Uadilifu wake katika jamii 4. Historia yake ya ubunifu, utendaji na uongozi 5. Exposure katika dunia ya leo 6. Ueledi na maarifa aliyojipatia kupitia elimu 7. Misimamo yake kuhusu masuala ya jamii. Haya ni kwa uchche tu.

Naiangalia jamii yetu sijaona mahali ambapo ujana umesaidia kiongozi au uzee umekuwa dawa ya uongozi.
Katika kipindi hiki cha uongozi wa ujana, taifa limekuwa katika vurugu ya maadili kuliko wakati mwingine wowote.
Hata wazee wameiga mfano na tumeona wazee walioapa kwa kutumia katiba wakifanya tusiyotarajia.

Blair, Obama, Clinton, Putin n.k hawakuchaguliwa kwasababu ni vijana, bali kwa mitazamo na fikra pevu na wote wana prove hivyo. Hii haina maana Churchil, Washington, Gandhi na Mandela wapo chini yao, la hasha.
Kigezo cha kuwalinganisha si umri ni yale niliyoyataja.

Yahya Jamein na Samwel Doe wamekuwa marais katika umri wa chini ya 30. Ni kipi cha ajabu tunachoweza kusema walikifanya tofauti na William Tolbert, Augustino Neto au Nassar?

Tuwaangalie viongozi kwa thamani na wasifu wala sio wajihi
 
Mkuu, hata jk wakati anaomba kuingia ikulu aliahidi kuipitia upya mikataba ya madini kwa lengo la kuiboresha, hiyo ilionekana kuwa ni maslahi ya taifa, ameshaipitia?
Mkuu Zitto ni Zitto n JMK ni yeye, walizaliwa tofauti na wanafanya kazi tofauti na wameishi na kulelewa tofauti na hata upeo wao wa uelewa ni tofauti. Kumhukumu Zitto kwa makosa ya JK ni UTAPIAMLO wa akili
 
MNATUPOTEZEA MUDA NA THREAD ZA KIPUUUZI NANI KATIKA NCHI HII ATAMPA ZITTO URAISI NANI??HATA CDM HATUWEZI KUMCHAGUA SIO TUU KUGOMBEA URAISI HATA UBUNGE 2015 HATUMTEUI LABDA AENDE NCCR KAMA SHEMEJI YAKE KAFULILA ILA CDM HATUMTEUI HATA KUGOMBEA UBUNGE

TOENI MADA ZA KUPOTEZA MUDA TUNAFANYA KAZI KUSOMA UPUUUZI,ETI ZITTO NA MAKAMBA ,MAKAMBA KWANZA SI MGONJWA 2015 ATAFIKA KWA AFYA YAKE UNADHANI??MWANGALIE VIZURI MTU ANATEMBEA KAMA ATAANGUKA KESHO

MASABURI NYiE
Hili shuzi kawapelekee wapumba.vu wenzio sio great thinkers
 
Wana JF

Juzi nilisoma gazeti la Nipashe nilikuta habari ya watu wengi wanaopinga hoja ya hawa wawili. Makamba na Zitto wanashauri umri wa kugombea uraisi ushushwe uwe chini ya miaka 40 yaani ewe miaka 35. Wengi wamepinga na kupendekeza ubaki hiyo miaka aruabaini kwa kuwa umri huu angalau mtu anakuwa ameshaanza kukomaa na kuweza kutawala kwa kiasi kikubwa mihemuko ya ujana na pia atakuwa ameshapitia uzoefu mbalimbali ikiwa ni pamoja ya kuweza kuongoza au kuingia katika tasisi ndogo ya ndoa na kupimwa jinsi alivyoimudu. Mwingine alichangia kuwa tuwe makini na vijana hawa kwa kuwa wanaongozwa na taama zao na agenda zao za siri, hili likanikumbusha uchaguzi uliopita wakati Zitto anapiga kampeni aliwaambia wapiga kura wamchague kwa mara ya mwisho safari nyingine atakoyokuja hatakuja kama mgombea ubunge bali nafasi nyingine ya juu zaidi, na cha kushangaza zaidi hakumpigia kampeni mgombea wa urais wa chama chake bali wa chama mpainzani wake. Mpaka leo hajaweka hadharani kuwa badala ya ubunge wake kwisha 2015 atafanya nini sasa kaja na hoja ya kupunguza umri wa uraisi, kwa mtu makini ukilinganisha na hayo aliyokuwa akiyasema na kampeni zake huko nyuma na mbaya zaidi badala ya kushirikiana na timu yake anakuja na kijana anayejulikana yuko chini ya EL na RA mabingwa wa kuweka viongozi madarakani mtu makini lazima ujiulize na udhani kuwa hapo kuna jambo linalosukwa la kuivurugia CHADEMA huko tunakokwenda? Bado huu ni mtazamo wangu tuu naweza kuwa sahihi au kinyume chake.
 
Back
Top Bottom