Tusiwe kama punguawani wa akili. Hivi Zitto angeongoza ujumbe wa CDM kumuona Rais kuhusu mapendekezo ya rasimu ya katiba si ndio mngesema kuwa anajipendekeza kwa Rais. Nashukuru Zitto hakuwepo na waliokuwepo ni wale mnaoamini ndio CDM damu. Kila jambo akifanya Zitto na watu wa CCM bila nyie kuangalia manufaa yake kwa taifa anaonekana msaliti, kwanini tumefikia hapa?. Ama kweli waswahili walisema 'Kunyata anyate kinyonga, akinyata kicheche anavizia kuku'. Zitto nakusihi kuwa endelea kuweka mbele maslahi ya taifa, sababu watu hawajui kuwa unatekeleza maslahi ya chama chako CDM.